Jinsi VVU vilivyoongezeka kwa zaidi ya 1000% katika taifa hili dogo la pasifiki
Miaka Kumi: huu ni umri wa mtoto mdogo aliye na Virusi Vya Ukimwi (VVU) ambaye Sesenieli Naitala aliwahi kumwona.
Alipoanzisha mtandao wa Survivor Advocacy Network huko Fiji mwaka 2013, yule mvulana bado hajazaliwa. Sasa yeye ni mmoja wa maelfu ya Wafiji ambao wameambukizwa virusi vinavyoenezwa kwa damu katika miaka ya hivi karibuni, wengi wao wakiwa na umri wa miaka 19 au chini, na wengi kupitia matumizi ya dawa za kujidunga kwa sindano.
"Wazee wengi wanaanza kutumia dawa," alisema Bi. Naitala, ambaye shirika lake hutoa msaada kwa wafanyikazi wa ngono na watumiaji wa dawa huko Suva, mji mkuu wa Fiji. "Yeye (yule mvulana) alikuwa miongoni mwa wale vijana walioshiriki sindano mitaani wakati wa Covid."
Katika miaka mitano iliyopita, Fiji taifa dogo katika Pasifiki Kusini lenye watu chini ya milioni moja limekuwa mahali ambapo mojawapo ya milipuko ya VVU yenye kuongezeka kwa kasi duniani imechukua kasi.
Mwaka 2014, nchi hiyo ilikuwa na watu wasiozidi 500 walio na VVU.
Kufikia 2024 idadi hiyo ilipanda hadi takribani 5,900 ongezeko la mara kumi na moja.
Mwaka huo huo, Fiji iliripoti visa vipya 1,583 ongezeko la mara kumi na tatu kulinganisha na wastani wake wa miaka mitano.
Kati ya hao, 41 walikuwa na miaka 15 au chini, ikilinganishwa na 11 tu mwaka 2023.
Takwimu kama hizo zilimfanya waziri wa afya na huduma za matibabu nchini humo kutangaza mlipuko wa maambukizi ya VVU mwezi Januari.
Wiki iliyopita, waziri msaidizi wa afya Penioni Ravunawa alionya Fiji inaweza kurekodi zaidi ya watu 3,000 walioambukizwa VVU ifikapo mwisho wa 2025.
"Hili ni janga la kitaifa," alisema. "Na haipunguzi."
BBC ilizungumza na baadhi ya wataalamu, mawakili na wafanyikazi walio mstari wa mbele kubaini ongezeko hilo la maambukizi ya virusi limetokana na nini.
Wengi walisema kwamba, kadiri uelewa wa jinsi VVU vinanavyozwa na unyanyapaa unavyopungua, watu wengi wamekuwa wakijitokeza na kupima.
Wakati huo huo, walibaini kuwa idadi kubwa ya watu wengi hawajajumuishwa kwenye takwimu rasmi, hii ikimaanisha kwamba kiwango cha halisi cha maambukizi kinaweza kuwa kikubwa zaidi kuliko hata idadi zilizovunja rekodi zinavyoashiria.
'Mke wangu anahofia unyumba, mimi naogopa kufa' - Athari za kufungiwa USAID15 Februari 2025
Hatua ya Trump kuondoa ufadhili; Wafanyakazi katika mashirika Tanzania wana siutafahamu5 Februari 2025
Agizo la Trump kusitisha usambazaji wa dawa za HIV ,TB na Malaria, ina athari gani Afrika?29 Januari 2025
Msingi wa mlipuko wa VVU Fiji ni kuongezeka kwa matumizi ya dawa, ngono isiyokuwa salama, kugawana sindano na "bluetoothing".
"Bluetoothing," pia huitwa "hotspotting", ni tabia ambapo mtumiaji wa sindano apiga dawa, kuvuta damu baada ya sindano, kisha kuinyunyiza katika mtu mwingine yule mwingine anaweza kufanya hivyo kwa mtu wa tatu, na kadhalika.
Kalesi Volatabu, mkurugenzi wa NGO Drug Free Fiji, amewahi kuona tukio hilo mwenyewe.
Mwezi Mei uliyopita, alipokuwa akitembea mapema asubuhi katika Suva kuwapa elimu na msaada watumiaji wa dawa mitaani, alipokuwa kwa kona, aliona kundi la watu saba au nane wakiwa wamekusanyika.
"Niliona sindano ikiwa na damu ilikuwa mbele yangu," anakumbuka. "Mwanamke huyo mdogo, tayari alikuwa amechomwa sindano na alikuwa anatoa damu na kisha umeona wasichana wengine, watu wazima, wakisubiri kuja kuchomwa kwa sindano hiyo.
"Sio sindano pekee wanazogawana wanashiriki damu pia."
Bluetoothing pia imeripotiwa huko Afrika Kusini na Lesotho, nchi mbili ambazo zina baadhi ya viwango vya juu vya VVU duniani.
Fiji, tabia hiyo imekuwa maarufu katika miaka michache iliyopita, kulingana na bi Volatabu na bi Naitala.
image quote pre code