Chanzo cha Tatizo la Choo Kigumu yaani Constipation na Kukosa choo kabsa

Chanzo cha Tatizo la Choo Kigumu yaani Constipation na Kukosa choo kabsa

#1

Chanzo cha Tatizo la Choo Kigumu yaani Constipation na Kukosa choo kabsa

Nini Husababisha Constipation/ Kukosa Choo Au Kupata Choo Kigumu?

Umewahi kujiuliza kwanini unakosa choo kwa muda mrefu au kupata choo kigumu na kwa shida, huku ukipata maumivu makali wakati wa kujisaidia? Kwa kiasi kikubwa kukosa choo na choo kigumu husababishwa na mkusanyiko wa sababu nyingi

Constipation Ni Nini?

Constipation inalezwa kwamba ni ugumu wa kutoa uchafu wote kwenye tumbo, hii ni kutokana na choo kuwa kigumu. Kwa maaana nyingine ni kwamba ni hali ya kupungua kwa kasi ya utoaji kwa uchafu/kinyesi tumboni ama kupata choo kigumu au kukosa choo kabsa kwa muda mrefu

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

SABABU;

- Sababu hizi ni pamoja na lishe yako, kiasi gani mwili wako unaushugulisha, na na jinsi unavocontrol stress/msongo wa mawazo. 

Sababu kubwa kabisa ikiwa ni ulaji wa vyakula vyenye kiwango kidogo sana cha kambakamba/fibers na matumizi kidogo ya maji .

Unapopata constipation baadhi ya dalili huanza kujitokeza kwenye mfumo wa chakula kama; kupungua wa kasi ya utoaji wa kinyesi au uwepo wa kiasi kidogo cha kinyesi, kuchelewa kwa utolewaji wa kinyesi kuliko kawaida. Kama unaumwa magonjwa kama Irritable bowel syndrome (IBS) au ugonjwa mwingine kwenye mfumo wa chakula basi yaweza kuwa ndio chanzo cha constipation.

Sababu za kukosa choo na choo kigumu

Hapa chini ni sababu zinopelekea upate constipation

1. Lishe mbovu: Vyakula vilivyosindikwa sana, sukari, nafaka iliyokobolewa, pombe. Vyakula vilivyoongezwa sukari na kemikali za kutunza chakula kisiharibike na mafuta mabaya huleta ugumu kwenye utengenezaji na utolewaji wa kinyesi na hivo kukupelekea kukosa choo kwa muda mrefu.

2. Msongo wa mawazo: Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kupata mcharuko/mpambano ndani ya mwili (inflammation) na kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.

3. Kutoshughulisha mwili: Mazoezi yanasaidia kuimarisha mzunguko wa damu kwenye mfumo wa chakula na kuimarisha misuli na hivo kurahisisha utolewaji wa kinyesi. Utafiti unasema watu wanaotumia mda mwingi wakiwa wamekaa hasa maofsini wanaongoza kwa kuapata matatizo ya kukosa choo kwa mda mrefu.

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

4. Matumizi ya baadhi ya vidonge: Baadhi ya vidonge husababisha kukosa choo kwa muda mrefu na kupata choo kigumu. Mfano dawa za kupunguza maumivu, dawa za kuconrtol stress, dawa za kulevya, virutubisho vya calcium na magnesium na antiacids.

5. Ukuaji wa bacteria wabaya kwenye mfumo wa chakula: Bacteria wazuri/normal flora waliopo kwenye mfumo wa chakula tunawaita probiotics husaidia kwenye uchakataji wa chakula. Ndio maana kuna umuhimu wa kula vyakula vyenye kambakamba kwa sababu ni mbolea nzuri kwa bacteria wazuri kukua na kufanya kazi.

Tiba Ya Lishe Kwa Tatizo La kukosa choo na choo kigumu

Kwa mgonjwa unayekosa choo kwa muda mrefu unapoanza safari ya kutibu constipation kwa kutumia lishe basi kumbuka kufahamu vyakula gani ule kwa sana, vyakula gani usile, na virutubisho gani utumie na pia baadhi ya mtindo wa maisha kurekebisha ili ujizuie kupata constipation na utibu ukiwa nyumbani mwako.

Vyakula kwa ajili ya mgonjwa wa constipation ni

- Vyakula vyenye kambakamba/fibers kwa wingi: Kwenye mlo wako weka vyakula vingi vyenye kambakamba au nyuzinyuzi mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani, na mbegu. Parachichi, broccoli, apple na viazi vitamu

- Mbogamboga za kijani: licha ya kuwa na kambakamba nyingi kwenye mboga za kijan, pia kunamdini mengi ya magnesium ambayo tumeona hapo juu husaidia katika ufanyaji kaz mzuri wa misuli na hivo kupunguza tatizo la constipation.

- Tumia kinywaji cha uvuguvugu: kama una tatizo la constipation jaribu kutumia chai ya moto asubuhi, au tumia maji yaliyochanganywa na limau, chai ya kuding kutoka china ni nzuri zaidi unaweza kuipata ofsini kwetu, inakusaidia kutibu tatizo hili haraka kwa sababu imeongezwa mimea tiba mingi.

Vyakula vya kuacha kabisa kutumia kwa mgonjwa ni pomoja na

  • Vyakula vilivyokaushwa kwenye mafuta
  • Vyakula na vinywaji vilivyopikwa kwenye joto kali sana mfano maziwa yaliyosindikwa
  • Unga uliokobolewa na kusafishwa kupita kiasi
  • Vinjwaji vyenya caffeine kwa wingi kama kahawa na baadhi ya chai

•Soma: Chanzo cha tatizo la kuwashwa mwilini baada ya Kuoga

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Reply


image quote pre code
مشاركة: