Showing posts with label Jukwaa la teknolojia. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la teknolojia. Show all posts

Teknolojia mpya ya “nyumba zinazoelea” Afyaclass Forum •

Kampuni ya Air Danshin Systems nchini Japan imebuni teknolojia mpya ya “nyumba zinazoelea” inayolenga kulinda makazi dhidi ya athari za tetemeko la ardhi.

Teknolojia hiyo hufanya kazi kwa kutumia vihisi (sensors) vinapogundua mtikisiko wa ardhi. Mara moja, mifuko maalum ya hewa iliyobanwa hujaa na kuinua nyumba kwa sentimita chache kutoka ardhini. Hatua hii husaidia kupunguza mtikisiko mkali unaoweza kusababisha uharibifu mkubwa.

Baada ya tetemeko kupungua na ardhi kutulia, nyumba hurudi chini taratibu kwenye msingi wake bila madhara.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, mfumo huu umefanya kazi vizuri katika matetemeko madogo, na kwa sasa unaendelea kuboreshwa ili uweze kulinda nyumba hata wakati wa matetemeko makubwa zaidi.

Ubunifu huu unaonekana kuwa hatua muhimu katika kupunguza athari za majanga ya asili nchini Japan, ambayo ni moja ya nchi zinazokumbwa mara kwa mara na matetemeko ya ardhi.

0 Comment

Jilinde kwa kufanya haya Kwenye Simu Yako ya AndroidAfyaclass Forum •

Katika ulimwengu wa sasa ambao teknolojia imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku, simu za Android zimebeba taarifa nyingi muhimu kuanzia namba za benki, majina ya watu wa karibu, nywila, picha binafsi, hadi mawasiliano ya kikazi. Hata hivyo, pamoja na urahisi huu, zipo pia hatari nyingi kama udukuzi, wizi wa taarifa, na matumizi mabaya ya data yanayoweza kumkumba mtumiaji wa simu bila kutegemea.

Ndiyo maana ni muhimu kuhakikisha kuwa simu yako ina setingi sahihi za usalama, ambazo sio tu zinakuweka salama, bali zinakusaidia kurejesha au kufuta taarifa zako iwapo simu itapotea. Makala hii inakuelekeza hatua kwa hatua setingi muhimu unazopaswa kuhakikisha ziko sawa kwenye Android yako.

1. Weka Screen Lock Imara

Screen lock ndiyo ngao ya kwanza ya ulinzi wa simu yako. Inajumuisha PIN, password au pattern. Cha msingi ni kuhakikisha unachagua namba au mchoro ambao hauwezi kubashirika kirahisi.

• Epuka: 1234, 0000, tarehe ya kuzaliwa

• Tumia: Mchanganyiko mgumu wa namba au herufi

Jinsi ya kuweka: Settings → Security → Screen Lock

Kwa kuongeza usalama, tumia pia fingerprint au face unlock, ambavyo vinazuia watu wasiokuwa na ruhusa kufungua simu yako kwa urahisi.

2. Washa Find My Device

Hii ni moja ya huduma muhimu zaidi kwenye Android. Inakusaidia:

  • Kuona simu yako ilipo
  • Kuilia kama imepotea
  • Kui-lock ili mtu asiitumie
  • Kufuta kila kitu iwapo huwezi kuipata tena

Ni ulinzi wa uhakika kwa mtu yeyote anayehifadhi taarifa nyeti kwenye simu.

Jinsi ya kuiwasha: Settings → Security → Find My Device → ON

3. Zima “Install Unknown Apps”

Moja ya njia kubwa zinazotumiwa na wadukuzi ni kukufanya usakinishe programu zisizo rasmi ambazo zina virusi. Android ina sehemu ya kuzima kabisa ruhusa ya apps zisizotoka Play Store.

Jinsi ya kufanya:

Settings → Security → Install Unknown Apps → OFF

Kwa kutumia hii, simu yako itakataa kusakinisha programu yoyote isiyo salama.

4. Kagua Ruhusa za Apps (App Permissions)

Kila programu inayoingia kwenye simu inaomba ruhusa fulani. Lakini si lazima kila app iwe na ruhusa zote. Kwa mfano:

Kwa nini app ya torchi ipate ruhusa ya camera?

Kwa nini app ya mchezo (game) ipate ruhusa ya location?

Hizi ni ishara za hatari.

Lichunguze: Settings → Apps → Permissions

Ondoa ruhusa zisizokuwa na uhusiano wa moja kwa moja na kazi ya app.

5. Sasisha Simu na Apps Mara kwa Mara (Updates)

Android inatoa updates kwa ajili ya kuongeza usalama na kuzuia udhaifu unaoweza kutumiwa na wadukuzi. Usipuuze updates.

• Updates Android OS

•Updates Apps kupitia Play Store

• Washa Auto-update

Updates ni kama kinga ya mwili zinakufanya uwe salama kila siku.

6. Linda Notification Zako Kwenye Lock Screen

Watu wengi hawajui kuwa taarifa zinazoonekana kwenye lock screen zinaweza kuibiwa na mtu anayepita karibu. Mfano:

  • Meseji za benki
  • Codes
  • Ujumbe binafsi
  • Barua pepe za kazini

Unaweza kuzificha au kuzuia zionekane kabisa.

Njia: Settings → Notifications → Lock Screen Notifications → Hide Sensitive Content

7. Weka Two-Factor Authentication (2FA)

Hata kama mtu atajua password zako, 2FA humzuia kuingia kwenye akaunti zako bila kuthibitisha kwa msimbo wa ziada.

Hii ni muhimu kwa:

  • Google account
  • WhatsApp
  • Instagram
  • Facebook

Ikiwezekana, tumia Google Authenticator kwa usalama zaidi.

8. Backup ya Data Muhimu

Hakikisha taarifa zako hazipotei hata kama simu yako ikipotea au ikiharibika. Backup hukusaidia kurejesha vitu kama:

  • Picha
  • Namba za simu
  • Faili muhimu
  • Apps

Njia: Settings → Google → Backup → ON

9. Usitumie Public Wi-Fi Kuingia Kwenye Akaunti Nyeti

Public Wi-Fi mara nyingi haijaimarishwa kiusalama na inaweza kukuweka kwenye hatari ya wizi wa taarifa. Ikiwezekana:

Tumia data ya simu

Au tumia Wi-Fi yenye password inayojulikana

Hii ni hatua muhimu sana kwa watu wanaotumia simu kufanya kazi za benki au malipo mtandaoni.

10. Ondoa Apps Usizotumia

Kadri unapokuwa na apps nyingi, ndivyo unavyoongeza hatari ya usalama. Baadhi zinaweza kufuatilia mtu au kuwa na virusi.

Chukua dakika tano tu:

Settings → Apps → Uninstall

Futa programu ambazo hutumii tena.

Hitimisho

Usalama wa simu yako ya Android ni jukumu lako, na jambo la faraja ni kwamba hatua nyingi za kujilinda ni rahisi na za haraka kuweka. Kwa kuhakikisha setingi sahihi ziko mahali, unajilinda dhidi ya:

✔ Wizi wa taarifa

✔ Udukuzi

✔ Kupoteza data

✔ Kufunguliwa simu bila ruhusa

✔ Uharibifu wa akaunti zako mtandaoni

Android imejengwa kwa mfumo thabiti wa usalama lazima tu mtumiaji aweke setingi sahihi.

0 Comment

Elon Musk na Ujio wa XChat mfumo mpya wa mawasilianoAfyaclass Forum •

Elon Musk, mmiliki wa jukwaa la X (zamani Twitter), ametambulisha rasmi XChat, mfumo mpya wa mawasiliano ulioundwa kuboresha faragha, kasi na uhuru wa mazungumzo ya kidijitali.

XChat imejengwa kwa teknolojia ya kisasa, ikiwa na usanifu wa lugha ya Rust, na kutumia mbinu za usalama zinazofanana na zile za Bitcoin, kwa lengo la kuimarisha faragha na kuzuia udukuzi wa taarifa za watumiaji.

Huduma Kuu za XChat

Usalama wa End-to-End Encryption: Ujumbe unasomwa tu na mtumaji na mpokeaji.

Ujumbe Unaofutika (Disappearing Messages): Ujumbe huondolewa baada ya muda maalumu.

Simu za Sauti na Video: Bila kuhitaji namba ya simu.

Kutuma Mafaili Bila Mipaka: Rahisi kwa watumiaji kushiriki taarifa kubwa.

Tofauti na majukwaa mengine ya mawasiliano, XChat inalenga kuwapa watumiaji uhuru zaidi, udhibiti kamili wa data zao, na faragha ya hali ya juu, hasa kwa wale wanaopendelea mawasiliano bila kuunganishwa na namba ya simu.

Wataalamu wa teknolojia wanaona XChat kama zaidi ya app ya kawaida ya chat, bali sehemu ya mkakati mpana wa Elon Musk wa kuifanya X kuwa “everything app” jukwaa linalojumuisha mawasiliano, biashara, na huduma mbalimbali za kidijitali.

Hata hivyo, wachambuzi wamesema bado kuna haja ya uhakiki zaidi wa kiufundi ili kuthibitisha kiwango kamili cha usalama, hasa katika masuala ya data na metadata.

Kwa sasa, XChat inaendelea kutolewa kwa awamu kwa watumiaji wa jukwaa la X, huku ikitarajiwa kupanuka zaidi siku zijazo.

0 Comment

Gharama za Smartphone kuongezeka zaidi 2026,Kisa AIAfyaclass Forum •

Dunia inaenda kushuhudia ongezeko maradufu la mauzo ya simu janja kuanzia mwaka 2026 tofauti na ilivyo kawaida, na hii ni kwa sababu ya ongezeko la gharama ya uzalishaji wa chipset zinazoendesha simu janja. 

Mabadiliko ya teknolojia ya leo yanayotegemea uendeshaji wa mifumo ya AI, unahitaji chip zenye uwezo wa kufikiri na kuchakata data kwa kasi ya juu. 

Taarifa ya jarida la BUSINESS WORLD inaeleza kuwa dunia inaelekea zama mpya za “super smartphones,” ambazo zitakua na uwezo mkubwa maradufu zaidi tofauti za simu janja za zamani, na mabadiliko haya yanahitaji uwekezaji kwenye chipset zinazoendesha simu janja zote duniani.

Kampuni kubwa za utengenezaji chipset duniani zimeanza kuuza chipset hizi kwa bei ya ongezeko la 10% jambo litakalowalazimu kampuni za simu duniani kupandisha gharama za mauzo ya simu ili kumudu gharama mpya za utengenezaji wa simu janja zao.

Umejipangaje kununua simu janja mpya mwaka 2026?

0 Comment

Samsung Yaipita Iphone kama kampuni Bora ya Simu DunianiAfyaclass Forum •

Samsung Yaipita Iphone kama kampuni Bora ya Simu Duniani

Ingawa watu wengi wanabishana kuhusu Ubora, na muundo wa simu hasa kamera kati ya kampuni hizi mbili, lakini imeripotiwa Samsung imeuza simu nyingi zaidi kuliko simu za Iphone za kampuni ya Apple

Katika matoleo ya hivi majuzi Samsung iliuza karibu simu Milioni 62 huku Apple ikiuza zaidi ya Simu Milioni 60, Pengo hilo Limetafsiriwa katika takriban asilimia 21 ya uuzaji wa kimataifa wa Samsung dhidi ya asilimia 17 kwa Apple.


Ni ipi kampuni yako bora hapa ??😂

________________________________

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD