Fahamu kuhusu faida za uji wa kimea,Wataalam wa afya waeleza

Fahamu kuhusu faida za uji wa kimea,Wataalam wa afya waeleza

#1

Fahamu kuhusu faida za uji wa kimea,Wataalam wa afya waeleza



Mbegu za nafaka zilizooteshwa zina  vimeng’enyo hai    ambavyo  husaidia  uyeyushwaji  wa chakula.

Uyeyushwaji wa chakula huanzia mdomoni ambapo husaidiwa na mate na kutafuna, na kwamba uyeyushaji huo baadaye huendelea tumboni.

Lakini kama ulikuwa hujui, magonjwa kama kuharisha huzorotesha uyeyushwaji  wa  chakula  na  ufyonzwaji  wa virutubisho mwilini.

Vile vile, dawa za antibaotiki  pia huharibu bakteria  wazuri  wanaosaidia  uyeyushwaji wa chakula  tumboni  na  hivyo  kufanya  uyeyushwaji na ufyonzwaji kuwa mgumu.

Hata hivyo, ufyonzwaji  wa  virutubisho  hufanyika  kwa  kiasi kikubwa  kwenye utumbo mwembamba.

Hivyo ili kukabiliana na uzorotesha wa uyeyushaji wa chakula, Ofisa lishe, kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe(TFNC), Elizabeth Lyimo, anasema mbegu za nafaka zilizooteshwa zina  vimeng’enyo hai    ambavyo  husaidia  uyeyushwaji  wa chakula.

Anazitaja baadhi ya mbegu hizo ni jamii ya mikunde, mahindi, mtama, ulezi, uwele, choroko, maharage na nyingine.

Anasema kuotesha mbegu mbalimbali huongeza kiasi cha protin, vitamin na madini katika chakula hicho.

Anabainisha kuwa uji wa kimea ni moja wapo ya vyakula vinavyosaidia na kuboresha  uyeyushwaji wa chakula na ufyonzwaji wa virutubisho mwilini.

Anasema mtu anayetumia uji wa kimea  hupata virutubishi vingi kutokana na kuongezeka kwa virutubishi na uwezo wa mwili kufyonza virutubishi hivyo kutoka katika vyakula mbalimbali.

“Uji wa kimea unaweza kupikwa kwa kutumia unga wa kimea peke yake au kwa kupika uji mzito kwa kutumia unga wa kawaida kisha kulainisha kwa kutumia kimea”anasema Lyimo.

Anasema uji wa kimea unapika kama unavyopika uji wa kawaida wa mahindi au ulezi.

Lyimo anasema tofauti ya uji wa kimea na ule wa unga wa kawaidia,  ni kwamba unga mwingi zaidi hutumika unapopika uji wa kimea kuliko unapopika uji wa kawaida kwani hauwi mzito mapema.

Anasema kwanza mtu anatakiwa kuchagua nafaka ambayo ni bora, nzuri na ambayo haijashambuliwa na wadudu.

Baada ya hapo, unaondoa uchafu kwa kusafisha kwa maji safi na kuweka katika chombo safi kisha unaloweka kwa maji kwa muda wa siku nzima.

Anasema baada ya kuloweka siku nzima, kesho yake nafaka hiyo unaiosha mpaka itakate na isitoe povu  na baada ya hapo unaiweka katika chombo safi kisha unafunika na kuweka mahali penye giza ili nafaka inapoota isipate mwanga wa jua.

Nafaka hiyo itakaa katika sehemu isiyokuwa na mwanga kwa siku mbili au tatu ili iote kwa kiasi na iwapo itatoa ukungu,  safisha tena nafaka hiyo mpaka utakapoona maji hayatoi povu.

Mtaalamu huyo anasema baada ya hapo nafaka hiyo utaianika kwa siku kadhaa juani mpaka itakapokuwa kavu na baada ya hapo unaweza kusaga au kutwanga na kupata unga wa kimea.

REPLY HAPA


image quote pre code