Mitihani ya Kidato cha Sita (ACSEE) na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kuanza Leo May 05
Mitihani ya Kidato cha Sita (ACSEE) na Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada kuanza Leo May 05, 2025 Tanzania Bara na Zanzibar ambapo kwa Kidato cha Sita jumla ya Watahiniwa 134,390 wamesajiliwa kufanya mtihani huu kwa mwaka huu 2025 ambapo Watahiniwa wa Shule ni 126,957 na Watahiniwa wa Kujitegemea ni 7,433.
Katibu Mtendaji wa NECTA, Dr.Said Mohamed akiongea Jijini Dar es salaam leo May 04,2025 amesema “Mtihani wa Ualimu utakamilika May 19 , 2025 na Kidato cha Sita May 26, 2025, mtihani wa Kidato cha Sita utafanyika katika jumla ya Shule za Sekondari 982 na Vituo vya Watahiniwa wa Kujitegemea 245, mtihani wa Ualimu utafanyika katika Vyuo vya Ualimu 68”
“Jumla ya Watahiniwa 10,895 wamesajiliwa kufanya Mtihani wa Ualimu May 2025, kati ya Watahiniwa hao, 3,100 ni wa ngazi ya Stashahada na 7,795 ni wa ngazi ya Cheti, kwa ngazi ya Stashahada, Wanaume ni 1,751 sawa na asilimia 56.48 na Wanawake ni 1,349 sawa na asilimia 43.52”
Reply
image quote pre code