Ajali ya Air India Vifo vyafikia Watu 133

Ajali ya Air India Vifo vyafikia Watu 133

#1

Ajali ya Air India Vifo vyafikia Watu 133



Mamlaka nchini India zimethibitisha kuwa Watu 133 wamefariki hadi sasa  kufuatia ndege ya abiria ya Air India iliyokuwa inatokea nchini India kwenda London nchini Uingereza kuanguka na kuwaka moto leo June 12,2025 katika eneo la Ahmedabad India muda mfupi baada ya kupaa ikiwa na Watu 242, ripoti zinasema  vifo vinahofiwa kuongezeka.

Air India imesema waliokuwa kwenye ndege hiyo ni pamoja na abiria 169 Raia wa India, abiria 53 Raia wa Uingereza, Wareno saba na Raia wa Canada nmoja na tayari Timu za dharura zipo eneo la tukio kutoa msaada, bado sababu za ndege hiyo kupoteza mawasiliano na kuanguka haijawekwa wazi.

Ndege hiyo ni Boeing 787-8 Dreamliner yenye usajili namba VT-ANB na serial namba 36279 na ilipelekwa kuanza kazi India January 2014.

REPLY HAPA


image quote pre code