Showing posts with label videos. Show all posts
Showing posts with label videos. Show all posts

Chanzo cha Tatizo la Choo Kigumu yaani Constipation na Kukosa choo kabsaAfyaclass Forum •

Chanzo cha Tatizo la Choo Kigumu yaani Constipation na Kukosa choo kabsa

Nini Husababisha Constipation/ Kukosa Choo Au Kupata Choo Kigumu?

Umewahi kujiuliza kwanini unakosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu na kwa shida, huku ukipata maumivu makali wakati wa kujisaidia? Kwa kiasi kikubwa kukosa choo na choo kigumu husababishwa na mkusanyiko wa sababu nyingi

Constipation Ni Nini?

Constipation inalezwa kwamba ni ugumu wa kutoa uchafu wote kwenye tumbo, hii ni kutokana na choo kuwa kigumu. Kwa maaana nyingine ni kwamba ni hali ya kupungua kwa kasi ya utoaji kwa uchafu/kinyesi tumboni ama kupata choo kigumu au kukosa choo kabsa kwa muda mrefu

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

SABABU;

- Sababu hizi ni pamoja na lishe yako, kiasi gani mwili wako unaushugulisha, na na jinsi unavocontrol stress/msongo wa mawazo. 

Sababu kubwa kabisa ikiwa ni ulaji wa vyakula vyenye kiwango kidogo sana cha kambakamba/fibers na matumizi kidogo ya maji .

Unapopata constipation baadhi ya dalili huanza kujitokeza kwenye mfumo wa chakula kama; kupungua wa kasi ya utoaji wa kinyesi au uwepo wa kiasi kidogo cha kinyesi, kuchelewa kwa utolewaji wa kinyesi kuliko kawaida. Kama unaumwa magonjwa kama Irritable bowel syndrome (IBS) au ugonjwa mwingine kwenye mfumo wa chakula basi yaweza kuwa ndio chanzo cha constipation.

Sababu za kukosa choo na choo kigumu

Hapa chini ni sababu zinopelekea upate constipation

1. Lishe mbovu: Vyakula vilivyosindikwa sana, sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe. Vyakula vilivyoongezwa sukari na kemikali za kutunza chakula kisiharibike na mafuta mabaya huleta ugumu kwenye utengenezaji na utolewaji wa kinyesi na hivo kukupelekea kukosa choo kwa muda mrefu.

2. Msongo wa mawazo: Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) na kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.

3. Kutoshughulisha mwili: Mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi. Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

4. Matumizi ya baadhi ya vidonge: Baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu. Mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.

5. Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula: Bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula. Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vyenye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bacteria wazuri kukua na kufanya kazi.

Tiba Ya Lishe Kwa Tatizo La kukosa choo na choo kigumu

Kwa mgonjwa unayekosa choo kwa muda mrefu unapoanza safari ya kutibu constipation kwa kutumia lishe basi kumbuka kufahamu vyakula gani ule kwa sana, vyakula gani usile, na virutubisho gani utumie na pia baadhi ya mtindo wa maisha kurekebisha ili ujizuie kupata constipation na utibu ukiwa nyumbani mwako.

Vyakula kwa ajili ya mgonjwa wa constipation ni

- Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi: Kwenye mlo wako weka vyakula vingi vyenye kambakamba au nyuzinyuzi mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, apple na viazi vitamu

- Mbogamboga za kijani: licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijan, pia kunamdini mengi ya magnesium ambayo tumeona hapo juu husaidia katika ufanyaji kaz mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la constipation.

- Tumia kinywaji cha uvuguvugu: kama una tatizo la constipation jaribu kutumia chai ya moto asubuhi, au tumia maji yaliyochanganywa na limau, chai ya kuding kutoka china ni nzuri zaidi unaweza kuipata ofsini kwetu, inakusaidia kutibu tatizo hili haraka kwa sababu imeongezwa mimea tiba mingi.

Vyakula vya kuacha kabisa kutumia kwa mgonjwa ni pomoja na

  • Vyakula vilivyokaushwa kwenye mafuta
  • Vyakula na vinywaji vilivyopikwa kwenye joto kali sana mfano maziwa yaliyosindikwa
  • Unga uliokobolewa na kusafishwa kupita kiasi
  • Vinjwaji vyenya caffeine kwa wingi kama kahawa na baadhi ya chai

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



0 Comment

MADHARA YA SUKARI KUZIDI KWENYE DAMU KWA MUDA MREFUAfyaclass Forum •

    SUKARI

• • • • •

MADHARA YA SUKARI KUZIDI KWENYE DAMU KWA MUDA MREFU


Uwepo wa sukari iliyozidi kiasi cha kawaida mwilini kwa muda mrefu huharibu mshipa wa fahamu wa vagus (vagus nerve),


 ambao huongoza utendaji kazi wa viungo vya ndani ya mwili hasa upumuaji,mmeng’enyo wa chakula pamoja na mapigo ya moyo. Huongoza pia matendo yasiyo ya hiari ya mwili kama vile kutapika,kukohoa pia kupiga chafya

-

Kwa watu walio na sukari nyingi mwilini,uwezo wa neva ya vagus katika kuratibu miondoko ya chakula kutoka kwenye tumbo kwenda kwenye utumbo hupungua. Unaweza usiwe na hisia za njaa kabisa,


unaweza kuanza kusumbuliwa na kiungulia cha mara kwa mara,maumivu ya tumbo,kutapika pamoja na kusumbuliwa sana na tatizo la choo kigumu. Fika hospitalini upime sukari yako!


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

TATIZO LA KULEGEA KWA UKE Pamoja na Chanzo ChakeAfyaclass Forum •

UKE

• • • •

TATIZO LA KULEGEA KWA UKE


Kulegea kwa uke ni moja ya mada inayowakuna sana wakina mama na wakina dada . Wengi hupendelea zaidi kuwa na uke uliobana ili kuwafurahisha wenza wao. 


Kuna nadharia dhana potofu nyingi sana kuhusu suala la uke wengine huamini kwamba Uke unatakiwa kupoteza hali ya kutanuka na kusinyaa na kuwa mkubwa miaka yote.


Uke ni kiungo chenye lastiki maana yake kinaweza kunanuka ili kuruhusu kutoka mfano mtoto na vitu kuingia yani uume. Lakini haitachukua muda mrefu kwa uke kusinyaa na kurudi katika hali ya kawaida.


Uke hutanuka, kulegelea  na kuongezeka ukubwa kiasi fulani kadiri umri unavoongezeka na unavozaa zaidi. Sasa endelea kusoma makala yetu hii ili ufahamu vyema uke wako pamoja na fikra potofu kuhusu uke.


Nataka nikwambie kulegea kwa uke ni dhana mbaya ambayo inatumika kuwadhalilisha wanawake, na inawatokea zaidi hasa pale wanapoachana na wanaume zao. 


Wanaume hutumia hiki kama kigezo na silaha ya kuwadhalilisha wanawake kwamba wana uke mpana na wenye maji (bwawa) kitendo ambacho siyo kizuri. 


Soma: Tatizo la Uke Kujamba,Chanzo,Dalili na Tiba


Dhana potofu ni kwamba mwanamke mwenye kulegea kwa uke amekutana kimapenzi na wanaume wengi. Ukweli ni kwamba haijalishi umekutana na wanaume wangapi uke ni lastiki unaweza kutanuka na kusinyaa na ukaendelea kuwa kwenye ubora wake kama kawaida


Je Inawezekana Kutibu Kulegea Kwa Uke?


Uke Uliokaza siyo Kitu cha Lazima Sana


Ni muhimu kufahamu kwamba kuwa na uke uliokaza sana inaweza kuashiria una tatizo la kiafya hasa pale unapoingiliwa na kupata maumivu makali pamoja na kwamba mwenza wako amekuandaa vizuri.


 Mwili wa mwanamke unaposisimka misuli ya uke inalegea ili kuruhusu uume kupenya vizuri.


Kama misuli ya uke bado imekaza basi itakufanya upate maumivu makali sana na hutofurahia na kumaliza tendo la ndoa. 


Kama tatizo la maumivu ya uke yataendelea basi weka apointment na dactari wa magonjwa ya wanawake ili upate vipimo na ushauri zaidi maana unaweza kuwa na matatizo yafuatayo;


- Hujaandaliwa vizuri na uke kutolowa inavotakiwa


Mwili wa mwanamke unaposisimuliwa basi huweza kutoa majimaji ya asili ambayo hulaishisha uke. Hivo hakikisha mwenza wako anakuaanda vizuri kabla ya kukuingilia. Kama una tatizo la kupata majimaji kidogo haijalishi umeandaliwa kiasi gani basi


- Maambukizi au ugonjwa kama vile kwenye via vya uzazi yaani PID,Fangasi,UTI n.k


Maambukizi hasa ya kupitia ngono ni chanzo cha kupata maumivu wakati wa tendo.


- Ajali na Msongo wa mawazo kupita kiasi.


Ajali kwenye maeneo ya nyonga na mfumo wa uzazi kwa ujumla inaweza kusababisha maumivu makali wakati watendo la ndoa na kukaza kwa uke. Hivo hakikisha umepona vizuri kabla hujaanza kushiriki ngono


- Tatizo la Viginismus


Vaginismus ni tatizo la uke ambapo misuli ya uke inaweza kukaza pasipo hiyari ya mwanamke na hio kuzuia uume kupenya. Wanawake wachache sana hukubwa na tatizo hili yaweza kuwa mmoja kati ya wanawake 500. 


Tatizo hili linaweza kuletekezwa na hofu na msongo wa mawazo. dactari anaweza kutumia tiba zaidi ya moja katika kutatua shida hii ikiwemo kuongea na mgonjwa na kumshauri ama kutumia vifaa vya kutanua uke.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




0 Comment

MADHARA YA MTOTO KUNYWA MAJI YA UCHUNGU AU UZAZIAfyaclass Forum •


MAJI YA UZAZI

• • • • •

MADHARA YA MTOTO KUNYWA MAJI YA UCHUNGU AU UZAZI

Moja ya ishara ya tatizo hili ni mtoto kutokulia baada ya kuzaliwa

Baada ya mtoto kunywa maji ya uchungu au uzazi wakati wa kuzaliwa huweza kupata madhara mbali mbali kama vile;

1. Kuziba kwa njia ya hewa ambayo huweza kusababisha tatizo la upungufu wa oxygen kwenye ubongo

2. Kuwa na matatizo ya ubongo

3. Kuwa na tatizo la upumuaji

4. Kuwa na tatizo la mapafu 

5. Maambukizi ya magonjwa mbali mbali hasa baada ya mtoto kunywa maji ya uzazi ambayo yamechanganyika na kinyesi kwa kitaalam hujulikana kama meconium

6. Kupatwa na tatizo la kukakamaa mwili

7. Kulegea viungo mbali mbali vya mwili

8. Kuwa na tatizo la kuharisha 

9. Kuwa na tatizo la kutapika

10. Mtoto kupatwa na tatizo la Pneumonia

N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Maji haya ya Uzazi hufanya kazi muhimu wakati Mtoto anakua kwenye uterasi ya mama yake.  Majimaji haya humkinga mtoto anayekua dhidi ya matuta na mapigo kwa mwili wa mama. Maji haya yanakuza ukuaji wa misuli na mifupa.  Na, wakati mwingine mtoto akimeza ndani ya tumbo, maji ya amniotic husaidia njia ya utumbo wa mtoto kuendelea vizuri.

 Kwa bahati mbaya, ikiwa mtoto huvuta maji ya amniotic wakati wa mchakato wa kuzaliwa, matatizo makubwa yanaweza kutokea.  Kupitisha maji haya kwenye bomba la upepo au mapafu kwa bahati mbaya huweza kusababisha tatizo ambalo kitaalam hujulikana kama aspiration, and amniotic fluid aspiration, Na hali hii huweza kusababisha matatizo makubwa ikiwa haitatambuliwa na kutibiwa mara moja.

Jinsi ya Kugundua Kwamba Mtoto amekunywa Maji ya Uzazi

Kupitia Dalili Mbali mbali ikiwemo hizi;
  • Mtoto kupata Shida ya Kupumua
  • Mtoto kukoroma sana
  • Mtoto kuwa na kikohozi ambacho hakiishi
  • Kupatwa na tatizo la kukakamaa mwili 
  • Kuwa na tatizo la kutapika
  • Kuwa na tatizo la kuharisha 
  • Kulegea viungo mbali mbali vya mwili n.k

Wafanyikazi wa Afya wanaweza kugundua tatizo la meconium aspiration kwa kuangalia kiowevu cha amniotiki wakati wa kuzaliwa ikiwa kuna uwepo wa meconium. 

 X-ray ya kifua pia inaweza kufanywa.  Mtoto ambaye amekunywa meconium anaweza kuwa na shida ya kupumua, au kupumua haraka;  kutoa sauti au kelele za gurgling wakati wa kupumua;  shida inayoonekana wakati wa kupumua au kuonekana kuwa na kifua kilichojaa;  au kuwa na rangi ya tofauti kwenye ngozi na kucha.

Kunywa meconium ni hali ambayo hutokea kwa idadi ndogo ya watoto wanaozaliwa,Ila  Inapotokea, inaweza kutishia maisha yao.

Meconium, kama ilivyo kwa kinyesi chochote, ina bakteria ambayo, ikiwa haitatibiwa mara moja, inaweza kusababisha nimonia kukua.  Katika baadhi ya matukio, nimonia inaweza kusababishwa na maambukizi ya virusi, lakini visa vingi vya nimonia kwa watoto wachanga ni maambukizi ya bakteria.

 Nini cha Kufanya Ikiwa Mtoto kanywa Maji ya Uchungu au Uzazi?

 Ikiwa mtoto anashukiwa kunywa maji ya Uzazi anaweza kupewa dawa mbali mbali ikiwemo jamii ya antibiotics.  Kwa sababu mtoto mchanga anaweza kuwa na mfumo mdogo au Dhaifu wa kinga, antibiotics inaweza kuwa msaada muhimu.  

Ikihitajika, wataalam wa Afya wanaweza kumweka mtoto kwenye kipumuaji ili kupunguza mzigo kwenye mapafu ya mtoto mchanga na kuleta utulivu wa kupumua.

 Oksijeni pia inaweza kuhitaji kusimamiwa.  Katika hali mbaya zaidi, mtoto anaweza kuhitaji oksijeni ya membrane ya nje (ECMO) kusaidia au kuchukua nafasi ya utendakazi wa mapafu.

 Wakati mwingine inawezekana kuzuia mtoto kunywa maji ya Uzazi yenye meconium.  Kwa mfano, ikiwa wafanyakazi wa Afya wanashuku kuwa kiowevu cha amniotiki kina meconium, wanaweza kuagiza utiaji amnioin wakati wa leba, ambayo inaruhusu kiowevu kilicho na meconium kutolewa.

Lakini kwa Hali Flani,matibabu ya Upasuaji kwa Ajili ya mama kujifungua(C-section) inaweza pia kufaa Zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

0 Comment
Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD