Showing posts with label magonjwa ya wanaume. Show all posts
Showing posts with label magonjwa ya wanaume. Show all posts

Uume kuvimba husababishwa na Nini?Afyaclass Forum •

Uume kuvimba husababishwa na Nini?

Uume kuvimba kunaweza kusababishwa na sababu mbalimbali, kulingana na hali ilivyo. Hizi ndizo Sababu kubwa;

1. Maambukizi ya Vimelea mbali mbali vya magonjwa

-Maambukizi ya bakteria au fangasi (hasa chini ya ngozi ya kichwa cha uume)

-Magonjwa ya zinaa kama 

  • kisonono, 
  • klamidia, 
  • au kaswende

Dalili Zake huambatana na maumivu, usaha, harufu mbaya au kuwashwa

2. Msuguano au jeraha

-Kujamiiana kwa nguvu au muda mrefu bila kuwa na hali ya ulainishi Ukeni au kuwa na Ukavu Ukeni

-Kujikuna au kuumia

Huweza kusababisha uvimbe wa muda na maumivu pia.

3. Tatizo la Allergy / mzio

-Dhidi ya Vitu kama Kondomu (latex)

-Sabuni, mafuta au dawa za kupaka

Huweza kuleta uvimbe pamoja na hali ya kuwashwa kwenye Uume

4. Hali ya Kuziba na maji kujikusanya eneo moja (Edema)

Maji kujikusanya kwenye ngozi ya uume

Mara nyingine huonekana bila maumivu makali,Lakini huweza kusababisha Uume kuvimba

 5. Tatizo la Phimosis au Paraphimosis

Hapa Ngozi ya kichwa cha uume hushindwa kurudi kawaida

Hali hii ni hatari ukichelewa kupata Tiba→ huhitaji Matibabu ya haraka sana.

6. Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI)

Wakati mwingine maambukizi kama ya UTI huweza kusababisha Uume Kuvimba pia pamoja na maumivu wakati wa kukojoa au Hisia ya kuwaka moto wakati wa kukojoa n.k.

MUONE DAKTARI HARAKA KAMA:

-Uume umevimba na una maumivu makali

- Kuna usaha unatoka au damu zinatoka

- Unapata homa

- Uume umevimba sana na ngozi imekaza

Hali imekaa zaidi ya siku 2–3 bila kupungua

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma pia hapa:

0 Comment

Madhara ya kupiga punyeto kwa vijanaAfyaclass Forum •

Madhara ya punyeto kwa Vijana,Soma Hapa Kufahamu ukweli wa Mambo

Tabia hii imekuwa ikiwaathiri Wanaume Wengi kwa hivi Sasa,Je unazifahamu athari au Madhara ya Punyeto?

Madhara ya kujichua/punyeto kwa mwanaume ni kushindwa kusimamisha uume muda mrefu. Hayo ndio madhara makubwa yanayowaletea wanaume wengi shida. …

Kufanya Punyeto , wengi wanatumia Mkono kuchua uume, kuminya uume kutafuta raha msisimko haraka haraka.

Kuminya uume kwa viganja vyako vya mkono au kugandamiza sehemu inapelekea kuua Neva (nerve) misuli na mishipa ya damu matokeo yake uume unakuwa hauna nguvu kutokana na misuli kuchoka na kujenga usugu Uume unakuwa mwembamba na kuwa sugu!.

Husababisha magonjwa kwenye tezi dume na njia ya mkojo

Kujichua mara nyingi kwa siku kunaweza kusababisha bakteria kupata nafasi ya kuenea kutoka mikononi hadi kwenye sehemu za siri, kisha kuongezeka, na kusababisha maambukizi ya njia ya mkojo, au tatizo la prostatitis sugu lenye dalili kama vile: 

  • kukojoa mara kwa mara wakati wa mchana, kuwasha sehemu za siri,n.k. 

Kujichua mara kwa mara na kusababisha damu kwenye mkojo ni jambo la nadra, lakini linaweza kutokea ikiwa unajichua kupita kiasi. Sababu kuu pia ni kutokana na kuvimba kwa sehemu za siri. 

Kwa kuongezea, "kujichua" mara nyingi na kusababisha kumwaga mara kwa mara kutaharibu figo, na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa figo.

Kupungua kwa ubora wa tendo la ndoa na uzalishaji(fertility)

Kujichua kwa muda mrefu hufanya iwe vigumu zaidi kwa sehemu za siri za kiume kutoa manii wakati wa tendo la ndoa, na kuhitaji msisimko mkali kutoka kwa mkono hadi kutoa manii. Kuanzia hapo, sehemu za siri huonekana kuwa na dalili nyingi hatari kama vile kutofanya kazi vizuri kwa uume au tatizo la upungufu wa nguvu za kiume au kutokuwa na nguvu za kiume.

Zaidi ya hayo, kujichua kupita kiasi kunaweza kupunguza idadi ya manii kwa nusu na kupunguza mwendo na uhai wa manii, na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa uwezo wa uzalishaji kwa Mwanaume.

Athari za Kisaikolojia

Kujichua kupita kiasi kunaweza kusababisha uraibu kwa urahisi, huku mawazo yakizunguka kila mara kuhusu ngono na kujifurahisha. 

Kujichua mara kwa mara kunaweza kuathiri vibaya mfumo mkuu wa neva na kusababisha dalili mbalimbali kama vile;

  • maumivu ya korodani, 
  • kupoteza kumbukumbu, 
  • na udhaifu wa mwili kwa Ujumla. 

Ikumbukwe kwamba tafiti nyingi kuhusu kujichua zimeonyesha kuwa watu walio na uraibu wa kujichua wana viwango vya chini vya umakini ikilinganishwa na wale wanaojichua mara chache.

Kupungua kwa Nia ya Mahusiano Halisi ya kimapenzi(au kupungua kwa hamu ya kufanya mapenzi na Mtu halisi)

Kujichua mara kwa mara kunaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya wanaume kufanya mapenzi na wenzi wao. Sababu kuu ni kwamba kujisisimua ili kupata raha kumekuwa tabia ambayo ni vigumu kuiacha. Hii inaathiri pakubwa furaha ya wanandoa, hasa wanandoa waliooana.

Madhara mengine ukikutana na mwanamke ukichomeka unamwaga mbegu za kiume hapo hapo na nguvu zinaisha mwili unahitaji upumzike kwanza.

 Mwili unazoea(condition action) pia na uume nao unazoea punyeto Ile raha mtu anayopata wakati wa kujichua ni ya kiwango cha juu sana kiasi kwamba hakuna kitu kingine ambacho kinaweza kuleta raha ya namna hiyo kwenye mazingira yake. Hii ndio inasababisha wengi kushindwa kuacha mchezo huo!

 PUNYETO

Kila kitu chenye faida basi kina hasara zake. Tabia hii ya kupiga puchu au punyeto hufanyika kwa watu wengi, huku ikichangiwa na sababu mbali mbali kama vile;

  • Kupenda kuangalia picha na video za ngono kila mara
  • Kukaa kwa muda mrefu pasipo kukutana na mwanamke kimwili
  • Hisia za kimapenzi zilizokithiri n.k.

MADHARA MENGINE YA KUPIGA PUCHU(punyeto) NI PAMOJA NA;

• Kuwa na shida ya kushindwa kujidhibiti na kuwahi kukojoa wakati wa mapenzi kabla ya mwenzako

• Kupungua kwa Nguvu za kiume, endapo tabia hii inafanyika kila siku

• Athari katika mishipa ya uume

• Kupatwa na uchovu wa mwili uliokithiri

• Kupatwa na shida ya maumivu ya kiuno au mgongo

• Kuweka kupata maumivu ya mishipa ya uume mara kwa mara

• Kupatwa na maumivu ya korodani kwa baadhi ya wanaume.

N.K

ANGALIZO; EPUKA Haya ili kuacha tabia hii

– Epuka kuangalia picha pamoja na video za ngono mara kwa mara

– Epuka kukaa na watu wenye tabia hii ya kupiga puchu kila mara

 ➡️ MADHARA YA KUFANYA PUNYETO(MASTERBATION)

Punyeto ni tendo la kutomasa uume ili kujisisimua kimapenzi hadi kufikia kileleni (climax). Pia ni tendo la kujitafutia ashiki binafsi hasa kwa kuchochea viungo vya uzazi.

MADHARA YA UFANYAJI MASTERBATION PUNYETO

huambatana na madhara makubwa ya kiafya na leo tutaangalia madhara kumi ya kujipa raha mwenyewe kwa kutumia muono wako au kwa jina Jingine “PULI”

1. punyeto humfanya mtu  awe mlegevu bila kuwa na nguvu kabisa mda wote kwani nguvu nyingi hutumika kwenye tendo hilo kuliko hata nguvu zinazotumika zinapokutana nyama kwa nyama.

2. Husababisha mwanamume kutoa mbegu haraka kipindi cha tendo la ndoa na mwanamke na kushindwa kumfikisha mwanamke kileleni…. (Premature ejaculation)

anaweza akajikuta akigusa tu “nanii” ndani ya dakika cha he mheshimiwa anatapika.

3. Ni moja ya chanzo Kikuu cha kupoteza nguvu za kiume, uume kusinyaa na kukosa nguvu kwa sababu ya kuharibu mishipa ya fahamu wakati MTU akijisugua katika kulitafuta bao.

4. Hupunguza idadi ya mbegu za kiume (low sperm count) hivyo ni mbaya sana kwa watu wanaotafuta mtoto.

5. Husababisha mtu kusahau sahau sana na kushindwa kufanya vitu kwa makini zaidi.

6. Huleta utumwa wa kifikra kwani ukishaanza huwezi kuacha kirahisi (addiction).

7. Punyeto husababisha mwanamke au mwanamume kukosa hamu kabisa na mwenza wake hivyo kuleta usumbufu kwenye mahusiano..

8. Punyeto ni chanzo kikuu cha ngono za jinsia moja shuleni na vyuoni ambazo huambukiza magonjwa ya Zinaa kama Gono, kaswende na Ukimwi kirahisi sana.

9. Husababisha msongo mkubwa wa. mawazo kwani mara nyingi kila umalizapo tendo hilo unajuta sana na kuapa kwamba hutorudia tena lakini ikifika mida Fulani “sabuni kama kawa”

10. Kijana kuondokwa na haja ya kuoa au kuolewa kwani anachokitaka anahis anakipata na kupelekea kushindwa kuandaa familia yake

Amua sasa kuacha mchezo huo mchafu

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Soma pia hii:

https://www.afyaclass.com/2024/06/madhara-ya-punyetosoma-hapa-kufahamu.html

Rejea Source:

  • https://www.vinmec.com/eng/blog/harm-of-masturbating-a-lot-en
  • https://avalclinics.com/blogs/side-effects-of-masturbation-in-male-daily/

2 Comment

Tatizo La Mwanaume Kuota Matiti,Mwanaume kuwa na MatitiAfyaclass Forum •

Tatizo La Mwanaume Kuota Matiti,Mwanaume kuwa na Matiti

Article written by: 
Dr.Ombeni Mkumbwa

Tatizo hili la Mwanaume kuota matiti(Gynecomastia) huhusisha kuongezeka kwa tishu ndani ya tezi za matiti ya Mwanaume, Na Uwiano usio sawa wa vichocheo(imbalance of the hormones) vya estrogen pamoja na testosterone ndyo sababu kubwa ya tatizo hili.


Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama Mwanamke..

SABABU ZA TATIZO HILI

➖ Chanzo Kikubwa cha Tatizo hili Ni Mvurigiko wa vichocheo vya Mwili ambapo Kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance.

Mvurugiko wa vichocheo mwilini (Hormonal imbalance) hausumbui wanawake tu kama tulivyozoea kusikia. Tatizo hili huweza kuwapata Na Wanaume pia

 Tatizo hili huanza kuonekana kwa ukubwa wake kadri umri wa mwanamme unapozidi kuongezeka kwa kuwa vichocheo vya kiume (Testosterone) hupungua huku vile vya kike (Estrogen) vikianza kuongezeka. 

Ndipo hali hii husababisha baadhi ya tabia za kike kuonekana kwa mwanaume,Mfano mwanaume kuota matiti,kuwa na hips n.k

Kwa siku za hivi karibuni,mambo haya pia yameanza kutokea kwa vijana walio na umri mdogo

DALILI ZA TATIZO HILI

-Mojawapo ya dalili za uwepo wa tatizo hili ni kuongezeka kwa ukubwa wa matiti ambayo wakati mwingine huanza hadi kutoa majimaji,

-uchovu usio na sababu maalumu,

-kuongezeka sana kwa uzito wa mwili (unene uliopitiliza) 

-pamoja na kupungua sana kwa hamu ya tendo la ndoa au hata kushindwa kulishiriki kikamilifu.

 Ni vizuri ukazifuatilia dalili hizi kwa umakini ili ukiziona upate Msaada wa haraka

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!


TATIZO LA MWANAUME KUOTA MATITI(gynecomastia)

Tatizo hili linatokea kwa Baadhi ya wanaume,na hata kupelekea Wanaume hao kuwa na Matiti kama Mwanamke.

Tatizo hili la Mwanaume kuota matiti(Gynecomastia) huhusisha kuongezeka kwa tishu ndani ya tezi za matiti ya Mwanaume, Na Uwiano usio sawa wa vichocheo(imbalance of the hormones) vya estrogen pamoja na testosterone ndyo sababu kubwa ya tatizo hili.

Tatizo hili la Gynecomastia linaweza kuathiri titi moja au yote mawili, na wakati mwingine ukubwa wa matiti hutofautiana kati ya titi moja na jingine hata kama yote yanaongezeka.

Kumbuka: Sio kila matiti yakiongezeka ni tatizo la Gynecomastia, Inaweza kuwa hali inayojulikana kama Pseudogynecomastia,

Pseudogynecomastia: 

Hali hii huhusisha kuongezeka kwa mafuta na sio tishu ndani ya matiti ya Mwanaume.

Dalili za Tatizo la Matiti kuongezeka(Gynecomastia) ni pamoja na;

- Mwanaume kuanza kupata maumivu ya matiti

- Matiti kuanza kuongezeka ukubwa

- Kuhisi hali ya msisimko wa tofauti kwenye matiti baada ya kuyasugua,kugusa au kuguswa na nguo n.k

Hakikisha unapata Matibabu haraka ikiwa;

  • Matiti yako yanavimba zaidi
  • Unapata maumivu ya matiti
  • Matiti yanaanza kutoa maji,usaha au damu
  • Unahisi kitu kigumu kwenye titi au matiti
  • Chuchu kuingia ndani
  • Ngozi kujikunja Zaidi n.k

Sababu Zinazoongeza hatari Zaidi ya Mwanaume kuota Matiti

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu zinazoongeza hatari Zaidi ya Mwanaume kupata tatizo hilo:

1. Mwanaume kufikia Umri wa balehe(Puberty).

2. Kuwa Mtu mzima Zaidi

3. Kuwa na tatizo la Uzito Mkubwa au Unene

4. Matumizi ya baadhi ya dawa jamii ya anabolic steroids hasa kwa Wanariadha

5. Kuwa na Matatizo mengine ya kiafya kama vile;

  • Magonjwa ya Ini
  • Magonjwa ya Figo
  • Magonjwa ya Tezi la Thyroid
  • Kuwa na Uvimbe(tumors)
  • Au matatizo mengine kama vile, Klinefelter syndromen.k
Chanzo cha Tatizo la Mwanaume kuota matiti

Kwa wanaume wakati wa kuzaliwa, mwili hutengeneza homoni ya kiume inayojulikana kama testosterone.  Pia hutengeneza kiasi kidogo cha homoni ya estrojeni.  Tatizo la Mwanaume kuota matiti au Gynecomastia Linaweza kutokea wakati kiasi cha testosterone katika mwili huwa kidogo ikilinganishwa na estrogen.  Kupungua huku kunaweza kusababishwa na hali ambazo hupunguza testosterone au kuzuia athari zake.  Au inaweza kusababishwa na hali zinazopandisha kiwango cha estrojeni.

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu ambazo huweza kuleta mabadiliko hayo kwa Mwanaume;

(1) Mabadiliko ya Vichocheo mwilini(Natural hormone changes)

Homoni za testosterone na estrojeni hudhibiti tabia zinazohusu jinsia ya mtu.  Testosterone hudhibiti sifa kama vile ujengaji wa misuli na nywele za mwili.  Estrojeni hudhibiti sifa zinazojumuisha ukuaji wa matiti.n.k

 Viwango vya estrojeni ambavyo viko juu sana au havina uwiano na viwango vya testosterone vinaweza kusababisha tatizo la Mwanaume kuota matiti au gynecomastia.

(2) Hali ya kuota Matiti toka utotoni(Gynecomastia in infants).

 Zaidi ya nusu ya watoto wa kiume huzaliwa na matiti yaliyoongezeka kutokana na athari za estrojeni wakati wa ujauzito.  Titi lililovimba kwa kawaida hupotea ndani ya wiki 2 hadi 3 baada ya kuzaliwa.

 (3) Hali ya kuota Matiti(Gynecomastia) wakati wa kubalehe.  

Gynecomastia inayosababishwa na mabadiliko ya homoni wakati wa kubalehe ni ya kawaida kwa kiasi fulani.  Mara nyingi, tishu za matiti zilizovimba hupotea bila matibabu ndani ya miezi 6 hadi miaka 2.

(4) Hali ya Kuota Matiti(Gynecomastia) kwa watu wazima.  

Takriban Asilimia 24% hadi 65% ya wanaume wenye umri wa miaka 50 hadi 80 hupata tatizo hili la kuota matiti yaani gynecomastia.  

Lakini watu wazima wengi walio na hali hiyo hawana dalili.

(5) Matumizi ya Dawa

Zipo baadhi ya Dawa ambazo huweza kuchangia uwepo wa tatizo la kuota matiti kwa Mwanaume yaani gynecomastia.  Mfano wa Dawa hizo ni pamoja na;

- Dawa jamii ya Anti-androgens ambazo hutumika kutibu matatizo kama Saratani ya Tezi dume(enlarged prostate and prostate cancer). Mfano wa dawa hizo ni pamoja na;
  • flutamide,
  •  finasteride (Proscar, Propecia)
  • spironolactone (Aldactone, Carospir).
- Dawa jamii ya Anabolic steroids na androgens

- Dawa kwa ajili ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi(Antiretroviral medicines). Mfano;
  •   efavirenz.
- Pamoja na dawa Zingine kama vile;
  •  Adderall.
  • Anti-anxiety medications, kama diazepam (Valium).
  • Dawa jamii ya Tricyclic antidepressants.
  • Dawa jamii ya Opioids,kutibu maumivu ya muda mrefu
  • Dawa kama omeprazole (Prilosec).
  • Matibabu ya Saratani,Chemotherapy n.k
  • Dawa za magonjwa ya moyo kama digoxin (Lanoxin) na calcium channel blockers.
  •  metoclopramide
(6) Unywaji wa Pombe 

Watu wengi hawafahamu kwamba,Unywaji wa Pombe kupita kiasi huongeza hatari ya Mwanaume kupata tatizo hili pia.

Recreational drugs, illegal drugs and alcohol
Substances that can cause gynecomastia include:

(7) Matumizi ya Dawa za Kulevyia

Hapa nazungumzia dawa mbali mbali za Kulevyia kama vile;
  • Marijuana.
  • Heroin.
  • Methadone (Methadose).
(8) Matatizo Mengine ya Kiafya;

Hali fulani za Kiafya zinazoathiri usawa wa homoni zinaweza kusababisha au kuhusishwa na tatizo la Mwanaume kuwa na matiti(gynecomastia).  Hali hizo ni pamoja na:

 • Tatizo la Hypogonadism

Matatizo ambayo hupunguza kiwango cha testosterone ambayo mwili huitengeneza yanaweza kuhusishwa na tatizo la Mwanaume kuota matiti gynecomastia.  Baadhi ya mifano ni ugonjwa wa Klinefelter na upungufu wa utendaji kazi wa tezi la pituitari.

• Kuzeeka.  

Mabadiliko ya homoni yanayotokea wakati wa kuzeeka yanaweza kusababisha tatizo la Mwanaume kuota matiti , hasa kwa watu ambao ni overweight,Yaani wenye Uzito mkubwa kupita kiasi.

 • Uvimbe.  

Vivimbe vingine vinaweza kutengeneza homoni zinazobadilisha usawa wa homoni za mwili.  Hii ni pamoja na uvimbe unaohusisha korodani, tezi za adrenal au tezi ya pituitari.

 • Tatizo la Hyperthyroidism.  

Katika hali hii, tezi ya thyroid hutoa kiasi kikubwa cha homoni ya thyroxine. Hali hii huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo la Mwanaume kuota matiti 

• Kushindwa kwa figo. 

 Takribani nusu ya watu wanaopata matibabu ya dialysis hupata tatizo la gynecomastia kutokana na mabadiliko ya homoni.

Hivo hali hii huweza kuongeza hatari ya kupata tatizo la Mwanaume kuota matiti 

  Kushindwa Kufanya kazi kwa Ini na tatizo la cirrhosis. 

 Mabadiliko katika viwango vya homoni kuhusiana na matatizo ya ini na dawa za kutibu tatizo la cirrhosis, Na pia huhusishwa na tatizo la Mwanaume kuota matiti.

• Utapiamlo na njaa. 

Wakati mwili haupati lishe ya kutosha, viwango vya testosterone hupungua.  Lakini viwango vya estrojeni vinabaki sawa.  Hii husababisha kutokuwa na usawa wa homoni, Na matokeo yake huongeza hatari ya Kupata tatizo la Mwanaume kuota matiti 

 • Bidhaa za mitishamba
 Mafuta mengine ya mimea yaliyotumiwa katika shampoos, sabuni au lotions yamehusishwa na tatizo la Mwanaume kuota matiti . 

 Hizi ni pamoja na mti wa chai au mafuta ya lavender.  Uwezekano huu ni kutokana na misombo katika mafuta ambayo inaweza kuiga estrojeni au kuathiri testosterone.

 Sababu zinazoongeza hatari ya Kupata tatizo la Mwanaume kuota matiti 

Sababu za hatari kwa gynecomastia ni pamoja na:

  1.  Kubalehe.
  2.  Umri mkubwa.
  3.  Unene kupita kiasi.
  4.  Matumizi ya anabolic steroids
  5.  Hali fulani za kiafya.  Hizi ni pamoja na ugonjwa wa ini na figo, ugonjwa wa tezi, ugonjwa wa Klinefelter na baadhi ya uvimbe.
 Madhara ya tatizo la Mwanaume kuota matiti(Gynecomastia)

Gynecomastia ina matatizo machache ya kimwili.  Lakini inaweza kusababisha wasiwasi wa afya ya akili kutokana na mabadiliko ya jinsi kifua kinavyoonekana.

Jinsi ya  Kuzuia tatizo la Mwanaume kuota matiti 

Sababu kadhaa za tatizo hili zipo ndani ya udhibiti wako, Hivo ukizingatia unaweza kupunguza hatari ya kupata tatizo la Mwanaume kuota matiti :

 ✓ Usitumie madawa ya kulevya.  Mifano ni pamoja na anabolic steroids, amfetamini, heroini na bangi.

 ✓ Punguza au kaa mbali na pombe, Hii Inasaidia kutokunywa pombe.  Ikiwa unakunywa, fanya kwa kiasi.  Hiyo ina maana si zaidi ya vinywaji viwili kwa siku kwa wanaume.

✓ Fanya mazoezi ya mwili na dhibiti Uzito wako wa mwili

✓ Usitumie dawa hovio pasipo maelekzo ya kina kutoka kwa Wataalam wa afya.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

Rejea Link:

  • https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/gynecomastia/symptoms-causes/syc-20351793
  • https://my.clevelandclinic.org/health/symptoms/16227-enlarged-male-breast-tissue-gynecomastia
  • https://emedicine.medscape.com/article/120858-overview
  • https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK430812/
  • https://www.nhs.uk/conditions/gynaecomastia/
  • https://www.webmd.com/men/what-is-gynecomastia

0 Comment

Ngozi ya korodani kuwasha na kuvimba chanzoAfyaclass Forum •

Ngozi ya korodani kuwasha na kuvimba ni tatizo linaloweza kusababishwa na mambo kadhaa.

Hapa chini ni sababu kuu, dalili, na cha kufanya

 Sababu Zinazowezekana ni pamoja na:

  1. Maambukizi ya fangasi (Fungal infection / Tinea cruris)

    • Kuwasha sana
    • Ngozi kuwa nyekundu au nyeupe
    • Harufu isiyo ya kawaida n.k.
  2. Mzio (Allergy)

    • Kutokana na matumizi ya Sabuni kali, detergent, manukato
    • Kondomu au mafuta ya kupaka n.k.
  3. Maambukizi ya bakteria

    • Ambapo huweza kuambatana na maumivu, uvimbe, au usaha
  4. Joto na jasho kupita kiasi

    • Kuvimba na kuwasha hasa kwa kuvaa nguo zinazobana Sana pamoja na kutokana na hali ya mwili kuzalisha jasho kupita kiasi.
  5. Magonjwa ya zinaa (STIs)

    • Magonjwa ya zinaa pia huweza kusababisha hali hii, hasa hasa Kama kuna vidonda, usaha, au maumivu wakati wa kukojoa
  6. Majeraha madogo au kujikuna sana

    • Husababisha ngozi kuvimba au kuwa kama imeungua
Dalili za Hatari 

Muone mtaalamu wa afya haraka kama kuna:

  • Maumivu makali ya ghafla
  • Kuvimba upande mmoja kwa kasi
  • Homa
  • Ute au usaha
  • Korodani kuwa ngumu au laini kupita kawaida
 Nifanye Nini Nyumbani?

✔️ Osha kwa maji safi, kausha vizuri
✔️ Vaa chupi za pamba (cotton), zisizobana
✔️ Epuka kujikuna
✔️ Usitumie krimu za steroid (kama Betnovate) bila ushauri wa daktari
✔️ Kama ni fangasi, krimu za antifungal zinaweza kusaidia

⚠️ Muhimu

Kama dalili zinaendelea zaidi ya siku 3–5, au zinaongezeka, ni lazima kumuona daktari kwa uchunguzi sahihi. Usijitibu kiholela.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Uume kusimama legelege,Uume kulegea,uume kulala chanzo na TibaAfyaclass Forum •

Uume kusimama legelege,Uume kulegea,uume kulala chanzo na Tiba

Uume kulegea na kusinyaa (kupungua ukubwa au kulegea misuli ya uume) inaweza kusababishwa na mambo mbalimbali ya kiafya au kisaikolojia. Sababu kuu ni:



1. Sababu za kiafya

  • Mzunguko wa damu hafifu – Shida za mishipa (atherosclerosis, shinikizo la damu, kisukari) hupunguza mtiririko wa damu kwenda uume.
  • Upungufu wa homoni – Kiwango cha chini cha testosterone kinaweza kusababisha uume kulegea na kusinyaa.
  • Matumizi ya dawa – Baadhi ya dawa za presha, depression, au usingizi huathiri nguvu za kiume.
  • Magonjwa sugu – Kisukari, magonjwa ya figo, ini au neva.
  • Ugonjwa wa Peyronie – Kuzalisha kovu kwenye uume husababisha kubadilika umbo, kusinyaa au maumivu.

2. Sababu za kisaikolojia

  • Msongo wa mawazo na wasiwasi
  • Msongo wa kijamii/kiafya (hofu ya kushindwa, matatizo ya kifamilia)
  • Unyogovu au depression

3. Sababu za mtindo wa maisha

  • Uvutaji sigara na pombe kupita kiasi – Huharibu mishipa ya damu.
  • Lishe duni na kutofanya mazoezi – Hupunguza afya ya mishipa na homoni.
  • Unene kupita kiasi – Hupunguza testosterone na kusababisha matatizo ya nguvu za kiume.

✅ Ushauri:

  • Angalia mtindo wa maisha (lishe bora, mazoezi, epuka sigara/pombe).
  • Fanya vipimo vya afya (sukari, shinikizo la damu, testosterone).
  • Ongea na daktari wa mfumo wa mkojo au afya ya uzazi (urologist).
  • Ikiwa ni ya kisaikolojia, msaada wa kisaikolojia na ushauri wa kimaisha husaidia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU NA TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD