Showing posts with label ugonjwa wa Malaria. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa Malaria. Show all posts

Kwanini Malaria hushambulia Zaidi Watoto,hasa walio chini ya Miaka 5?Afyaclass Forum •

Kwanini Malaria hushambulia Zaidi Watoto,hasa walio chini ya Miaka 5?

Malaria hushambulia zaidi watoto, hasa walio chini ya miaka 5, kwa sababu hizi kuu:

1. Kinga yao bado haijakomaa

Watoto wadogo hawajapata kinga ya kutosha dhidi ya vimelea vya malaria (Plasmodium).
Watu wazima katika maeneo yenye malaria mara nyingi hupata maambukizi mara nyingi na mwili hujenga kinga ya kiasi, watoto hawana hiyo.

2. Kinga kutoka kwa mama huisha mapema

Mtoto hupata kinga fulani kutoka kwa mama akiwa tumboni pamoja na kinga kutoka kwa maziwa ya mama hasa katika miezi3 ya kwanza, lakini huisha ndani ya miezi 6–9. Baada ya hapo mtoto hubaki katika hatari zaidi ya kupata malaria.

3. Miili yao hushindwa kupambana haraka

Kwa watoto:

  • Homa hupanda haraka
  • Vimelea huongezeka kwa kasi
  • Dalili huwa kali (degedege, upungufu wa damu)n.k.

Hii hufanya malaria iwe hatari zaidi kwao kuliko kwa watu wazima.

4. Wanang’atwa zaidi bila kutambua

Watoto:

  • Hulala bila kujifunika vizuri
  • Wakati mwingine hawalali ndani ya chandarua
  • Hawajui kujikinga na mbu

5. Upungufu wa damu na lishe

Watoto wengi hupata:

  • Upungufu wa damu
  • Utapiamlo

Hali hizi hupunguza uwezo wa mwili kupambana na malaria.

Kwa nini malaria ni hatari zaidi kwa watoto?

Kwa sababu inaweza kusababisha:

  • Tatizo la Malaria kali Zaidi (severe malaria)
  • Degedege
  • Kupoteza fahamu
  • Kifo kama haitatibiwa mapema
Njia bora za kuwalinda watoto
  • ✔️ Kulala chini ya chandarua chenye dawa
  • ✔️ Kuwahi hospitali mtoto akipata homa
  • ✔️ Kuondoa mazalia ya mbu nyumbani
  • ✔️ Kufuata chanjo za malaria pale zinapotolewa
0 Comment

Ugonjwa wa Malaria wazidi kuua Watoto duniani,WHOAfyaclass Forum •

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema Alhamisi kuwa watu takribani 610,000—wengi wao wakiwa watoto—wamefariki dunia mwaka 2024 kutokana na ugonjwa wa malaria.

Mbu ndio chanzo kikuu cha malaria ambayo inachangia ongezeko la vifo kote ulimwenguni

WHO imeonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa maambukizi kutokana na kuenea kwa dawa zisizo na ufanisi, mabadiliko ya tabianchi na kupunguzwa kwa ufadhili kwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ongezeko la visa na vifo limeripotiwa zaidi katika Ethiopia, Madagascar na Yemen, wakati nchi 47 zimetajwa kuwa hazikuwa na maambukizi ya malaria mwaka 2024. Idadi hiyo ya vifo imeongezeka kidogo ikilinganishwa na mwaka 2023, huku maambukizi mapya yakipanda kutoka milioni 273 hadi milioni 282 ndani ya mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria wa WHO, Daniel Ngamije Madandi, amesema kuongezeka kwa usugu dhidi ya dawa za malaria, kupungua kwa ufanisi wa viuatilifu vinavyotumika kwenye vyandarua, mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro isiyomalizika vyote vimechangia kuongezeka kwa maambukizi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Vifo vitokanavyo na malaria pia vimeongezeka

Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa kuongezeka kwa vifo katika kipindi cha 2015 hadi 2024 kunahusishwa na ongezeko la idadi ya watu, ambapo visa vya vifo vimepanda kutoka 59 hadi 64 kwa kila watu 100,000 waliokuwa katika hatari ya kuambukizwa. Hata hivyo, kiwango cha vifo kilipungua kidogo mwaka uliopita, kutoka 14.9 hadi 13.8 kwa kila watu 100,000.

Kwa upande wa ufadhili, WHO imesema uwekezaji katika kudhibiti malaria ulikuwa dola bilioni 3.9 mwaka 2024—chini sana ya lengo la zaidi ya dola bilioni 9 zinazohitajika.

"Ufadhili mdogo wa kukabiliana na malaria unaleta hatari ya kurejea kwa kasi kubwa kwa ugonjwa huu,” alisema Ngamije.

Ameongeza kuwa zana mpya na bora zaidi—ikiwemo matibabu, vipimo na chanjo—ni muhimu ili kuokoa maisha, na akazitaka serikali za nchi zilizoathirika kuchukua jukumu la kuhakikisha vinawafikia wananchi.

Mwezi Januari mwaka huu, Marekani ilitangaza kupunguza ufadhili wa misaada ya kimataifa, hatua ambayo WHO imeonya kuwa imeathiri kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya malaria na juhudi za kuokoa maisha.

0 Comment

Wagonjwa wa Malaria waliongezeka duniani 2024,WHOAfyaclass Forum •

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema ugonjwa wa malaria uliwaua takribani watu 610,000 duniani kote mwaka 2024.


Ripoti ya mwaka ya WHO kuhusu malaria iliyotolewa Alhamisi, imeeleza kuwa visa vya ugonjwa huo vimeongezeka zaidi nchini Ethiopia, Madagascar na Yemen.

Idadi hiyo ni juu kidogo ikilinganishwa na vifo vya 2023, huku maambukizi mapya yakipanda kutoka milioni 273 hadi takribani milioni 282.

Baada ya hatua kubwa kupigwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, mapambano dhidi ya malaria yamekuwa yakisuasua katika muongo mmoja uliopita.

Nchi kadhaa hazina malaria

Hata hivyo, nchi 47 zimethibitishwa kutokuwa na malaria.

Daniel Ngamije Madandi, Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria wa WHO, amesema watu wengi bado wanapoteza maisha kutokana na ugonjwa ambao unaweza kuzuilika na kutibika.

WHO imesema kuongezeka kwa maambukizi kunachangiwa na ongezeko la dawa zisizo na ubora wa kutibu malaria, mabadiliko ya tabianchi na kupungua kwa ufadhili.

0 Comment

Dalili kuu za Ugonjwa wa Malaria,Chanzo na TibaAfyaclass Forum •

Ugonjwa wa Malaria,chanzo,dalili,Madhara na Tiba yake

Malaria ni Ugonjwa ambao huwasumbua watu wengi na Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ambayo huongeza idadi ya Vifo hasa kwa nchi Zinazoendelea.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO); Ulimwenguni kote mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa visa vya malaria milioni 249 na vifo 608,000 vya malaria katika nchi 85.”

Malaria ni Ugonjwa Gani?

Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea vinavyojulikana kama Plasmodium.Vimelea hivi huenezwa na mbu jike aina ya anofelesi (anopheles). Lakini watu wengi huelewa kwamba malaria husababishwa na mbu. Mbu huyu husaidia katika usambazaji tu wa vimelea husika.

Aina ya vimelea ambavyo humdhuru binadamu kati ya vimelea vingi vya Plasmodium ni:

• Plasmodium Vivax

• Plasmodium Falciparum

• Plasmodium Malariae

• Plasmodium Oval

Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO); Ulimwenguni kote mwaka 2022, kulikuwa na wastani wa visa vya malaria milioni 249 na vifo 608,000 vya malaria katika nchi 85.”

Dalili za Ugonjwa wa Malaria

Fahamu kwamba,miongoni mwa dalili za mwanzoni kabsa kwa Ugonjwa wa malaria ni Mtu kuwa na Homa,maumivu ya kichwa na kuhisi baridi au mwili kutetemeka(fever, headache and chills).

Dalili za Ugonjwa wa Malaria kwa Mtu mara nyingi huanza ndani ya siku 10–15 za kuumwa na Mbu aliye na vimelea wa Malaria yaani infected mosquito.

Dalili zake zinaweza zisiwe kali kwa baadhi ya watu, hasa kwa wale ambao awali walikuwa na maambukizi ya malaria. Kwa sababu dalili zingine za malaria sio maalum au zinaweza zisieleweke kwa haraka, kupimwa mapema ni muhimu.

Baadhi ya maambukizi ya Ugonjwa wa malaria yanaweza kusababisha Ugonjwa mbaya na hata Vifo. Watoto wachanga, watoto chini ya miaka 5, wajawazito, wasafiri na watu wenye VVU au UKIMWI wako katika hatari kubwa zaidi.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za Ugonjwa wa Malaria;

1. Mwili kukosa nguvu na kuchoka kupita kiasi

2. Baadhi ya Watu kuwa na dalili za kuchanganyikiwa,kama Dalili kali Zaidi za Ugonjwa wa Malaria(severe symptoms).

Dalili Zingine Kali Zaidi ni pamoja na;

  • Kupata Shida ya Kupumua
  • Kukojoa Mkojo mweusi
  • Kuwa na manjano,ngozi na macho kubadilika rangi na kuwa manjano, kwa kitaalam jaundice n.k

3. Kupata Homa

4. Mwili kutetemeka na kuhisi baridi kali

5. Kupata Maumivu makali ya Kichwa Mara kwa Mara

6. Kupata maumivu ya misuli,joints pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

7. Kuhisi kichefuchefu na kutapika

8. Kuharisha

9. Kupata Maumivu ya Tumbo

10. Na baadhi ya Watu huanza kukohoa n.k

Watu wenye dalili kali za Malaria wanatakiwa kupata Msaada wa haraka Zaidi ili kuepusha kupata madhara Zaidi, Na matibabu ya mapema kwa Ugonjwa huu huzuia maambukizi kuwa mabaya Zaidi.

Maambukizi ya malaria wakati wa ujauzito pia yanaweza kusababisha kujifungua mtoto kabla ya wakati au kuzaliwa kwa mtoto mwenye uzito mdogo. Pia hata Vifo huweza kutokea katika kipindi hiki.

Madhara ya Ugonjwa wa Malaria(Complications)

Ugonjwa wa Malaria huweza kusababisha Vifo,  na Kwa mujibu wa shirika la Afya Duniani(WHO); inakadiriwa kuwa takribani asilimia 94% ya Vifo vyote vinavyotokana na Ugonjwa wa Malaria hutokea Africa — Hasa kwa Watoto wenye umri wa chini ya Miaka 5.

Na Vifo hivo vya Ugonjwa wa Malaria huweza Kutokana na  Madhara haya;

~ Malaria kuleta athari kwenye Ubongo(Cerebral malaria).   Ikiwa seli za damu zilizojaa vimelea huziba mishipa midogo ya damu kwenye ubongo wako (cerebral malaria), uvimbe wa ubongo wako au uharibifu wa ubongo unaweza kutokea. Malaria hii  inayoshambulia ubongo inaweza kusababisha kifafa na kukosa fahamu.

~ Matatizo ya Upumuaji(Breathing problems). Hii ni kutokana na Maji kuweza kujikusanya kwenye mapafu (pulmonary edema) kisha kukusababisha upate shida sana ya kupumua,

Haya pia huweza kuwa Madhara ya Ugonjwa wa Malaria.

~ Viungo vya Mwili kushindwa kufanya kazi(Organ failure). Malaria inaweza kuharibu figo au ini au kusababisha wengu kupasuka. Yoyote kati ya hali hizi inaweza kuhatarisha maisha.

~ Kusababisha Upungufu wa Damu(Anemia). Ugonjwa wa Malaria unaweza kusababisha usiwe na kiwango cha kutosha cha Seli nyekundu za damu yaani red blood cells, Hali ambayo huweza kuathiri pia usambazaji wa kutosha wa hewa ya Oxygen kwenye tishu mbali mbali za mwili.

~ Tatizo la Upungufu wa Sukari kwenye Damu(Low blood sugar). Aina kali za malaria zinaweza kusababisha sukari kuwa chini kwenye damu (hypoglycemia), Sukari kuwa chini sana kwenye damu inaweza kusababisha kukosa fahamu au kifo.

Pia Ugonjwa wa Malaria huweza kusababisha Madhara mengine makubwa ikiwemo;

  • Mtu kuchanganyikiwa
  • Madhara kwa mama mjamzito; Maambukizi ya malaria wakati wa ujauzito pia yanaweza kusababisha kujifungua mtoto kabla ya wakati au kuzaliwa kwa mtoto mwenye uzito mdogo. Pia hata Vifo huweza kutokea katika kipindi hiki.

Jinsi ya kuzuia maambukizi ya Malaria

1. Hakikisha unazuia mazalia ya mbu

Fyeka vichaka na ondoa madimbwi ya maji katika  maeneo yanayokuzunguka.

2. Zuia kung’atwa na mbu, Zipo njia mbali mbali ambazo huweza kutumika ili kuzuia kung’atwa na Mbu ikiwemo;

i. Matumizi ya vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu

ii. Matumizi ya dawa za kupulizia za kuua mbu majumbani

iii. Matumizi ya dawa za kupaka za kuua mmbu

3. Dawa za kuzuia malaria kwa kina mama wajawazito (IPT)

Sulfadoxine Pyrimethamine (SP) hutolewa kwa kina mama katika wiki ya 20 na wiki ya 36 ya ujauzito.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD