Showing posts with label ugonjwa wa kisukari. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa kisukari. Show all posts

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukariAfyaclass Forum •

Utafiti:Utapiamlo unaweza kusababisha aina mpya ya kisukari

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health unaonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina mpya ya ugonjwa wa kisukari unasababishwa na njaa.

Wataalamu wa afya wamependekeza kutambuliwa rasmi kwa aina hiyo mpya ya kisukari inayotokana na utapiamlo, hatua hiyo ya utambuzi itasaidia kupambana na ugonjwa huo katika nchi zinazoendelea zinazokumbwa na njaa na umaskini.

Utafiti uliochapishwa katika jarida la The Lancet Global Health, unaonesha zaidi ya watu milioni 25 duniani wanaishi na aina hii ya kisukari, ambayo huathiri zaidi vijana walio na umri chini ya miaka 30. Tofauti na aina nyingine za kisukari, aina hii haihusiani na unene bali na uzito mdogo unaosababishwa na ukosefu wa lishe bora.

Shirikisho la Kimataifa la Kisukari limeunga mkono pendekezo la kuitambua rasmi aina hii kama kisukari aina ya 5, licha ya kuwa aina ya 3 na 4 bado hazijapewa uhalali wa kisayansi.

Aina za kawaida za ugonjwa wa kisukari zinazojulikana, ni aina ya pili, kwa kimombo "DiabetesType two", ambayo husababishwa na hali ya mtu kunenepa sana au kuwa na uzito kupita kiasi na watu wazima mwili wa mgonjwa huwa sugu dhidi ya homoni ya insulin. Aina nyingine ni ile ya kwanza, kwa kimombo Diabetis Type one, ambayo hugundulika tangu utotoni, na ambayo hutokana na kongosho kushindwa kuzalisha insulin ya kutosha.

Awali, Shirika la Afya Duniani liliwahi kuainisha kisukari kinachohusiana na utapiamlo katika miaka ya 1980 na 1990, lakini utambuzi huo uliondolewa mwaka 1999 kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano ya kitaalamu.

Tangu wakati huo, tafiti mbalimbali zimeendelea kuonyesha uhusiano kati ya utapiamlo na kisukari, lakini bado haijafahamika wazi jinsi hali hiyo inavyosababisha ugonjwa huo. Aidha, haijulikani iwapo matibabu yak yanaweza kuwa ya kawaida ya kisukari  ambayo mara nyingi hulenga kupunguza uzito kama wanavyoshauriwa wagonjwa wa kisukari wengine wenye uzito mkubwa.

Wataalamu wanashauri kuwa njia bora ya kukabiliana na kisukari aina ya 5 ni kuimarisha juhudi za kupambana na njaa na umaskini. Wanapendekeza watu wapewe chakula cha bei nafuu chenye virutubisho vya kutosha kama vile dengu, kunde, nafaka zilizoongezwa mafuta na nafaka zenye virutubisho.

Ugonjwa huo wa kisukari aina ya 5 huathiri uzalishaji wa insulini mwilini, lakini si kwa kiwango kikubwa kama kisukari aina ya 1. Watafiti wanasema wagonjwa wengi wa aina hii wanatoka katika nchi kama Bangladesh, Ethiopia, India, Indonesia, Nigeria, Uganda, Pakistan na Rwanda.

0 Comment

Ukweli kuhusu lishe kwa wagonjwa wenye kisukariAfyaclass Forum •

Wengi huamini kuwa mtu mwenye kisukari haruhusiwi kula vyakula fulani kabisa.



Katika jamii nyingi, suala la lishe kwa mtu mwenye kisukari limezungukwa na taarifa nyingi zinazochanganya.

Wengi huamini kuwa mtu mwenye kisukari haruhusiwi kula vyakula fulani kabisa.

Wengine hufikiri lazima ale chakula maalum kinachopatikana kwa gharama kubwa, huku baadhi wanamini mtu mwenye kisukari hawezi tena kufurahia mlo wa kawaida kama wengine.

Ukweli wa kisayansi na kimaisha ni tofauti kabisa na dhana hizi potofu, ambazo zikiendelea kushamiri, huongeza hofu, unyanyapaa na hata kuchangia utapiamlo miongoni mwa watu wanaoishi na kisukari.

Ni muhimu kuelewa kwamba lishe sahihi ni msingi wa udhibiti wa kisukari. Hata hivyo, lishe hii si ya kifahari kama wengi wanavyoamini. 

Kanuni kuu ni kula chakula chenye uwiano sahihi na virutubisho, wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji ya kutosha. Kinachobadilika kwa mtu mwenye kisukari ni umakini wa ulaji wa wanga na muda wa kula. 

Wengi wanaamini kuwa mtu mwenye kisukari hatakiwi kula wanga kabisa. Watu wengi hudhani wanga kama wali, ugali, viazi au mihogo ni marufuku. Ukweli ni kwamba mwili unahitaji wanga kwa ajili ya nishati. Kile kinachoshauriwa ni kuchagua wanga wenye nyuzinyuzi nyingi kama vile ugali wa dona, viazi,maboga, mihogo au viazi vitamu kwa kiasi kinachodhibitiwa.

Jamii nyingi huamini kuwa mtu mwenye kisukari akila matunda, anajihatarisha zaidi. Hili pia si sahihi. 

Matunda ni sehemu muhimu ya lishe bora, lakini ni lazima kuchagua matunda yenye sukari ya wastani kama papai, chungwa, embe, tufaa  na matunda mengine ila ulaji wake pia uwe ni wa kiasi sahihi.

Wengine wanamini kuwa mtu mwenye kisukari haruhusiwi tena kula chakula chochote kwenye sherehe na kushiriki hafla.

Hili husababisha unyanyapaa na kuwafanya wengine kuwaona wagonjwa wa kisukari kama watu wasioweza kufurahia maisha. 

Ukweli ni kwamba mtu mwenye kisukari anaweza kula chakula chochote, ila anapaswa kufanya uamuzi ambao hautaweza kupandisha viwango vya sukari.

Changamoto inayochangia upotoshaji huu ni ukosefu wa elimu sahihi kuhusu kisukari. Watu wengi wanategemea taarifa kutoka kwa marafiki, mitandao ya kijamii au kusikia habari za mtaani badala ya kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa lishe na madaktari.

Kisukari si hukumu ya kuishi maisha ya kula kwa mashaka au kuachana na vyakula vyote vizuri. Badala yake, ni muhimu kwa wenye kisukari kuanza kujifunza, kupanga na kufurahia mlo wa afya wenye uwiano sahihi. 

Kushiriki kwenye mafunzo ya lishe bora, na chakula cha pamoja kama familia,ni kati ya mambo ya kudumishwa na mgonjwa.

Kisukari hakitakiwi kuwa sababu ya kuvunjika moyo, bali sehemu ya maisha inayodhibitika na hatimaye mgonjwa  kuishi kwa matumaini

0 Comment

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidiaAfyaclass Forum •

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia.

Kutana na Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2 Diabetes) toka mwaka 1984.

Aliandika hivi “My Go-to Tips If You’re Newly-Diagnosed With Type 2 Diabetes” By Ilene Raymond Rush Diagnosed since 1984. Anasema;

Ikiwa ungeuliza ni nini kimeongeza udhibiti wangu wa Sukari na taswira ya mwili kwa miaka mingi hii nikiwa na ugonjwa wa kisukari cha aina ya 2, unaweza kushangazwa na jibu langu.

Nimekuwa nikifuata mlo unaohusisha mboga mboga zenye kiwango cha chini cha wanga au low carbs” kwa hakika umesaidia, pamoja na kutumia dawa zangu kwa mashariti yote, kufuatilia kiwango cha sukari yangu kwenye damu, na kupata muda wa kufanya mazoezi ya kawaida ya mwili, nimepata matokeo ya kuvutia zaidi kutokana na kuinua vitu vizito pia.

Hivo mbinu za Ilene Raymond Rush ambaye aligunduliwa Kisukari aina ya Pili(Type 2 Diabetes, ni Pamoja na;

  • Kula Mlo wenye afya unaohusisha mboga mboga zenye kiwango cha chini cha wanga au low carbs”,
  • pamoja na kutumia dawa zake kwa mashariti yote,
  • kufuatilia kiwango cha sukari yake kwenye damu kila mara,
  • na kupata muda wa kufanya mazoezi ya kawaida ya mwili,

Kwa yeye pia amepata matokeo ya kuvutia zaidi kutokana na kuinua vitu vizito,

Anasema; Ikiwa jibu langu linakutatanisha, ujue kwamba masomo ya kisayansi yananiunga mkono. Mafunzo endelevu ya ukinzani ikiwemo kunyanyua vitu vizito(Sustained resistance training) yanayofanywa mara moja hadi tatu kwa wiki kwa siku zisizofuatana, sio tu kwamba hupunguza sukari ya damu lakini inaweza kuboresha upinzani wa insulini (ambapo insulini inazuiwa kuingia kwenye seli, na kusababisha kuongezeka kwa glucose katika damu).

Lakini sio hivyo tu. Kusukuma chuma kunaweza pia kuimarisha afya ya moyo, kupunguza mafuta (hasa karibu na tumbo), kuimarisha mifupa yako, na kukugeuza kuwa kijana, “Anasema”.

Tahadhari: Kwa baadhi ya watu walio na kisukari, kuinua Vitu vizito kunaweza kusababisha sukari kwenye damu kupanda kwa muda kwa sababu ya adrenaline inaweza kuongeza sukari.

Kwa hivyo ni vyema kupima sukari yako kabla na baada ya mazoezi na, ikihitajika, zungumza na daktari wako kuhusu marekebisho yoyote ambayo unaweza kuhitaji kufanya katika dawa au lishe yako na hata MAZOEZI YA kufanya.

Na, kama ilivyo kwa mazoezi yoyote, ikiwa una matatizo ya kisukari, pamoja na ugonjwa wa neva au matatizo ya moyo, zungumza na mtaalamu wako kabla ya kuanza utaratibu wa kuinua vitu Vizito.

Zingatia Vidokezo hivi Muhimu kwako;

1. Hakikisha unaendelea kujifunza kuhusu Sukari yako,

ikiwemo kusoma makala mbali mbali na kuendelea kupata Elimu ya kutosha.

2. Jifunze kuifuatilia Sukari yako, ikiwemo kupima mara kwa mara, na kujua vitu vinavyoiathiri haraka.

3. Fahamu kuhusu Mlo Sahihi kwa Mgonjwa wa Sukari

4. Tumia dawa ulizopewa kwa Usahihi, na kuzingatia mashariti yote

5. Epuka Matumizi ya kilevyi chochote ikiwemo Pombe au Sigara.

Rejea Link;

https://www.webmd.com/20240412/my-go-to-tips-if-youre-newly-diagnosed-with-type-2-diabetes

Kama ndiyo Umegunduliwa ugonjwa wa Kisukari,Soma hii itakusaidia
0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD