Showing posts with label Mtanzania apoteza maisha Israeli. Show all posts
Showing posts with label Mtanzania apoteza maisha Israeli. Show all posts

Serikali ya Israel yatambua mwili wa mwanafunzi wa Tanzania aliyekuwa mateka GazaAfyaclass Forum •

Serikali ya Israel imethibitisha kuwa mwili wa marehemu Joshua Luito Mollel, mwanafunzi kutoka Tanzania aliyechukuliwa mateka katika Ukanda wa Gaza tarehe 7 Oktoba 2023, umetambuliwa rasmi.

Utambulisho huo umefanywa na Kituo cha Kitaifa cha Tiba ya Uchunguzi wa Vifo kwa ushirikiano na Polisi ya Israel na Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF).

Familia ya marehemu imejulishwa rasmi, na mwili wake umerejeshwa nchini Israel.

Serikali ya Israel imetoa salamu za rambirambi kwa familia ya Mulal na kwa familia zote za mateka waliopoteza maisha.

Serikali na Jeshi la Ulinzi la Israel wamesisitiza kuwa wanaendelea kufanya kila juhudi kuhakikisha kuwa miili ya mateka wote inarejeshwa kwa maziko yenye heshima.

Vilevile, serikali imeitaka Hamas kutekeleza makubaliano na kurejesha miili ya mateka waliobaki.

Wamesema hawatapumzika hadi kila mmoja arejeshwe nyumbani. via Bbc.

0 Comment

TANZIA: Mtanzania alietekwa nchini Israel Afariki duniaAfyaclass Forum •

TANZIA: Mtanzania alietekwa nchini Israel Afariki dunia

Mmoja kati ya wanafunzi wawili wa Tanzania waliotekwa na wapiganaji wa Hamas wakati wa uvamizi wao Israel amefariki.

Mmoja kati ya wanafunzi wawili wa Tanzania waliotekwa na wapiganaji wa Hamas wakati wa uvamizi wao Israel amefariki. Kulingana na taarifa kutoka kwa serikali ya Tanzania iliotumwa katika vyombo vya habari bwana Clemence Felix Mtenga , alikua hajulikani alipo tangu uvamizi wa wapiganaji wa Hamas nchini Israel mnamo tarehe saba mwezi Oktoba 2023.

TANZIA: Mtanzania alietekwa nchini Israel Afariki dunia
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD