Ugonjwa wa Mapafu dalili zake,Chanzo na Tiba
Ugonjwa wa Mapafu ni nini?
Tunapozungumzia Ugonjwa wa Mapafu au Lung disease hatumaanishi kitu kimoja,bali tunamaanisha mjumuisho wa magonjwa yote yanayoathiri mapafu na kuzuia utendaji kazi wa kawaida wa Mapafu.
Tafsiri hii inamaanisha ni Zaidi ya Ugonjwa Mmoja tunapozungumzia Ugonjwa wa Mapafu, hivo Daktari akikuambia Una Ugonjwa wa Mapafu,Muulize Upi.
hebu tuangalia Makundi haya ambayo tumeyachambua kuhusu Magonjwa yanayoathiri Mapafu;
(1) Airway diseases -- Kundi hili hujumuisha Magonjwa ambayo huathiri mirija (njia ya hewa) inayosafirisha oksijeni na gesi nyingine kuingia na kutoka kwenye mapafu.
Na mara nyingi husababisha kupungua size ya mirija ya hewa na kuifanya njia kuwa nyembamba zaidi(narrowing) au kuziba kabsa kwa njia za hewa. Magonjwa haya yanayoathiri njia ya hewa ni pamoja;
- Ugonjwa wa asthma au Pumu,
- chronic obstructive pulmonary disease (COPD) n.k.
(2) Lung tissue diseases -- Magonjwa haya huathiri muundo wa tishu za mapafu,kusababisha makovu au kuvimba kwa tishu za mapafu n.k
Kovu au kuvimba kwa tishu hufanya mapafu kushindwa kupanuka kikamilifu na kusababisha ugonjwa wa kuzuia mapafu kufanya kazi(restrictive lung disease).
Hii inafanya kuwa vigumu kwa mapafu kuchukua oksijeni na kutoa kaboni dioksidi, Watu walio na aina hii ya ugonjwa wa mapafu mara nyingi husema wanahisi kama "wamevaa sweta au fulana inayobana sana kifua hali inayowafanya wasipumue vizuri"
Mfano wa Magonjwa haya yanayoathiri tishu za Mapafu ni pamoja na;
- Pulmonary fibrosis
- Na sarcoidosis
(3) Lung circulation diseases -- Magonjwa haya huathiri mishipa ya damu kwenye mapafu. Husababishwa na kuganda, makovu, au kuvimba kwa mishipa ya damu.
Yanaathiri uwezo wa mapafu kuchukua oksijeni na kutoa kabonidioksidi,Magonjwa haya yanaweza pia kuathiri kazi ya moyo.
Mfano wa ugonjwa wa mzunguko wa damu kwenye mapafu ni;
- shinikizo la juu la damu kwenye mapafu(pulmonary hypertension)
Aina Za Magonjwa ya Mapafu ambazo hujulikana Zaidi
- Ugonjwa ambayo hujulikana kama Chronic obstructive pulmonary disease (COPD) N.k
Dalili za Ugonjwa wa Mapafu
- Kupata Shida ya kupumua,kukosa pumzi
- Mgonjwa kuhisi hali ya Kifua kubana,kifua kuwa kizito
- Mgonjwa kukohoa
- Mgonjwa kutoa Sauti wakati wa kupumua maarufu kama Wheezing Sound
- Mgonjwa kupata maumivu ya kifua
- Mgonjwa Kutoa makohozi mazito,Usaha,makohozi yaliyochanganyika na Damu n.k
Chanzo cha Ugonjwa wa Mapafu
• Maambukizi ya Vimelea mbali mbali kama vile
- Bacteria,
- Virusi
- Fangasi n.k
• Sababu za Kigenetics,mambo ya kurithi n.k
• Sababu za kimazingira kama vile; Kukaa Sehemu zenye kemikali kama viwandani,Maeneo ya vumbi sana,Sumu
• Uvutaji wa Sigara,Mfano Miongoni mwa Sababu kubwa ya Saratani ya Mapafu ni pamoja na Uvutaji wa Sigara
• Matatizo ya Kinga mwili n.k
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY
image quote pre code