Head

Mkuu wa WHO Atembelea Uganda Kupambana na Ebola

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Tedros Adhanom Ghebreyesus, yuko nchini Uganda kufuatilia juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola ambao umeanza kuenea kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa WHO, Uganda imefanikiwa kuchukua hatua za haraka za kukabiliana na ugonjwa huo hatari, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uchunguzi wa mipakani, upimaji wa haraka na ufuatiliaji wa watu wanaoweza kuwa wameambukizwa.

Tedros amesema kuwa mfumo wa afya wa Uganda unaendelea kufanya kazi kwa ufanisi katika kudhibiti maambukizi mapya, hasa baada ya kugundua baadhi ya visa kwa watu waliowasili kutoka maeneo yaliyoathirika nchini Kongo.

Pia,Hali nchini Kongo bado ni ya wasiwasi mkubwa baada ya maambukizi ya Ebola kuongezeka na kuvuka zaidi ya visa 500, huku pia vifo vikiendelea kuripotiwa. Mamlaka za afya zinasema zinaendelea na operesheni za dharura ili kudhibiti maambukizi na kuzuia ugonjwa huo kuenea zaidi.

Mashirika ya kimataifa yameongeza msaada wa kibinadamu, ikiwa ni pamoja na dawa, vifaa vya kinga na msaada wa kifedha kusaidia nchi zilizoathirika kukabiliana na mlipuko huo.

#Reply

#5Replies