Mtoto Hope anayesumbuliwa na ugonjwa wa seli mundu, akabidhiwa kwa Dkt. Godwin Mollel
Mtoto Hope Justo Mboya mwenye umri wa miaka minne anayesumbuliwa na ugonjwa wa seli mundu, amekabidhiwa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel na wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kusaidiwa kupata matibabu.
Tukio hilo limefanyika wakati wa ziara ya Dkt. Mollel kwenye kambi ya matibabu ya macho bure siku ya Mai 03, 2025 mkoani humo na kuhudumia zaidi ya wananchi elfu mbili.
"Matibabu ya ugonjwa wa seli mundu kwa mtoto huyo yanakadiriwa kugharimu shilingi milioni tisini (90), ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amejitolea kudhamini gharama zote za matibabu hayo.
Dkt. Mollel ameipongeza familia ya mtoto huyo kwa imani waliyoionesha kwa Serikali na kusisitiza kuwa Wizara ya Afya itaendelea kushirikiana na wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinawafikia wananchi wote, hususan watoto wenye uhitaji maalum.
Reply
image quote pre code