Showing posts with label Jukwaa la michezo. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la michezo. Show all posts

Fahamu Nchi sita zimeyaaga mashindano ya Afcon 2025Afyaclass Forum •

Fahamu Nchi sita zimeyaaga mashindano ya Afcon 2025

Nchi sita zimeondolewa kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika la 2025 nchini Morocco huku mashindano hayo yakiingia katika mechi za mwisho za makundi.

Comoros, Zambia na Zimbabwe zimekuwa timu za hivi karibuni kuondolewa, zikijiunga na Botswana, Gabon na Equatorial Guinea, ambazo tayari ziliondoka baada ya kushindwa kukusanya pointi katika raundi za awali.

Timu ya kwanza kuondolewa katika AFCON 2025 ilikuwa Botswana. Equatorial Guinea na Gabon zilifuata.

Comoro ni timu ya kwanza iliyoshika nafasi ya tatu kuondolewa, kwani walimaliza mechi yao ya tatu tayari wakiwa chini ya timu nne kati ya tano zilizoshika nafasi ya tat.

Ushindi wa Afrika Kusini wa mabao 3-2 dhidi ya Zimbabwe ulimaliza safari ya majirani zao. Zimbabwe ilimaliza ikiwa ya mwisho na pointi moja, ikithibitisha kuondolewa kwao.

Mashindano hayo yanayoendelea Morocco, yataendelea leo kwa Uganda kukutana na Nigeria, Tanzania dhidi ya Tunisia, Bostwana kukipiga na DR Congo na Benin kuchuana na Senegal.

0 Comment

Tanzania na Uganda wamelazimika kugawana alama baada ya kutoka sare ya 1–1Afyaclass Forum •

Tanzania na Uganda wamelazimika kugawana alama baada ya kutoka sare ya 1–1 katika dabi ya Afrika Mashariki ya kwenye michuano ya AFCON 2025, matokeo ambayo yanaacha hatima ya timu zote mbili ikining'inia kuelekea michezo ya mwisho ya kundi.

Kipindi cha kwanza kilikuwa chini ya udhibiti wa Uganda, waliocheza kwa kujiamini na kuwabana Tanzania katika nusu yao ya uwanja. Cranes walionekana kuwa na mpango mzuri wa kumiliki mpira na kushambulia kupitia mipira ya juu, lakini walikosa umakini katika eneo la mwisho.

Kipindi cha pili kilipoanza, Tanzania walibadilika. Ndani ya dakika 10 za mwanzo, Taifa Stars waliongeza kasi na kuanza kuucheza mpira kwenye nusu ya Uganda, shinikizo lililozaa penati ambayo Simon Msuva aliitumia vyema kuiweka Tanzania mbele.

Hata hivyo, dakika 15 za mwisho waganda waliongeza nguvu na kuanza kuingia kwa kasi katika eneo la Tanzania, hali iliyowalipa walipopata bao la kusawazisha kupitia Uche Ikpeazu.

0 Comment

Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, amchakaza mpinzani wake kutoka Nigeria, EriboAfyaclass Forum •

Bondia nyota wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameendeleza ubabe baada ya kushinda kwa knockout (KO) dhidi ya mpinzani wake kutoka Nigeria, Eribo, katika pambano lililofanyika usiku wa leo kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki — Dar es Salaam.

Mwakinyo alimaliza kazi ndani ya mizunguko miwili tu, akitumia umakini na kasi kubwa, jambo lililowafanya mashabiki waliokuwa ukumbini kusimama kwa shangwe.

Ushindi huo umeonekana kama faraja kwa Watanzania wengi, hususani baada ya timu ya taifa, Taifa Stars, kupata matokeo mabaya dhidi ya Nigeria kwenye michuano ya AFCON 2025.

Mwakinyo ameahidi kuendelea kupambana na kuipa heshima Tanzania kimataifa kupitia ndondi

0 Comment

Super Eagles ya Nigeria imeishinda Tunisia 3-2 na kufuzu kwa Raundi ya 16 ya AFCONAfyaclass Forum •

Super Eagles ya Nigeria iliishinda Tunisia 3-2 na kufuzu kwa Raundi ya 16 ya AFCON

Super Eagles ya Nigeria imefuzu kwa raundi ya 16 ya Kombe la Mataifa ya Afrika linaloendelea nchini Morocco.

Nyota hao wa Nigeria waliishinda Tunisia 3-2 Jumamosi usiku katika Uwanja wa Fez kwa mabao kutoka kwa Victor Osimhen, Wilfried Ndidi, na Ademola Lookman, na kuhakikisha timu hiyo inafuzu kutoka kundi lao.

Victor Osimhen alifungua bao dakika ya 44 kupitia krosi kutoka kwa Ademola Lookman kabla ya mapumziko. Katika dakika ya 50, nahodha wa timu hiyo, Widfred Ndidi alifunga bao la pili dakika ya 50, akisaidiwa tena na Lookman.

Lookman aliongeza bao la tatu dakika ya 70, kufuatia pasi ya Osimhen.

 Wakati huo huo, Tunisia ilifanikiwa kupata bao moja kupitia Montassar Talbi, kabla ya penalti ya dakika za mwisho kufungwa na Ali Al-Abdi.

Matokeo hayo yanamaanisha kuwa Nigeria ina pointi sita kutokana na mechi mbili, huku Tunisia ikibaki ya pili ikiwa na pointi tatu.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD