Breaking: Chukueni tahadhari dhidi ya uwepo wa COVID 19Afyaclass Forum •
Breaking: Chukueni tahadhari dhidi ya uwepo wa COVID 19
Wizara ya Afya imesema imeendelea kufanya ufuatiliaji wa karibu na kutoa taarifa za kila siku kuhusu magonjwa ya mlipuko pamoja na tetesi za uwepo wa magonjwa hayo nchini ambapo imesema tangu February hadi April 2025, ufuatiliaji wa virusi vya Covid 19 umeonesha ongezeko la maambukizi kutoka 1.4% (Wagonjwa wawili kati ya Watu 139 waliopimwa) mwezi February hadi 16.3% (Wagonjwa 31 kati ya 190 waliopimwa) mwezi March, na kisha 16.8% (Wagonjwa 31 kati ya Watu 185 waliopimwa) mwezi Aprili 2025.
Taarifa iliyotolewa leo May 20,2025 na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe imesema “Ugonjwa wa UVIKO-19, ambao ulitangazwa kwa mara ya kwanza nchini March 2020, umeendelea kuwepo kwa kiwango cha chini kama yalivyo magonjwa mengine ya mfumo wa njia ya hewa, hali ya kuongezeka na kupungua kwa ugonjwa huu imekuwepo kila mwaka tangu kutangazwa kwa ugonjwa huu mwaka 2020, kwa kipindi hiki ongezeko hili linaonekana zaidi katika Mkoa wa Dar es salaam, Wizara ya Afya inaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa nchini na kutoa taarifa”
“Katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Aprili 2025, tumeshuhudia ongezeko la tetesi zinazohusiana na magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa katika jamii hapa nchini, hasa katika mkoa wa Dar es salaam, kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa, ambayo imekuwepo tangu mwaka 2008, tumekuwa tukifuatilia mwenendo wa magonjwa haya ili kubaini aina za vimelea vinavyosababisha maambukizi, ongezeko la visa, pamoja na uwezekano wa kujitokeza kwa kirusi kipya chenye uwezo wa kusambaa kwa haraka”
“Vipimo vya maabara vimebaini kuongezeka na kupungua kwa virusi vya influenza hali ambayo imekuwa ikionekana pia katika miaka iliyopita na ndiyo maana hujulikana kama ‘Seasonal influenza”, vipimo vimeonesha kuwa hakuna kirusi kipya kinachoweza kusambaa kwa haraka na kusababisha mlipuko wa aina ya Pandemiki” Cc:MillardAyoUPDATES
Breaking News;Papa mpya apatikanaAfyaclass Forum •
Breaking News;Papa mpya apatikana
Moshi mweupe umeonekana ukifuka kutoka kwenye bomba la moshi katika Kanisa la Sistine Chapel, ni wazi mchakato wa upigaji kura umekamilika na makadinali wamemchagua mrithi wa Papa Francis.
Bado hatujui ni nani amechaguliwa, lakini itaonekana wazi watakapotokea kwenye roshani ya Kanisa la Sistine, ndani ya kama saa moja.
Roshani inayokodolewa macho
"Viva Papa"
Umati wa watu unaimba "Viva papa", ambayo ina maana ya "maisha marefu Papa" kwa Kiitaliano.
Muziki unaendelea kuchezwa kutoka kwa bendi ambayo sasa iko chini ya roshani katika uwanja wa St Peter's Square.
Nini kinatokea sasa?
Makadinali wateule sasa wamemchagua Papa mpya na mambo yatakwenda kwa haraka sana kuanzia sasa.
Kwa vile moshi mweupe umetokea, kawaida, Papa mpya ataonekana kwenye roshani upande wa moja kwa moja na uwanja wa St Peter's Square ndani ya saa moja ijayo.
Papa mpya sasa anaongozwa hadi kwenye chumba kidogo karibu na Kanisa la Sistine ambapo atavaa mavazi meupe ya papa.
Kardinali mkuu hivi karibuni atathibitisha uamuzi huo kwa maneno "Habemus Papam" - Kilatini ikimaanisha "tuna Papa" - na kumtambulisha Papa mpya kwa jina lake alilochagua la papa.
Umati wajawa na furaha na kuomba wakisherehekea Papa mpya
Shangwe isiyo na kifani yashuhudiwa upande wa waumini huku moshi mweupe ukifuka, kila mtu akiwa anakimbilia kuuona.
Watu wanaruka juu na chini kwa furaha, wengine wanaomba huku wakiwa wanatazama angani. Wanandoa kutoka Ugiriki wanasema "ni tukio ambalo ni nadra sana kutokea maishani", na kuongeza kuwa watasubiri kuona Papa mpya akitokea kwenye roshani.
Katina eneo lote la Kanisa la Sistine, kengele zinalia kwa nguvu sana na zinasikika kila mahali huku watu wakishangilia na kupiga mayowe kwa furaha.
Sauti hapa ni nzuri sana, kengele zinalia kwa nguvu sana na zinasikika kila mahali huku watu wakishangilia na kupiga mayowe kwa furaha.
Bendera zinapeperushwa huku watu wakikumbatiana wakati mchakato wa kumtafuta kiongozi wa kanisa katoliki ukifikia tamati.
Bendi inacheza muziki
Bendi maalum iliyovalia nguo za rangi ya buluu na samawati inaonekana ikicheza muziki huku ikipita katikati ya umati wa watu huko Vatikani.
Wanaotembea kando yao ni Walinzi wa Uswizi, wakiwa wamevalia sare zao za mistari ya bluu na njano.
Umati wanapiga makofi na kuinua simu ili kunasa picha hiyo.
Nini Faida ya kutumia Gari kali Siku ya Harusi?Afyaclass Forum •
Nini Faida ya kutumia Gari kali Siku ya Harusi?
Bila shaka ushahudhuria vikao vya sherehe mbalimbali iwe sendoff, harusi na nyingine zenye kufanana na hizo, ukaona namna kamati za maandalizi zinavyohaha kuhakikisha maharusi wanatumia magari mazuri siku ya tukio.
Si ajabu ukaona watu wanafikia hata hatua ya kugombana kuhusu gari la maharusi, huyu akisema aina fulani ya gari ndo nzuri lakini gharama kubwa, mwingine akisema tusijali gharama tuichukue tu kama bajeti ipo.
Sasa kuna mdau anasema ushawahi kujiuliza faida ya kutumia gari kali ni ipi? Yaani usiku mtu anatumia gari kali kwenye harusi anapelekwa ukumbini kisha hotelini, halafu asubuhi anaondoka na Bajaji kuelekea nyumbani kwake, mbwembwe zote zimeisha! Je tumsaidie mdau mawazo au asubiri kwenye shughuli yake aone?
Nimefanyiwa upasuaji mara 100 na siachi' Nini Ushauri wako hapaAfyaclass Forum •
Nimefanyiwa upasuaji mara 100 na siachi' Nini Ushauri wako hapa
Abby Wu alikuwa na umri wa miaka 14 tu alipofanyiwa upasuaji wa urembo bandia kwa mara ya kwanza.
Baada ya kupata matibabu ya homoni, uzito wa mwili wa Abby uliongezeka kutoka kilo 42 hadi kilo 62 ndani ya miezi miwili.
Mwalimu wake wa michezo ya kuigiza aligundua mabadiliko hayo ya mwili.
Mwalimu wangu aliniambia, ''ulikuwa nyota lakini sasa umekuwa mnene kupita kiasi. Chagua moja uondoke kwa tasnia hii au upunguze kilo,'' anakumbuka alichoambiwa kipindi hicho akisubiri kufanya mtihani wake wa tamthilia.
Mama yake Abby aliingilia kati na kuamua kumpeleka kufanyiwa upasuaji wa kuondoa mafuta tumboni na miguuni.
Abby anavuta kumbukumbu jinsi mamake alivyompa motisha akisubiri kufanyiwa operesheni hiyo.
''Kuwa mkakamavu na uingie ufanyiwe. Ukitoka hapo utakuwa mrembo zaidi.''
Upasuaji huo ulimuacha na makovu. Abby alipatiwa dawa za kupunguza uchungu lakini alikuwa macho akifanyiwa operesheni hiyo.
''Ningeona kiasi cha mafuta kilichotolewa mwilini mwangu na damu iliyokuwa ikinivuja,'' anasema.
"Upasuaji ulifanya kazi. Nilijiamini na kuwa na furaha zaidi, siku baada ya siku. Nadhani mama yangu alifanya chaguo sahihi."
Sasa Abby ana umri wa miaka 35 na amefanyiwa upasuaji wa urembo mara mia moja ikimgharimu dola nusu milioni.
Anamiliki kliniki ya ulimbwende katikati mwa mji wa Beijing na amekuwa mtu tajika katika tasnia ya upasuaji wa plastiki nchini China.
Lakini upasuaji huo pia unaathari zake kwa mwili.
Akiwa amekaa mbele ya kioo anajipodoa ili kuficha makovu ya sindano za kupunguza unene usoni, utaratibu anaoufanya kila mwezi ili kuhakikisha uchanga usoni mwake nakuhakikisha hana ngozi zilizolegea baada ya upasuaji wa kupunguza taya uliondoa mifupa mingi.
Lakini anasisitiza kuwa hajutii upasuaji wa urembo aliyofanya kufikia sasa akiamini kuwa mamake hakukosea kumuanzisha katika ulimbwende huu.








