Ajira 2,460 reli Dar – Makutopora kutolewa na TRC
DAR ES SALAAM: Ajira 2,460 zinatarajiwa kutolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC), katika utekelezaji wa mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kwa vipande viwili vya Kutoka Dar es Salaam mpaka Makutopora.
Hayo yamebainishwa wakati wa ziara ya siku mbili ya Bodi ya Wakurugenzi TRC, kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa SGR na MGR, kati ya Kigoma – Tabora na Tabora Mwanza iliyoanza Agosti 19, 2025.
Katika ajira hizo 2,460 utekekezaji wake ni awamu, ambapo katika mwaka wa fedha 2024/25 zaidi ya watumishi 500 wameshaajiriwa na mwaka huu wa fedha 2025/26 marajio ni kuajiri watumishi 272 na TRC itaendelea kuajiri kufikia watumishi 2,460.
Wakati utekekezaji wa utoaji ajira rasmi za Shirika ukiendelea, jumla ya ajira 115,000 kutoka mkandarasi zimeshawanufaisha Watanzania 115,000 zikiwemo za vijana wa elimu ya darasa la saba na viwango vingine vya elimu katika fani mbalimbali.
Mchanganuo wa ajira hizo 115,000 kutoka kwa mkandarasi, ni kwamba ajira 35,000 ni za moja kwa moja na zaidi ya 80,000 ni zisizo za moja kwa moja zikijumuisha makundi mbalimbali kama baba na mama lishe, bodaboda, bajaji na watoa huduma za makampuni mbalimbali ya mawasiliano kama mocha, line za simu nk
image quote pre code