Maumivu wakati wa kukojoa (Dysuria) ni hali ya kuhisi kuungua, kuchoma au maumivu wakati wa kutoa mkojo. Hali hii inaweza kumpata mwanamke au mwanaume, na chanzo kinaweza kutofautiana kutegemea jinsia na hali ya kiafya. Hapa chini ni sababu kuu kwa kila jinsia:
SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA KWA MWANAMKE
1. Maambukizi kwenye njia ya mkojo (UTI)
Hii ndiyo sababu kuu kwa wanawake.
Bakteria huingia kwenye urethra na kusababisha maambukizi.
Dalili kuu ikiwemo: Maumivu wakati wa kukojoa, kukojoa mara kwa mara, harufu mbaya ya mkojo, mkojo kuwa na rangi isiyokawaida,maumivu ya viungo,homa n.k.
2. Maambukizi ya ukeni ambayo
Husababishwa na fangasi (candida), bakteria, au Trichomoniasis.
Hali hii Inaweza kuathiri uke na kusababisha maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa.
Yapo Maambukizi ya zinaa (STIs)
- Kama vile Chlamydia, Gonorrhea, Herpes au Trichomoniasis.
- Maambukizi haya huweza kuambatana na dalili kama vile uchafu ukeni, maumivu chini ya tumbo, maumivu wakati wa kukojoa na kuwashwa sehemu za Siri.
3. Matumizi ya sabuni au kemikali kali Ukeni
Baadhi ya Sabuni za kuosha uke, poda, au dawa za kupunguza harufu zinaweza kusababisha mabadiliko makubwa ya hali asilia ya ukeni kutokana na kemikali kali au viambato flani ndani yake,hali ambayo huweza kupelekea hatari ya mashambulizi zaidi ya fangasi au bacteria na kuleta dalili kama vile kuwasha na maumivu wakati wa kukojoa au tendo la ndoa.
4. Matatizo ya kibofu cha mkojo
Pia Kuvimba au kuambukizwa kwa kibofu cha mkojo kunaweza kusababisha maumivu wakati wa kukojoa.
SABABU ZA MAUMIVU WAKATI WA KUKOJOA KWA MWANAUME
1. Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)
Hali hii pia huweza kuwa miongoni mwa Sababu kubwa sana za maumivu wakati wa kukojoa,kuhisi hali ya kuungua au kuwaka moto wakati wa kukojoa kwa Mwanaume.
2. Maambukizi au magonjwa ya zinaa (STIs)
Magonjwa ya Zinaa kama vile;
- Chlamydia, Gonorrhea, Herpes ni sababu kubwa pia ya maumivu kwa wanaume.
Dalili zinaweza kujumuisha usaha kutoka kwenye uume, kuwasha, na maumivu wakati wa kukojoa.
3. Ugonjwa wa Tezi Dume au (kuvimba kwa tezi dume - Prostate)
Hali hii Huathiri wanaume hasa wenye umri wa kati au wazee.
Dalili huweza kuwa: Maumivu wakati wa kukojoa, maumivu ya nyonga, Sehemu ya chini ya tumbo, na kujisikia hali ya kubanwa mkojo mara kwa mara.
4. Kuvimba kwa korodani au epididymis (orchitis/epididymitis)
Ingawa maumivu ni kwenye korodani, yanaweza kusambaa hadi urethra na kuleta maumivu wakati wa kukojoa.
5. Kuwepo kwa mawe kwenye kibofu au figo
Mawe yanaweza kukwaruza njia ya mkojo na kusababisha maumivu makali wakati wa kutoa mkojo.
SABABU ZINGINE ZA JUMLA ZINAZOWEZA KUTOKEA KWA WOTE (MWANAMKE & MWANAUME)
- Kunywa maji kidogo,hii hukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa kama UTI
- kuwa na Vidonda ndani ya urethra au kibofu
- Tatizo la Saratani ya kibofu au urethra (ingawa ni nadra lakini inawezekana pia)
Je,Unatatizo hili na hujapata Tiba bado?
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code