Watoto wa kike waamua kufuata nyayo za Baba yao ambaye ni Rubani

Watoto wa kike waamua kufuata nyayo za Baba yao ambaye ni Rubani

#1

Familia ya Nahodha Wale Makinde na binti zake watatu, Mopelola, Oluwaseun, na Oluwafunmilayo, kutoka Nigeria wamefanya mapinduzi ya usafiri wa anga kwa kuvunja vizuizi na kuleta mabadiliko.



Watoto hao wa kike waliamua kufuata nyayo za Baba yao ambaye ni Rubani wa helikopta katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Nigeria (NCAA).

Mopelola, binti mkubwa zaidi, alifuata ndoto za Baba yake na kuwa Rubani stadi wa helikopta, akionyesha nguvu ya kufanya kazi kwa bidii na uvumilivu. 

Oluwaseun, binti wa kati, pia alikwenda angani kupaisha Helikopta akithibitisha kuwa wanawake wanaweza kufaulu katika nyanja ambayo uwepo wao mara nyingi hutiliwa shaka.

Oluwafunmilayo, mdogo kabisa, alichagua njia tofauti katika urubani kama rubani wa ndege za kawaida (Fixed wing) na kuthibitisha kuwa kuna njia nyingi za kuacha alama katika sekta hiyo.

Hadithi ya familia ya Makinde ni ukumbusho kwamba changamoto ni hatua za kufikia lengo na kwamba uvumilivu na dhamira ni ufunguo wa mafanikio.

REPLY HAPA


image quote pre code