Showing posts with label Lishe. Show all posts
Showing posts with label Lishe. Show all posts

Fahamu Vyakula ambavyo vitakufanya utoe hewa chafuAfyaclass Forum •

Kutoa hewa chafu ni kawaida, mtu wa kawaida hufanya mara 5-15 kwa siku. Kwa kweli, kuwa na gesi nyingi kwa siku fulani inaweza kweli kuwa ishara ya afya njema, ikiwa unasahau kuhusu usumbufu wowote au aibu iliyoweza kusababisha.



Hiyo ni kwa sababu vyakula vinavyotengeneza hewa chafu huwa na wanga, zenye nyuzinyuzi nyingi, ambazo mwili wako hauwezi kuzivunjavunja lakini bakteria kwenye utumbo wako wanaweza.

Kwa hivyo ni vyakula gani vinakufanya utoe hewa chafu, ambayo hewa yako yako kuwa na harufu, na unapaswa kushauriana na daktari wakati gani?

1. Vyakula vya mafuta

Vyakula vya mafuta hupunguza kasi ya usagaji chakula, jambo ambalo linaweza kuviacha vikiwa kujazana kwenye utumbo wako, vikichacha na kutoa harufu mbaya.

Nyama za mafuta ni ngumu kwa sababu zina wingi wa amino acid methionine, ambayo ina sulphur.

Sulphur huvunjwa na bakteria wa utumbo wako kuwa salfa ya hidrojeni, harufu ya yai lililooza na 'huongeza' harufu ya gesi inayotolewa na vyakula vingine unavyokula pamoja na nyama.

2. Maharage

Maharage na dengu huwa na nyuzinyuzi nyingi, lakini pia zina raffinose, sukari changamano ambayo hatuichakati vizuri.

Sukari hizi huingia kwenye utumbo, ambapo utumbo wako hutumia kwa ajili ya nishati, hivyo kusababisha hidrojeni, methane na hata salfa inayonuka.

3. Mayai

Kinyume na imani maarufu, mayai hayatufanyi wengi wetu kutoa hewa chafu.

Lakini zina methionine iliyojaa sulphur. Kwa hivyo ikiwa hutaki kutoa harufu mbaya, usile mayai pamoja na vyakula vinavyosababisha utoaji wa hewa chafu kama vile maharagwe au nyama ya mafuta.

4. Vitunguu

Vitunguu maji, vitunguu swaumu, mbigiri vyote vina fructans, wanga ambao unaweza kusababisha gesi tumboni.

5. Maziwa

Maziwa kutoka kwa ng'ombe na mbuzi yana lactose, sukari ambayo inaweza kusababisha gesi kuongezeka.

Zaidi ya hayo, karibu 65% ya idadi ya watu wazima duniani wana kiwango cha kutovumilia lactose, na kula vyakula vitokanavyo na maziwa kunaweza kuwaacha wakihisi kuvimbiwa na gesi.

0 Comment

Faida Za Nanasi Mwilini mwako,Soma hapa kufahamuAfyaclass Forum •

Nanasi ni tunda la kitropiki ambalo huchukua miaka mitatu kukomaa. Nanasi ni tamu, huongeza vitamini na virutubisho mbalimbali kwa afya ya mlaji. Pia hupambana na magonjwa.

Nanasi lina faida mbalimbali za afya, ikiwa ni pamoja na kuboresha usagaji wa chakula, kuondoa hatari ya saratani, na kuondoa maumivu.

Hata hivyo, wale walio na mzio wanapaswa kuepuka matunda haya na wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kuwa waangalifu.

Kupambana na magonjwa

Tunda hili lina utajiri mkubwa wa vitamini C na magnishiamu. Vitamini C ni muhimu katika kusaidia kinga ya mwili.

Magnishiamu husaidia kupambana na seli zinazoweza kuleta madhara katika mwili, husaidia kuzuia uvimbe ambao unaweza kusababisha saratani na magonjwa mengine sugu.

Nanasi ni chanzo muhimu cha kupambana na magonjwa. Kutumia nanasi mara kwa mara kunaweza kukupunguzia hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kisukari.

Usagaji wa chakula

Tunda hili lina enzaimu wa kusaidia usagaji chakula waitwao bromelain, ambao husaidia kurahisisha usagaji wa chakula.

Bromelain huvunja molekuli za protini, ikimaanisha utumbo wako mdogo unaweza kuzifyonza kwa urahisi zaidi.

Hilo ni muhimu sana kwa watu walio na upungufu wa maji ya kongosho, hali inayoifanya kongosho kutotengeneza vimeng’enya vya kutosha vya kusaga chakula.

Kwa kuwa lina nyuzinyuzi nyingi, pia husaidia mfumo wa usagaji chakula na kuboresha afya ya vijidudu vyenye faida ambavyo hukaa kwenye utumbo wako.

Uponyaji baada ya kuumia

Tafiti kadhaa zinaonyesha kuwa bromelain ambayo pia inapatikana katika nanasi, husaidia kupunguza uvimbe na michubuko baada ya jeraha au upasuaji.

Nanasi linaweza kuwa muhimu ikiwa utakula kabla ya ung’oaji wa jino, husaidia kupunguza maumivu na kutoa ahueni kama vile dawa ya kuzuia maambukizi.

Utafiti wa taasisi ya Vitro (uliofanywa katika maabara), pia umeonyesha bromelain husaidia katika uponyaji wa jeraha.

Kupunguza maumivu ya viungo

Tatizo la maumivu ya viungo, ni ugonjwa unaohusisha viungo kuvimba, kuwa vyekundu na kuleta maumivu. Ugonjwa huu ni matokeo ya mfumo wa kinga kushambulia tishu zenye afya kimakosa.

Tafiti nyingi, zilizoanzia miaka ya 1960, zimeonyesha jinsi bromelaini inavyoweza kuwa muhimu katika kutuliza maumivu yanayohusiana na viungo.

Maumivu ya viungo huathiri zaidi ya watu wazima milioni 54 huko Marekani. Kuna aina nyingi za ugonjwa wa maumivu ya viungo, lakini mengi ya magonjwa hayo huhusisha kuvimba kwa viungo.

Virutubisho vya bromelaini, husaidia kuondoa maumivu katika sehemu ya chini ya mgongo kama sawa na matibabu ya maumivu.

Kusaidia kinga ya mwili

Utafiti wa wiki tisa wa watoto wa shule ambao walikula kiasi cha wastani cha mananasi kila siku, walikuwa na hatari ndogo sana ya kuambukizwa virusi au bakteria kuliko wale ambao hawakula.

Mbali na hayo, wale waliokula kiasi kikubwa walipata mara nne ya idadi ya seli nyeupe za kinga za kupambana na maambukizi.

Nanasi pia kusaidia kurekebisha mfumo wa kinga, na linaweza kuwa bora kwa wale walio na kinga dhaifu za mwili.

Kusaidia mfumo wa moyo

Kwa mara nyingine tena, ni bromelain ambayo inaonekana kuwa na umuhimu kwa moyo na mfumo wa mzunguko wa damu, kwa kuzuia au kupunguza ukali wa mshtuko wa moyo.

Uchunguzi kwa wanyama unaonyesha bromelain pia huzuia shinikizo la damu, kuganda kwa damu kwa kuzuia utengenezwaji wa protini inayoitwa fibrin ambayo inahusika katika kuganda kwa damu.

Kupunguza hatari ya pumu

Juisi ya nanasi pia inaweza kuwa na ufanisi katika kupunguza dalili zinazohusiana na pumu. Katika utafiti wa wanyama, watafiti waligundua kuwa bromelain zinaweza kuwa na faida kwa watu wanaoishi na pumu.

Zaidi ya hayo, nanasi lina vitamini C, ambavyo hulainisha mirija ya mapafu. Na katika matukio ya mashambulizi ya pumu kutokana na baridi, vitamini C vilikuwa ya manufaa

Nanasi ni salama kwa kila mtu?

Kama huna mzio na nanasi, kwa ujumla inatambulika kuwa nanasi ni salama kwa watu wengi na ni sehemu ya lishe bora.

Hata hivyo, kula au kunywa kiasi kikubwa kunaweza kusababisha shida ya usagaji chakula. Jambo jingine ni kujiepusha kula nanasi ambalo halijaiva kwa sababu, linaweza kusababisha kuhara na kuwasha koo.

Zaidi ya hayo, ikiwa unakabiliwa la asidi ya reflux, nanasi linaweza kuongeza dalili zako. Asidi hiyo inaweza kusababisha kiungulia.

Wale wanaotumia dawa za kupunguza damu wanapaswa kukumbuka kwamba bromelaini iliyo katika nanasi inaweza kuathiri uwezo wa damu kuganda na inapoliwa kwa wingi, na kwa kushirikiana na dawa za kupunguza damu, inaweza kuongeza hatari ya kutokwa na damu.

Licha ya faida zake, ni muhimu kukumbuka kuwa juisi ya mananasi ina nyuzinyuzi kidogo lakini ina sukari nyingi sana.

Hii inamaanisha haitakuwa na uwezo wa kukujaza tumbo lako kama kula nanasi la kawaida la kiwango hicho hicho, lakini inaweza kusababisha uzito kwa baadhi ya watu.

Via:Bbc



0 Comment

Lishe bora kwa Watoto ni Ipi? Soma baadhi ya dondooAfyaclass Forum •

Kama mzazi, mahitaji ya lishe ya mtoto wako mchanga na mtoto aliyekuwa kidogo ni wazi kuwa ni kipaumbele, na ni rahisi kuhisi kulemewa na habari nyingi za mitandaoni.

Vyakula ambavyo mtoto hula katika miaka yao ya mapema vinaweza kuathiri tabia zao za ulaji baadaye maishani.

Kwa hiyo ni muhimu kuanzisha uhusiano mzuri na chakula tangu umri mdogo. Mtoto wako anapoanza kula vyakula vigumu.

Ili kuhakikisha mahitaji ya virutubishi ya mtoto wako yanatimia, unapaswa kuzingatia milo mitatu kwa siku. Milo hii inapaswa kujumuisha vyakula kutoka kila moja ya vikundi vitano vikuu vya chakula.

Vyakula vya protini, kama vile samaki, nyama, mayai na kunde. Wanga, kama viazi na wali. Matunda na mboga za rangi tofauti. Maziwa na bidhaa za maziwa.

Miezi sita ya mwanzo

Katika miezi sita ya kwanza, maziwa ya mama au maziwa ya unga ya watoto, hutoa nguvu na virutubisho vingi kwa mtoto wako anavyohitaji hadi kufikia umri wa miezi sita.

Vitamini D ni moja ya virutubisho muhimu. Watoto wanaotumia maziwa ya unga kila siku hawana haja ya kuongeza virutubisho vya vitamin D, lakini watoto wanaonyonyeshwa pekee wanapaswa kupewa virutubisho hivyo.

Serikali ya Uingereza pia inapendekeza watoto wote wenye umri wa miezi sita hadi miaka mitano wapate nyongeza ya vitamini A, C na D kila siku.

Maziwa ya ng’ombe hayapendekezwi kama kinywaji cha kila siku kwa watoto wachanga kabla ya umri wa mwaka mmoja.

Protini ni muhimu kwa mtoto

Protini ni muhimu kwa ukuaji, ukuaji wa ubongo na kuifanya mifupa imara na yenye nguvu. Vinavyojenga protini ni asidi ya amino, ambayo lazima itoke kwenye chakula. Kuna asidi 20 tofauti za amino, tisa ni muhimu katika lishe ya mtoto.

Protini za wanyama – kama vile nyama, samaki, mayai, maziwa, mtindi na jibini – zina asidi zote tisa muhimu za amino na huchukuliwa kuwa muhimu zaidi kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto.

Protini za nafaka, kama vile maharagwe na kunde, huhesabiwa kuwa ni protini zisizo kamili, kumaanisha zinakosa moja au zaidi ya asidi muhimu ya amino na lazima zitumike na vyanzo vingine vya protini ili kutoa asidi zote zinazohitajika.

Serikali ya Uingereza inapendekeza kula samaki mara mbili kwa wiki, ikiwa ni pamoja na samaki wenye mafuta.

Mazao ya mashambani au yaliyosindikwa ni mazuri, lakini kumbuka kuwa mazao yaliyokaushwa na ya makopo huwa na chumvi nyingi.

Wanga kwa mtoto

Maelezo ya picha,Vyakula vya wanga ni muhimu kwa sababu ni chanzo muhimu cha nishati ya mwili na hutoa nyuzi nzuri kwa usagaji chakula.

Watoto wanahitaji wanga katika kila mlo – mkate, viazi, wali. Hata hivyo, watoto wadogo (hasa wale walio chini ya umri wa miaka miwili) wanaweza kupata ugumu wa kusaga aina za nafaka, na nyuzinyuzi zinaweza kuwafanya wajisikie kushiba haraka, hivyo kuhatarisha hamu yao ya kula.

Kidogo kidogo mpe wanga wenye nyuzi ili mfumo wa usagaji chakula wa mtoto wako uweze kukabiliana na nyuzinyuzi za wanga.

Vyakula vya wanga ni muhimu kwa sababu ni chanzo muhimu cha nguvu na hutoa nyuzi ambazo ni nzuri kwa usagaji chakula.

Matunda na mboga kwa mtoto

Matunda na mboga hutoa vitamini, madini na nyuzi. Inashauriwa kuanza kuwapa watoto baada ya umri wa miezi sita.

Saizi ya kutumikia inategemea umri, urefu na shughuli za mwili za mtoto, kwa hivyo hakuna sheria zilizowekwa. Njia rahisi ni kumpa kiasi ambacho kinafaa kwenye kiganja cha mkono wa mtoto wako.

Matunda yaliyokaushwa yanapaswa kupewa watoto pamoja na mlo mwingine badala ya kumpa kama yalivyo, kwani kiwango cha juu cha sukari kinaweza kusababisha kuoza kwa meno.

Vipi kuhusu maziwa?

Unapomnyonyesha mtoto wako, ni vyema kuendelea kumnyonyesha, ikiwa unaweza, ambayo itasaidia lishe yake wakati wa kumpa aina nyingine za chakula.

Maziwa yote na bidhaa za maziwa (ikiwa ni pamoja na maziwa, mtindi na jibini) ni chanzo muhimu cha kalsiamu na iodini, pamoja na vitamini A, D na B12.

Baada ya umri wa mwaka mmoja unaweza kumpa maziwa ya ng’ombe na inashauriwa kumpa maziwa mara mbili kila siku kama vile maziwa, jibini, mtindi au jibini.

Kwa watoto wenye umri wa mwaka moja hadi miwili, chagua maziwa yoyote, kwani ni muhimu kwa ukuaji na kupata vitamini muhimu.

Zaidi ya hayo, maziwa yenye mafuta kidogo huenda yasitoe kalori au vitamini vinavyohitaji. Unaweza kumpa maziwa yenye mafuta, ilimradi tu mtoto wako anakula aina mbalimbali za vyakula na kupata uzito kawaida.

Maziwa na bidhaa za maziwa zenye mafuta kidogo zina kalsiamu nyingi kama yale yaliyo na mafuta mengi, lakini maziwa yenye mafuta kidogo yanapaswa kuepukwa hadi mtoto wako atakapofikisha umri wa miaka mitano.

Inafaa kukumbuka kuwa mtindi wa viwandani mara nyingi hupakiwa na sukari, hivyo epuka mtindi wenye ladha. Badala yake, chagua mtindi wa asili.

Mafuta na sukari kwa mtoto

Ingawa watoto wanahitaji kiasi fulani cha mafuta ili kukua, haipendekezi kumpa kiasi kikubwa cha mafuta ya aina yoyote.

Siagi ni chanzo cha nishati ya mwili, muhimu kwa watoto wadogo ambao wanakua haraka na wanafanya kazi za kimwili.

Mafuta pia ni muhimu ili kuwezesha ngozi kupata vitamini fulani, ikiwa ni pamoja na vitamini A, D, E na K. Ni muhimu kwa kazi ya kinga na utendaji wa ubongo.

Mafuta yanapatikana katika samaki, karanga, mbegu na mafuta yao. Hata hivyo, karanga nzima na mbegu zinapaswa kuepukwa hadi mtoto wako awe na umri wa miaka mitano kutokana na hatari ya kupaaliwa.

Vinywaji laini, pipi, biskuti na keki – mara nyingi huwa na sukari nyingi. Ulaji wa vyakula vilivyoongezwa sukari, mafuta na chumvi nyingi kupita kiasi ni mojawapo ya sababu kuu zinazochangia unene wa kupindukia.

Vitafunio kwa mtoto

Ni muhimu kwa mtoto wako mdogo kula vitafunio vinavyofaa (sio kula mara kwa mara) ili kudumisha hamu yao ya kula.

Kadiri unavyomsaidia mtoto wako kujua wakati wa kula, ndivyo atakavyoweza kuamua ni chakula gani anachopaswa kula anapokua.

Wakati watoto wanapoomba chakula, angalia ili kuhakikisha kuwa hana kiu, kwani wakati mwingine huchanganyikiwa.

Matunda kama zabibu, ni chaguo zuri kwa watoto. Vilevile, kutafuna vitu kama karoti, tango au nyanya pia ni chaguo nzuri.

Juisi inaweza kuwa njia nzuri ya kuhimiza watoto kuongeza ulaji wao wa vitamini C, kwa mfumo wao wa kinga, uzalishaji wa nishati na kuzuia upungufu wa damu.

Lakini kula matunda bora kwa watoto (na meno yao) kuliko juisi. Hasa juisi zinazoongezwa sukari, ambayo ni vyema kupunguza kutumia. Kinachofaa zaidi ni kuyafanya maji kuwa kinywaji kikuu cha mtoto wako na usimzidishe glasi moja ndogo ya juisi safi ya matunda isiyo na sukari kwa siku.

Credits:Bbc

Lishe bora kwa Watoto ni Ipi? Soma baadhi ya dondoo
0 Comment

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwiliniAfyaclass Forum •

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwilini

By DK. SHITA SAMWEL

Upo uvumi wa miaka mingi duniani kuhusu ulaji maini na figo za ng’ombe, mbuzi na kuku kuwa una madhara kutokana na ogani hizo kufanya kazi ya kuondoa sumu mwilini.

Kiujumla minofu ya nyama ya wanyama wanaoliwa ni moja ya vyakula ambavyo huwa na virutubisho mbalimbali, ikiwamo protini nyingi, iliyo muhimu kwa afya zetu.

Katika nyama hiyo, moja ya sehemu ambazo zina virutubisho vingi zaidi kuliko unavyoweza kupata katika minofu ni ogani ya ini. Sehemu hii ina protini nyingi zaidi kuliko ile inayopatikana katika minofu.

Ini ni ogani kubwa kuliko nyingine ndani ya tumbo, lina kazi kubwa na muhimu katika mwili, ikiwamo kuvunjavunja na kuchakata sumu, kemikali na dawa zenye usumu.

Vitu hivyo bila kuchakatwa na ini vikiingia katika mfumo wa damu na kusambaa maeneo mbalimbali ya mwili moja kwa moja zinaweza kudhuru.

Hapa unapata picha kuwa ini inafanya kazi hiyo tu, halifanyi kazi ya kuzihifadhi sumu hizo. Kazi hiyo ambayo kitabibu hujulikana kama detoxication.

Ikiwa utakula kitu chenye sumu au hata dawa lazima itapita katika ini, itavunjwa vunjwa hatimaye kufifishwa au kuondolewa sumu, aidha kwa kubadilishwa kuwa katika hali isiyo na madhara.

Baadaye baada ya uchakataji huo huweza kufika katika figo, ambazo zenyewe huchuja damu na kuondoa takasumu na mabaki yasiyohitajika mwilini kwa njia ya mkojo.

Figo nayo ina kazi nyingi, lakini kazi kuu mbili huwa ni kuondoa takasumu mwilini na kuweka usawa wa maji na madini.

Mkojo unaotengenezwa na figo ni salama, ambao huhifadhiwa katika kibofu mpaka pale mwili utakapohisi haja. Mkojo umebeba sumu za urea na nyingine zinazokuwa sumu endapo tu zitabaki ndani ya mwili kwa kiwango kikubwa.

Na wenyewe siyo sumu unapokuwa nje ya mwili. Kwa hiyo ile imani potofu ambayo unaweza kuikuta mtaani au mitandaoni kuwa ulaji wa maini na figo si sahihi, hawana ufahamu wa kina juu ya kazi za ini na figo kisayansi.

Kama ini na figo zingekuwa zinahifadhi sumu, ina maana kuwa ulaji wake ungelikuwa si salama. Maana makali ya sumu hizo yangekuwa palepale na ingeliweza kumdhuru yule atakayekula ogani hizi.

Ini huwa na kazi nyingi mwilini, ikiwamo kuhifadhi viini lishe, uundwaji wa protini, kudhibiti sukari ya mwili, kudhibiti joto la mwili, kuzalisha nyongo ambayo inahusika kusaga vyakula vya mafuta.

Kutokana na kazi zake, ndiyo maana huwa limesheheni virutubisho vingi vyenye faida kubwa kiafya kwa mlaji, ikiwamo madini kama kopa, chuma, patasiamu na vitamini kama A, B na D.

Protini inayopatikana katika ini huwa ni nyingi, ikiwa katika ubora wa juu ukilinganisha na ile ya minofu.

Kwa upande wa madaktari wa mifugo, wanashauri kutokula mnyama mgonjwa au ambaye amekula kitu na kumfanya aumwe.

Ndiyo maana inashauriwa kula nyama ambayo imekaguliwa na mabwana afya, ambazo ndizo zinazouzwa katika masoko ya nyama au machinjio maalumu.

Ulaji wa figo na maini ni salama kwa sababu zinavunja vunja, kufifisha sumu na hatimaye kuziondoa mwilini. Ogani hizi hazihifadhi sumu yoyote mwilini. Ni salama kuliwa na ni chanzo kikubwa cha viinilishe.

 

Maini, figo chanzo kikuu cha viinilishe mwilini
0 Comment

Tafiti zote zinazohusu chakula na lishe kufanyiwa uchunguzi wa kimaabaraAfyaclass Forum •

Tafiti zote zinazohusu chakula na lishe kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara

Na. WAF – Dar Es Salaam

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepanga kuweka sharti kwa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwenye tafiti zozote nchini zinazohusisha masuala ya chakula na lishe katika Maabara ya Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC).

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Februari 20, 2024 wakati wa ziara yake ya kukagua na kuona kazi zinazofanywa na Taasisi ya Chakula na Lishe kwa upande wa Maabara iliyopo Mikocheni Jijini Dar Es Salaam.

“Tunampango wa kufanya uchunguzi wa kimaabara kwa mtu yeyote au shirika lolote linalofanya tafiti zinazohusu masuala ya chakula na lishe, lazima zithibitishwe na ushahidi wa kisayansi baada ya sampuli kuchukuliwa na kuletwa katika maabara hii, isiwe tu ni tafiti za kwenye makaratasi.” Amesema Waziri Ummy.

Waziri @ummymwalimu amesema maabara hiyo ya chakula na lishe ni moja ya maabara kubwa na zinazoaminika katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ambapo amefurahishwa na kazi wanazofanya ikiwa ni pamoja na kuja na ushahidi wa kisayansi.

“Lakini pia kuna utafiti ambao wameufanya na kushauri kwamba wataalamu wa Afya wanashauri na kuelekeza watoto wa umri chini ya miezi Sita wasipewe chakula kingine chochote zaidi ya maziwa na mama”. Amesema Waziri Ummy.

Maabara hiyo imegawanyika katika sehem Tatu ambayo ni maabara ya chakula (food chemistry) ambayo inafanya uchunguzi wa viinilishe (macro and micro nutrients), maabara inayofanya uchunguzi wa viashiria vya viini lishe mwilini (micronuient biomarkers), na maabara inayofanya uchunguzi wa hali ya lishe (body composition) ikiwa ni pamoja na kugundua kama chakula kimeharibika.

Mwisho, Waziri Ummy ametoa wito kwa Watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kufanya mazoezi, kupunguza matumizi ya sukari na chumvi ili kuepuka kupata magonjwa yasiyoambukiza kwa kuwa yamekuwa yakiongezeka kila siku.

Tafiti zote zinazohusu chakula na lishe kufanyiwa uchunguzi wa kimaabara
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD