Mtoto kuwa na macho ya njano,Shida ni nini?
Mtoto kuwa na macho ya njano mara nyingi huwa ni dalili ya hali inayoitwa Jaundice, inayojulikana pia kama “manjano”. Hali hii hutokea pale mwili unapokuwa na kiwango kikubwa cha bilirin (bilirubin) kwenye damu. Bilirubin ni rangi ya njano inayozalishwa wakati chembechembe nyekundu za damu zinapovunjwa mwilini. Ini likishindwa kuondoa bilirubin vizuri, macho na ngozi huanza kuwa ya njano.
Kwa watoto wachanga, manjano ni hali ya kawaida sana katika siku za kwanza baada ya kuzaliwa, hasa kwa watoto waliozaliwa kabla ya muda au wenye ini ambalo bado halijakomaa vizuri. Madaktari wa wanaeleza kuwa hali hii mara nyingi huisha yenyewe ndani ya wiki chache bila madhara makubwa.
Dalili kuu ni:
- Macho kuwa ya njano
- Ngozi kuwa ya njano
- Mtoto kuchoka sana au kulala kupita kiasi
- Kushindwa kunyonya vizuri
- Mkojo kuwa wa rangi ya njano iliyokolea
- Kinyesi kuwa cheupe au cha rangi isiyo ya kawaida
Kwa watoto wakubwa au watu wazima, macho ya njano yanaweza kuashiria matatizo makubwa zaidi kama:
- Magonjwa ya ini
- Maambukizi ya homa ya ini
- Kuziba kwa njia za nyongo
- Kuvunjika kwa chembechembe nyekundu za damu kwa kasi
- Matatizo ya kongosho au nyongo
Madaktari hupima kiwango cha bilirubin kwa kutumia vipimo vya damu ili kujua ukubwa wa tatizo na matibabu yanayohitajika.
Kwa watoto wachanga wenye manjano kali, matibabu yanaweza kujumuisha mwanga maalum wa hospitali unaoitwa phototherapy, ambao husaidia kupunguza bilirubin mwilini.
Ni muhimu mzazi kumpeleka mtoto hospitali haraka ikiwa:
- Njano inaongezeka haraka
- Mtoto hashiki ziwa vizuri
- Ana homa
- Analia sana kwa sauti kali
- Analala kupita kiasi au kuonekana dhaifu

.jpeg)



Post a Comment
Related Discussions...