Ugonjwa wa fizi,chanzo,Dalili na TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa fizi,chanzo,Dalili na Tiba

Hapa tunazungumzia matatizo ambayo huathiri Tishu zinazozunguka Meno yako.

Huu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya fizi na huhusisha matokeo mbali mbali kama vile kuvimba kwa fizi, Fizi kutoa damu, Fizi kuuma N.K

CHANZO CHA UGONJWA WA FIZI

Zipo Sababu mbali mbali zinazopelekea Mtu kupata shida ya Fizi ikiwemo;

- Mtu kushambuliwa na magonjwa mbali mbali ambayo huathiri tisu za meno maarufu kama Periodontal diseases

- Mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria,fangasi,virusi N.K

- Kuumia kwa tisu za meno au fizi kutokana na sababu mbali mbali kama vile; Kuchomwa na kitu cha ncha kali N.K

- Mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ambao ni ngumu kuudhibiti yupo kwenye hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya Fizi

Dalili za Ugonjwa wa Fizi

DALILI ZA UGONJWA WA FIZI NI PAMOJA NA;

1. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kwenye fizi hasa wakati wa kula kitu chochote.

2. Fizi za mgonjwa kutoa damu.

3. Fizi za mgonjwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana kuliko kawaida.

4. Mgonjwa kupatwa na shida ya Fizi kuvimba.

5. Kuwa na vidonda au michubuko kwenye ngozi ya fizi. n.k

MATIBABU YA UGONJWA WA FIZI

- Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu japo hutegemea chanzo husika cha ugonjwa huu.

Hivo ni vizuri mgonjwa kupata uchunguzi kwa kina pamoja na kupata matibabu sahihi kulingana na Shida yake.

KUMBUKA; Usafi wa kinywa ni muhimu sana ili kusaidia kuondoa uchafu wa chakula au mabaki ya chakula, kusaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni pamoja na kukukinga na magonjwa mbali mbali ya Fizi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

2 Comment

Ugonjwa wa Mapafu dalili zake,Chanzo na TibaAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Mapafu dalili zake,Chanzo na Tiba

Ugonjwa wa Mapafu ni nini?

Tunapozungumzia Ugonjwa wa Mapafu au Lung disease hatumaanishi kitu kimoja,bali tunamaanisha mjumuisho wa magonjwa yote yanayoathiri mapafu na kuzuia utendaji kazi wa kawaida wa Mapafu.

Tafsiri hii inamaanisha ni Zaidi ya Ugonjwa Mmoja tunapozungumzia Ugonjwa wa Mapafu, hivo Daktari akikuambia Una Ugonjwa wa Mapafu,Muulize Upi.

hebu tuangalia Makundi haya ambayo tumeyachambua kuhusu Magonjwa yanayoathiri Mapafu;

(1) Airway diseases -- Kundi hili hujumuisha Magonjwa ambayo huathiri mirija (njia ya hewa) inayosafirisha oksijeni na gesi nyingine kuingia na kutoka kwenye mapafu. 

Na mara nyingi husababisha kupungua size ya mirija ya hewa na kuifanya njia kuwa nyembamba zaidi(narrowing) au kuziba kabsa kwa njia za hewa.  Magonjwa haya yanayoathiri njia ya hewa ni pamoja;

  • Ugonjwa wa asthma au Pumu, 
  • chronic obstructive pulmonary disease (COPD) n.k.

(2) Lung tissue diseases -- Magonjwa haya huathiri muundo wa tishu za mapafu,kusababisha makovu au kuvimba kwa tishu za mapafu n.k

Kovu au kuvimba kwa tishu hufanya mapafu kushindwa kupanuka kikamilifu na kusababisha ugonjwa wa kuzuia mapafu kufanya kazi(restrictive lung disease). 

Hii inafanya kuwa vigumu kwa mapafu kuchukua oksijeni na kutoa kaboni dioksidi, Watu walio na aina hii ya ugonjwa wa mapafu mara nyingi husema wanahisi kama "wamevaa sweta au fulana inayobana sana kifua hali inayowafanya wasipumue vizuri" 

Mfano wa Magonjwa haya yanayoathiri tishu za Mapafu ni pamoja na;

  • Pulmonary fibrosis
  • Na sarcoidosis

(3) Lung circulation diseases -- Magonjwa haya huathiri mishipa ya damu kwenye mapafu.  Husababishwa na kuganda, makovu, au kuvimba kwa mishipa ya damu. 

Yanaathiri uwezo wa mapafu kuchukua oksijeni na kutoa kabonidioksidi,Magonjwa haya yanaweza pia kuathiri kazi ya moyo.  

Mfano wa ugonjwa wa mzunguko wa damu kwenye mapafu ni;

  • shinikizo la juu la damu kwenye mapafu(pulmonary hypertension)
Watu walio na hali hizi mara nyingi huhisi ugumu wa kupumua.

Aina Za Magonjwa ya Mapafu ambazo hujulikana Zaidi

Tuangalie aina za magonjwa ya Mapafu ambazo hutokea sana;

- Ugonjwa wa Asthma au Pumu

- Saratani ya Mapafu

- Ugonjwa wa Nimonia

- Ugonjwa wa Mapafu kujaa Maji

- Ugonjwa wa Mapafu kuziba

- Ugonjwa wa TB

- Ugonjwa ambayo hujulikana kama Chronic obstructive pulmonary disease (COPD) N.k

Dalili za Ugonjwa wa Mapafu

Dalili zinaweza kutokea kulingana na aina ya Ugonjwa husika,ila kwa ujumla Mgonjwa huweza;
  • Kupata Shida ya kupumua,kukosa pumzi
  • Mgonjwa kuhisi hali ya Kifua kubana,kifua kuwa kizito
  • Mgonjwa kukohoa
  • Mgonjwa kutoa Sauti wakati wa kupumua maarufu kama Wheezing Sound
  • Mgonjwa kupata maumivu ya kifua
  • Mgonjwa Kutoa makohozi mazito,Usaha,makohozi yaliyochanganyika na Damu n.k

Chanzo cha Ugonjwa wa Mapafu 

• Maambukizi ya Vimelea mbali mbali kama vile

  • Bacteria,
  • Virusi
  • Fangasi n.k

• Sababu za Kigenetics,mambo ya kurithi  n.k

• Sababu za kimazingira kama vile; Kukaa Sehemu zenye kemikali kama viwandani,Maeneo ya vumbi sana,Sumu

• Uvutaji wa Sigara,Mfano Miongoni mwa Sababu kubwa ya Saratani ya Mapafu ni pamoja na Uvutaji wa Sigara

• Matatizo ya Kinga mwili n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Tatizo La Tonses,chanzo Na TibaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo La Tonses,chanzo Na Tiba

Tatizo la tonses au wengine huliita tatizo la Tonsil ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa tonses kwa kitaalam Tonsillitis Tatizo hili mara nyingi huathiri watoto ingawa hata watu wazima huweza kupata pia.

Tatizo hili huambatana na Dalili mbali mbali, Sasa katika makala hii tuangalie Dalili Zake,Chanzo pamoja na Tiba Yake.

Dalili za Tatizo la Tonses

Dalili kubwa za Tatizo la Tonses ni pamoja na:

  • Eneo la Tonses kubadilika rangi na kuwa jekundu
  • Kuvimba eneo la tonses
  • Kupata shida ya kumeza kitu
  • Au kupata maumivu wakati wa kumeza kitu
  • Homa
  • Kuhisi hali ya Vidonda kooni,Sore throat
  • Tezi za shingoni maarufu kama Lymph nodes kuongezeka ukubwa,kuuma n.k
  • Sauti kukwaruza
  • Kutoa harufu mbaya Mdomoni au puani
  • Kupata maumivu ya Shingo
  • Shingo kukakamaa
  • Kupata maumivu ya Kichwa n.k

Chanzo cha Tatizo la Tonses

Tatizo la Kuvimba kwa Tonses husababishwa na maambukizi ya Vimelea vya magonjwa kama vile bacteria au Virusi. 

Na jamii ya bacteria inayohusika Zaidi ni pamoja na Streptococcus pyogenes au group A streptococcus, Pia jamii zingine za Streptococcus pamoja na bacteria wengine huweza kusababisha tatizo la tonses kuvimba.

Vitu ambavyo huongeza hatari ya Kupata Tatizo la Tonses

-Umri; Tatizo la kuvimba kwa Tonses mara nyingi huathiri watoto, Kuvimba kwa tonses kunakosababishwa na maambukizi ya bakteria ni kawaida sana kwa watoto wa miaka 5 hadi 15.

- Kuwa kwenye Mazingira ya kupata Vimelea vya Magonjwa kwa Urahisi mara kwa mara(Frequent exposure to germs). Mfano;Watoto wanaokwenda shule wanakuwa na mawasiliano ya karibu na wenzao, Hii inawafanya mara kwa mara wakabiliwe na maambukizi ya virusi au bakteria ambayo yanaweza kusababisha tatizo la kuvimba kwa tonses.

Je, ni Kwanini Tonses hushambuliwa?

Tonses ni safu ya kwanza ya mfumo wa kinga ya Mwili dhidi ya bakteria na virusi Wanaoingia kinywani mwako.  Kazi hii inaweza kufanya tonses kuwa katika hatari Zaidi ya kuambukizwa na kuvimba.  

Hata hivyo, kazi ya mfumo wa kinga kwa tonses hupungua baada ya kubalehe - jambo ambalo linaweza kuchangia matukio ya kuvimba kwa tonses kupunguza Zaidi kwa watu wazima.

Matibabu ya Tatizo la Tonses

Kwa matibabu ya tatizo la kuvimba kwa Tonses, Tiba kamili hutegemea na chanzo husika, Mfano kama chanzo ni maambukizi ya bacteria Mgonjwa atapewa Dawa jamii ya antibiotics, Lakini kama Chanzo ni maambukizi ya Virusi kuna uwezekano mkubwa wa shida hii kuisha yenyewe ndani ya Siku 7 mpaka 10, pamoja na njia Zingine huweza kutumika ikiwemo; kupata muda wa kutosha wa kupumzika na kulala, kunywa maji ya Kutosha, kutibu dalili zingine kama Maumivu,Homa n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ugonjwa Wa Typhoid,Homa Ya Matumbo,Dalili,Chanzo Na TibaAfyaclass Bongo Social •

UGONJWA WA TYPHOID,HOMA YA MATUMBO,DALILI,CHANZO NA TIBA

Ugonjwa wa Typhoid,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa Typhoid ni Ugonjwa wa homa ya matumbo,hujulikana pia kama Typhoid fever au enteric fever, na chanzo chake ni maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama salmonella bacteria. 

Maji kuchafuliwa pamoja na vyakula tunavyokula huweza kupelekea bacteria hawa kusambaa na kuingia kwenye miili yetu,kisha kupelekea ugonjwa wa typhoid au homa ya matumbo.

DALILI ZA UGONJWA WA TYPHOID

Dalili zinaweza kuanza polepole, mara nyingi huonekana wiki 1 hadi 3 baada ya mtu kuathiriwa na bakteria kama hawa wa salmonella

Dalili za Awali ni zipi;

Dalili za awali ni pamoja na;

1. Mtu kuwa na Homa,

Homa ambayo huanzia chini na kuongezeka siku nzima, ikiwezekana kufikia 104 degrees Fahrenheit (40 degrees Celsius).

2. Mwili kutetemeka

3. Kupata maumivu ya Kichwa

4. Mwili kuchoka sana na kuwa dhaifu

5. Kupata maumivu ya Misuli

6. Kupata Maumivu ya Tumbo

7. Kuharisha au wengine kupata Choo kigumu(constipation).

8. Wengine hupata upele au Rashes kwenye ngozi.

9. Baadhi pia huweza kuwa na dalili zingine kama vile;

  • Kupata kikohozi
  • Kukosa Hamu ya kula
  • Kutoa Sana jasho n.k

Dalili za baadae;

Wiki chache baada ya dalili kuanza, ugonjwa unaweza kusababisha matatizo katika tumbo. Watu wanaweza kuwa na:

– Maumivu makali ya Tumbo

– Tumbo kuvimba Sana n.k

Pia Maambukizi yanayosababishwa na bakteria hawa tumboni yanaweza kuenea katika mwili wote na kusababisha hali inayoitwa sepsis.

Chanzo cha Ugonjwa wa Typhoid

Aina ya bakteria inayoitwa Salmonella enterica serotype typhi ndyo husababisha homa ya matumbo au Ugonjwa wa Typhoid. Aina zingine za bakteria wa salmonella husababisha ugonjwa kama huo unaoitwa paratyphoid fever.

Watu hupata bakteria hawa kwa kiasi kikubwa katika maeneo ambayo milipuko ya Ugonjwa wa Typhoid hutokea mara nyingi. Bakteria hutoka nje ya mwili kwenye kinyesi na mkojo wa watu wanaobeba bakteria.

Bila kuosha mikono kwa uangalifu baada ya kwenda Chooni, bakteria wanaweza kupita kutoka kwenye mikono hadi kwa vitu vingine kama maji,chakula n.k au kwa watu wengine.

Bakteria pia wanaweza kuenea kutoka kwa mtu ambaye hubeba bakteria. Wanaweza kuenea kwenye chakula ambacho hakijapikwa, kama vile matunda mabichi ambayo hayana maganda.n.k

Pia Katika maeneo ambayo maji hayatibiwi ili kuua vijidudu, unaweza kuchukua bakteria kutoka kwenye chanzo hicho. Hii inajumuisha maji ya kunywa, kutumia barafu iliyotengenezwa kwa maji ambayo hayajatibiwa, au kwa kunywa maziwa au juisi ambayo haijasafishwa vizuri(unpasteurized milk or juice). n.k

IKIWA UNA SHIDA HII KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Mjamzito Anaweza Kufanya Tendo La NdoaAfyaclass Bongo Social •

Mjamzito Anaweza Kufanya Tendo La Ndoa

JE KUNA MADHARA YOYOTE ENDAPO MAMA MJAMZITO AKIFANYA TENDO LA NDOA?

Hakuna madhara yoyote endapo mama mjamzito atafanya tendo la ndoa ikiwa mama huyo hana tatizo lolote, Hivo katika kufanya tendo la ndoa kwa mjamzito kuna angalizo, inaweza kuwa Salama au isiwe Salama kulingana na hali ya mama mjamzito husika.

tuangalie matatizo ambayo huweza kupelekea iwe vigumu kwa mama mjamzito kufanya tendo la Ndoa.

Matatizo ambayo huweza kusababisha Mama mjamzito asifanye Tendo la Ndoa(Pregnancy complications)

Ikiwa una matatizo ya ujauzito, kama vile kupata leba kabla ya wakati(preterm labor) au matatizo kwenye kondo la nyuma(placenta), unapaswa kuzungumza na daktari wako akuangalie na kutoa majibu ikiwa ni salama kwako kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito au la. 

Yapo baadhi ya matatizo ambayo huweza kuweka zuio la wewe kushiriki tendo la ndoa ukiwa mjamzito, na matatizo hayo ni kama vile;

1. Kuvuja damu sana

Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa ukiwa mjamzito ikiwa una tatizo la kutokwa na damu nyingi, kwani  kufanya hivo inaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu zaidi,

Lakini pia sio salama kushiriki tendo la ndoa ukiwa mjamzito ikiwa una tatizo la damu kushindwa kuganda yaani coagulopathy n.k,

2. Chupa ya Uzazi kupasuka

Ikiwa wewe ni mjamzito na chupa ya Uzazi imepasuka, Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa, kwani inaweza kuongeza hatari ya kupata maambukizi(infections). 

3. Kuwa na matatizo kwenye shingo ya kizazi(Cervical problems)

Mjamzito Unapaswa kuepuka kufanya tendo la ndoa ikiwa una matatizo yoyote kwenye shingo ya kizazi chako, kwani unaweza kuwa katika hatari kubwa ya kupata leba mapema,

Matatizo hayo ni pamoja na Shingo ya kizazi kulegea na kushindwa kuhimili ujauzito n.k.

4. Kupata Leba mapema au kabla ya wakati, Mimba kuharibika zenyewe n.k

Kwa mama mjamzito mwenye matitizo kama haya ni vizuri kuongea na Wataalam wa afya na kupewa Ushauri sahihi wa jinsi ya kushiriki tendo la ndoa.

HIVO; kufanya tendo la ndoa endapo huna tatizo lolote lile wakati wa ujauzito ni salama kabsa kwako

Bonus Tips; MAMA MJAMZITO AZINGATIE HAYA;

- Mahudhurio ya Kliniki kwa mama mjamzito ni muhimu sana

-  Mjamzito Apende kulala ubavu, hasa ubavu wake wa kushoto kuliko kulalia mgongo, na hili lifanyike hasa ujauzito ukiwa mkubwa

- Mjamzito Asivae nguo za kumbana sana, viatu virefu,mikanda tumboni n.k

- Mjamzito Apende kufanya mazoezi mara kwa mara, ujauzito sio ugonjwa,kiasi kwamba muda wote unalala kitandani.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD