Kuvimba kwa Uume wa Mtoto kwa Mbele sababu ni ipi?Afyaclass Forum •

Kuvimba kwa Uume wa Mtoto kwa Mbele sababu ni ipi?

Kuvimba kwa ngozi ya mbele ya uume (govi) kwa mtoto mara nyingi husababishwa na mambo haya:

1. Maambukizi (Balanitis au Balanoposthitis)

Hii ni kuvimba kwa kichwa cha uume na govi kunakosababishwa na maambukizi ya:

  • Bakteria
  • au Fangasi (kama Candida)

Dalili zake:
  • Uume kuwa mwekundu na kuvimba
  • Maumivu au mtoto kulia wakati wa kukojoa
  • Wakati mwingine usaha au harufu mbaya kutokea eneo hili

2. Kujikusanya kwa uchafu chini ya govi

Kwa watoto wadogo govi huwa halijafunguka kabisa (hali ya kawaida). Uchafu au mkojo ukibaki ndani unaweza kusababisha uvimbe.

3. Kuumia au msuguano

Inaweza kutokana na:

  • Diaper alizovaa kubana sana
  • Kuguswa au msuguano sana wakati wa kuoshwa n.k.

4. Hali inayoitwa Phimosis

Kwa watoto wadogo govi huwa halivutiki nyuma kabisa. Wakati mwingine linaweza kuvimba kidogo hasa likijaa mkojo kabla ya kutoka.

Mambo ya kufanya nyumbani:

  • Osha uume kwa maji safi ya uvuguvugu
  • Badilisha diaper mara kwa mara
  • Usivute govi kwa nguvu (kwa mtoto mdogo ni kawaida lisivutike)

Mwone daktari haraka kama:

  • Uvimbe ni mkubwa sana
  • Kuna usaha au harufu kali
  • Mtoto analia sana wakati wa kukojoa
  • Hatoi mkojo vizuri
  • Homa ipo

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Ndizi 1 tu husaidia kupunguza na kuondoa Maumivu wakati wa HedhiAfyaclass Forum •

Kwa Mwanamke anayepata maumivu makali wakati wa hedhi anaelewa jinsi maumivu hayo yanavyokuwa. Sasa hapa kuna kitu rahisi ambacho kinaweza kusaidia kidogo - ndizi.

Ndizi zina magnesiamu na vitamini B6, ambazo zote zina jukumu la kulegeza misuli na kupunguza Mkazo. Maumivu ya hedhi hutokea kwa sababu uterasi yako inasisimka na kubana zaidi(Contracts) ili kutoa utando wake. Magnesiamu husaidia kulegeza misuli laini, ambayo inaweza kupunguza nguvu ya mikazo hiyo. Utafiti fulani pia unaonyesha kwamba viwango vya kutosha vya magnesiamu vinaweza kupunguza prostaglandini -ambayo husababisha maumivu yanayoambatana na mikazo.

Hivi ndivyo ndizi inavyoweza kukusaidia wakati wa hedhi:

• Magnesiamu ndani yake husaidia kulegeza misuli ya uterasi

• Vitamini B6 inaweza kupunguza uvimbe,Mkazo na mabadiliko ya hisia

• Sukari asilia hutoa nishati ya haraka ikiwa unahisi dhaifu sana mwilini

• Potasiamu husaidia kuzuia maumivu ya misuli na uchovu

Ndizi moja haitaondoa kabsa maumivu makali, lakini inaweza kuwa msaada wa kupunguza maumivu na wa asili kama sehemu ya lishe bora kwa ujumla.

 Kwa matokeo bora, changanya na:

• Kunywa maji Vizuri,Uji au maziwa,Tangawizi,Maji ya uvuguvugu n.k.

• Kufanya mazoezi mapesi kama kujinyoosha au kutembea

• Kutumia Warm compress kwenye tumbo la chini

• Kulala vya kutosha n.k.

Kumbuka: Ikiwa maumivu yako ya hedhi ni makali, Hali inazidi kuwa mbaya, au yanaathiri maisha yako ya kila siku, ni muhimu kushauriana na mtaalamu wa afya. Hali kama vile endometriosis au PCOS zinahitaji mwongozo sahihi wa kimatibabu. Na Kwa ushauri zaidi unaweza kutuma Neno Afyaclass Inbox.

0 Comment

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni) Afyaclass Forum •

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni)

Kuhisi kitu kukwama kooni (kama kuna kitu kimekwama au kimekaza kooni) mara nyingi huitwa kwa kitaalamu Globus Sensation. Hali hii inaweza kutokea hata kama hakuna kitu halisi kilichokwama.

Sababu zinazoweza kusababisha

  1. Misuli ya koo kukaza–  kwa Sababu mbali mbali ikiwemo Msongo wa mawazo,au wasi wasi n.k
  2. Asidi kupanda kutoka tumboni – hali iitwayo kitaalam Acid Reflux  inaweza kufanya koo lihisi kama kuna kitu.
  3. Maambukizi ya koo – kama yale ambayo husababisha tonsils kuvimba.
  4. Uvimbe wa tezi ya koo
  5. Mate kuwa machache au koo kukauka.
  6. Kuna chakula au kitu kimekwama kweli (hasa kama ulimeza kitu kigumu kama mfupa).

Dalili zinazoambatana na hali hii

  • Kuhisi kama kuna donge kooni
  • Ugumu kidogo wa kumeza
  • Kukohoa mara kwa mara
  • Koo kukauka au kuwaka moto,kuwasha n.k

Ufanye nini kwa haraka

  • Kunywa maji ya uvuguvugu polepole.
  • Jaribu kumeza chakula laini kama uji au ndizi.
  • Epuka vyakula vyenye pilipili nyingi, kahawa na soda kama asidi inahusika.
  • Punguza stress.

Nenda hospitali haraka kama:

  • Unashindwa kumeza kabisa
  • Kuna maumivu makali kooni
  • Unapumua kwa shida
  • Dalili zinaendelea zaidi ya wiki 2
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
0 Comment

Ugonjwa Wa Macho Kuwasha Chanzo Na TibaAfyaclass Forum •

Ugonjwa Wa Macho Kuwasha Chanzo Na Tiba

Tatizo la macho kuwasha ni tatizo ambalo huwapata watu wengi na kuleta kero kubwa kama vile kupikicha macho kila dakika, macho kutoa machozi yenyewe N.K

Chanzo Cha Tatizo La Kuwashwa Macho

Zipo sababu mbali mbali ambazo huweza kuchangia mtu kuwashwa macho,na miongoni mwa sababu hizo ni kama vile;

- Kuwa na allegy ya baadhi ya vitu kama vile, Maji ya kisima,maji ya mvua, Sabuni,mafuta,Moshi N.K

- Tatizo la Macho kuwa makavu(Dry Eye Syndrome): Tatizo hili hupelekea macho kukosa Ulainishi wa kutosha hivo hali ya kuwasha hutokea.

- Dalili za macho kushambuliwa na baadhi ya magonjwa  mbali mbali ya macho

- Macho kuingiwa na dawa,perfume,Moshi au kitu chochote chenye baadhi ya  kemikali

- Hali ya Vidonda,Michubuko au Vipele ndani ya Jicho

- Baadhi ya watu huwashwa sana na macho baada ya kuingiwa na Vitu kama vitunguu, hali ambayo huweza kukaa kwa muda kidogo kabla ya kuisha yenyewe

- Jicho kuingiwa na vitu kama mchanga, pilipili N.K

Dalili Za Tatizo La Kuwashwa Macho

- Kuhisi hali ya kuchoma ndani ya jicho

- Macho au jicho kubadilika rangi na kuwa jekundu

- Macho kutoa matongo tongo yenyewe

- Macho kuanza kutoa machozi yenyewe

- Macho kuwasha

MADHARA YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO

- Macho kubadilika rangi na kuwa mekundu

- Huathiri uwezo wa uono wa macho yako

- Macho kuvimba

- Macho kutoa matongo tongo yenyewe

- Macho kutoa machozi yenyewe

- Kero ya kupikicha na kukuna macho kila dakika

MATIBABU YA TATIZO LA KUWASHWA MACHO

- Tiba hutegemea chanzo cha tatizo hili, lakini kwa upande wa dawa zipo dawa mbali mbali ambazo huweza kutumika kutibu tatizo hili kabsa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD