Showing posts with label Dawa. Show all posts
Showing posts with label Dawa. Show all posts

Dawa ya gonorrhea,Dawa ya gono,Dawa ya Kutibu Kisonono Afyaclass Forum •

Dawa ya Kutibu Kisonono Kabsa,Wengi Mnaita Gono

Je, ni Ipi dawa sahihi ya kutibu Ugonjwa wa Kisonono(gonorrhea)?

Kisonono ni ugonjwa wa Zinaa ambao husabababishwa na maambukizi ya bacteria wanaojulikana kama Neisseria gonorrhoeae,

Ugonjwa huu wa kisonono ndyo hujulikana kama Gonorrhea au kwa kifupi wengi hupenda kuita “Gono”, Soma Zaidi hapa;

Dalili za Ugonjwa wa Kisonono au Gono

Kwa Wanawake:

1. Kutokwa na Usaha au uchafu usio wa kawaida kwenye uke (unaoweza kuwa na rangi ya njano au kijani).

2. Kupata Maumivu au kuhisi hali ya kuungua wakati wa kukojoa.

3. Kupata Maumivu chini ya tumbo

4. Kutokwa damu katikati ya mzunguko wa hedhi au baada ya tendo la ndoa.

5. Kupata Maumivu kwenye sehemu ya haja kubwa (ikiwa eneo hilo limeathiriwa). n.k

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

- Kutokwa na usaha kwenye Uume

- Uchafu wa majimaji meupe, ya njano, au ya kijani kutoka kwenye uume.

- Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

- Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

- Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

- Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

- Kupata maumivu kwenye korodani.

- Kupata Maumivu au uvimbe katika sehemu ya haja kubwa (ikiwa maambukizi yameathiri eneo hilo).

- Joto la mwili kupanda au kuwa na homa n.k.

Dawa ya Kutibu Kisonono

Dawa za kisonono au Gono huweza kutibu kabsa tatizo hili likaisha ikiwa umepata tiba Sahihi na hujakutana na mazingira hatarishi ya kupata maambukizi haya tena baada ya Tiba.

Ni muhimu sana kupata Maelekezo kamili kutoka kwa Wataalam wa afya Wakati wa Kutumia Dawa za kutibu kisonono kwani badala ya kutibu Kisonono unaweza kusababisha tatizo lingine linalojulikana kama “Usugu wa Dawa” ambapo vimelea hivi vya bacteria hutengeneza usugu kwenye dawa-Antimicrobial resistance”

Kwa hivi Sasa,Ukinzani huu kwenye Ugonjwa wa kisonono unazidi Kuongezeka, Hali ambayo hupelekea dawa ya Kutibu kwa mafanikio Ugonjwa wa Gono au kisonono Kuzidi kuwa Ngumu kuipata.

Hivo ni muhimu sana baada ya kupata dalili za gono au kugundulika una ugonjwa wa Kisonono, hakikisha unapata dawa ya Kisonono ambayo ni sahihi kwa tatizo lako, Usijaribu kila aina ya Dawa.

Hauhitaji Jaribio la kutibu ugonjwa wa Kisonono – ufuatiliaji wa dawa ya Kisonono au matibabu Sahihi ili kuhakikisha kuwa maambukizi yametibiwa kwa ufanisi – Ni muhimu Zaidi.

Ikiwa dalili za mtu zinaendelea kwa zaidi ya siku chache baada ya kupokea matibabu, anapaswa kurudi kwa mtoa huduma wa afya ili kutathminiwa upya,

Kuhusu Kipindi cha Matibabu:

Wagonjwa wanaotibiwa maambukizi ya koo wanashauriwa kufanyiwa kipimo cha uhakiki wa tiba (test of cure) siku 7–14 baada ya matibabu, kwa sababu koo ni eneo gumu zaidi kuponya maambukizi.

Kwa wagonjwa wengine (wasio na maambukizi ya koo), matibabu kwa dozi moja ya sindano mara nyingi hutosha, na hakuna haja ya kipimo cha uhakiki wa tiba isipokuwa dalili zitaendelea au maambukizi yawe sugu.

wanaume na wanawake walio na ugonjwa wa gono au kisonono wanapaswa kupimwa tena miezi mitatu baada ya matibabu ya maambukizi ya awali, bila kujali kama wanaamini kwamba wenzi wao walitibiwa kwa mafanikio.

Dawa ya gono;

Kwa Mujibu wa vituo vya kudhibiti na Kuzuia magonjwa “The Centers for diseases control and Prevention- CDC”

Wanashauri kwenye matibabu ya Ugonjwa wa Kisonono au Gono; dawa ambapo huweza kutumika ni pamoja na;

  • Sindano
  • Na Vidonge

Ingawa dawa hizi Zitazuia maambukizi ya Gono hazitaweza kurudisha madhara yoyote yaliyosababishwa na Ugonjwa huu wa Kisonono au Gono.

NB: Hakikisha unaongea na Wataalam wa afya kwa kina kabla ya kutumia dawa yoyote ya Gono ili kupata maelekzo sahihi kulingana na hali yako.

NA KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Uvida) Unasababishwa na nini?Afyaclass Forum •

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Uvida) Unasababishwa na nini?

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa (UVIDA) unasababishwa hasa na matumizi mabaya au yasiyo sahihi ya dawa za kutibu maambukizi. Sababu kuu ni hizi:

Sababu zinazosababisha UVIDA

1. Kutotumia dawa kwa usahihi

Kuacha dawa kabla ya siku kuisha.

Kunywa dozi ndogo isiyo sahihi.

Kunywa mara chache kuliko ilivyoelekezwa.

2. Matumizi ya dawa bila ushauri wa daktari

Kujitibu bila vipimo.

Kunywa dawa alizotumia mtu mwingine.

3. Matumizi ya dawa yasiyo sahihi kwa ugonjwa husika

Kutumia antibiotiki kutibu magonjwa yasiyotokana na bakteria (k.m. mafua ya virusi).

4. Dawa feki au zenye ubora duni

Haziuui vimelea wote, hivyo waliobaki hujijengea usugu.

5. Matumizi ya dawa kwa wingi katika mifugo na kilimo

Dawa hutumika kuharakisha ukuaji wa mifugo au kuzuia magonjwa bila sababu, kisha usugu huenea kwa binadamu kupitia chakula/mazingira.

6. Maambukizi ya mara kwa mara

Kunywa dawa mara nyingi huongeza nafasi ya vimelea kujifunza “kujilinda” dhidi ya dawa.

Matokeo ya UVIDA

  • Dawa hazifanyi kazi tena.
  • Maambukizi hudumu muda mrefu.
  • Gharama za matibabu huongezeka.
  • Hatari ya kifo huongezeka.

Jinsi ya kuzuia UVIDA

Tumia dawa ulizoandikiwa tu na mtaalamu.

Maliza dozi yote hata ukijisikia vizuri.

Epuka kununua dawa bila vipimo/ushauri.

Epuka kutumia antibiotics ovyo kwa mifugo.

Tumia vipimo kubaini ugonjwa kabla ya dawa.

0 Comment

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Uvida) changamoto hatari ZaidiAfyaclass Forum •

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa (Uvida) changamoto inayofanya maradhi ya kawaida kuwa hatari kubwa inayotishia maisha, kimya kimya.

Kwa mujibu wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (Africa CDC), Uvida hutokea pale dawa zinazotumika kuua vimelea vya ugonjwa zinaposhindwa kufanya kazi kutokana na vimelea kuwa sugu dhidi ya nguvu ya dawa hizo. 

Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa Uvida unasababisha vifo vya moja kwa moja zaidi ya milioni 1.3 duniani huku ikichangia vifo milioni 5 kila mwaka.

Mbali na athari za kiafya, tatizo hili linatishia pia uchumi wa dunia ambapo inakadiriwa kuwa ifikapo mwaka 2030, gharama za tatizo hili kimataifa zinatarajiwa kufikia hadi Dola  za Marekani trilioni 3.4 (sawa na takriban Sh9,860 trilioni).

0 Comment

Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawaAfyaclass Forum •

Tarehe 18 - 24 Novemba: Wiki ya Kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu usugu wa vijiumbemaradhi dhidi ya dawa

Usugu wa dawa za viuavijumbemaradhi (AMR) unatishia uzuiaji thabiti na matibabu ya maambukizi yanayosababishwa na vijidudu mbalimbalimbali. 

Picha: WHO Usugu wa dawa za viuavijumbemaradhi (AMR) unatishia uzuiaji thabiti na matibabu ya maambukizi yanayosababishwa na vijidudu mbalimbalimbali.

Kuanzia jana tarehe 18 inaanza Wiki ya Kimataifa ya Kuelimisha Umma kuhusu Usugu wa Vijiumbemaradhi dhidi ya dawa. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO, linaonya kuwa usugu wa vimelea vya magonjwatayari unatishia mifumo ya afya, uchumi na uhakika wa chakula.

Kwa kaulimbiu “Chukua Hatua Sasa: Linda Leo Yetu, Linda Mustakabali Wetu,” WHO inatoa wito kwa serikali, wahudumu wa afya, wakulima, wadau wa mazingira na umma kuchukua hatua madhubuti kutekeleza ahadi za kisiasa ili kupunguza kuenea kwa maambukizi sugu ya dawa. Wiki hii itaendelea hadi tarehe 24 japokuwa uelimishaji umma kuhusu tatizo hili la usugu wa magonjwa ni jambo endelevu.

Usugu wa vijumbemaradhi, au AMR, hutokea pale bakteria, virusi, fangasi na vimelea wanapobadilika na kutoitikia tena dawa. Wataalamu wa afya wanaonya kuwa hali hii inafanya maambukizi kuwa magumu zaidi kutibu na inaongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa, kusababisha ugonjwa mkali na hata vifo. Kadri viua vijasumu na dawa nyingine zinavyopoteza ufanisi, maambukizi yaliyokuwa rahisi kutibu hapo awali yanaweza kuwa hatari zaidi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) linasema kuwa AMR imekuwa ikiongezeka kwa miongo kadhaa, kwa kiasi kikubwa kutokana na matumizi mabaya au kupindukia ya viua vijasumu kwa binadamu, wanyama na katika kilimo. Kutokana na hilo, mpango wa kimataifa wa kukabiliana na AMR uliidhinishwa na Baraza la Afya Duniani mwaka 2015, ukilenga kuboresha ufuatiliaji, matumizi sahihi ya dawa na kuongeza uelewa wa umma.

Moja ya nguzo kuu za mpango huo ni mawasilianona hapa ndipo wiki hii inapochukua nafasi yake. Kampeni hii ya kila mwaka inalenga kuongeza uelewa kuhusu usugu kwa dawa na kuhamasisha tabia bora miongoni mwa umma, watunga sera na wadau wote wa “One Health,” wakiwemo wahudumu wa afya ya binadamu, afya ya wanyama na mazingira.

Mamlaka za afya zinasisitiza kuwa kupunguza AMR kunahitaji uwajibikaji wa pamoja. Matumizi sahihi ya viua vijasumu, usafi, chanjo na mifumo imara ya afya ni muhimu katika kuzuia maambukizi na kupunguza kasi ya ueneaji wa AMR.

Kadri maadhimisho ya mwaka huu yanavyoendelea, mashirika ya afya duniani yanatoa wito kwa serikali, wataalamu na jamii kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya AMR, yakionya kwamba bila hatua za pamoja, dunia inaweza kuelekea katika enzi mpya ambapo maambukizi rahisi yanaweza tena kuwa hatari na kusababisha vifo.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD