Klabu ya Simba yamtimua kocha wake Dimitar Pantev (49)

Klabu ya Simba yamtimua kocha wake Dimitar Pantev (49)

#1

Klabu ya Simba yamtimua kocha wake Dimitar Pantev (49)

Klabu ya Simba SC imethibitisha kusitisha mkataba na Meneja Mkuu wake, Dimitar Pantev (49), pamoja na wasaidizi wake wawili, Vitomir Vutov (53) na Byoko Kamenov (49), wote raia wa Bulgaria, baada ya pande zote kufikia makubaliano ya pamoja.

Taarifa kutoka kwa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC imeeleza kwamba hatua hii ni sehemu ya mabadiliko ya kiutendaji ndani ya klabu hiyo, ikiwa ni jitihada za kurekebisha hali ya timu.

Kwa sasa, Kocha Selemani Matola ameteuliwa kuongoza kikosi cha Simba SC kwa muda hadi pale klabu itakapokamilisha mchakato wa kumsaka kocha mkuu mpya.

Klabu hiyo, ambayo mwaka jana ilifika fainali ya Kombe la Shirikisho, imeanza vibaya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, baada ya kupoteza michezo miwili ya awali.

Simba ilipoteza nyumbani 1-0 dhidi ya Petro de Luanda na ugenini 2-1 dhidi ya Stade Malien.

Bodi ya Simba SC imeahidi kuwa mchakato wa kupata kocha mpya unafanyika haraka, huku ikilenga kurejesha rekodi nzuri ya timu kwenye michuano ya kimataifa.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code