Tukio la kushangaza lililoripotiwa nchini Brazil liliwaacha Watu wakiwa na mshangao, baada ya msichana mwenye umri wa miaka 19 kujifungua mapacha wenye baba tofauti.
Kitaalamu, hali hii adimu inajulikana kama Heteropaternal Superfecundation, ambayo hutokea pale ambapo mayai mawili yanatolewa na yakaweze kurutubishwa na mbegu za wanaume wawili tofauti katika kipindi kimoja cha ovulesheni.
Vipimo vya vinasaba (DNA) vilithibitisha kuwa watoto hao wawili wanashirikiana mama mmoja, lakini kila mmoja ana baba tofauti.
Kisa kama hiki ni nadra sana kutokea duniani, na ni wachache tu waliowahi kuripotiwa katika historia ya tiba.
Wataalamu wa afya wamesema tukio hilo linaonesha upekee na ugumu wa mifumo ya uzazi wa binadamu, na kwamba sayansi bado inaendelea kugundua mambo mapya kuhusu maajabu ya asili ya mwanadamu.









image quote pre code