UGONJWA WA MATENDE, VISABABISHI VYAKE PAMOJA NA DALILI ZAKE
Tweet
Matende ni Ugonjwa unaosababisha Ngozi pamoja na Tisu za Chini ya Ngozi kuwa Nene.Ugonjwa huu huathiri maeneo mbali mbali Kama mikono,Miguu, korodani,Figo n.k
VISABABISHI VYA UGONJWA HUU WA MATENDE
Matende husababishwa na Vimelea jamii ya minyoo au PARASITIC WORMS ambavyo hujulikana kwa jina la Wuchereria Bancrofti,Brugia Malayi,B.Timori ambapo vyote huenezwa na Mbu jike aina ya Culex quinquefasciatus na jamii ya Mbu Dume Anopheles Species,Wakati huo Minyoo aina ya Brugia Roundworms huenezwa na Mbu anayejulikana kama Mansonia Mosquitoes ambapo hawa hueneza ugonjwa huu kutoka kwa Mtu mmoja kwenda kwa Mwingine.
ZIPI NI DALILI ZA UGONJWA WA MATENDE
- Dalili kubwa ya kuwepo kwa Ugonjwa wa Matende ni kuvimba sehemu ya chini ya Mwili Kama Miguu na Vidole vyake
- Ngozi ya Sehemu iliyoathirika huwa Ngumu sana na kukakamaa
- Sehemu au kiungo kilichoathirika Kushindwa kufanya chochote
- Ngozi kuwa nene na Ngumu
- Kupata maumivu ya sehemu iliyoathirika
- Homa pamoja na maumivu ya Kichwa
- Kuwepo kwa vidonda maeneo yaliyothirika Mfano kwenye Miguu na vidole vyake
- Kupatwa na Kichefuchefu na Kutapika
- Kuwepo kwa Mistari ya Rangi Nyekundu kwenye Miguu au mikono
- Kupata maumivu kwenye Viungo Pamoja na Joint
VIPIMO;
Kuna vipimo mbalimbali ikiwemo vya Kuchunguza Damu na Hadubini, ( Blood examination with Microscope)
.
.
REPLY HAPA
image quote pre code