Watu nane(8) wafariki kwa kupigwa risasi nchini Austria
Takribani watu 8 wamefariki dunia katika tukio la ufyatuaji risasi lililofanyika katika shule moja huko Graz, Austria, Jumanne.
Mshukiwa wa tukio hilo amefariki dunia pia, kulingana na meya wa mji huo.
Meya Elke Kahr, ameelezea tukio hilo kama "mkasa mbaya" kulingana na shirika la habari la Austria. Shirika hilo la habari limeongeza kuwa waliofariki ni wanafunzi 7 na mtu mzima mmoja.
Kahr amesema watu wengi wamekimbizwa hospitali kutokana na majeraha. Polisi inasema inaamini kwamba aliyefanya tukio hilo alikuwa pekeyake.
Maafisa maalum wa polisi ni miongoni mwa walioitwa katika shule hiyo ya BORG Dreierschützengasse, iliyoko karibu kilomita moja kutoka kituo cha kihistoria cha Graz.
Graz ni mji wa pili mkubwa nchini Austria na uko kusini mashariki mwa nchi hiyo ukiwa na takriban wakaazi 300,000.
REPLY HAPA
image quote pre code