Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amesema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesajili na kutambua Watu 1,145,334 wenye umri wa miaka 18 na kuendelea katika kipindi cha Julai 2025 hadi Aprili 2026.

Katambi amesema idadi hiyo imeongezeka ikilinganishwa na Watu 844,994 waliosajiliwa katika kipindi kama hicho mwaka 2024/25.

Akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo leo Mei 25, 2026, Katambi amesema NIDA imeendelea kufanya usajili na utambuzi wa Watu Nchini wakiwemo raia wa Tanzania, Wageni Wakaazi, Walowezi pamoja na Wakimbizi.

Amesema hadi sasa jumla ya Watu 27,186,421 wameshasajiliwa na kutambuliwa sawa na asilimia 86.4 ya lengo la kusajili Watu 31,477,938 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Katika hatua nyingine Katambi amesema NIDA imeendelea kupanua huduma zake kwa Watanzania wanaoishi Nje ya Nchi ambapo Watu 156 wamesajiliwa katika Balozi za Tanzania zilizopo Canada, Marekani, Uingereza na Umoja wa Falme za Kiarabu katika kipindi hicho.

Amesema tangu mwaka 2023 jumla ya Watanzania 1,465 wanaoishi Nje ya Nchi wamepatiwa huduma ya usajili na utambuzi kupitia Balozi mbalimbali. Via#MillardAyoUPDATES

...See more

WEKA COMMENT YAKO HAPA(MAONI)KUHUSU MADA HII

Related Discussions...