Showing posts with label ajali mbaya. Show all posts
Showing posts with label ajali mbaya. Show all posts

RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea SameAfyaclass Forum •

 DAR ES SALAAM;RAIS Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia ajali iliyotokea jana Same mkoani Kilimanjaro, huku akiwataka madereva waendelee kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani.

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya ndugu zetu 37 na majeruhi 30 kutokana na ajali ya barabarani iliyotokea jana jioni eneo la Sabasaba, Barabara Kuu ya Moshi - Tanga, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, kwa magari mawili kugongana na kuungua moto.

"Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka. Ninatoa salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Nurdin Babu, familia zote za wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki. Mwenyezi Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu.

“Kama ambavyo nilieleza Juni 27 katika hotuba yangu ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ajali za barabarani zimeendelea kugharimu maisha ya wapendwa wetu. Ninawasisitiza madereva kuendelea kuzingatia kwa umakini mkubwa sheria za usalama barabarani, na Jeshi la Polisi kuendelea kusimamia kikamilifu sheria hizo," ameandika Rais Samia kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii.

0 Comment

TANZIA: Watu 36 wafariki dunia kwa ajali wilayani Same,Magari yawaka motoAfyaclass Forum •

Ajali hiyo  imetokea leo Jumamosi  Juni 28,2025  ikihusisha basi la abiria kampuni ya Chanel One lililokuwa likitokea Moshi kwenda Tanga na Toyota coaster lilikuwa likitokea Same kwenda Moshi.



Same. Wakati shughuli ya uokoaji na uondoshaji wa miili ikiendelea katika eneo ambalo ajali ya basi la abiria la kampuni ya Chanel One na basi dogo aina ya Toyota Coaster yaliyogongana uso kwa uso na kuwaka  moto, watu 36 wamethibitishwa kupoteza maisha huku 23 wakijeruhiwa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi ambaye yupo eneo la tukio usiku huu amethibitisha huku akisema ni taarifa za awali.

"Miili iliyotolewa eneo la tukio mpaka sasa ni  36 na majeruhi 23 ambao wamekimbizwa hospitali na bado zoezi linaendelea,"amasema Kamanda Mkomagi 

Hata hivyo, taarifa kutoka eneo la tukio ni kwamba abiria waliokuwa wamepanda coaster kuja  Moshi mjini walikuwa wakienda kwenye sherehe ya harusi ambayo inafanyika katika ukumbi wa Kuringe hall, ambao upo Moshi mjini.



0 Comment

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali ARUSHAAfyaclass Forum •

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali iliyotokea Februari 25. 2024 katika eneo la Ngaramtoni mkoani Arusha
na kusababisha vifo vya watu 25 na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa.

Kwa sasa Apelo anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Arusha, Mount Meru ambapo ameishukuru Serikali kwa huduma nzuri za matibabu anazopatiwa hospitalini hapo.

Amesema kwa namna ajali hiyo ilivyokuwa na huduma alizopatiwa kama asingekuwa Tanzania angekuwa amekwishafariki dunia na kwamba ukarimu wa Watanzania ndio uliookoa maisha yake.

“Kwa ajali hii ningekuwa nchini kwetu tayari ningekuwa nimepoteza maisha, kwani kule bila kulipia huduma za matibabu hupatiwi huduma, lakini kwa Tanzania walivyo wakarimu na weledi wameweza kuokoa maisha yangu mpaka sasa naendelea vizuri na naweza kuongea,” Amesema raia huyo wa Togo

Apelo alikuja Tanzania kushiriki kwenye semina iliyokuwa ikifanyika mkoani Arusha, ambapo pia walikwenda kufanya utalii na walipokuwa wakirejea ndipo wakapata ajali.

Raia wa Togo ni miongoni mwa watu waliokuwemo katika ajali ARUSHA
0 Comment

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25Afyaclass Forum •

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25

Gari la Shule ya Mchepuo wa Kiingereza ya New Vision, likinyanyuliwa baada ya kugongwa na lori katika eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), wilayani Arumeru leo Jumamosi Februari 24, 2024 katika Barabara Kuu ya Arusha-Namanga

Ajali ilitokea Februari 24, 2024 eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), wilayani Arumeru ikihusisha magari manne.

Arusha. Idadi ya vifo vilivyotokana na ajali iliyohusisha magari manne eneo la Kibaoni (Ngaramtoni), Barabara Kuu ya Arusha-Namanga imeongezeka na kufikia 25, majeruhi wakiwa 21.

Ajali ilitokea Jumamosi Februari 24, 2024 ikihusisha lori na magari mengine madogo matatu.

Akitoa taarifa jana usiku katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Kamishna wa Polisi Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Awadhi Juma Haji amesema miongoni mwa waliofariki  wanawake ni 11, akiwamo mtoto mdogo wa kike na raia wa kigeni saba.

Ajali ilihusisha lori lenye namba za usajili KAC 943 H aina ya Mack lenye tela namba ZF 6778 mali ya kampuni ya KAY Construction ya Nairobi nchini Kenya.

“Idadi ya majeruhi ni 21 kati yao wanaume ni 14 na wanawake ni saba,” amesema.

Magari mengine yaliyopata ajali katika tukio hilo ni T 623 CQF aina ya Nissan Caravan, T 879 DBY aina ya Mercedes Benz Saloon na T 673 DEW aina ya Toyota Coaster mali ya shule ya mchepuo wa Kingereza ya New Vision.

Kuhusu chanzo cha ajali, amesema uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa ni kufeli mfumo wa breki wa lori, hivyo kusababisha liyagonge magari mengine yaliyokuwa mbele yake.

Amesema Jeshi hilo linaendelea kumsaka dereva wa lori hilo anayedaiwa kutoroka baada ya ajali.

Awali, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo alitaja idadi ya waliofariki kuwa ni 15 na kati yao raia wa kigeni walikuwa watatu.

Credits:Mwananchi.

Idadi waliofariki dunia kwenye Ajali Arusha yafika 25
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD