Afyaclass DALILI ZA MTU MWENYE UPUNGUFU WA VITAMIN D Mwilini

 VITAMIN D

• • • • •

DALILI ZA MTU MWENYE UPUNGUFU WA VITAMIN D  Mwilini


Katika makala hii tunazungumzia tatizo la upungufu wa vitamin D mwilini yaani kwa kitaalam Vitamin D deficiency. Kwa  ujumla, vitamin mbali mbali ni muhimu sana kwenye mwili wako na kila aina ya vitamin ina kazi zake mwilini, hapa nazungumzia mfano; vitamin A, Vitamin B6, Vitamin C, Vitamin D, Vitamin B9, Vitamin B12 n.k


Upungufu wa vitamin D mwilini unasababishwa na nini? Na dalili zake ni zipi?(soma makala hii)


CHANZO CHA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI NI PAMOJA NA;


- Kula vyakula ambavyo havina vitamin D  kwa muda mwingi


- Kukaa mbali na jua kwa muda mrefu kwani utengenezaji wa vitamin D mwilini mwako hutegemea pia jua.


- Figo zako kushindwa kubadilisha vitamin D kuwa katika hali ya kutumika zaidi hasa kwa watu wenye umri mkubwa


- Kuwa na ngozi nyeusi sana, tafiti zinaonyesha melanini huweza kupunguza ngozi kutengeza vitamin D pale inapopigwa na jua


- Tatizo la mfumo wako wa umeng'enyaji kushindwa kufyoza vizuri vitamin D mbali na chakula unachokula chenye vitamin vya kutosha.


DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI


- Kupata maumivu ya mgongo mara kwa mara


- Kupata maumivu ya misuli,joint pamoja mifupa ya mwili mara kwa mara


- Kuwa na tatizo la vidonda kutokupona haraka


- Uchovu wa mwili kupita kiasi


-  kuwa na tatizo la Nywele kukatika sana na kunyonyoka zenyewe


- Watoto kuwa na shida ya matege


- Kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara kutokana na kinga yako ya mwili kutokufanya kazi vizuri

N.k


TIBA YA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI


- Matibabu ya upungufu wa vitamin D mwilini huhusisha matumizi ya vyakula vyenye kiwango cha kutosha cha vitamin D, Dawa zakusaidia umeng'enyaji pamoja na ufyozwaji wa vitamin D mwilini, pamoja na matumizi ya Virutubisho mbali mbali yaani supplements


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




You, Mehreen and others

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
Karibu Afyaclass Forum Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Forum ASANTE.
UNDERSTOOD