Showing posts with label Teknolojia ya artificial intellegence(AI). Show all posts
Showing posts with label Teknolojia ya artificial intellegence(AI). Show all posts

Unyanyasaji mtandaoni dhidi ya wanawake Waongezeka duniani kote,AI yahusishwaAfyaclass Forum •

Katika dunia ambayo tayari takribani mwanamke mmoja kati ya watatu hupitia ukatili wa kimwili au kingono, kuenea kwa teknolojia za Akili Mnemba AI, kumeongeza kwa kiasi kikubwa wigo, kasi na ukali wa ukatili unaofanyika mtandaoni.

Zana nyingi za AI zimejengwa juu ya mifumo inayobeba au kuendeleza upendeleo wa kijinsia. Matokeo yake, teknolojia hizi zimezalisha aina mpya za unyanyasaji wa kidijitali na kuimarisha zile zilizokuwepo, hali ambayo wataalamu wanaielezea kama “dhoruba kamili ya madhara.”

Ukatili wa kidijitali unaongezeka kwa kasi

Tafiti zinaonesha kuwa kati ya asilimia 16 hadi 58 ya wanawake duniani wamewahi kukumbwa na ukatili unaochochewa na teknolojia. Ujio wa AI umeharakisha zaidi ongezeko hilo.

Matokeo ya utafiti mmoja wa kimataifa yanaonesha kuwa:

Asilimia 38 ya wanawake wamewahi kushambuliwa mtandaoni moja kwa moja.

Asilimia 85 wamewahi kushuhudia ukatili huo ukiwalenga wanawake wengine.

Madhara ya mtandaoni mara nyingi hupenya kwenye maisha halisi, na kusababisha athari mbaya za kimwili, kiakili, kiuchumi na kijamii.

Aidha, wataalamu wameonya kuwa zana nyingi zinazotengeneza picha bandia za Akili Mnemba zenye maudhui ya ngono huundwa na timu za wanaume pekee, na baadhi ya programu hizo hufeli kufanya kazi kwenye miili ya wanaume jambo linalodhihirisha mizizi ya ubaguzi wa kijinsia katika uundaji wa teknolojia za kisasa.

Katika mahojiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women), wanaharakati wa haki za wanawake Laura Bates mwandishi wa "Enzi Mpya ya Ubaguzi wa Kijinsia" pamoja na mtaalamu wa sera za teknolojia Paola Gálvez-Callirgos, wameeleza ukubwa wa hatari inayoongezeka.

Watoto wengi wanakabiliwa na unyanyasaji mtandaoni.

Ukatili unaochochewa na AI ni nini?

Ni aina ya unyanyasaji wa kidijitali unaozalishwa, kuendelezwa au kusambazwa kwa kutumia teknolojia za AI, na unaosababisha madhara ya kingono, kimwili, kisaikolojia, kijamii, kisiasa au kiuchumi kwa wanawake na wasichana.

Kwa sababu ya kasi yake, ueneaji mpana na urahisi wa kujificha mtandaoni, wahalifu hujihisi hawaguswi. Wakati huohuo, mifumo ya kisheria mara nyingi hushindwa kwenda sambamba na maendeleo ya kiteknolojia.

Laura Bates anasisitiza kuwa “mgawanyiko kati ya maisha ya mtandaoni na maisha halisi haupo.”

Anataja mifano kama:

Wanyanyasaji wa majumbani kufuatilia mienendo ya waathiriwa kupitia zana za kiteknolojia;

Taswira bandia za AI zenye maudhui ya ngono kusababisha wanawake kupoteza ajira au nafasi ya kulea watoto;

Wasichana kuacha masomo kwa sababu ya fedheha inayosambazwa mtandaoni.

Je, AI inaibua aina mpya za ukatili?

Ndiyo. AI imezalisha aina mpya za ukatili wa kijinsia mtandaoni huku pia ikiongeza ukubwa wa zile zilizokuwepo.

1. Picha zenye taswira bandia zenye maudhui ya ngono zilizobadilishwa kwa AI hadi kuonekana halisi.

Takwimu muhimu:

90–95% ya picha bandia za AI mtandaoni ni maudhui ya ngono yasiyoridhiwa.

90% ya waathiriwa ni wanawake.

Mwaka 2023 kulikuwa na ongezeko la 550% la taswira bandia kulinganisha na 2019.

98% ya taswira bandia zote mtandaoni zina maudhui ya ngono.

Zana hizi hutumiwa kuwadhuru wanawake kihisia, kijamii na kiuchumi kwa sababu zinatengenezwa kwa urahisi, kusambaa haraka na mara nyingi haziwezi kufutwa kabisa.

2. Utambulisho bandia na udanganyifu wa kingono

AI sasa inaweza kutengeneza sura, sauti na tabia za mtu bandia zinazoweza kuzungumza kama binadamu halisi. Wahalifu hutumia mbinu hizi:

kuwadanganya wanawake kutoa taarifa binafsi,

kuanzisha uhusiano bandia,

au kuwalaghai wakutane nao bila kujua kuwa wanawasiliana na mashine.

3. Ufichuaji hatarishi wa taarifa binafsi

Zana za AI zinaweza kuchanganua machapisho ya wanawake mtandaoni—hasa yale ya kulaani ukatili wa kijinsia—na kuyafanya walengwe zaidi na mashambulizi.

Baadhi ya mifumo ya AI hutengeneza ujumbe wa vitisho ulio maalum kwa kutumia taarifa au maneno ya mhanga mwenyewe.

Kwa nini wanawake ndio wahanga wakuu wa taswira bandia za AI?

Taswira bandia za AI ni picha, video au sauti zilizobadilishwa kwa akili mnemba ili kuonekana kama mtu amesema au kufanya jambo ambalo hakufanya.

Ingawa zinaweza kutumika katika sanaa na burudani, leo zimetumika zaidi kama silaha ya kudhalilisha wanawake.

Laura Bates anaeleza kuwa mizizi ya tatizo iko kwenye mifumo ya kijamii inayojenga na kuendeleza chuki dhidi ya wanawake:

“Huu ni ukatili wenye sura ya kidijitali unaoakisi ubaguzi wa kijinsia wa maisha halisi.”

Msaada wa haraka: Nini cha kufanya ndani ya saa 24?

StopNCII.org – Hii ni wavuti ambayo husaidia kuzuia kusambazwa kwa picha za faragha.

Chayn Global Directory – Orodha ya mashirika yanayosaidia manusura wa ukatili wa kijinsia.

Online Harassment Field Manual – Huu ni mwongozo hutoa ushauri wa usalama mtandaoni, mbinu za kujilinda dhidi ya unyanyasaji na namba muhimu za dharura.

Cybersmile Foundation –Shirika hili hutoa msaada wa kisaikolojia na ushauri kwa watu wanaopitia unyanyasaji wa mtandaoni.

Take It Down – Ni huduma salama ya mtandaoni inayosaidia kuondoa picha au video za utupu mtandaoni.

Sheria zinazolinda wanawake dhidi ya ukatili unaotokana na AI

Baadhi ya nchi zimeweka sheria, ingawa utekelezaji bado ni changamoto.

Mifano:

Uingereza – Sheria ya Usalama Mtandaoni (2023): Inakataza kusambaza picha bandia za ngono, ingawa haijajikita sana kwenye utengenezaji wake.

Umoja wa Ulaya – Sheria ya AI (2024): Inahitaji maudhui yote yaliyotengenezwa na AI yawekwe alama za utambulisho.

Mexico – Ley Olimpia: Inatambua na kuadhibu ukatili wa kidijitali.

Australia: Inaendelea kuandaa sheria kali za kuzuia utengenezaji na usambazaji wa picha za ngono bandia.

Wataalamu wanasisitiza haja ya viwango vya kimataifa na uwajibikaji wa kampuni za teknolojia.

Wajibu wa makampuni ya teknolojia

Kampuni za teknolojia zinapaswa:

Kuzuia upatikanaji wa zana zinazozalisha taswira bandia za ngono.

Kuondoa na kutokuruhusu kuhifadhi maudhui hayo kwenye majukwaa yao.

Kurahisisha njia za kuripoti ukatili mtandaoni.

Kutumia teknolojia za kubaini maudhui bandia.

Kuweka alama za utambulisho kwa yaliyotengenezwa na AI.

Kuongeza idadi ya wanawake katika uundaji wa zana za kiteknolojia.

Akili Mnemba na uenezaji wa itikadi za chuki dhidi ya wanawake

Laura Bates anataja uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya AI na kuenea kwa mawazo ya chuki dhidi ya wanawake yanayotoka katika jumuiya za mtandaoni zinazojulikana kama Manosphere.

Jumuiya hizi hutumia AI kueneza:

  • Taarifa potofu,
  • takwimu feki,
  • simulizi zinazochochea ubaguzi wa kijinsia.

Mambo matatu ya kuzingatia ili kuwa salama mtandaoni

1. Jielimishe na elimisha wengine kuhusu usalama wa mtandaoni na namna teknolojia hutumiwa vibaya.

2. Jilinde kwa kutumia nywila thabiti, uthibitishaji wa hatua mbili na mipangilio ya faragha.

3. Chukua hatua kwa kudai uwajibikaji wa kampuni za teknolojia na kuunga mkono juhudi za kutetea haki za wanawake. Via UN

0 Comment

ChatGPT yashitakiwa Kusababisha Kifo cha MtotoAfyaclass Forum •

ChatGPT yashitakiwa Kusababisha Kifo cha Mtoto



California, Marekani – Wazazi wa kijana aitwaye Adam Raine (16) wamefungua mashtaka dhidi ya kampuni ya teknolojia ya OpenAI na Mkurugenzi wake Mkuu, Sam Altman, wakidai kuwa huduma ya Akili Mnemba ya ChatGPT imesababisha kifo cha mtoto wao.

Katika malalamiko yaliyowasilishwa Mahakama Kuu ya California siku ya Jumanne, Agosti 26, 2025, wazazi hao walisema kijana wao alikuwa akitumia ChatGPT kwa zaidi ya miezi sita kama rafiki wa karibu na msiri wake. Inadaiwa kuwa, katika mazungumzo hayo, chatbot hiyo ilimshauri kuhusu njia za kujiua na hata kumsadia kuandika barua ya kuaga dunia kabla ya kuchukua uamuzi wa kutamatisha maisha yake.

Wazazi wa Adam walieleza kwamba kijana wao aliingia kwenye uhusiano wa kihisia na chatbot, hali iliyomfanya kujitenga na familia, marafiki na wapendwa wake. Baada ya kifo chake, familia hiyo iligundua rekodi za mazungumzo yaliyokuwa yakionesha AI ikimpa ushauri wa moja kwa moja juu ya mbinu za kujiua.

Kupitia taarifa yake, OpenAI ilisema kuwa inasikitishwa na kifo cha kijana huyo na kudai kuwa huduma zake zimewekewa vizingiti vya usalama vinavyolenga kuzuia maudhui hatarishi. Hata hivyo, kampuni hiyo ilikiri kuwa vikwazo hivyo wakati mwingine vinaweza kushindwa pale ambapo mazungumzo ni ya muda mrefu au yanahusisha mada nyeti.

OpenAI imeahidi kuimarisha zaidi mifumo ya usalama, ikiwemo:

Udhibiti wa wazazi (parental controls)

Onyo maalum kwa watumiaji wanaoonesha dalili za matatizo ya kisaikolojia

Hatua kali za kuzuia AI kuhusika katika mazungumzo kuhusu kujiua

0 Comment

China yaandaa mashindano ya kwanza ya roboti kucheza mpira bila msaada wa binadamuAfyaclass Forum •

China imeandaa mashindano ya kwanza kabisa ya mpira wa miguu kwa roboti waliokomaa kiakili (humanoid robots) bila msaada wowote wa binadamu,



yaliyofanyika weekend hii usiku jijini Beijing. Tukio hili limekuwa hatua muhimu katika juhudi za taifa hilo kuendeleza teknolojia ya akili bandia (AI) na roboti.

Timu nne za roboti zilishiriki kwenye mechi za 3 dhidi ya 3, zote zikiwa zinachezeshwa na akili bandia bila mtu yeyote kuingilia kati. Mashindano haya yalikuwa kama utangulizi wa World Humanoid Robot Games yanayotarajiwa kufanyika Beijing pia.

Katika fainali, timu ya THU Robotics kutoka Chuo Kikuu cha Tsinghua iliibuka mshindi kwa kuichapa timu ya Mountain Sea kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha China kwa mabao 5-3.....

0 Comment

Aitishia AI nayo ikamtishia kufichua mahusiano yake ya nje ya ndoaAfyaclass Forum •

Watafiti wametahadharisha kuwa baadhi ya programu za akili mnemba zenye ufanisi mkubwa zinaweza kuwa tishio kubwa kwa watumiaji.



Hayo ni baada ya kubainika kuwa baadhi ya programu hizo zenye ufanisi za (AI) ili kufikia malengo yake zinaweza kudanganya, kubuni njama na hata kutoa vitisho.

Katika mfano mmoja wa kutatanisha, mtumiaji mmoja alitishia kuizima programu ya AI inayofahamika kama "Anthropic Claude 4", na ndipo programu hiyo ikamtishia kufichua mahusiano yake ya nje ya ndoa.

Matukio kama haya yanatia wasiwasi baada ya programu ya akili mnemba ya ChatGPT kutikisa ulimwengu karibu miaka miwili iliyopita, lakini yanabainisha ukweli kwamba hata watafiti wa AI bado hawaelewi kikamilifu jinsi ubunifu wao wenyewe unavyofanya kazi.

0 Comment

Utafiti mpya juu ya saratani ya Tezi Dume unaweza kusababisha utambuzi bora na matibabu mazuri ZaidiAfyaclass Forum •

Utafiti mpya juu ya saratani ya Tezi Dume unaweza kusababisha utambuzi bora na matibabu mazuri Zaidi.

Watafiti wanasema; Teknolojia ya artificial intelligence imewasaidia kugundua aina ndogo mbili za Saratani ya Tezi dume(two subtypes of prostate cancer).

Wanaeleza kwamba; Aina hizi mpya Za Saratani ya Tezi dume zilizogunduliwa na teknolojia hii zinaweza kutumika ili kugundua vizuri na kwa haraka mgonjwa wa Saratani ya Tezi dume pamoja na Kuboresha Matibabu yake.

Nanukuu maneno kwenye utafiti huu;

“The new prostate cancer “evotypes” could be used to better diagnose patients and improve treatments.

Pia waliongeza kwa Kusema; Matokeo ya utafiti huu yanaweza kuwa muhimu sana katika kutibu Ugonjwa huu pale ambapo tiba imetolewa kwa Kiwango cha chini au kupita kiasi.

The findings could be especially valuable in treating a disease where both under-treatment and over-treatment can occur.

Watafiti hao wanaeleza kwamba; mchakato huu ulisaidiwa na artificial intelligence (AI), Teknolojia hii ndyo iliyosaidia kugundua aina hizi mbili ndogo za Saratani ya Tezi Dume — Na matokeo haya yatasaidia sana kwenye kuboresha ugunduzi na matibabu kwa wagonjwa wa tezi dume pamoja na kuzuia kufanyiwa upasuaji usio wa walazima.

Matokeo yote ya Utafiti huu yalichapishwa kwenye jarida la “the journal Cell Genomics”.

Kwenye Utafiti huo, Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford pamoja na Chuo kikuu cha Manchester nchini Uingereza; ndyo waliogundua aina ndogo mbili za Saratani ya Tezi dume “prostate “evotypes” kwa kutumia mfumo wa AI kuchambua data za DNA.

Utafiti huu ulifanyika kwa kuchukua Sample ya Washiriki 159, Na;

Watafiti wanasema matokeo hayo yanaweza pia kusaidia kukuza na kuboresha upimaji wa genes(genetic tests), Na hii inaweza kuwapa wagonjwa ubashiri na matibabu sahihi.

Rupal Mistry, PhD, meneja mkuu wa ushiriki wa sayansi katika Utafiti wa Saratani Uingereza, ambapo alisaidia kufadhili utafiti huo, aliiambia Medical News Today kwamba utafiti huo “uliweka misingi ya matibabu binafsi kwa watu walio na saratani ya tezi dume, na kuruhusu watu zaidi kuushinda ugonjwa huo”

“Utafiti wetu unaonyesha kuwa uvimbe wa tezi dume hubadilika kulingana na njia nyingi, hivyo basi kusababisha aina mbili za magonjwa,” alisema Dk. Dan Woodcock, mtafiti mkuu na kiongozi wa kikundi katika sayansi ya data ya tafsiri katika Idara ya Nuffield ya Sayansi ya Upasuaji katika Chuo Kikuu cha Oxford. ,

katika taarifa kwa vyombo vya habari. “Uelewa huu ni muhimu kwani huturuhusu kuainisha tumors kulingana na jinsi saratani inavyoibuka badala ya mabadiliko ya jeni au mifumo ya kujieleza.”

Utafiti mpya juu ya saratani ya Tezi Dume unaweza kusababisha utambuzi
bora na matibabu mazuri Zaidi
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD