Dkt. Tareq Gharaibeh, mtaalamu wa magonjwa ya kifua na usingizi, alieleza katika mahojiano kuwa:
"Tabia ya kuzungumza wakati wa usingizi haina chanzo maalum kilichothibitishwa kisayansi. Hata hivyo, imebainika kuwa hali hii huongezeka miongoni mwa watu wanaokumbwa na hali ya kuchanganyikiwa, na usingizi mzito unaosababishwa na usafiri wa haraka katika maeneo ya saa kadhaa,
ambayo huvuruga saa ya ndani ya mwili, au mdundo wa mzunguko (jet lag) kutokana na safari za mbali, au wale ambao hupata usingizi kwa viwango visivyo vya kawaida yaani, mtu analala kidogo sana kwa muda mrefu halafu baadaye analala kwa muda mrefu zaidi."
"Vichochezi vingine ni pamoja na kukosa pumzi wakati wa usingizi (sleep apnea), msongo wa mawazo, na wasiwasi wa kihisia. Vitu hivi vyote huongeza uwezekano wa mtu kuzungumza akiwa usingizini.
Aidha, utafiti mmoja wa kisayansi umeonesha kuwa urithi wa kinasaba (genetics) huweza kuchangia. Ikiwa mzazi au ndugu yako wa karibu ana tabia ya kuongea usingizini, kuna uwezekano mkubwa nawe ukaipata."
Kuhusu kama maneno yanayozungumzwa usingizini yana maana au la, Dkt. Gharaibeh alisema:
"Mara nyingi maneno hayo huwa yanaeleweka kimuundo lakini hayana maana yoyote halisi. Huwa ni kauli zisizo na muktadha, miito, au sauti za kawaida. Mtu hawezi kuyakumbuka kwa sababu hutokea katika hatua ya usingizi ambapo kumbukumbu haifanyi kazi kikamilifu."









image quote pre code