Ugonjwa wa PCOS (Polycystic Ovary Syndrome): Chanzo, Dalili na Madhara

PCOS (Polycystic Ovary Syndrome) ni ugonjwa unaoathiri mfumo wa homoni kwa wanawake walio katika umri wa uzazi. Ni moja ya sababu kuu za matatizo ya hedhi, ugumba na mabadiliko ya homoni kwa wanawake duniani. Takribani wanawake milioni 170 duniani wanaishi na PCOS, kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO).

Tatizo hili hujulikana kama PCOS (Polycystic Ovary Syndrome) na Sasa hivi pia hujulikana kama polyendocrine metabolic ovarian syndrome (PMOS)

PCOS Husababishwa na Nini?

Chanzo halisi cha PCOS bado hakijajulikana kikamilifu, lakini wataalamu wanaamini kuwa mambo yafuatayo huchangia:

  1. Kurithi kutoka kwa familia (genetics) – Ikiwa mama au dada yako ana PCOS, uwezekano wa kuipata huongezeka.
  2. Kiwango kikubwa cha homoni za kiume (androgens) – Hali hii huathiri utolewaji wa mayai kutoka kwenye ovari.
  3. Insulin resistance – Mwili hushindwa kutumia insulini vizuri, hali inayoongeza hatari ya kisukari aina ya pili.
  4. Uvimbaji wa muda mrefu mwilini (chronic inflammation) – Unaweza kuchochea uzalishaji wa homoni za kiume.

Dalili za PCOS

Dalili hutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwingine, lakini zinazojitokeza mara nyingi ni:

  • Hedhi zisizo za kawaida au kukosa hedhi kabisa.
  • Kushindwa kupata ujauzito.
  • Kuota nywele nyingi usoni, kifuani au mgongoni,mwanamke kuwa na ndevu.
  • Chunusi sugu.
  • Kupungua au kunyonyoka kwa nywele kichwani.
  • Kuongezeka uzito hasa tumboni.
  • Ngozi kuwa na madoa meusi shingoni, makwapani au sehemu za siri.
  • Uchovu wa mara kwa mara.
  • Mabadiliko ya hisia kama msongo wa mawazo na wasiwasi.

Madhara ya PCOS

Bila matibabu au usimamizi mzuri, PCOS inaweza kusababisha:

  • Ugumba au ugumu wa kupata ujauzito.
  • Kisukari aina ya pili.
  • Shinikizo la damu.
  • Magonjwa ya moyo.
  • Kuongezeka kwa mafuta mabaya mwilini.
  • Saratani ya mfuko wa uzazi (endometrial cancer).
  • Msongo wa mawazo na matatizo ya afya ya akili.

PCOS Hutambuliwaje?

Madaktari hutumia:

  • Historia ya hedhi na dalili.
  • Vipimo vya damu vya homoni.
  • Kipimo cha sukari na mafuta mwilini.
  • Ultrasound kuangalia ovari.

Matibabu ya PCOS

Hakuna tiba ya kuondoa PCOS kabisa, lakini dalili zake zinaweza kudhibitiwa kwa:

  • Kupunguza uzito ikiwa una uzito kupita kiasi.
  • Mazoezi ya mara kwa mara.
  • Lishe bora yenye sukari kidogo.
  • Dawa za kurekebisha hedhi.
  • Dawa za kusaidia kupata ujauzito kwa wanaotaka watoto.
  • Dawa za kudhibiti insulin resistance kama metformin kwa ushauri wa daktari.

Kumbuka;

PCOS ni ugonjwa wa homoni unaoweza kuathiri afya ya uzazi, uzito wa mwili na afya kwa ujumla. Kutambua dalili mapema na kupata ushauri wa daktari kunaweza kusaidia kudhibiti ugonjwa huu na kuboresha ubora wa maisha.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma Zaidi:https://www.afyaclass.com/2021/06/ugonjwa-wa-polycystic-ovary_8.html

Vyanzo vilivyotumika (Links)

WHO: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/polycystic-ovary-syndrome

Mayo Clinic: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/pcos/symptoms-causes/syc-20353439

NHS: https://www.nhs.uk/conditions/polycystic-ovary-syndrome-pcos

CDC: https://www.cdc.gov/pcos

Johns Hopkins Medicine: https://www.hopkinsmedicine.org/health/conditions-and-diseases/polycystic-ovary-syndrome-pcos

Office on Women's Health: https://www.womenshealth.gov/a-z-topics/polycystic-ovary-syndrome

Cleveland Clinic: https://my.clevelandclinic.org/health/diseases/8316-polycystic-ovarian-syndrome-pcos

NIH: https://www.nichd.nih.gov/health/topics/pcos

...See more

Reply

Discussions