Showing posts with label Klabu ya Simba. Show all posts
Showing posts with label Klabu ya Simba. Show all posts

Klabu ya Simba yamtimua kocha wake Dimitar Pantev (49)Afyaclass Forum •

Klabu ya Simba yamtimua kocha wake Dimitar Pantev (49)

Klabu ya Simba SC imethibitisha kusitisha mkataba na Meneja Mkuu wake, Dimitar Pantev (49), pamoja na wasaidizi wake wawili, Vitomir Vutov (53) na Byoko Kamenov (49), wote raia wa Bulgaria, baada ya pande zote kufikia makubaliano ya pamoja.

Taarifa kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imeeleza kwamba hatua hii ni sehemu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya klabu hiyo, ikiwa ni jitihada za kurekebisha hali ya timu.

Kwa sasa, Kocha Selemani Matola ameteuliwa kuongoza kikosi cha Simba SC kwa muda hadi pale klabu itakapokamilisha mchakato wa kumsaka kocha mkuu mpya.

Klabu hiyo, ambayo mwaka jana ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho, imeanza vibaya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, baada ya kupoteza michezo miwili ya awali.

Simba ilipoteza nyumbani 1-0 dhidi ya Petro de Luanda na ugenini 2-1 dhidi ya Stade Malien.

Bodi ya Simba SC imeahidi kuwa mchakato wa kupata kocha mpya unafanyika haraka, huku ikilenga kurejesha rekodi nzuri ya timu kwenye michuano ya kimataifa.

0 Comment

Klabu ya Simba kuelekea nchini Mali kukipiga dhidi ya Stade MalienAfyaclass Forum •

Klabu ya Simba kuelekea nchini Mali kukipiga dhidi ya Stade Malien

Klabu ya Simba inatarajiwa kuanza safari yake alfajiri ya Alhamisi, Novemba 27, kuelekea nchini Mali kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien.

Wekundu wa Msimbazi watamenyana na wenyeji Stade Malien mnamo Novemba 30, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, mchezo ambao utapigwa majira ya saa 1 usiku.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD