Takwimu za Saratani kwa Ujumla:Fahamu kwamba Kila mwaka, inakadiriwa kesi milioni 1.1 za saratani hurekodiwa barani Afrika, huku watu 700,000 wakipoteza maisha kwa ugonjwa huo, kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO).
Lakini kulingana na WHO, "mwili hudhibiti maambukizi ya saratani kwa asilimia 90 ya watu na kuzuia maambukizi ya virusi vya magonjwa ya zinaa (Human papilloma virus HPV), lakini aina hatari ya virusi vya HPV, ndio sababu ya saratani ya kizazi na inahusishwa na saratani ya vulva, uke, mdomo/koo, uume na sehemu ya haja kubwa."
Mwaka 2019, HPV ilisababisha kesi 620,000 za saratani kwa wanawake na kesi 70,000 kwa wanaume ulimwenguni. Shirika la WHO la uchunguzi wa saratani duniani, linasema kwa nchini Ghana, saratani ya koo kwa mwaka 2022 ni ya 17 kwa maambukizi kati ya saratani thelathini na mbili. Na kesi mpya 227 zilirekodiwa mwaka huo na maambukizi ya miaka mitano ni 626. Barani Afrika, kesi mpya zilikuwa 10,665 mwaka huo, na maambukizi ya miaka mitano ni 28,077.
Saratani ya Koo ni Nini?
Saratani ya koo ni aina ya saratani ambayo hutokea eneo la koo,na pia huhusisha mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula kuanzia kwenye koo mpaka mwisho tumbo linapoanzia.
Aina za Saratani ya Koo
Kuna aina kuu mbili za saratani ya koo:
-
Squamous cell carcinoma:
- Hutokea katika sehemu ya juu na ya kati ya koo.
- Hutokea sana kwa watu wanaovuta sigara au kunywa pombe kupita kiasi.
-
Adenocarcinoma:
- Hutokea zaidi kwenye sehemu ya chini ya koo, karibu na tumbo.
- Ina uhusiano mkubwa na ugonjwa wa Acid reflux, fetma, na Barrett’s esophagus.
Visababishi vya Saratani ya Koo
- Matumizi ya tumbaku na Uvutaji wa Sigara
- Kunywa pombe kupita kiasi
- Tatizo la Acid Reflux: Kuwa na matatizo ya tumbo ambayo huhusisha acid kurudi kutoka tumboni kupanda juu kwenye koo yaani ACID REFLUX kwa kitaalam.
- Ulaji wa vyakula vya moto sana au vilivyohifadhiwa kwa chumvi nyingi
- Upungufu wa vitamini (hasa vitamini A na zinki)
- Maambukizi ya HPV (Human Papilloma Virus)
- Upungufu wa lishe bora
- Umri mkubwa (zaidi ya miaka 50): Zamani saratani ya koo ilikuwa inawapata sana watu wazima,ila kwa hivi sasa saratani ya koo huwapata hata Vijana wadogo kabsa.
- Unene kupita kiasi
- Kuwa Mwanaume (wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake)
Dalili za Saratani ya Koo
Dalili huweza kuanza taratibu na kuongezeka kadri muda unavyopita:
- Mtu kushindwa kumeza mate au kupata shida ya kumeza kitu
- Maumivu makali wakati wa kumeza kitu au hisia ya kuchoma wakati wa kumeza
- Kikohozi cha mara kwa mara au sauti kubadilika
- Maumivu ya kifua na Mgongo
- Kupungua uzito bila sababu
- Kupatwa na shida ya Sauti kukwaruza
- Kutapika damu au kutoa damu kwenye mate
- Harufu mbaya ya mdomo
- Maumivu ya kifua au nyuma ya kifua
- Uchovu na udhaifu n.k.
Vipimo vya Kuchunguza Saratani ya Koo
- Endoscopy: Kamera ndogo huingizwa kupitia koo ili kuangalia mabadiliko.
- Biopsy: Sampuli ndogo ya tishu huchukuliwa wakati wa endoscopy ili kuchunguzwa kwenye maabara.
- CT Scan au MRI: Kwa kuangalia kusambaa kwa saratani.
- PET Scan: Huonyesha saratani katika mwili mzima.
- Barium swallow X-ray: Husaidia kuona koo wakati wa kumeza.
Matibabu ya Saratani ya Koo
Saratani hii hutibika kabsa endapo,itagundulika mapema kabla ya kufika stage mbaya.
Matibabu hutegemea hatua ya ugonjwa na hali ya mgonjwa kwa ujumla:
- Upasuaji (Esophagectomy): Kuondoa sehemu ya koo iliyoathirika.
- Mionzi (Radiotherapy): Kuua seli za saratani kwa kutumia miale.
- Dawa za saratani (Chemotherapy): Kuua au kupunguza ukuaji wa seli za saratani.
- Immunotherapy: Huchochea kinga ya mwili kupambana na saratani.
- Matibabu ya kusaidia: Kwa wagonjwa ambao saratani haiwezi kuondolewa kabisa, husaidia kupunguza maumivu au kuwezesha kumeza.n.k.
Namna ya Kuzuia Saratani ya Koo
- Epuka kuvuta sigara na matumizi ya tumbaku
- Punguza au acha kabisa pombe
- Dhibiti uzito kupita kiasi
- Kula chakula bora chenye matunda na mboga nyingi
- Tibu kwa wakati matatizo kama Acid reflux(GERD) au Barrett's esophagus
- Pima afya mara kwa mara kama uko kwenye hatari
Hitimisho
Saratani ya koo ni ugonjwa hatari lakini waweza kuzuilika au kugundulika mapema. Ikiwa una dalili zozote zilizotajwa, ni muhimu kumwona daktari mapema kwa uchunguzi na tiba. Kinga ni bora kuliko tiba!
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
REPLY HAPA
image quote pre code