Showing posts with label uzazi. Show all posts
Showing posts with label uzazi. Show all posts

Ajifungua Mapacha Wenye Baba TofautiAfyaclass Forum •

 Tukio la kushangaza lililoripotiwa nchini Brazil liliwaacha Watu wakiwa na mshangao, baada ya msichana mwenye umri wa miaka 19 kujifungua mapacha wenye baba tofauti.

Kitaalamu, hali hii adimu inajulikana kama Heteropaternal Superfecundation, ambayo hutokea pale ambapo mayai mawili yanatolewa na yakaweze kurutubishwa na mbegu za wanaume wawili tofauti katika kipindi kimoja cha ovulesheni.

Vipimo vya vinasaba (DNA) vilithibitisha kuwa watoto hao wawili wanashirikiana mama mmoja, lakini kila mmoja ana baba tofauti. 

Kisa kama hiki ni nadra sana kutokea duniani, na ni wachache tu waliowahi kuripotiwa katika historia ya tiba.

Wataalamu wa afya wamesema tukio hilo linaonesha upekee na ugumu wa mifumo ya uzazi wa binadamu, na kwamba sayansi bado inaendelea kugundua mambo mapya kuhusu maajabu ya asili ya mwanadamu.

0 Comment

Jinsi ya Kulea Watoto Mapacha(Soma hapa baadhi ya Tips)Afyaclass Forum •

 Jinsi ya Kulea Watoto Mapacha(Soma hapa baadhi ya Tips)

Hizi hapa ni baadhi ya dondoo au Tips za Kukusaidia kuwalea Watoto Mapacha kama una watoto hawa,

Vizuri! Hapa kuna baadhi ya vidokezo vya kufuata unapokwama kuhusu jinsi ya kuwalea mapacha wote wawili kwa wakati mmoja;

1. Watoto kulala kwa Pamoja, hii wataalam wa afya huita Co-bedding,

Watoto mapacha kulala sehemu moja kwa pamoja husaidia sana kwenye urekebishaji wa joto la Mwili(Body temperature regulation),

Na pia kusaidia watoto hawa kupata Usingizi mzuri zaidi,

Sio lazima watumie kila kitu kimoja,unaweza kuwaweka kila mtu na kitu chake ila wakiwa pamoja,

mfano; mito miwili,soft toys mbili za kuchezea, Chuchu mbili n.k

2. Wanyonyeshe watoto wote wawili kwa pamoja,

Jaribu kutumia mto wa kunyonyeshea kwa kulisha wote wawili kwa wakati mmoja,

Ikiwa unapata shida yoyote kwenye unyonyeshaji mfano maziwa kutoka kidogo n.k,

jaribu kulisha kwa njia mbadala huku mmoja akinyonyeshwa chuchu ya Mama na mwingine akinyonyeshwa kwa chupa baada ya maziwa kuwekwa humu,

Kisha Badili zamu zao wakati wa mlo wako unaofuata.

3. Wafanye walale pamoja kwenye kitanda kimoja.

4. Kama unatumia vitembezi yaani stroller,

Tumia vitembezi viwili wakati wanapelekwa sehemu moja kwenda nyingine

5. Kama unawafunika Blanketi Wafunike kwa Blanketi Moja wote wawili

Pia, jifunze jinsi ya kuwaweka kwenye blanketi pamoja.

6. Hakikisha kila mtoto anapata kumbatio lako, hivo kama unaweza washike wote wawili na kama huwezi washike kwa awamu,

yaani kushika na kulaza kila mtoto kwa njia mbadala.

7. Kama unatumia Mito,Jifunze kutumia mto wa watoto wachanga na sio Mito ya watu Wazima

8. Wakati unahitajika kubadilisha Nepi za watoto badilisha kwa haraka,

wabadilishe watoto nepi kwa haraka, usiwaache watoto wakae na nepi chafu kwa Muda mrefu,mfano nepi zenye mikojo,kinyesi n.k

9. Weka vitu vya watoto vya kuchezea kwenye eneo ambapo vikihijika wanapewa kwa urahisi zaidi,

10. Jifunze kuwaogesha kwa pamoja,

japo kulingana na mazingira yako wakati mwingine inaweza kuwa vigumu,

lakini wataalam wa afya hushauri kutokuonyesha upendeleo wowote kwa watoto hawa,

mapacha wamekaa pamoja kwa muda mrefu zaidi kuliko wewe unavyodhani, Waache wadumishe umoja wao,

Usionyeshe upendeleo kwa yeyote kati ya hao wawili,

Hivo ni baadhi ya Vitu vichache tu ambavyo vinaweza kukupa mwanga wakati wa Malezi ya Watoto Mapacha.

#Malezi #Mapacha

0 Comment

Tatizo La Kuziba Mirija Ya Uzazi,ChanzoAfyaclass Forum •

 TATIZO LA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Tatizo la kuziba mirija ya uzazi ni tatizo ambalo hutokea kwa wanawake wengi kwa hivi sasa,na ni miongoni mwa sababu kubwa za wanawake wengi kushindwa kubeba Mimba.

Je tatizo hili la kuziba kwa mirija ya uzazi chanzo chake ni nini? soma hapa chini kufahamu baadhi ya sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili la kuziba kwa mirija ya Uzazi.

CHANZO CHA TATIZO LA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na maambukizi kwenye via vyake vya uzazi mara kwa mara yaani pelvic inflammatory disease(PID)

- Mwanamke kuwa na historia ya kuumwa na kidole tumbo yaani Appendix kisha ikapasukia ndani

- Mwanamke kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa(Sexual transmitted diseases-STD's) kama vile; Ugonjwa wa kisonono(gonorrhea),tatizo la chlamydia n.k

- Tatizo la Endometriosis,ambapo huhusisha kukua kwa kuta za ndani ya tumbo la uzazi kuelekea nje

- Mwanamke kuwa na historia ya kufanyiwa upasuaji tumboni

- Mwanamke kupatwa na tatizo la maji kujaa kwenye mirija ya uzazi kisha kusababisha mirija ya uzazi kuziba na kuvimba,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hydrosalpinx

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy

- Mwanamke kuwa na tatizo la uvimbe kwenye mirija ya uzazi yaani Fibroids n.k

DALILI ZA TATIZO HILI LA KUZIBA KWA MIRIJA YA UZAZI

Kwa asilimia kubwa wanawake wengi wenye tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi hawaonyeshi dalili zozote,mpaka pale watakapoanza kupata shida ya kutokubeba mimba,ndipo huamua kufanya vipimo na kugundulika shida hii, Lakini endapo watapata dalili,basi miongoni mwa dalili hizi hapa chini huweza kuonekana;

• Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo eneo la kwenye kitovu,chini ya kitovu,pembeni upande mmoja au kwenye kiuno

• Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi

• Mwanamke kupata maumivu ya tumbo upande mmoja,hii hutokea sana kwa wanawake ambao tatizo la mirija ya uzazi kuziba chanzo chake ni maji kujaa na kuziba kwenye mirija ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hdyrosalpinx

• Baadhi ya wanawake hupata shida ya kutoa damu ukeni yaani vaginal bleeding n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUZIBA

✓ Kwanza ifahamike kwamba, mwanamke huweza kupata shida ya mirija ya uzazi kuziba upande mmoja au mirija yote miwili yaani kulia na kushoto,

Endapo kuziba kumetokea upande mmoja uwezekano wa mwanamke huyu kubeba mimba bado upo, ila Mwanamke huyu yupo pia kwenye hatari ya mimba hii kutunga nje ya kizazi, yaani kupatwa na tatizo la Ectopic pregnancy

Na endapo mirija yote miwili ya Uzazi imeziba ningumu sana kwa mwanamke huyu kubeba mimba mpaka atibiwe,

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA

Moja ya vipimo ambavyo huweza kufanyika ni pamoja na;

1. Kipimo cha Hysterosalpingograph(HSG),Kipimo hiki ni aina ya X-ray ambayo husaidia kuona ndani ya mirija ya uzazi

2. Na kipimo kingine ni Laparoscopy N.k

MATIBABU YA TATIZO LA KUZIBA MIRIJA YA UZAZI

Moja ya tiba kwenye tatizo hili ni pamoja na Mwanamke kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe,kuondoa Scars, au huduma ya Kuzibua mirija n.k Kutegemea na chanzo cha tatizo lenyewe.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment

Tatizo La Mirija Ya Uzazi Kujaa MajiAfyaclass Forum •

 TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Hydrosalpinx,hili ni tatizo la kujaa maji kwenye mirija ya uzazi au kwenye sehemu ya mwisho ya mirija ya uzazi na kisha kuvimba.

CHANZO CHA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI NI PAMOJA NA;

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na maambukizi kwenye via vyake vya uzazi mara kwa mara yaani pelvic inflammatory disease(PID)

- Mwanamke kuwa na historia ya kuumwa na kidole tumbo yaani Appendix kisha ikapasukia ndani

- Mwanamke kuwa na maambukizi ya magonjwa ya zinaa(Sexual transmitted diseases-STD's) kama vile; Ugonjwa wa kisonono(gonorrhea),tatizo la chlamydia n.k

- Tatizo la Endometriosis,ambapo huhusisha kukua kwa kuta za ndani ya tumbo la uzazi kuelekea nje

- Mwanamke kuwa na historia ya kufanyiwa upasuaji tumboni

- Mwanamke kupatwa na tatizo la maji kujaa kwenye mirija ya uzazi kisha kusababisha mirija ya uzazi kuziba na kuvimba,tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Hydrosalpinx

- Mwanamke kuwa na historia ya kupatwa na tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani Ectopic pregnancy

- Mwanamke kuwa na tatizo la uvimbe kwenye mirija ya uzazi yaani Fibroids n.k

DALILI ZA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Kwa asilimia kubwa wanawake wengi wenye tatizo hili la kuziba mirija ya uzazi na mirija kujaa maji hawaonyeshi dalili zozote,mpaka pale watakapoanza kupata shida ya kutokubeba mimba,ndipo huamua kufanya vipimo na kugundulika shida hii, Lakini endapo watapata dalili,basi miongoni mwa dalili hizi hapa chini huweza kuonekana;

• Mwanamke kupata maumivu makali ya tumbo eneo la kwenye kitovu,chini ya kitovu,pembeni upande mmoja au kwenye kiuno

• Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi

• Mwanamke kupata maumivu ya tumbo upande mmoja,hii hutokea sana kwa wanawake ambao tatizo la mirija ya uzazi kuziba chanzo chake ni maji kujaa na kuziba kwenye mirija ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Hdyrosalpinx

• Baadhi ya wanawake hupata shida ya kutoa damu ukeni yaani vaginal bleeding n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

✓ Kwanza ifahamike kwamba, mwanamke huweza kupata shida ya mirija ya uzazi kuziba upande mmoja au mirija yote miwili yaani kulia na kushoto,

Endapo kuziba kumetokea upande mmoja uwezekano wa mwanamke huyu kubeba mimba bado upo, ila Mwanamke huyu yupo pia kwenye hatari ya mimba hii kutunga nje ya kizazi, yaani kupatwa na tatizo la Ectopic pregnancy

Na endapo mirija yote miwili ya Uzazi imeziba ningumu sana kwa mwanamke huyu kubeba mimba mpaka atibiwe,

VIPIMO AMBAVYO HUWEZA KUFANYIKA

Moja ya vipimo ambavyo huweza kufanyika ni pamoja na;

1. Kipimo cha Hysterosalpingograph(HSG),Kipimo hiki ni aina ya X-ray ambayo husaidia kuona ndani ya mirija ya uzazi

2. Na kipimo kingine ni Laparoscopy N.k

3. Kipimo cha Ultrasound n.k

MATIBABU YA TATIZO LA MIRIJA YA UZAZI KUJAA MAJI

Moja ya tiba kwenye tatizo hili ni pamoja na Mwanamke kufanyiwa upasuaji wa kuondoa uvimbe,kuondoa Scars, au huduma ya Kuzibua mirija,matumizi ya dawa mbali mbali n.k Kutegemea na chanzo cha tatizo lenyewe.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD