Showing posts with label VVU. Show all posts
Showing posts with label VVU. Show all posts

Si Kila Mtu mwenye Mkanda wa Jeshi,Basi ana UKIMWIAfyaclass Forum •

Mkanda wa Jeshi,chanzo,dalili na matibabu yake

Fahamu kuhusu Mkanda wa Jeshi, maana yake,chanzo,dalili,pamoja na matibabu yake,kupitia makala hii.

Mkanda wa Jeshi

Mkanda wa Jeshi ni tatizo linalohusu maambukizi ya Virusi(Viral Infection) ambayo hutokana na reactivation ya varicella-zoster virus,

Tatizo hili la Mkanda wa Jeshi kwa jina lingine hujulikana kama Herpes zoster au Shingles.

Dalili za Mkanda wa Jeshi

Tatizo la Mkanda wa Jeshi huweza kuhusisha maumivu pamoja na uwepo wa vipele kwenye eneo flani yaani self-limited dermatomal rash,

Na mara nyingi mkanda wa jeshi huanza na maumivu kwenye eneo lililoathiriwa na virusi hawa,

ambapo huambatana na kuanza kujitokesha mabadiliko ya ngozi kwenye eneo hilo ndani ya siku 2 mpaka 3.

Mkanda wa jeshi ni jina linalotumika sana mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili.

Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.

Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto.

KUMBUKA: SIO KILA MWENYE MKANDA WA JESHI NI MUATHIRIKA WA UKIMWI

Watu ambao wapo kwenye hatari ya Kupata Mkanda wa Jeshi

‣ Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa,

Mfano; watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50,

utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi.     

‣  Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI na saratani.

‣ Tiba za mionzi na chemotherapy huweza kupunguza kinga ya mwili kwa mgonjwa na kumfanya awe kwenye hatari kubwa ya kupata mkanda wa jeshi.

Matibabu ya Mkanda wa Jeshi

Matibabu ya mkanda wa Jeshi ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya antiviral medications.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je,Mkanda wa Jeshi ni kiashiria kwamba una maambukizi ya Virusi vya Ukimwi?

Jamii imezoea kwamba Kila Mtu mwenye Mkanda wa Jeshi ni muathirika wa Ukimwi, ifahamike kwamba SIO KILA MWENYE MKANDA WA JESHI NI MUATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI,

mtu yoyote huweza kupata mkanda wa jeshi(herpes zoster/shingles) au maambukizi ya Varicella-Zoster Virus.

Ingawa Mkanda wa jeshi huweza kuwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI, saratani n.k.

Hitimisho

Ni munimu kufahamu kuhusu dalili za mkanda wa jeshi,ili zikianza kujutojeza upate msaada wa haraka zaidi,

Dalili za Mkanda wa Jeshi ni pamoja na;

Mkanda wa jeshi ni jina linalotumika sana mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili.

Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.

Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya LenacapavirAfyaclass Forum •

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya Lenacapavir

Shirika la Afya Duniani, WHO linatoa wito kwa serikali na washirika kutanua upatikanaji wa tiba mpya zilizoidhinishwa ikiwa ni pamoja na tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kupitia dawa ya Lenacapavir.

UN yasema kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa kumetatiza juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya HIV.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wanakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa, pamoja na kukwama kwa juhudi za kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Wakati huo huo, amesema kuna fursa kubwa muhimu na tiba mpya zenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa janga la Virusi Vya Ukimwi.

Ghebreyesus ameongeza kusema kupanua ufikiaji wa tiba kwa watu wanaokabiliwa na hatari zaidi ya maambukizi ya VVU kote duniani lazima liwe suala la kipaumbele kwa serikali zote na washirika.

WHO yahimiza mwelekeo wa pande mbili kukabiliana na VVU

Kwa kuadhimisha Siku hii ya UKIMWI Duniani chini ya kaulimbiu ''Kutokomeza janga, kubadilisha hatua dhidi ya UKIMWI"  WHO inahimiza mwelekeo wa pande mbili wa mshikamano na uwekezaji katika uvumbuzi ili kulinda na kuhamasisha jamii zilizo hatarini zaidi.

Shirika hilo limesema baada ya miongo kadhaa ya mafanikio, muitikio wa kukabiliana na VVU bado uko katika njia panda.

Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu 

Tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV, dawa ya Lenacapavir (LEN).Picha: Nardus Engelbrecht/AP Photo/picture alliance

Katika hatua nyingine, Shirika la UNAIDS limetahadharisha kwamba tangu Marekani na washirika wengine walipopunguza ufadhili wa ghafla mwaka huu, mfumo wa ikolojia unaoendeleza tiba na juhudi ya kuzuia maambukizi ya VVU katika nchi nyingi umetikiswa .

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie Byanyima, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva nchini Uswisi kwamba kiliniki zimefungwa ghafla na maelfu ya wafanyakazi wa afya wamepoteza kazi zao ama mishahara huku huduma za kuokoa maisha, upimaji, matibabu na kinga zikiendelea kutatizwa.

Takwimu za UNAIDS kuhusiana na maambuziki ya VVU

Byanyima amesema katika nchi 13, idadi ya watu wanaoanza matibabu imepungua ikilinganishwa na mwaka 2024. Amesema Uhaba wa vifaa vya kupimia VVU na madawa umeripotiwa katika nchi zikiwemo Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa huduma za kinga ambazo tayari zilikuwa zinakabiliwa na matatizo kabla ya mgogoro ndizo zilizoathirika zaidi.

Akiwasilisha ripoti mpya ya shirika hilo la UNAIDS, Byanyima aliitaja kuwa yenye changamoto kubwa. Katika ripoti hiyo, UNAIDS imesema mnamo mwaka 2024 takriban watu milioni 1.3 waliambukizwa HIV

UNAIDS | Winnie Byanyima UNAIDS | Winnie Byanyima 

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie ByanyimaPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Idadi hiyo ilikuwa asilimia 40 chini ya ile ya mwaka 2010, lakini ni zaidi ya mara tatu ya inavyohitajika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kumaliza janga la UKIMWI  kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo pia imesema mwaka jana, takriban watu 630,000 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI, hili likiwa punguzo la asilimia 54 tangu 2010, na asilimia 15 tangu 2020.

Pia imebainisha kuwa mwaka jana, tayari watu milioni 9.2 kati ya zaidi ya milioni 40 wanaoishi na VVU duniani kote walikuwa hawapati matibabu. Byanyima ameonya ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa, inaweza kusababisha maambukizi mapya milioni 3.3 kufikia mwaka 2030.

0 Comment

Serikali yafichua idadi ya wakazi wa Lagos wanaoishi na VVUAfyaclass Forum •

Serikali ya Jimbo la Lagos imefichua kwamba takriban wakazi 160,000 wanaishi na Virusi vya UKIMWI (VVU) kwa sasa.

Wakala wa Kudhibiti UKIMWI wa Jimbo la Lagos ulitangaza hili wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wa Siku ya UKIMWI Duniani 2025 uliofanyika Alhamisi, Novemba 27. 

Akiwasilisha ripoti ya maendeleo ya jimbo hilo mbele ya waandishi wa habari huko Alausa, Ikeja, Afisa Mkuu Mtendaji wa LSACA, Dkt. Folakemi Animashaun, alisema takwimu hizo zinaonyesha makadirio ya hivi karibuni kuanzia Januari hadi Septemba 2025. 

"Kuanzia Januari hadi Septemba 2025, Jimbo la Lagos kwa sasa lina wastani wa wakazi 160,000 wanaoishi na VVU, ambapo watu 147,466 wanatumia matibabu ya kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI," alisema.

 Animashaun aliupongeza uongozi wa Gavana Babajide Sanwo-Olu, akibainisha kuwa msaada wake "unaimarisha mifumo yetu ya afya na mitandao ya jamii, kuhakikisha kwamba kila juhudi za kuzuia, kugundua, na kutibu VVU zinawezeshwa na kudumishwa."

0 Comment

Afrika Kusini kunufaika na chanjo mpya ya kupambana na VVUAfyaclass Forum •

Afrika Kusini taifa lenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI limeingia kwenye orodha ya nchi za kwanza kunufaika na chanjo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi, iitwayo Lenacapavir.

Chanjo hii itakayoleta mapinduzi katika sekta ya afya, inawalenga watu ambao bado hawajaambukizwa, lakini wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kupitia dawa hii, mtu atahitaji kuchoma sindano mbili tu kwa mwaka, kwani hulinda mwili dhidi ya virusi vya UKIMWI kwa kipindi cha hadi miezi sita.

Katika juhudi za kukomesha maambukizi mapya ya virusi vya  UKIMWI , serikali ya Afrika Kusini inapanga kuzindua rasmi dawa hii ya muda mrefu ambayo wataalamu wanasema inaweza kubadilisha mwelekeo wa mapambano dhidi ya virusi hivyo.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Dokta Aaron Motsoaledi, amefafanua kwamba chanjo hii haibadilishi tiba za walioathirika, bali inawalenga watu walio salama, lakini wako katika hatari ya kuambukizwa virusi hivyo.

''Hii si kwa ajili ya matibabu, bali ni kwa ajili ya kinga. Wale ambao tayari wanaishi na VVU wataendelea na tiba zao za sasa. Chanjo hii ni kwa wale ambao bado hawajaambukizwa, lakini wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, '' alisema Dokta Motsoaledi.

Katika majaribio ya kliniki, Lenacapavir imeonyesha matokeo ya kuvutia hasa miongoni mwa wasichana ambao ni wazazi , kundi ambalo linaongoza kwa maambukizi mapya barani Afrika.

''Katika majaribio, dawa hii ilionekana kuwa na ufanisi wa asilimia 100. Msichana yeyote anayepokea chanjo hizo mbili kwa mwaka anahakikishiwa ulinzi kamili dhidi ya kuambukizwa virusi vya UKIMWI, " alieleza Daktari huyo.

Kauli ya WHO kuhusu chanjo hiyo

Kwa upande wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Mkurugenzi Mkuu Tedros Adhanom Ghebreyesus, anasema mafanikio haya yanaweza kuwa hatua muhimu kuelekea kukomesha kwa UKIMWI barani Afrika.

''Japo tunakabiliwa na changamoto nyingi, chanjo hii yenye nguvu ya kinga inaweza kuisaidia Afrika Kusini kufikia lengo lake la kuumaliza UKIMWI,'' alisisitiza Ghebreyesus.

Kwa muda mrefu, hospitali nyingi nchini  Afrika Kusini  zimekuwa zikizidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa wa UKIMWI, huku wengi wao wakirudi wakiwa na hali mbaya baada ya kusitisha tiba. Ujio wa Lenacapavir unatarajiwa kupunguza mzigo huo, kwa kuwa watu wengi zaidi watafanikiwa kujikinga mapema kabla ya kuambukizwa.

Joseph Nkosi, mkaazi wa Pretoria anazungumzia umuhimu wa chanjo hii, ambapo anasema itasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

''Dawa hii itawasaidia sana vijana wa Afrika Kusini, na pia itasaidia kupunguza ongezeko la maambukizi mapya, '' alisema mkaazi mmoja wa mji wa Pretoria.

Cha kuvutia zaidi, ni kwamba chanjo hii ambayo hapo awali iligharimu dola elfu 28 za Marekani kwa mwaka, sasa itauzwa kwa dola 40 pekee, chini ya asilimia 0.1 ya bei ya awali. Hili limewezekana baada ya kampuni ya Gilead kutoa leseni za bure kwa wazalishaji wengine, kwa msaada wa mashirika kama Clinton Health Access Initiative na Taasisi ya Gates.

Chanjo inayoleta matumaini makubwa

Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa afya Barani Afrika Limakatso Lebina anasema, kwa sasa hii ndiyo dawa ya kwanza duniani yenye nguvu kubwa dhidi ya UKIMWI:

''Hii ndiyo mara ya kwanza kuona dawa ya  kinga dhidi ya VVU  inayotoa ulinzi wa asilimia 100 kwa wanawake waliochoma sindano. Wote waliotumia hawakuambukizwa, tofauti na wale waliotumia dawa za kumeza kila siku.''

Wataalamu wanasema chanjo hii inaweza kuwa ngao muhimu ya kinga kwa makundi yenye hatari kubwa kama vile wasichana walioko kwenye balehe, vijana wa kike, na wanaotumia dawa za kulevya kwa kujidunga.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI , UNAIDS, zaidi ya watu milioni 40 duniani wanaishi na virusi vya UKIMWI. Na iwapo hata asilimia 4 tu ya watu wataanza kutumia sindano hii, inaweza kupunguza hadi asilimia 20 ya maambukizi mapya duniani.

Kwa sasa, Afrika Kusini inasubiri kibali rasmi kutoka kweny Mamlaka ya Bidhaa za Afya, SAPRA, ili kuanza kutoa dawa hii hatua kwa hatua katika hospitali za umma.

0 Comment

Jinsi VVU vilivyoongezeka kwa zaidi ya 1000% katika taifa hili dogo la pasifikiAfyaclass Forum •

Jinsi VVU vilivyoongezeka kwa zaidi ya 1000% katika taifa hili dogo la pasifiki



Miaka Kumi: huu ni umri wa mtoto mdogo aliye na Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambaye Sesenieli Naitala aliwahi kumwona.

Alipoanzisha mtandao wa Survivor Advocacy Network huko Fiji mwaka 2013, yule mvulana bado hajazaliwa. Sasa yeye ni mmoja wa maelfu ya Wafiji ambao wameambukizwa virusi vinavyoenezwa kwa damu katika miaka ya hivi karibuni, wengi wao wakiwa na umri wa miaka 19 au chini, na wengi kupitia matumizi ya dawa za kujidunga kwa sindano.

"Wazee wengi wanaanza kutumia dawa," alisema Bi. Naitala, ambaye shirika lake hutoa msaada kwa wafanyikazi wa ngono na watumiaji wa dawa huko Suva, mji mkuu wa Fiji. "Yeye (yule mvulana) alikuwa miongoni mwa wale vijana walioshiriki sindano mitaani wakati wa Covid."

Katika miaka mitano iliyopita, Fiji taifa dogo katika Pasifiki Kusini lenye watu chini ya milioni moja limekuwa mahali ambapo mojawapo ya milipuko ya VVU yenye kuongezeka kwa kasi duniani imechukua kasi.

Mwaka 2014, nchi hiyo ilikuwa na watu wasiozidi 500 walio na VVU.

Kufikia 2024 idadi hiyo ilipanda hadi takribani 5,900 ongezeko la mara kumi na moja.

Mwaka huo huo, Fiji iliripoti visa vipya 1,583 ongezeko la mara kumi na tatu kulinganisha na wastani wake wa miaka mitano.

Kati ya hao, 41 walikuwa na miaka 15 au chini, ikilinganishwa na 11 tu mwaka 2023.

Takwimu kama hizo zilimfanya waziri wa afya na huduma za matibabu nchini humo kutangaza mlipuko wa maambukizi ya VVU mwezi Januari.

Wiki iliyopita, waziri msaidizi wa afya Penioni Ravunawa alionya Fiji inaweza kurekodi zaidi ya watu 3,000 walioambukizwa VVU ifikapo mwisho wa 2025.

"Hili ni janga la kitaifa," alisema. "Na haipunguzi."

BBC ilizungumza na baadhi ya wataalamu, mawakili na wafanyikazi walio mstari wa mbele kubaini ongezeko hilo la maambukizi ya virusi limetokana na nini.

Wengi walisema kwamba, kadiri uelewa wa jinsi VVU vinanavyozwa na unyanyapaa unavyopungua, watu wengi wamekuwa wakijitokeza na kupima.

Wakati huo huo, walibaini kuwa idadi kubwa ya watu wengi hawajajumuishwa kwenye takwimu rasmi, hii ikimaanisha kwamba kiwango cha halisi cha maambukizi kinaweza kuwa kikubwa zaidi kuliko hata idadi zilizovunja rekodi zinavyoashiria.

'Mke wangu anahofia unyumba, mimi naogopa kufa' - Athari za kufungiwa USAID15 Februari 2025

Hatua ya Trump kuondoa ufadhili; Wafanyakazi katika mashirika Tanzania wana siutafahamu5 Februari 2025

Agizo la Trump kusitisha usambazaji wa dawa za HIV ,TB na Malaria, ina athari gani Afrika?29 Januari 2025

Msingi wa mlipuko wa VVU Fiji ni kuongezeka kwa matumizi ya dawa, ngono isiyokuwa salama, kugawana sindano na "bluetoothing".

"Bluetoothing," pia huitwa "hotspotting", ni tabia ambapo mtumiaji wa sindano apiga dawa, kuvuta damu baada ya sindano, kisha kuinyunyiza katika mtu mwingine yule mwingine anaweza kufanya hivyo kwa mtu wa tatu, na kadhalika.

Kalesi Volatabu, mkurugenzi wa NGO Drug Free Fiji, amewahi kuona tukio hilo mwenyewe.

Mwezi Mei uliyopita, alipokuwa akitembea mapema asubuhi katika Suva kuwapa elimu na msaada watumiaji wa dawa mitaani, alipokuwa kwa kona, aliona kundi la watu saba au nane wakiwa wamekusanyika.

"Niliona sindano ikiwa na damu ilikuwa mbele yangu," anakumbuka. "Mwanamke huyo mdogo, tayari alikuwa amechomwa sindano na alikuwa anatoa damu na kisha umeona wasichana wengine, watu wazima, wakisubiri kuja kuchomwa kwa sindano hiyo.

"Sio sindano pekee wanazogawana wanashiriki damu pia."

Bluetoothing pia imeripotiwa huko Afrika Kusini na Lesotho, nchi mbili ambazo zina baadhi ya viwango vya juu vya VVU duniani.

Fiji, tabia hiyo imekuwa maarufu katika miaka michache iliyopita, kulingana na bi Volatabu na bi Naitala.

0 Comment

Dawa ya PrEP inavyotumika kuepuka maambukizi ya VVUAfyaclass Forum •

Dawa ya PrEP inavyotumika kuepuka maambukizi ya VVU

Dawa za Kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi Maarufu kama PEP AU PREP,

Pre-exposure prophylaxis (PrEP) ni dawa zinazotumiwa ili kuzuai maambukizi ya Virusi vya Ukimwi,

Dawa hizi zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa endapo tu zimetumiwa kama inavyotakiwa.

PrEP huweza kupunguza hatari ya mtu kupata maambukizi ya Ukimwi baada ya kufanya ngono isiosalama na muathirika wa Ukimwi kwa asilimia 99%.

PrEP hupunguza kabsa hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya kujichoma na sindano,kujikata na wembe ambao umetumiwa na muathirika wa Ukimwi na hatari zingine kama hizi

• PrEP hupungua ufanisi wake kabsa wa kufanya kazi kama umezitumia isivyo sahihi,

Hakikisha Unatumia Dawa hizi za PEP ndani ya Masaa 72 toka uwe kwenye hatari ya Kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

PrEP haziwezi kuzuia wewe kupata Magonjwa ya Zinaa(STDs), Hivo kujikinga na magonjwa kama haya bado Condom ni Njia ya kutumia na ni Salama kwako.

KUMBUKA: Kuna PreP na PEP,

Prep- Ni Pre-exposure prophylaxis, na unatumia kabla ya kuwa kwenye mazingira ya hatari

PEP- Ni post-exposure prophylaxis, na unatumia baada ya kuwa kwenye mazingira ya hatari

PrEP stands for pre-exposure prophylaxis.PEP stands for post-exposure prophylaxis.
As indicated by ‘pre’, you start to take it before you may be exposed to HIV.As indicated by ‘post’, you start to take it after a single event that may have exposed you to HIV.
0 Comment

Maambukizi ya VVU yapungua hadi asilimia 1.7% mkoani lindiAfyaclass Forum •

Maambukizi ya virusi vya ukimwi yamepungua kufikia asilimia 1.7 mkoa wa Lindi

Na. WAF – Lindi

Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI yamepungua katika Manispaa ya Mkoa wa Lindi kutoka asilimia 2 hadi asilimia 1.7 Mwaka 2023 ambayo imepelekea kufikia malengo ya 95-95-95 katika Mkoa huo huku viongozi wa Mkoa huo wametakiwa kutobweta waendelee kuchukua hatua kwa kutoa elimu.

Wazir @ummymwalimu amesema hayo jana Februari 29, 2024 akiwa katika ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Lindi baada ya kutembelea katika kituo cha Afya Mnazimmoja, kituo cha Afya cha Mjini, Zahanati ya Nachingwea pamoja na kutembelea Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi.

“Niwapongeze Mkoa wa Lindi Mmefikia malengo ya 95-95-95 ambapo asilimia 96 ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI wanajua kwamba wana maambukisi ya UKIMWI, asilimia 95 ya watu wenye maambukizi wapo kwenye dawa na katika asilimia hiyo 95 ya wanaotumia dawa Virusi vimefubazwa.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amewataka wananchi kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi, ulaji wa vyakula kwa kupungua chumvi nyingi, sukari nyingi na mafuta mengi ili kuepuka kupata magonjwa Yasiyoambukiza ikiwemo Kisukari.

“Miaka Mitano iliyopita huwezi kuona Kisukari, huwezi kuona shinikizo la juu la damu kwenye magonjwa matano yanayowasumbua Watanzania wengi.” Amesema Waziri Ummy

Waziri Ummy anatarajia kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Lindi leo Machi 1, 2024 baada ya kutembelea katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (Sokoine) pamoja na kuzungumza na Kamati ya Afya Ngazi ya Mkoa (RHMT)na Kamati ya Afya Ngazi ya Wilaya (CHMT)

Maambukizi ya VVU yapungua hadi asilimia 1.7% mkoani lindi
0 Comment

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damuAfyaclass Forum •

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na saratani ya damu.

Paul Edmonds, mwenye umri wa miaka 68, kutoka California ambaye alitrend kwenye vichwa vya habari vya kimataifa mnamo 2023 alipotoa hadithi yake, bado hana athari za hali zote mbili miaka mitano baada ya kupandikizwa seli ambazo ziliondoa magonjwa yote mawili mwilini.

Katika makala mpya ya timu ya madaktari waliomtibu, madaktari walisema alipona rasmi saratani na miaka miwili kabla ya kutangazwa kuwa amepona VVU.

Safari ya matibabu ya Edmonds ilianza alipogundulika kuwa na UKIMWI mwaka 1988, wakati ambapo virusi hivyo viliua wanaume wengi wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Licha ya kuwatazama marafiki zake wengi wakifa kutokana na maambukizo hayo, hakufa, na aliishi hadi utambuzi mbaya wa leukemia mnamo 2018 nusura ukatize matumaini yake ya kuishi maisha marefu.

Alitibiwa saratani hiyo kwa tiba ya seli shina, ambayo inahusisha kuchukua nafasi ya seli zilizoharibiwa na chemotherapy na zile zenye afya kutoka kwa wafadhili, wakati madaktari waliona fursa ya kipekee: kupata wafadhili na mabadiliko ya jeni yanayokinzana na VVU.

Madaktari walitaka kujua kama wanaweza kuiga mafanikio ya wagonjwa wa awali ambao walikuwa wameripotiwa kuponywa VVU na saratani kwa njia hii.

Kulingana na kliniki ya City of Hope huko California, Edmonds ni mmoja wa watano walioshinda magonjwa yote mawili na mtu mzee zaidi kufanya hivyo.

‘Ninashukuru sana… siwezi kuwashukuru vya kutosha,’ Bw Edmonds alisema kuhusu madaktari wake katika kliniki ya City of Hope huko California.

Kupandikiza seli shina ni sehemu ya mwisho ya matibabu ya saratani ya damu kama vile leukemia na lymphoma.

Inatolewa wakati seli za shina zinazounda damu kwenye uboho wa mgonjwa zimeuawa na mionzi au chemotherapy.

Mnamo Novemba 2018, Bw Edmonds alianza matibabu,Alihitaji raundi tatu ili kufikia hatua nzuri, ambapo katikati ya Januari 2019 alifanikiwa.

Mwezi uliofuata alipokea seli kutoka kwa wafadhili wake.

Seli shina alizopewa zilikuwa na nakala mbili za mabadiliko ya nadra ya kijeni inayoitwa CCR5 delta-3, ambayo huwafanya watu kuwa sugu kwa VVU. Asilimia moja hadi mbili tu ya watu wana mabadiliko haya.

VVU hutumia kipokezi CCR5 kuingia na kushambulia mfumo wa kinga, lakini mabadiliko ya CCR5 huzuia virusi kuingia kwa njia hii.

Inakadiriwa kuwa watu milioni 36.3 wamekufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI tangu kuanza kwa janga hilo mnamo 1981.

Mwanaume wa Marekani anakaribia kutangazwa kuwa ameponywa VVU na
saratani ya damu
0 Comment

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi hii hapaAfyaclass Forum •

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi.

Utafiti mpya waonyesha; Novel RNA nanomedicine kupunguza kuzaliana kwa virusi vya Ukimwi yaani HIV replication kwa asilimia 73%,

Mpaka sasa hakuna Tiba kamili ya kuponyesha kabsa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(HIV/AIDS), ingawa dawa zinazotumika kwa waathirika wa VVU husaidia kudhibiti dalili zake kwa kiwango kikubwa.

Soma Zaidi hapa; Dawa zinazotumika kwa waathirika wa HIV

Watafiti wa Kanada wamebuni njia mpya ya kutumia RNA kusaidia kupambana na VVU kwa kutumia tiba ya jeni yaani “gene therapy”.

Takwimu zinaonyesha; Kufikia mwaka wa 2022, takriban watu milioni 39 duniani kote wanaishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi, vinavyojulikana zaidi kama VVU.

HIV(VVU) ni virusi vinavyoshambulia mfumo wa kinga ya mwili na seli zake nyeupe za damu. Hii inafanya mtu kuwa Kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi na magonjwa mengine.

Mpaka Hivi sasa, hakuna tiba ya VVU. Madaktari wanaweza kutumia tiba ya kurefusha maisha (ART) ili kusaidia kudhibiti ugonjwa huo. Hata hivyo, bado si tiba kamili ya kuondoa kabsa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(VVU).

Sasa, watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Waterloo nchini Kanada wamebuni njia ya kutumia ribonucleic acid (RNA) kulingana na Chanzo Kinachoaminika ili kupambana na VVU kwa kutumia tiba ya jeni(gene therapy).

Utafiti huu umechapishwa hivi karibuni kwenye jarida la “The Journal of Controlled Release”.

Je, ni nini RNA hufanya kwenye VVU(HIV)?

Kwa utafiti huu, watafiti waliunda nanomedicine mpya iliyojazwa na vifaa vya kijeni inayoitwa RNAs ndogo zinazoingilia (siRNA)

“siRNA ilichaguliwa kama tiba inayoweza kutumika kwa sababu inaweza kuundwa ili kudhibiti udhihirisho wa jeni maalum katika mwili,” mwandishi mkuu wa utafiti Dk. Emmanuel Ho, profesa msaidizi katika Shule ya Famasia katika Chuo Kikuu cha Waterloo, alielezea Medical News.

“Faida za hii ni pamoja na uwezekano mdogo wa athari kwa kulinganisha na dawa za kawaida za molekuli ndogo.”

Kwa vile siRNAs zinaweza kuamuru ni jeni ipi au protini zipi zinaweza kuguswa au kuzimwa kwenye seli, watafiti waliripoti kuwa zilisababisha kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi(VVU) kwa asilimia 73%.

Zaidi ya hayo, dawa mpya ya nanomedicine ilisaidia kukabiliana na masuala yanayowasilishwa na VVU linapokuja suala la autophagy “mpango wa kuchakata tena” wa mwili ambapo hutumia tena sehemu za seli za zamani na zilizoharibiwa na pia husaidia mwili kuondokana na virusi na bakteria.

“Dawa za sasa za VVU huingilia mzunguko wa maisha ya virusi katika hatua tofauti, hivyo mchanganyiko wa dawa ni muhimu kukandamiza ukuaji wote wa VVU,”

“Ikiwa virusi vya UKIMWI vimezuiliwa kwenye seli iliyoambukizwa na seli itajiharibu yenyewe, basi virusi haviwezi kuzidi au kuzaliana mwili mzima na kuharibu seli muhimu za kinga, ziitwazo msaidizi wa T-cells.

Wakati chembe-saidizi za kutosha za T zinaharibiwa, mfumo wa kinga ya mtu hudhoofika na mtu anakuwa katika hatari ya kuambukizwa tena.”

Dk. Liu alisema pamoja na kwamba madaktari wanapata baadhi ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi, lakini hazijawa na nguvu nyingi na haziwezi kuzuia VVU peke yake.

“Dawa zenye nguvu zaidi za VVU kwa sasa ni zile zinazosimamisha mzunguko wa maisha ya virusi, lakini bado zina madhara ya muda mrefu, ingawa ni kwa kiasi cha chini sana kuliko dawa za VVU za kizazi cha kwanza.

Ikiwa dawa hii ya nanomedication itatumika kuzuia maambukizi ya VVU, inapaswa kusaidia katika kupunguza idadi ya maambukizi ya VVU ulimwenguni kote. Kuzuia VVU ni bora zaidi kuliko kujaribu kutibu wagonjwa ambao tayari wameambukizwa.

– Dk. Edward Liu, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza anasema; Bado kuna uhitaji unaoendelea wa matibabu mapya ya VVU,

Dk. Ho alisema kutokana na kukosekana kwa chanjo madhubuti ya VVU, tiba mpya za VVU bado zinahitajika.

“Matibabu ya sasa ya VVU husaidia kupunguza kiasi cha VVU mwilini, lakini kwa sasa hakuna tiba kamili,” alisema.

“Zaidi ya hayo, wagonjwa wengine wanaweza kupata aina za VVU zinazokinzana na dawa, na hivyo kufanya matibabu ya sasa yasiwe na matokeo.”

Tafiti za awali ziliripoti kuwa asilimia 10% ya watu wazima wanaoanza matibabu ya VVU wana ukinzani kwa aina ya tiba ya kurefusha maisha inayoitwa non-nucleoside reverse transcriptase inhibitors (NNRTSs)Chanzo Kinachoaminika kiliripoti.

Mbali na kupata UKIMWI, watu wenye VVU wako katika hatari kubwa ya magonjwa kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

RNA inaweza kusaidia kukulinda dhidi ya maambukizi ya VVU,Na Wanasayansi walitengeneza dawa mpya ya nanomedicine ili iweze kutumika kwa njia ya uke, kupunguza kuzaliana kwa virusi vya Ukimwi yaani HIV replication.

Dawa ya kupunguza kuzaliana kwa Virusi vya Ukimwi hii hapa
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD