Dalili za mimba ni zipi? Hebu nielewesheni wadau,mana sielewi, Je ni Period kuacha kutoka? au ni zipi?

...See more

3 Comments

  1. Ndyo Period kuacha kutoka Ipo pia

    ReplyDelete
  2. Hizi hapa ni baadhi ya dalili za Mwanamke mjamzito au mwanamke mwenye mimba;

    1. Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi(Kumiss period)

    2. Mwanamke kutema mate sana mara kwa mara

    3. Matiti kuuma pamoja na kujaa

    4. Kuhisi hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara

    5. Kukojoa mara kwa mara

    6. kupata uchovu wa mwili kupita kiasi

    7. Mapigo ya moyo kwenda mbio

    8. Kuwa mtu wa kukasirika mara kwa mara kwa baadhi ya Wanawake

    9. Tumbo kujaa mithili ya kuwa na Gesi

    10. Tumbo kukaza na kuvuta

    11. Kupata vidamu vidamu kidogo yaani Light spot, na hii hutokea wakati mtoto anajishikiza kwenye mji wa uzazi

    12. Kuanza kupata choo kigumu mara kwa mara yaani constipation

    13. Kuvimba pua, hii hutokana na mabadiliko ya vichocheo pamoja na mzunguko wa damu hali ambayo hupelekea kuvimba kwa Mucous membrane puani

    14. Kubadilika ngozi ya mwili hasa maeneo ya usoni, na kuwa na vitu vyeupe tofauti na rangi ya kawaida ya ngozi

    15. Kuanza kupata kiungulia mara kwa mara

    16. Kukosa usingizi

    17. Kubadilika mfumo wa kula, na kuanza kupenda baadhi ya vyakula na kuchukia baadhi ya vyakula

    18. Kuanza kupenda harufu za vitu flani na kuanza kuchukia harufu za baadhi ya vitu

    19. Kupenda kula mara kwa mara

    20. Kutapika mara kwa mara baada ya kula chakula n.k.....

    ReplyDelete

Post a Comment

Related Discussions...