Showing posts with label ugonjwa wa ukimwi. Show all posts
Showing posts with label ugonjwa wa ukimwi. Show all posts

Si Kila Mtu mwenye Mkanda wa Jeshi,Basi ana UKIMWIAfyaclass Forum •

Mkanda wa Jeshi,chanzo,dalili na matibabu yake

Fahamu kuhusu Mkanda wa Jeshi, maana yake,chanzo,dalili,pamoja na matibabu yake,kupitia makala hii.

Mkanda wa Jeshi

Mkanda wa Jeshi ni tatizo linalohusu maambukizi ya Virusi(Viral Infection) ambayo hutokana na reactivation ya varicella-zoster virus,

Tatizo hili la Mkanda wa Jeshi kwa jina lingine hujulikana kama Herpes zoster au Shingles.

Dalili za Mkanda wa Jeshi

Tatizo la Mkanda wa Jeshi huweza kuhusisha maumivu pamoja na uwepo wa vipele kwenye eneo flani yaani self-limited dermatomal rash,

Na mara nyingi mkanda wa jeshi huanza na maumivu kwenye eneo lililoathiriwa na virusi hawa,

ambapo huambatana na kuanza kujitokesha mabadiliko ya ngozi kwenye eneo hilo ndani ya siku 2 mpaka 3.

Mkanda wa jeshi ni jina linalotumika sana mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili.

Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.

Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto.

KUMBUKA: SIO KILA MWENYE MKANDA WA JESHI NI MUATHIRIKA WA UKIMWI

Watu ambao wapo kwenye hatari ya Kupata Mkanda wa Jeshi

‣ Mkanda wa jeshi huwapata zaidi watu wenye umri mkubwa,

Mfano; watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50,

utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 80 hupatwa na mkanda wa jeshi.     

‣  Vilevile huwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI na saratani.

‣ Tiba za mionzi na chemotherapy huweza kupunguza kinga ya mwili kwa mgonjwa na kumfanya awe kwenye hatari kubwa ya kupata mkanda wa jeshi.

Matibabu ya Mkanda wa Jeshi

Matibabu ya mkanda wa Jeshi ni pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali jamii ya antiviral medications.

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je,Mkanda wa Jeshi ni kiashiria kwamba una maambukizi ya Virusi vya Ukimwi?

Jamii imezoea kwamba Kila Mtu mwenye Mkanda wa Jeshi ni muathirika wa Ukimwi, ifahamike kwamba SIO KILA MWENYE MKANDA WA JESHI NI MUATHIRIKA WA VIRUSI VYA UKIMWI,

mtu yoyote huweza kupata mkanda wa jeshi(herpes zoster/shingles) au maambukizi ya Varicella-Zoster Virus.

Ingawa Mkanda wa jeshi huweza kuwapata zaidi watu waliopatwa na magonjwa yanayopunguza kinga za mwili, kama vile, UKIMWI, saratani n.k.

Hitimisho

Ni munimu kufahamu kuhusu dalili za mkanda wa jeshi,ili zikianza kujutojeza upate msaada wa haraka zaidi,

Dalili za Mkanda wa Jeshi ni pamoja na;

Mkanda wa jeshi ni jina linalotumika sana mitaani kuutaja ugonjwa unaoshambulia ngozi na kujenga tabaka la vijipele vikubwa venye majimaji ambavyo mara nyingi hukamata upande mmoja wa mwili.

Ingawa vijipele vya mkanda wa jeshi vinaweza kutokea sehemu yo yote ya mwili, mara nyingi hupenda kuota kifuani, shingoni, usoni, mgongoni na mikononi.

Vijipele hivi hukaa juu ya ngozi kwa muda wa wastani wa wiki mbili hadi sita kisha hupotea. Vipele vya mkanda wa jeshi huambatana na maumivu makali na kusikia ngozi kuwaka moto.

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuongezekaAfyaclass Forum •

Hatua ya Marekani kusitisha msaada wa kigeni umeathiri pakubwa mpango wa utafiti wa chanjo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) nchini Afrika Kusini, hatua yenye athari kubwa kote duniani na hususan barani Afrika.

Ilikuwa imesalia wiki moja tu kabla ya wanasayansi wa Afrika Kusini kuanza majaribio ya kimatibabu ya chanjo ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), na matumaini yalikuwa makubwa ili kufikia hatua nyingine ya kujaribu kukabiliana na moja ya magonjwa hatari zaidi katika historia.

Na ndipo barua pepe iliwasili ikiwaamuru wanasayansi hao kusitisha shughuli zote. Marekani chini ya utawala wa rais Donald Trump ulikuwa umesitisha ufadhili wake wote katika mradi huo wa majaribio. Taarifa hizo ziliwakwaza mno watafiti, wanaoishi na kufanya kazi katika eneo ambalo  watu wengi wanaishi na VVU  kuliko mahali pengine popote duniani.

Mradi huo wa utafiti unaoitwa BRILLIANT, ulikusudiwa kuwa wa hivi punde zaidi unaotumia mchanganyiko wa tofauti za vijinasaba na utaalamu wa kina wa eneo hilo ili kuwanufaisha waathirika wa virusi vya Ukimwi kote duniani.

Lakini dola milioni 46 kutoka Marekani zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya mradi huo zilitoweka, kufuatia kusitishwa kwa misaada ya kigeni na mfadhili mkuu duniani mapema mwaka huu, hasa kutokana na hatua ya Rais Donald Trump kutangaza kuwa kwa sasa anazingatia kwanza vipaumbele vya taifa lake.

Afrika Kusini yaathirika mno na hatua hiyo

Afrika Kusini imeathirika kwa kiasi kikubwa na hatua hiyo hasa baada ya Trump kutoa madai yasiyokuwa na msingi kwamba utawala umekuwa ukiwalenga jamii ya walio wachache wa Afrika Kusini, wazungu. Nchi hiyo imekuwa ikipokea takriban dola milioni 400 kwa mwaka kupitia mashirika ya misaada ya USAID na PEPFAR yanayolenga kukabiliana na VVU. Lakini sasa misaada yote hiyo imetoweka.

Glenda Grey, ambaye anaongoza mradi huo wa Brilliant, amesema bara la Afrika limekuwa na jukumu muhimu katika kufikia mafanikio ya  dawa za VVU , lakini kusitishwa kwa msaada wa Marekani kunatishia uwezo wa bara hilo kuendelea na jukumu hilo katika siku zijazo.

Maendeleo makubwa yaliyoshuhudiwa ni pamoja na majaribio ya kimatibabu ya dawa aina ya "lenacapavir", chanjo pekee duniani ya kuzuia kuenea kwa VVU ambayo muathirika huchomwa mara mbili kwa mwaka. Chanjo hiyo iliidhinishwa kwa matumizi rasmi hivi majuzi na mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA),  na utafiti wake uliwahusisha vijana wa Afrika Kusini.

"Tunafanya majaribio vizuri zaidi, kwa haraka na kwa bei nafuu kuliko mahali pengine popote duniani, na hivyo bila Afrika Kusini kuwa sehemu ya programu kama hizi, bila shaka dunia itaathirika zaidi." Grey alisema akisisitiza kuwa hayo ni maoni yake. Alibainisha kuwa wakati wa janga la UVIKO-19, Afrika Kusini ilichukua jukumu muhimu kwa kuzijaribu chanjo za Johnson & Johnson na Novavax, uchunguzi uliopelekea wanasayansi wa  Afrika Kusini  kugundua aina nyingine ya virusi hivyo.

Grey anasikitika kushuhudia katika taifa ambalo karibu asilimia 46 ya vijana hawana ajira, maabara zikiwa tupu huku maelfu ya wanasayansi wakiachishwa kazi ikiwa ni pamoja na timu ya watafiti wa Chuo Kikuu cha Witwatersrand iliyokuwa sehemu ya kitengo kinashiriki mpango wa majaribio wa kutengeneza chanjo hiyo ya kuzuia VVU. Ameongeza pia kuwa hatua hiyo inawanyima fursa ya kushirikiana na wanasayansi wengine wa Afrika.

Profesa Abdullah Ely aliyekuwa akiongoza timu hiyo ya watafiti amesema kazi waliyokuwa wakiifanya ilikuwa imeanza kuonyesha matokeo chanya yanayodhihirisha kuwa chanjo hizo zilikuwa na uwezo wa kutoa kinga, lakini akasikitika kuona kwamba juhudi zote hizo sasa zimelazimika kusitishwa.

BRILLIANT sasa inahangaika kutafuta fedha za kuokoa mradi huo .Ununuzi wa vifaa muhimu umesimama na idara ya afya ya Afrika Kusini inasema watafiti wapatao 100 wa mradi huo na wengine wanaohusishwa na miradi ya VVU wameachishwa kazi. Ufadhili wa mpango wa kuwahusisha wanafunzi wanaosomea udaktari katika majaribio ya miradi hiyo uko pia hatarini.

Serikali ya Afrika Kusini inakadiria kuwa miradi ya wanasayansi kuhusu magonjwa ya VVU  na hata kifua kikuu itapoteza karibu dola milioni 107 kutokana na hatua ya Marekani kusitisha misaada ya kigeni, huku ikisisitiza kuwa itakuwa vigumu kupata fedha zitakazoweza kuziba pengo la ufadhili wa Marekani.

Maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi kuongezeka

Hatua hiyo itapelekea pia dawa za kupunguza makali ya VVU kuwa vigumu kupatikana. Angalau maafisa wa afya 8,000 nchini Afrika Kusini waliokuwa wakifanya kazi katika mpango wa VVU tayari wamefutwa kazi, kulingana na serikali. Pia, timu ya wauguzi waliokuwa wakikusanya data na kufuatilia hali jumla ya wagonjwa ikiwa ni  pamoja na washauri wa ugonjwa wa VVU ambao wangeliweza kuwafikia wagonjwa walio katika mazingira magumu ya vijijini pia wametoweka.

Katika ziara yake nchini Afrika Kusini mwezi Juni, mkurugenzi mtendaji wa shirika la kupambana na Ukimwi la Umoja wa Mataifa,  UNAIDS Winnie Byanyima alitambua kuhusu dharura iliyopo na maisha ya mamilioni ya watu yaliyokuwa hatarini kutokana na hatua hiyo hasa ikizingatiwa kuwa miradi ya utafiti na huduma za afya nchini Afrika Kusini na kote barani Afrika ikifungiwa ufadhili.

Nchi nyingine ambazo zilikuwa zinategemea pakubwa ufadhili wa Marekani zikiwemo Zambia, Nigeria, Burundi na Ivory Coast tayari zinapambana ili kukidhi mahitaji yao kwa kutumia uwezo wao wa ndani, alisema Bi Byanyima lakini akasisitiza kuwa wanachokitoa hakitaweza kufidia ufadhili wa Marekani.

(Chanzo: AP)

0 Comment

UNAIDS inakadiria kutatokea maambukizi mapya ya VVU milioni 6 na vifo vya ziada ya milioni 4 kati ya 2025 na 2029Afyaclass Forum •

Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, UNAIDS leo limezindua ripoti yake ya mwaka huu wa 2025 ya hali ya Ugonjwa wa UKIMWI. “UKIMWI, Janga  na mabadiliko,” inayoonesha kuwa kuna janga kubwa la kifedha linalotishia kuvuruga mafanikio yaliyopatikana kwa miongo kadhaa, isipokuwa mataifa yatekeleze mabadiliko makubwa katika programu na ufadhili wa ugonjwa wa Virusi Vya Ukimwi, VVU, Imesema ripoti iliyotolewa leo na Shirika hilo la UNAIDS mjini Geneva Uswisi na Johannesburg, Afrika Kusini.



Ripoti hiyo inasisitiza athari za ghafla za upunguzaji mkubwa wa ufadhili kutoka kwa wafadhili wa kimataifa, hasa katika nchi zilizoathirika zaidi na VVU. Hata hivyo, inatoa mifano ya kuhamasisha ya nchi na jamii ambazo zimeonesha uimara kwa kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI licha ya changamoto kubwa.

Kati ya nchi 60 za kipato cha chini na cha kati zilizojumuishwa katika ripoti, 25 zimeonesha nia ya kuongeza bajeti zao za ndani kwa ajili ya kukabiliana na VVU ifikapo 2026. Ongezeko hili linakadiriwa kuwa la asilimia 8, sawa na takribani dola milioni 180 za Kimarekani — hatua nzuri lakini bado haitoshi kufidia upungufu wa ufadhili wa kimataifa katika nchi zinazoitegemea pakubwa.

Janga la kimataifa: Upungufu mkubwa wa fedha watishia kurejesha nyuma mafanikio

Licha ya mafanikio yaliyoonekana katika mwaka wa 2024, kupungua kwa misaada ya kimataifa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka wa 2025 umesababisha machafuko katika mifumo ya afya, kukatiza huduma za msingi za afya, na kupunguza huduma za kinga na tiba dhidi ya VVU.

Nchini Msumbiji pekee, zaidi ya wahudumu wa afya 30,000 wameathirika. Nchini Nigeria, idadi ya watu wanaoanza kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya VVU (PREP) imeshuka kutoka watu 40,000 hadi 6,000 kwa mwezi. Ikiwa huduma zinazofadhiliwa na Marekani zitakoma kabisa, UNAIDS inakadiria kutatokea maambukizi mapya ya VVU milioni 6 na vifo vya ziada ya milioni 4 kati ya 2025 na 2029.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS, Winnie Byanyima anasema, “Hii si pengo la kifedha tu -ni bomu linalosubiri kulipuka. Tumeona huduma zikisimama ghafla. Wahudumu wa afya wamerejeshwa nyumbani. Na watu, hasa watoto na makundi muhimu wakikosa huduma.”

Tayari kufikia 2024, watu milioni 9.2 waliokuwa wakiishi na VVU hawakuwa wakipata dawa za kuokoa maisha. Miongoni mwao, watoto 620,000 wenye umri wa miaka 0 hadi 14 hawakupata tiba, na kusababisha vifo vya watoto75,000.

Watu 630,000 walifariki dunia kutokana na UKIMWI, asilimia 61 kati yao wakiwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Wasichana balehe na wanawake vijana zaidi ya 210,000 wenye umri wa miaka 15–24 waliambukizwa ugonjwa wa VVU mwaka huo, wastani wa maambukizi mapya 570 kwa siku.

Huduma za kinga dhidi ya VVU zimevurugika pakubwa. Huduma zinazoendeshwa na jamii, ambazo ni muhimu kwa makundi ya pembezoni, zimekosa ufadhili kwa kasi ya kutisha. Mapema 2025, zaidi ya asilimia 60 ya mashirika ya wanawake yanayotoa huduma za VVU yalikuwa yamepoteza ufadhili au kulazimika kusitisha huduma zao.

Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) ulifikia wasichana na wanawake vijana milioni 2.3 wenye huduma za kina za kuzuia VVU mwaka 2024 na kuwezesha watu milioni 2.5 kutumia VVU PrEP, lakini programu hizi sasa zimeacha kabisa.

Wakati huo huo, ongezeko la sheria kandamizi dhidi ya mahusiano ya watu wa jinsia moja, utambulisho wa kijinsia, na matumizi ya dawa za kulevya limezidisha janga hili kwa kufanya huduma za VVU kutopatikana kwa watu wanaozihitaji zaidi. Nchi kama Uganda, Mali na Trinidad na Tobago zimeona mabadiliko ya hivi majuzi yenye madhara na ya ubaguzi kwa sheria zao za uhalifu zinazolenga watu muhimu, na kuwasukuma mbali zaidi kutoka kwa matunzo na kuongeza hatari yao ya kupata VVU.

Tumaini lipo: Nchi na jamii zinaibuka kulinda mafanikio ya tiba ya VVU

Afrika Kusini kwa sasa inafadhili asilimia 77 ya mapambano yake dhidi ya UKIMWI, na katika mapitio ya bajeti ya 2025, imepanga kuongeza bajeti ya afya kwa asilimia 5.9 kila mwaka kwa kipindi cha miaka 3 ijayo, ikiwa ni pamoja na asilimia 3.3 ya ongezeko la mwaka kwa programu za VVU na kifua kikuu. Serikali pia inanuia kuanzisha mfumo wa taarifa za wagonjwa, mfumo wa usambazaji wa dawa za muda mrefu, na mfumo wa ufuatiliaji wa akiba ya dawa katika vituo vya afya.

Kufikia Desemba 2024, nchi 7 — Botswana, Eswatini, Lesotho, Namibia, Rwanda, Zambia, na Zimbabwe,  zilikuwa zimefikia malengo ya 95-95-95: asilimia 95 ya watu wanaoishi na HIV wanajua hali yao, asilimia 95 ya hao wapo kwenye matibabu, na asilimia 95 ya waliopo kwenye tiba wana kiwango kidogo cha virusi mwilini.

Ripoti pia inaangazia matumaini mapya kupitia zana za kisasa za kuzuia maambukizi kama vile PrEP ya sindano ya muda mrefu kama Lenacapavir, iliyothibitishwa kuwa na ufanisi mkubwa katika majaribio ya kitaalamu , ingawa changamoto za upatikanaji na bei bado ni kubwa.

Bado kuna nafasi ya kugeuza janga hili kuwa fursa. Nchi zinaongeza fedha za ndani. Jamii zinaonesha mbinu zinazofanya kazi. Sasa tunahitaji mshikamano wa kimataifa kuunga mkono ujasiri wao.” amesema Bi. Byanyima

Wito wa mshikamano

Ripoti ya UNAIDS ya 2025 inahitimisha kwa wito wa dharura. Mapambano dhidi ya VVU hayawezi kutegemea rasilimali za ndani pekee. Jumuiya ya kimataifa lazima ijitokeze kufidia pengo la ufadhili, kusaidia nchi kufikia malengo ya kinga na tiba, kuondoa vikwazo vya kisheria na kijamii, na kuziwezesha jamii kuongoza njia.

UNAIDS inasisitiza kwamba kila dola inayowekezwa katika kupambana na VVU si tu kwamba inaokoa maisha, bali pia inaimarisha mifumo ya afya na kuchangia malengo mapana ya maendeleo. Tangu mlipuko wa ugonjwa huu uanze, vifo 26.9 milioni vimeepushwa kupitia tiba, na watoto milioni 4.4 wamelindwa dhidi ya maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

Bi. Byanyima anasema,  “Katika wakati huu wa janga, ulimwengu lazima uchague mabadiliko badala ya kurudi nyuma. Kwa pamoja, bado tunaweza kukomesha UKIMWI kama tishio kwa afya ya umma ifikapo 2030, kama tutachukua hatua sasa, kwa mshikamano na dhamira thabiti bila kuyumbayumba."

0 Comment

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwiAfyaclass Forum •

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi

Kuna njia nyingi ambazo hutumika ili kusaidia kuzuia maambukuzi ya Virusi vya ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine wakati wa kufanya mapenzi,

Kama umepima wewe na mwenza wako,Moja wenu kapata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja ili kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Hivi ni Vitu vya msingi sana vya Kuzungatia ikiwa mpo kwenye hali kama hii;

1. Hakikisheni mpo kwenye tiba,

Moja ya njia rahisi na inayofanya kazi ni kuhakikisha mwenza wako yupo kwenye matibabu na anafuata kanuni zote za Tiba ya HIV.

hii inasaidia kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine(An undetectable viral load makes HIV untransmittable).

2. Njia nyingine mpya ni kwa mwenza ambaye hana maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutumia dawa zinazoitwa PrEP

Kwa mwenza ambaye yupo NEGATIVE Anaweza kutumia PrEP, Hizi ni dawa za kunywa(vidonge) ambavyo husaidia kuzuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi kabla ya mtu kuwa kwenye mazingira ya hatari.

Na kwa mujibu wa tafiti mbali mbali PrEP zina uwezo mkubwa wa kufanya hivo.

3. Matumizi Sahihi ya kinga kama kondomu

Matumizi sahihi ya condomu kwa Mwanaume au mwanamke huweza kusaidia kupunguza uwezekano wa kusambaza maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

4. Jikinge na magonjwa mengine ya Zinaa(STI’s),

Ikiwa mwenza wako ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU), kuna uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa mengine ikiwemo ya Zinaa, kwa sababu ya kinga yake ya Mwili kuwa dhaifu Zaidi.

Hii huongeza hatari ya wewe kupata magonjwa mengine zaidi.

5. Mambi haya pia huweza kukuweka kwenye hatari zaidi ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi;

  • Viral Load kuwa juu
  • Muda wa kufanya mapenzi
  • Kufanya mapenzi katika mazingira magumu(roughness of sex), hapa hakuna maandalizi ya kutosha, mnafanya kwa nguvu kama kukomoana, kuchubuana n.k

Moja ya vitu muhimu vya kuchunguza kwa mwenza wako ikiwa ana maambukizi ya virusi vya Ukimwi(VVU) ni pamoja na VIRAL LOAD,

Kwa mujibu wa Utafiti mmoja ulionyesha kwa Watu ambao VIRAL LOAD ilikuwa chini uwezekano wa kusambaza maambukizi ulikuwa mdogo sana au sawa na Zero.

Utafiti huo Unasema;

 “The PARTNER study reported zero HIV transmissions after 900 couples had sex more than 58,000 times WITHOUT condoms. In this study undetectable viral load was defined as being less than 200 copies/m”.

Utafiti huu unaendelea kwa kusema; Hatari ya kupenya Virusi kwa Mtu anayefanya mapenzi bila kondomu na mtu ambaye ana kiwango cha juu cha virusi(HIGH VIRAL LOAD) inaweza kuwa juu Zaidi kama 1 kati ya 10 (hatari 10%). Lakini hatari ni sifuri kwa mtu ambaye anatumia matibabu(dawa) na ambaye ana kiwango cha chini sana cha virusi(LOW VIRAL LOAD) au kisichoonekana.

Mambo ya kuzingati wewe na Mwenza wako ikiwa mmoja wenu ana Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi

Je, wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua tahadhari gani?

Kuna tahadhari kadhaa ambazo wewe na mwenzi wako mnaweza kuchukua ili kuzuia kuambukizwa au kusambaza VVU kupitia ngono.

(1) Hakikisheni mnatumia njia za kujikinga kama condoms pamoja na njia nyingine

Mbinu za kujikinga kama vile kondomu huweza kusaidia kuzuia michubuko na kugusa maji maji ya mwili wakati wa kujamiiana na mtu anayeishi na VVU.

Vikitumiwa  ipasavyo, vizuizi hivi vinaweza kuzuia uambukizaji wa VVU na magonjwa mengine ya Zinaa.

Kutumia vilainishi au mafuta ya kutosha kunaweza pia kusaidia kupunguza hatari ya VVU, pia – bila kusahau, kufanya ngono kuwa bora zaidi.

(2) Hakikisheni mnatumia dawa muhimu ikiwemo ART, PrEP, na PEP

Kuna dawa chache zinazoweza kusaidia kuzuia maambukizi ya VVU:

ART: Mtu anayeishi na VVU anaweza kutumia dawa zinazojulikana kama ART ili kumsaidia kuwa na afya bora na kuzuia uambukizaji wa VVU.

Watu wengi wanaotumia dawa kama ilivyoagizwa wanaweza kupunguza kiwango chao cha virusi hadi kiwango kisichoonekana.

PrEP: Hii ina maana ya pre-exposure prophylaxis, PrEP ni dawa ambayo mtu asiye na VVU anaweza kutumia kabla ya kuingia kwenye mazingira hatarishi ili kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU kwa asilimia 99.

PEP: Hii ina maana ya Post-exposure Prophylaxis, PEP hutumika baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa,

au PEP, ni regimen ya dawa inayoweza kusaidia kupunguza hatari ya kuambukizwa VVU baada ya kuwa kwenye mazingira hatarishi ya kuweza kuambukizwa inapoanzishwa au kutumika ndani ya saa 72.

(3) Jengeni Utaratibu wa kufanya Vipimo mara kwa mara ikiwemo Vipimo vya magonjwa ya Zinaa(STIs)

Ni muhimu kwako na kwa mwenzi wako kupima magonjwa ya Zinaa mara kwa mara. Utambuzi wa mapema na matibabu ya magonjwa ya zinaa inaweza kupunguza hatari ya matatizo.

Kuwa na magonjwa ya zinaa kunaweza kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU.

(4) Fahamu Dalili kubwa za Ukimwi na magonjwa mengine ya Zinaa(STIs)

Kufahamu kuhusu dalili za magonjwa ya Zinaa(STI) ni muhimu kwa mtu yeyote anayeshiriki ngono.

Muone mtaalamu wa afya ukigundua mojawapo ya haya:

  • kutokwa na uchafu usio wa kawaida kutoka kwa njia ya haja kubwa, uume au uke
  • kutokwa na damu kusiko kwa kawaida ukeni, kama vile kutokwa na damu baada ya kujamiiana au katikati ya mzunguko wa hedhi
  • Kuhisi kuungua au maumivu wakati wa kukojoa
  • Kuhisi kukojoa mara kwa mara
  • Kuwa na vidonda au malengelenge kwenye au karibu na sehemu zako za siri,eneo la haja kubwa(mkundu) n.k
  • Kuwa na upele kwenye au karibu na sehemu zako za siri au mkundu
  • kuwashwa sehemu za siri n.k

(5) Hakikisheni mnapata Ushauri wa kutosha wa jinsi ya kuishi pamoja kutoka kwa wataalam wa afya.

Unaweza kufanya mapenzi na mtu mwenye ukimwi
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD