HomeAfyaclass Social Ask Dalili za mimba ni zipi? Afyaclass Bongo Social -May 22, 2026 3 Comments Dalili za mimba ni zipi? Hebu nielewesheni wadau,mana sielewi, Je ni Period kuacha kutoka? au ni zipi? ...See more 0 0 3
Ndyo Period kuacha kutoka Ipo pia
ReplyDeleteHizi hapa ni baadhi ya dalili za Mwanamke mjamzito au mwanamke mwenye mimba;
ReplyDelete1. Mwanamke kutokuona siku zake za hedhi(Kumiss period)
2. Mwanamke kutema mate sana mara kwa mara
3. Matiti kuuma pamoja na kujaa
4. Kuhisi hali ya kichefuchefu na kutapika mara kwa mara
5. Kukojoa mara kwa mara
6. kupata uchovu wa mwili kupita kiasi
7. Mapigo ya moyo kwenda mbio
8. Kuwa mtu wa kukasirika mara kwa mara kwa baadhi ya Wanawake
9. Tumbo kujaa mithili ya kuwa na Gesi
10. Tumbo kukaza na kuvuta
11. Kupata vidamu vidamu kidogo yaani Light spot, na hii hutokea wakati mtoto anajishikiza kwenye mji wa uzazi
12. Kuanza kupata choo kigumu mara kwa mara yaani constipation
13. Kuvimba pua, hii hutokana na mabadiliko ya vichocheo pamoja na mzunguko wa damu hali ambayo hupelekea kuvimba kwa Mucous membrane puani
14. Kubadilika ngozi ya mwili hasa maeneo ya usoni, na kuwa na vitu vyeupe tofauti na rangi ya kawaida ya ngozi
15. Kuanza kupata kiungulia mara kwa mara
16. Kukosa usingizi
17. Kubadilika mfumo wa kula, na kuanza kupenda baadhi ya vyakula na kuchukia baadhi ya vyakula
18. Kuanza kupenda harufu za vitu flani na kuanza kuchukia harufu za baadhi ya vitu
19. Kupenda kula mara kwa mara
20. Kutapika mara kwa mara baada ya kula chakula n.k.....
Asante sana Dr
DeletePost a Comment
Related Discussions...