Ugonjwa wa Malaria wazidi kuua Watoto duniani,WHO

Ugonjwa wa Malaria wazidi kuua Watoto duniani,WHO

#1

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limesema Alhamisi kuwa watu takribani 610,000—wengi wao wakiwa watoto—wamefariki dunia mwaka 2024 kutokana na ugonjwa wa malaria.

Mbu ndio chanzo kikuu cha malaria ambayo inachangia ongezeko la vifo kote ulimwenguni

WHO imeonya kuhusu hatari ya kuongezeka kwa maambukizi kutokana na kuenea kwa dawa zisizo na ufanisi, mabadiliko ya tabianchi na kupunguzwa kwa ufadhili kwa nchi zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ongezeko la visa na vifo limeripotiwa zaidi katika Ethiopia, Madagascar na Yemen, wakati nchi 47 zimetajwa kuwa hazikuwa na maambukizi ya malaria mwaka 2024. Idadi hiyo ya vifo imeongezeka kidogo ikilinganishwa na mwaka 2023, huku maambukizi mapya yakipanda kutoka milioni 273 hadi milioni 282 ndani ya mwaka mmoja.

Mkurugenzi wa Mpango wa Kimataifa wa Kupambana na Malaria wa WHO, Daniel Ngamije Madandi, amesema kuongezeka kwa usugu dhidi ya dawa za malaria, kupungua kwa ufanisi wa viuatilifu vinavyotumika kwenye vyandarua, mabadiliko ya hali ya hewa na migogoro isiyomalizika vyote vimechangia kuongezeka kwa maambukizi katika nchi za Afrika zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara.

Vifo vitokanavyo na malaria pia vimeongezeka

Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa kuongezeka kwa vifo katika kipindi cha 2015 hadi 2024 kunahusishwa na ongezeko la idadi ya watu, ambapo visa vya vifo vimepanda kutoka 59 hadi 64 kwa kila watu 100,000 waliokuwa katika hatari ya kuambukizwa. Hata hivyo, kiwango cha vifo kilipungua kidogo mwaka uliopita, kutoka 14.9 hadi 13.8 kwa kila watu 100,000.

Kwa upande wa ufadhili, WHO imesema uwekezaji katika kudhibiti malaria ulikuwa dola bilioni 3.9 mwaka 2024—chini sana ya lengo la zaidi ya dola bilioni 9 zinazohitajika.

"Ufadhili mdogo wa kukabiliana na malaria unaleta hatari ya kurejea kwa kasi kubwa kwa ugonjwa huu,” alisema Ngamije.

Ameongeza kuwa zana mpya na bora zaidi—ikiwemo matibabu, vipimo na chanjo—ni muhimu ili kuokoa maisha, na akazitaka serikali za nchi zilizoathirika kuchukua jukumu la kuhakikisha vinawafikia wananchi.

Mwezi Januari mwaka huu, Marekani ilitangaza kupunguza ufadhili wa misaada ya kimataifa, hatua ambayo WHO imeonya kuwa imeathiri kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya malaria na juhudi za kuokoa maisha.

Changia Mada hapa(Reply)


image quote pre code