Tinubu Akiri Ugumu wa Maisha Nigeria, Asema Naye Amepungua Uzito

Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, amesema kuwa mageuzi ya kiuchumi yaliyofanywa na serikali yake tangu alipoingia madarakani Mei 2023 yameleta changamoto kubwa kwa wananchi pamoja naye binafsi.

Akizungumza mjini Abuja baada ya kushinda uchaguzi wa mchujo wa urais wa chama cha APC, Tinubu alisema amekuwa akihisi presha kubwa kutokana na juhudi za kuimarisha uchumi wa nchi hiyo.

Rais huyo alikiri kuwa hali ya maisha imekuwa ngumu kwa wananchi wengi wa Nigeria, huku akisema hata yeye mwenyewe amepoteza usingizi na uzito kutokana na majukumu ya kuiongoza nchi katika kipindi hiki cha mpito wa kiuchumi.

“Nafahamu nini kinahitajika kuibadilisha nchi hii tuliyoikuta katika hali mbaya. Kama umepoteza usingizi, nami pia nimepoteza. Kama umepungua uzito, nami pia nimepungua. Lakini huwa nakumbuka jambo moja, mwaka 2022 niliomba kazi hii. Mlinisapoti na nikaipata, hivyo lazima niifanye,” alisema Tinubu.

Katika uchaguzi huo wa mchujo wa chama tawala cha APC, Tinubu alipata kura 10,999,162 dhidi ya mpinzani wake pekee, Stanley Osifo, aliyepata kura 16,503.

Uchaguzi huo ulifanyika katika maeneo yote 774 ya serikali za mitaa pamoja na kata 8,809 nchini Nigeria.

...See more

WEKA COMMENT YAKO HAPA(MAONI)KUHUSU MADA HII

Related Discussions...