WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya Lenacapavir

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya Lenacapavir

#1

WHO yatoa Wito dhidi ya upatikanaji wa tiba mpya za VVU ikiwemo dawa ya Lenacapavir

Shirika la Afya Duniani, WHO linatoa wito kwa serikali na washirika kutanua upatikanaji wa tiba mpya zilizoidhinishwa ikiwa ni pamoja na tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV kupitia dawa ya Lenacapavir.

UN yasema kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa kumetatiza juhudi za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya HIV.

Mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema wanakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na kupunguzwa kwa ufadhili wa kimataifa, pamoja na kukwama kwa juhudi za kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Wakati huo huo, amesema kuna fursa kubwa muhimu na tiba mpya zenye uwezo wa kubadili mwelekeo wa janga la Virusi Vya Ukimwi.

Ghebreyesus ameongeza kusema kupanua ufikiaji wa tiba kwa watu wanaokabiliwa na hatari zaidi ya maambukizi ya VVU kote duniani lazima liwe suala la kipaumbele kwa serikali zote na washirika.

WHO yahimiza mwelekeo wa pande mbili kukabiliana na VVU

Kwa kuadhimisha Siku hii ya UKIMWI Duniani chini ya kaulimbiu ''Kutokomeza janga, kubadilisha hatua dhidi ya UKIMWI"  WHO inahimiza mwelekeo wa pande mbili wa mshikamano na uwekezaji katika uvumbuzi ili kulinda na kuhamasisha jamii zilizo hatarini zaidi.

Shirika hilo limesema baada ya miongo kadhaa ya mafanikio, muitikio wa kukabiliana na VVU bado uko katika njia panda.

Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu Afrika Kusini, Cape Town 2024 | Kuzuia VVU na Lenacapavir katika Wakfu wa Afya wa Desmond Tutu 

Tiba mpya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya HIV, dawa ya Lenacapavir (LEN).Picha: Nardus Engelbrecht/AP Photo/picture alliance

Katika hatua nyingine, Shirika la UNAIDS limetahadharisha kwamba tangu Marekani na washirika wengine walipopunguza ufadhili wa ghafla mwaka huu, mfumo wa ikolojia unaoendeleza tiba na juhudi ya kuzuia maambukizi ya VVU katika nchi nyingi umetikiswa .

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie Byanyima, amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva nchini Uswisi kwamba kiliniki zimefungwa ghafla na maelfu ya wafanyakazi wa afya wamepoteza kazi zao ama mishahara huku huduma za kuokoa maisha, upimaji, matibabu na kinga zikiendelea kutatizwa.

Takwimu za UNAIDS kuhusiana na maambuziki ya VVU

Byanyima amesema katika nchi 13, idadi ya watu wanaoanza matibabu imepungua ikilinganishwa na mwaka 2024. Amesema Uhaba wa vifaa vya kupimia VVU na madawa umeripotiwa katika nchi zikiwemo Ethiopia na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Ameongeza kuwa huduma za kinga ambazo tayari zilikuwa zinakabiliwa na matatizo kabla ya mgogoro ndizo zilizoathirika zaidi.

Akiwasilisha ripoti mpya ya shirika hilo la UNAIDS, Byanyima aliitaja kuwa yenye changamoto kubwa. Katika ripoti hiyo, UNAIDS imesema mnamo mwaka 2024 takriban watu milioni 1.3 waliambukizwa HIV

UNAIDS | Winnie Byanyima UNAIDS | Winnie Byanyima 

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na Ugonjwa wa Ukimwi Winnie ByanyimaPicha: Salvatore Di Nolfi/KEYSTONE/picture alliance

Idadi hiyo ilikuwa asilimia 40 chini ya ile ya mwaka 2010, lakini ni zaidi ya mara tatu ya inavyohitajika kufikia lengo la Umoja wa Mataifa la kumaliza janga la UKIMWI  kama tishio la afya ya umma ifikapo mwaka 2030.

Ripoti hiyo pia imesema mwaka jana, takriban watu 630,000 walikufa kutokana na magonjwa yanayohusiana na UKIMWI, hili likiwa punguzo la asilimia 54 tangu 2010, na asilimia 15 tangu 2020.

Pia imebainisha kuwa mwaka jana, tayari watu milioni 9.2 kati ya zaidi ya milioni 40 wanaoishi na VVU duniani kote walikuwa hawapati matibabu. Byanyima ameonya ikiwa hali hiyo haitashughulikiwa, inaweza kusababisha maambukizi mapya milioni 3.3 kufikia mwaka 2030.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code