Showing posts with label Kampuni ya OpenAI. Show all posts
Showing posts with label Kampuni ya OpenAI. Show all posts

Sasa CHATGPT kuacha kushauri Wapenzi waachaneAfyaclass Forum •

Kampuni ya OpenAI imetangaza kuwa programu yake ya mazungumzo, ChatGPT, haitatoa tena majibu ya moja kwa moja kwa watumiaji wanaotaka ushauri wa kuachana na wapenzi wao.



Badala yake, ChatGPT itawaongoza watumiaji kutafakari kwa kina kwa kuwasaidia kupima faida na hasara kabla ya kufanya uamuzi .

OpenAI imesema hatua hiyo inalenga kulinda afya ya akili ya watumiaji, hasa wanapopitia changamoto binafsi. Pia, kampuni hiyo imeanza kushirikiana na wataalamu zaidi ya 90 wa afya ya akili kutoka nchi 30 ili kuhakikisha majibu yanayotolewa ni salama na yanayojali hali ya mtumiaji.

Mabadiliko mengine ni pamoja na ujumbe wa kuwakumbusha watumiaji kuchukua mapumziko wakati wa mazungumzo marefu ili kuepuka utegemezi kupita kiasi.

Kwa sasa, ChatGPT inatumiwa na zaidi ya watu milioni 700 kwa mwezi.

0 Comment

Sasa ChatGPT kufikiri kwa niaba ya MtumiajiAfyaclass Forum •

Kampuni ya OpenAI imetangaza kuzindua kipengele kipya katika akili mnemba yake ya ChatGPT kitakachomruhusu Roboti huyo kufanya baadhi ya majukumu ikiwemo kufikiri kwa niaba ya Mtumiaji ikiwa ni sehemu ya mapinduzi ya mtandao ambapo Watumiaji badala ya kuhama program kupata na kutafuta taarifa kwa mikono, atategemea Mawakala wa AI kufanya kila kitu.



Kipengele hicho kipya cha ChatGPT ambacho kimepewa jina la Wakala “Agent Mode” kitaanza kufanya kazi hivi karibuni na kitakwenda kuongeza ushindani katika Makampuni ya kiteknolojia hususani Google na OpenAI ambazo zote zinatengeneza akili mnemba ambayo ina lengo la kutoa usaidizi.

Aidha kwa mujibu wa OpenAI, kipengele hicho cha Wakala kwa sasa kitaiwezesha akili mnemba ya ChatGPT kufikiri na kutekeleza majukumu kwa kutumia mfumo wake wa kidigitali wa kompyuta (virtual computer) ambayo itaiwezesha kufanya mambo magumu kwa mafano Mtumiaji akiitaka imwangalizie kalenda na kumwambia matukio yajayo pamoja na kuiambia ikusaidie kutaja viungo vitakavyotumika kwa aina ya chakula itaweza kufanya hivyo.

Aidha katika video ya maelezo OpenAI Mtumiaji mmoja aliiambia ChatGPT iweze kumwandalia na kumshauri aina ya mavazi ya kuvaa kwa ajili ya harusi na kutaka impe mapendekezo ya nguo tano tofauti kama vile kanisani, hotelini na ukumbini na ilifanya hivyo ambapo kwa mujibu wa OpenAI kipengele hicho kipya kitapatkana kwa wale ambao watalipia kuanzia ChatGPT Pro, Plus au Team Plan.

Aidha ChatGPT imesema kipengele hicho kipya kimekuja na hatari katika kupambana na taarifa za faragha za Watumiaji wake ambapo kampuni hiyo imeendelea kuonya kuwa watumiaji wake wasitoe taarifa zao za muhimu na za faragha kwa akili mnemba hiyo ambapo pia wamesema kuwa haitaweza kufanya kazi na kufikia sehemu kama Baruapepe ambazo zitahitaji uangalizi wa mtuniaji mwenyewe pamoja na kazi hatarishi kama vile kazi za kibenki.

0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD