Showing posts with label Jukwaa la Afya. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la Afya. Show all posts

Je,Dalili ya Kwanza ya HIV ni Mafua?Afyaclass Forum •

Watu wengi wanaoambukizwa HIV hupata dalili ndani ya wiki 2–6 baada ya kuambukizwa, lakini sio wote hupata “mafua” au dalili zozote.

Hali zinavyoweza kuwa:

1.Wengine hupata dalili kama za mafua: homa, maumivu ya kichwa, koo kuuma, uchovu, au tezi kuvimba.

2.Wengine hupata dalili tofauti kama: upele wa ngozi, kuharisha, jasho la usiku, au vidonda mdomoni.

3.Wengine hawapati dalili kabisa kwa miezi au hata miaka......!!!!

Soma hapa Zaidi Dalili Zote za Mwanzo za HIV:

https://www.afyaclass.com/2024/09/dalili-za-ukimwi-jinsi-ya-kugundua-na.html?m=1

0 Comment

Hii ni aina ya damu adimu zaidi ulimwenguniAfyaclass Forum •

Ni mtu mmoja tu kati ya watu milioni sita mwenye aina nadra sana ya damu iitwayo Rh null. Sasa watafiti wanajaribu kuizalisha katika maabara, wakitumaini kuwa siku moja itaweza kuokoa maisha.

Utoaji wa damu umeleta mageuzi makubwa katika tiba za kisasa. Iwapo mtu atapata jeraha au kuhitaji upasuaji mkubwa, damu iliyotolewa na wengine huweza kuwa tiba ya kuokoa uhai.

Hata hivyo, si kila mtu anayefaidi na huduma hii muhimu. Watu wenye aina adimu za damu mara nyingi hupata shida kubwa kutafuta damu inayooana na yao.

Miongoni mwa aina adimu zaidi duniani ni Rh null, inayopatikana kwa watu 50 tu wanaojulikana.

Iwapo mtu mwenye aina hii atapata ajali inayohitaji damu, nafasi ya kuipata inayooana na hiyo ni ndogo sana.

Kwa sababu hii, hushauriwa kugandisha damu yao wenyewe kwa matumizi ya baadaye.

Lakini licha ya nadra yake, aina hii pia inathaminiwa sana na wanasayansi.

Katika ulimwengu wa tiba na utafiti, mara nyingi huitwa "damu ya dhahabu" kwa sababu ya matumizi yake ya kipekee.

Inaweza pia kusaidia kufanikisha ndoto ya kuunda damu ya ulimwengu mzima (universal blood) damu inayoweza kutolewa kwa karibu kila mtu bila hatari ya mwitikio wa kinga.

Watu watatu wamesimama wakiwa watoto wachanga waliochorwa ukutani. Mchoro inaonyesha mikono miwili mikubwa, moja nyekundu na moja ya chungwa iliyoshikilia maumbo na aina za damu zimeandikwa "A, B, AB, na O" ndani yake.

Kwa nini aina ya damu hutofautiana

Aina ya damu huamuliwa na uwepo au kutokuwepo kwa alama maalum (antijeni) kwenye uso wa seli nyekundu. Hizi ni protini au sukari zinazotambulika na mfumo wa kinga.

"Ukipokea damu yenye antijeni tofauti na zako, mwili hutengeneza kingamwili kuzishambulia," anaeleza Profesa Ash Toye wa Chuo Kikuu cha Bristol. "Ukipokea tena damu ya aina hiyo, madhara yake yanaweza kuwa hatari."

Mifumo mikuu inayosababisha mwitikio mkubwa wa kinga ni ABO na Rhesus (Rh).

A ina antijeni A

B ina antijeni B

AB ina yote

O haina yoyote

Kila moja inaweza kuwa Rh chanya au hasi.

Watu wa O hasi mara nyingi huonekana kama wachangiaji wa "kila mtu", lakini hili si sahihi kikamilifu.

Kufikia 2024 kulikuwa na zaidi ya makundi 47 ya damu na antijeni 366, hivyo mtu wa O hasi bado anaweza kupata mwitikio wa kinga kutokana na antijeni nyingine.

Zaidi ya hapo, pia kuna zaidi ya antijeni 50 za Rh.

Hivyo, mtu anaposema ni Rh hasi, kwa kawaida huashiria tu antijeni Rh(D), huku nyingine zikiendelea kuwepo.

Pia kuna aina mbalimbali za antijeni za Rh duniani kote, hivyo kufanya iwe vigumu kupata zinazolingana na wafadhili wa kweli, hasa kwa watu kutoka asili za makabila madogo katika nchi fulani.

Mkono wenye glavu umeshikilia slaidi ya glasi yenye matone ya damu yakipimwa, ikionyesha sampuli zenye rangi tofauti na miitikioChanzo cha picha,Getty Images

Maelezo ya picha,Aina ya damu ya Rh null hupatikana katika watu 50 tu wanaojulikana ulimwenguni

Watu wenye Rh null hawana antijeni zote 50 za Rh.

Kwa hiyo hawawezi kupokea aina nyingine ya damu, lakini damu yao inaweza kupewa karibu watu wote wenye aina tofauti za Rh.

Ikiwa mtu ana O Rh null, damu yake huwa ya thamani sana kwa kuwa inaweza kutolewa kwa watu wengi sana, ikiwemo wale wenye aina zote za ABO.

Katika dharura ambapo aina ya damu ya mgonjwa haijulikani, O Rh null inaweza kutolewa kwa hatari ndogo ya mzio.

Hii ndiyo sababu wanasayansi duniani kote wanajaribu kuizalisha maabara.

"Rh [antijeni huchochea] mwitikio mkubwa wa kinga na kwa hivyo ikiwa huna [yao] kabisa basi kimsingi hakuna kitu cha kuguswa nayo katika suala la Rh," asema Prof Toye.

"Kama ungekuwa aina ya O na Rh null basi hilo ni jambo la kawaida kabisa. Lakini bado kuna makundi mengine ya damu ambayo bado unapaswa kuzingatia."

Asili ya aina ya damu ya Rh null

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kuwa Rh null husababishwa na mabadiliko ya jeni yanayoathiri protini muhimu iitwayo RHAG, ambayo husaidia uundaji wa antijeni za Rh.

Mabadiliko hadi kwenye protini hii huvuruga kutengenezwa kwa antijeni nyingine za Rh.

Mwaka 2018, Prof. Toye na timu yake walifanikiwa kuunda damu ya Rh null maabara kwa kutumia teknolojia ya Crispr-Cas9 kufuta jeni za antijeni za makundi matano makuu yanayosababisha kutopatana kwa damu: ABO, Rh, Kell, Duffy na GPB.

"Tulisuluhisha ikiwa tutaondoa tano, basi hiyo ingeunda seli inayolingana kabisa, kwa sababu ilikuwa na vikundi vitano vya damu vilivyo na shida zaidi vilivyoondolewa," anasema Prof Toye.

Kwa kufanya hivyo waliunda seli zilizo sambamba na makundi yote makubwa ya damu, ikiwemo aina adimu kama Rh null na Bombay phenotype, aina nyingine nadra sana inayopatikana kwa mtu mmoja kati ya watu milioni nne.

Watu walio na kundi hili la damu hawawezi kupewa O, A, B au AB damu.

Hata hivyo, matumizi ya uhariri wa jeni bado yamezuiliwa na sheria kali katika nchi nyingi, hivyo huenda ikachukua muda mrefu kabla ya damu hii kupitishwa kwa matumizi ya hospitali.

Juhudi za kutengeneza damu ya maabara

Professa Toye ameshaunda kampuni ijulikanayo kama Scarlet Therapeutics, inayokusanya damu kutoka kwa watu wenye aina adimu za damu kwa ajili ya kuunda mistari ya seli itakayoweza kuzalisha seli nyekundu bila kikomo.

Damu hii inaweza kugandishwa kwa matumizi ya dharura.

"Ikiwa tunaweza kuifanya bila kuhariri, basi ni nzuri, lakini kuhariri ni chaguo kwetu," anasema.

"Sehemu ya kile tunachofanya ni kuchagua wafadhili kwa uangalifu kujaribu kufanya antijeni zao zote ziendane iwezekanavyo kwa watu wengi. Kisha pengine itatubidi kuhariri jeni ili kuifanya iendane na kila mtu." Via:BBC

0 Comment

Kwanini watu huzungumza usingizini na je maongezi hayo hueleweka?Afyaclass Forum •

Dkt. Tareq Gharaibeh, mtaalamu wa magonjwa ya kifua na usingizi, alieleza katika mahojiano kuwa:

"Tabia ya kuzungumza wakati wa usingizi haina chanzo maalum kilichothibitishwa kisayansi. Hata hivyo, imebainika kuwa hali hii huongezeka miongoni mwa watu wanaokumbwa na hali ya kuchanganyikiwa, na usingizi mzito unaosababishwa na usafiri wa haraka katika maeneo ya saa kadhaa,

ambayo huvuruga saa ya ndani ya mwili, au mdundo wa mzunguko (jet lag) kutokana na safari za mbali, au wale ambao hupata usingizi kwa viwango visivyo vya kawaida yaani, mtu analala kidogo sana kwa muda mrefu halafu baadaye analala kwa muda mrefu zaidi."

"Vichochezi vingine ni pamoja na kukosa pumzi wakati wa usingizi (sleep apnea), msongo wa mawazo, na wasiwasi wa kihisia. Vitu hivi vyote huongeza uwezekano wa mtu kuzungumza akiwa usingizini. 

Aidha, utafiti mmoja wa kisayansi umeonesha kuwa urithi wa kinasaba (genetics) huweza kuchangia. Ikiwa mzazi au ndugu yako wa karibu ana tabia ya kuongea usingizini, kuna uwezekano mkubwa nawe ukaipata."

Kuhusu kama maneno yanayozungumzwa usingizini yana maana au la, Dkt. Gharaibeh alisema:

"Mara nyingi maneno hayo huwa yanaeleweka kimuundo lakini hayana maana yoyote halisi. Huwa ni kauli zisizo na muktadha, miito, au sauti za kawaida. Mtu hawezi kuyakumbuka kwa sababu hutokea katika hatua ya usingizi ambapo kumbukumbu haifanyi kazi kikamilifu."

0 Comment

Muda sahihi wa kusoma kipimo chako cha ukimwi Afyaclass Forum •

Nmekuwa nikipata simu nyingi na maswali mengi juu ya shida hii…

Watu wengi wanajipima HIV wanaona kipimo chao kimesoma line moja ya C-Control ikiwa na maana ya NEGATIVE, lakini baada ya Muda wanaona kuna Mstari Zaidi ya Mmoja, hali ambayo inafawanya kupaniki sana na kuwa na hofu kubwa, wakihisi tayari wana maambukizi.

Je ni nini cha kufanya au unakosema wapi? au je tayari una maambukizi?

Zingatia vitu hivi Muhimu sana wakati unajipima mwenyewe HIV;

✓ hakikisha umeangalia Expire date ya kipimo chako,

Unaweza usipate majibu sahihi ikiwa kipimo chako kimeshakwisha muda wake wa matumizi.

✓ Sababu nyingine ya Msingi sana ni Muda wa Kusoma majibu yako,

Muda sahihi wa kusoma kipimo chako cha ukimwi ni kuanzia dakika 10, 15 mpaka 20.

Na baadhi ya Vipimo utakuta wamekuandikia kabsa na Muda wa Kusoma majibu yako, Hakikisha unazingatia sana hili.

Ukisoma Majibu yako Nje ya Muda unaotakiwa, Hapa ndipo Makosa(Error) hutokea kwenye Kipimo chako, na Kuanza kupata majibu ambayo sio sahihi,

Unaweza kupata Majibu kana kwamba Tayari umeshaathirika kumbe Sio, Swala ni muda wa kusoma majibu.

Mwingine anaweza kujipima Sasa hivi Mstari mmoja ukatokea, anakuja Kusoma Majibu yake kesho anakuta kuna Mistari miwili kana kwamba tayari kaathirika.

Zingatia Muda….!!!!

0 Comment

Ugonjwa wa mpox na dalili zake,Fahamu hapa ugonjwa huu wa homa ya nyaniAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa mpox na dalili zake,Fahamu hapa ugonjwa huu wa homa ya nyani


 

Ugonjwa Wa Mpox,chanzo,dalili Na Tiba yake

Ugonjwa wa homa ya nyani au Mpox ni ugonjwa ambalo unasababishwa na virusi, Ugonjwa huu unasababishwa na virusi ambao hujulikana kwa jina la Mpox ambapo hapo awali vilijulikana kama MonkeyPox. Mpox Virus wapo kwenye kundi la Orthopoxvirus genus ndani ya familia ya Poxviridae.

Ugonjwa wa homa ya nyani kwa binadamu(Human Mpox),Mara ya kwanza kabsa uliripotiwa Mwaka 1970 nchini DRC(Democratic Republic of the Congo) kwa kijana mmoja wa Miaka 9 aliyekuwepo kwenye eneo ambalo ugonjwa wa Smallpox ulishaondolewa tangu mwaka 1968. Ndipo visa vingine vikaanza kuripotiwa na maeneo mengine, (Disease history Source:WHO)

Dalili za Ugonjwa wa Mpox

DALILI ZA UGONJWA HUU WA Homa ya Nyani NI PAMOJA NA;

– Mtu kuwa na homa pamoja na mwili kutetemeka

– Kupata maumivu makali ya kichwa

– Mwili kuchoka kupita kawaida

– Mwili kukosa nguvu na kuwa dhaifu sana

– Lymph nodes kuanza kuvimba ambapo kwa lugha nyingine hujulikana kama lymphadenopathy

– Kupata maumivu ya viungo,joints pamoja na misuli ya mwili

– Kupata maumivu ya mgongo(back ache)

– Kutokewa na UPELE kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wako kama vile; Usoni, kwenye mikono pamoja na viganja vya mikono,
miguuni,machoni,,mdomoni,sehemu za siri n.k

Upele huu unaweza kuwasha sana, na hata baadae huweza kutumbuka kabsa,

Mwili huweza kubaki na makovu au alama alama.

UGONJWA HUU WA HOMA YA NYANI(MPOX) husambaa kutokana na ukaribu(Close contact) kwa mtu,wanyama au vitu ambavyo tayari vina virusi hawa wa Mpox.

Unaweza kuupata kwa njia ya ya mgusano sehemu zenye majeraha, kupitia body fluids zote kama vile damu,mate,jasho n.k, kutoka kwa Mtu au wanyama wenye Virusi hawa(Mpox virus).

Virusi vya MPox vinaweza kuingia mwilini kupitia kwenye ngozi iliyo na jeraha au michubuko yoyote, au kwa njia nyingine kama vile njia ya upumuaji au kupitia macho, pua pamoja na mdomo.

Pia Uenezwaji wake unaweza kuwa  kwa kugusana na wanyama walioambukizwa kama vile nyani, panya na kindi ,kupitia vitu kama vile matandiko au nguo za mgonjwa mwenye virusi hawa.

- Ugonjwa wa Homa ya Nyani unaweza kusambaa kutoka kwa mtu mwenye maambukizi kwenda kwa mwingine kwa njia zifuatazo; kupitia maji maji ya mwili ikiwemo mate, matapishi, jasho, mkojo, matone ya mfumo wa njia ya hewa na ngozi kupitia kugusana na kujamiana na mtu mwenye maambukizi ama kutumia vifaa, matandiko au kugusa sehemu zilizo na vimelea vya ugonjwa huu. Aidha, ugonjwa huu unaweza pia kuenezwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu.

- Dalili kuu ya Homa ya Nyani ni upele, malengelenge au vidonda kwenye mwili hasa, mikono na miguu, kifuani, usoni na wakati mwingine sehemu za siri. Dalili nyingine ni homa, uchovu, maumivu ya kichwa, misuli, mgongo, uchovu na kuvimba mitoki.

- Ugonjwa huu wa homa ya nyani haujaingia nchini, hivyo, ni vyema tukashirikiana kuhakikisha nchi yetu inabaki kuwa salama. Wizara inatoa tahadhari kwa Wananchi wote kuchukua hatua za kujikinga na ugonjwa wa huu kwa kutekeleza yafuatayo;-

i. Kutoa taarifa kupitia namba 199 bila malipo endapo utamuona mtu mwenye dalili za Homa ya Nyani(Mpox).

ii. Kuepuka kugusa majimaji ya mwili au ngozi ya mtu mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya nyani(Mpox).

iii. Kuepuka kusalimiana kwa kupeana mikono, kukumbatiana na kubusiana mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox).

iv. Kuepuka kugusana na mtu yeyote mwenye dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

v. Kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono.

vi. Epuka kula au kugusa mizoga au wanyama mfano nyani au swala wa msituni.

vii. Safisha na kutakasa vyombo vilivyotumika na mhisiwa au mgonjwa pamoja na maeneo yote yanayoguswa mara kwa mara.

viii. Kuvaa barakoa iwapo itabidi kukaa na kuongea kwa karibu na mtu mwenye dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

ix. Kuwahi katika vituo vya huduma za afya unapoona dalili za ugonjwa wa Homa ya Nyani(Mpox).

x. Watoa huduma za afya kuzingatia miongozo ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi (IPC) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.

Via:WizaraafyaTz.

MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA NYANI(Mpox)

Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani hauna tiba(no cure),bali watalaam wa afya hudhibiti dalili zinazotokana na ugonjwa huu wa homa ya nyani.

Kwa Sasa Shirika la Afya Duniani(WHO) limeidhinisha Chanjo za Kutumika Kuzuia Ugonjwa huu wa Homa ya Nyani. #SOMA Zaidi hapa Kuhusu WHO na Chanjo hii ya Mpox

Hata hivo ugonjwa huu huisha wenyewe kwa kipindi flani baada ya kumpata mtu.

Fahamu pia,Maambukizi haya ya ugonjwa wa homa ya nyani(Mpox) huisha yenyewe na hudumu kati ya siku 14 na 21.


Mpox ni nini? Mpox/Homa ya Nyani

Kumekua na mlipuko barani Africa, nchi za jirani pia zimetangaza kua na wagonjwa wa mpox. Hivi karibuni hata mabara mengine yameanza kutangaza uwepo wa ugonjwa huu kwa kasi, hiii imepelekea WHO kuutangaza ugonjwa wa homa ya nyani kama janga la kimataifa. Hata hivyo nchini Tanzania bado hakujatangazwa kupatikana kesi ya ugonjwa huu.

Homa ya nyani ni ugonjwa unaosababishwa na virusi.virusi hivi ni familia moja na virusi vinavyosababisha smallpox au ndui kwa kiswahili.

Tuone historia ya Homa ya nyani kifupi.

Homa ya nyani sio ugonjwa mpya, umegundulika mwaka 1958 katika nyani waliokua wakifanyiwa tafiti. Kesi ya kwanza ya homa ya nyani kwa binadamu iligundulika mwaka 1970 nchini  DRC.

Tangu wakati huo kumekua na kesi chache barani africa hasa  africa ya kati na afrika ya magharibi. Lakini mwaka 2022 tumeanza kuona ugonjwa huu ukienea kwa kasi maeneo ambayo sio endemic na hata nje ya bara la Africa.

Ugonjwa wa Homa ya Nyani Unaambukizwaje

  1. Mji maji au mate yanatotoka kinywani wakati wa Kuongea, kukohoa au kuoiga chafya. (Droplets)
  2. Aina zote za ngono zinaweza kuambukiza, hii inajuimuisha kumbusu mtu mwenye mpox(All forms of sexual contact including kissing)
  3. Kukutana au kugusana ngozi na mtu mwenye homa ya nyani (Skin to skin contact)
  4. Kuvaa nguo au kutumia mashuka na foronya za mtu mwenye homa ya nyani. (Sharing clothes and/or bedding)
  5. KUgusa au kula wanya walioathirika au mizoga.

Dalili za Ugonjwa wa Homa ya Nyani

  1. Upele (una wezakutokea kwenye ngozi, mdomoni, ukeni, au ndani ya njia ya haja kubwa)
  2. Homa
  3. KUskia maumivu kwenye koo. (Sore throat)
  4. Maumivu Kichwa
  5. Maumivu ya Misuli
  6. Maumivu ya mgongo
  7. Uchovu wa kupitiliza usio elezeka
  8. Kuvimba tezi

Tiba na chanjo ya Ugonjwa wa homa ya Nyani

  1. Homa ya nyani isiokua na dalili kali (severe) hupona yenyewe ndani ya wiki 2-4 ( self limiting)
  2. Nenda kituo cha afya kuhakiki kama ni mpox na sio kitu kingine.
  3. Matibabu ya upele na kutibu dalili zingine kama homa kali na maumivu ya misuli yanaweza kupatikana

Chanjo ya homa nyani ipo lakini bado haipatikani nchi nyingi za Africa.


Watu walio katika hatari Ya kupata Homa ya nyani yenye Dalili Kali (severe).

  1. Watoto chini ya mwaka mmoja
  2. Wajawazito
  3. Watu wenye upungufu wa kinga mwilini.

Watu walio katika hatari ya kupata homa ya nyani

  1. Watoa huduma ya afya
  2. Wanaofanya kazi katika mkusanyiko/msongamano  wa watu wengi
  3. Watu wenye wenza wengi ( multiple sexual partners)
  4. Watu wenye kujihusisha na biashara ya ngono
  5. Wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja pia wametajwa kuwa na hatari ya kupata.

Jinsi ya kujikinga na Ugonjwa wa Homa ya Nyani

  1. Epuka sehemu zenye msongamano  ambazo utagusana na watu
  2. Nawa mikono kabla ya kujigusa, kula, au unapotoka kwenye mizunguko
  3. Tumia kinga wakati wa kujamiiana
  4. Epuka kugusa wanyama wanaumwa au mizoga bila kujua ugonjwa au sababu ya kifo.

Jinsi ya kuwalinda wengine endapo wewe umeathirika na Ugonjwa wa Homa ya Nyani.

  1. Kaa nyumbani au katika chumba chako mwenyewe kama inawezekana.
  2. Osha mikono mara nyingi kwa sabuni na maji au na vitakasa mikono, hasa kabla au baada ya kugusa vidonda.
  3. Vaa barakoa na funika vidonda unapokuwa karibu na watu wengine hadi upele wako upone.
  4. Weka ngozi yako kavu na bila kufunikwa (isipokuwa unapokuwa chumbani na mtu mwingine).
  5. Epuka kugusa vitu katika maeneo ya pamoja na safisha maeneo ya pamoja mara kwa mara.
  6. Fuata maelekezo ya daktari katika kutibu vipele/vidonda.
  7. Tumia dawa za kupunguza maumivu zinazopatikana bila agizo la daktari kama vile paracetamol au ibuprofen.

 Nini cha kuepuka kuhusu Ugonjwa wa Homa ya Nyani

Kupasua au kukuna vipele/malengelenge. Hii inaweza kuweka vijidudu kwenye vidonda na kusababisha vishambuliwe na bakteria au kuchelewa kupona kwa vidoonda. Au kusambaza zaidi mwilili.

Credits|Article By;

Dr Ladina Msigwa

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD