Tanzania na Uganda wamelazimika kugawana alama baada ya kutoka sare ya 1–1 katika dabi ya Afrika Mashariki ya kwenye michuano ya AFCON 2025, matokeo ambayo yanaacha hatima ya timu zote mbili ikining'inia kuelekea michezo ya mwisho ya kundi.
Kipindi cha kwanza kilikuwa chini ya udhibiti wa Uganda, waliocheza kwa kujiamini na kuwabana Tanzania katika nusu yao ya uwanja. Cranes walionekana kuwa na mpango mzuri wa kumiliki mpira na kushambulia kupitia mipira ya juu, lakini walikosa umakini katika eneo la mwisho.
Kipindi cha pili kilipoanza, Tanzania walibadilika. Ndani ya dakika 10 za mwanzo, Taifa Stars waliongeza kasi na kuanza kuucheza mpira kwenye nusu ya Uganda, shinikizo lililozaa penati ambayo Simon Msuva aliitumia vyema kuiweka Tanzania mbele.
Hata hivyo, dakika 15 za mwisho waganda waliongeza nguvu na kuanza kuingia kwa kasi katika eneo la Tanzania, hali iliyowalipa walipopata bao la kusawazisha kupitia Uche Ikpeazu.









image quote pre code