Hii hapa ndyo bei ya kupima DNA TanzaniaAfyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema matokeo ya uchunguzi wa DNA (kuhakiki uhalali wa Watoto kwa Wazazi) ni ya uhakika na kwamba gharama ya uchunguzi ni Tsh. Laki moja kwa sampuli ya Mtu mmoja hivyo kwa uchunguzi wa Baba, Mama na Mtoto jumla ni Tsh. Laki 3 na malipo yote hufanyika Benki.

Akiongea leo November 30,2023 Jijini Dar es salaam Mkemia Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dr. Fidelis Mafumiko amesema ili kupata huduma ya uchunguzi zipo taratibu za kuzifuata ambapo Mteja haendi moja kwa moja kupima DNA ila anawakilishwa na Taasisi zilizotajwa kisheria ili kumuombea Mteja huduma ya uchunguzi, Taasisi hizo ni Ustawi wa Jamii, Mawakili, Mahakama, Jeshi la Polisi kwa masuala yanayohusu jinai n.k.

“Taasisi hizo zitaandika barua ya maombi ya kupatiwa huduma kwa niaba ya Mteja husika kwenda kwa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, na baada ya kulipia gharama sampuli zitachukuliwa na uchunguzi utafanyika na majibu yatatolewa kwa Taasisi iliyoandika barua ambapo Mteja atapata majibu kupitia Taasisi hizo ndani ya wastani wa siku 27 za kazi (kutegemea na aina ya sampuli).

Hii hapa ndyo bei ya kupima DNA Tanzania
0 Comment

Umuhimu wa vitamin D kwenye mifupa, fahamu hapaAfyaclass Bongo Social •

Umuhimu wa vitamin D kwenye mifupa, fahamu hapa

Vitamin D, inajulikana kwa jina la “vitamin ya jua,” ni muhimu sana kwa afya ya mifupa. Ina jukumu kubwa katika kusaidia mwili kuchukua na kutumia madini ya kalsiamu na fosforasi, ambayo ni muhimu kwa afya bora ya mifupa.

Kwa hiyo, umuhimu wa vitamin D kwenye mifupa hautiliwi tu maanani kwa sababu ya jukumu lake katika kuimarisha mifupa, bali pia kwa kuwa inaweza kusaidia kuzuia magonjwa kadhaa ya mifupa.

Vitamin D inapopatikana kwa kiasi cha kutosha mwilini, inachochea seli zinazohusika na mifupa (osteoblasts) kuzalisha protini inayoitwa osteocalcin, ambayo ni muhimu kwa kubadilisha kalsiamu kuwa mifupa imara.

Kwa kufanya hivyo, vitamin D inasaidia katika kuzuia upotevu wa kalsiamu kutoka kwenye mifupa, ambao unaweza kusababisha mifupa kuwa dhaifu na kuongeza hatari ya kuvunjika.

Utafiti unaonyesha kwamba upungufu wa vitamin D unaweza kusababisha magonjwa ya mifupa kama vile osteoporosis na osteomalacia.

Osteoporosis, kwa mfano, ni hali inayosababisha mifupa kuwa dhaifu na rahisi kuvunjika. Hali hii inaweza kuwa hatari, hasa kwa watu wa umri wa uzee, na inaweza kusababisha maumivu makali na upungufu wa uwezo wa kutekeleza shughuli za kila siku.

Kwa kuongeza, vitamin D ina jukumu muhimu katika kuzuia matege au rickets, hali inayojitokeza hasa katika utotoni.

Rickets inasababisha mifupa kulegea na kuwa na umbo la kupinda kutokana na upungufu wa kalsiamu na fosforasi,

Watoto walio katika hatari kubwa ya kupata Matege(rickets) ni wale ambao hawapati kiasi cha kutosha cha vitamin D, hususan kutokana na upungufu wa jua au lishe duni.

Ni muhimu kutambua kuwa mwili wetu hautoi vitamin D yenyewe kwa kiasi kikubwa, na hivyo tunategemea vyanzo vingine kama vile jua, vyakula, au virutubisho.

Jua ni chanzo kikuu cha vitamin D, na muda mfupi wa miale ya jua kila siku unaweza kutoa mahitaji ya mwili. Hata hivyo, wakati mwingine, mazingira kama vile hali ya hewa, muda wa mwanga wa jua, na matumizi ya kinga za jua yanaweza kupunguza uzalishaji wa vitamin D mwilini.

Lishe pia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa kutosha wa vitamin D. Vyakula kama samaki wa maji baridi, mayai, na vyakula vilivyoboreshwa na vitamin D vinaweza kuwa sehemu ya lishe yenye afya kwa ajili ya kudumisha afya bora ya mifupa.

Katika visa vya upungufu wa vitamin D, virutubisho vinaweza kuchukuliwa chini ya usimamizi wa kitaalamu wa afya. Hata hivyo, ni muhimu kuzingatia kwamba kama vile vitu vingine vyote, vitamin D inapaswa kutumiwa kwa kiasi kinachofaa, na watu wanapaswa kushauriana na wataalamu wa afya kabla ya kuanza matumizi ya virutubisho.

Kwa kumalizia, umuhimu wa vitamin D kwenye mifupa ni dhahiri katika kudumisha afya bora ya mifupa na kuzuia magonjwa ya mifupa. Kwa kuzingatia vyanzo vya vitamin D na kuhakikisha lishe bora, tunaweza kuweka mifupa yetu katika hali nzuri na kuimarisha afya yetu kwa ujumla.

Umuhimu wa vitamin D kwenye mifupa, fahamu hapa
0 Comment

Mzunguko wa HEDHI kuathiri uwezo wa Mwanamke kubeba MimbaAfyaclass Bongo Social •

Mzunguko wa HEDHI kuathiri uwezo wa Mwanamke kubeba Mimba

• • • • •

JE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI UNAWEZA KUATHIRI UWEZO WAKO WA KUBEBA MIMBA?

Hili ni swali ambalo baadhi ya wanawake hujiuliza sana hasa wakiwa na matatizo katika mizunguko yao ya hedhi pamoja na tatizo la kutokubeba mimba,

Ukweli ni kwamba mzunguko wako wa hedhi unaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la wewe kutokubeba mimba,

Hapa nazungumzia wanawake ambao wana matatizo mbali mbali kwenye mzunguko wa hedhi kama vile;

✓ Mzunguko wa hedhi ambao hubadilika badilika au usio kuwa na siku maalumu yaani kwa kitaalam tunaita Irregular menstrual cycle

✓ Kuchelewa sana kupata siku zao za hedhi,mfano kwa baadhi ya wanawake huweza kukaaa miezi miwili,mitatu N.k pasipo kuona hedhi

✓ Kublid damu nyingi na kwa muda mrefu bila kukata mfano zaidi ya wiki moja mtu anablid

✓Na ambao kila wakipata hedhi huonyesha dalili ya maambukizi ya magonjwa mengine kama vile; Mwanamke kupata hedhi ambayo inaenda sambamba na kuvimba mwili,miguu N.k,

hedhi inayoenda sambamba na kichefuchefu pamoja na kutapika sana

hedhi inayoenda sambamba na kuumwa sana hadi kufikia hatua ya kulazwa hospital N.k

Hivo wanawake wenye matatizo haya hata uwezo wa kubeba mimba huweza kuwa mdogo,

– lakini pia wengine hawajui kuhesabu siku za hatari katika mzunguko wao wa hedhi, hivo kufanya mapenzi siku ambazo hata ujauzito hawawezi kupata,

Kumbuka kuna aina kuu tatu ya mizungo ya hedhi kwa wanawake Mfano

• Mzunguko mfupi ambao ni mzunguko wa siku 21

• Mzunguko wa wastani ambao ni Mzunguko wa siku 28

• Na mzunguko mrefu ambo ni Mzunguko wa siku 30,33, 35 N.k

HITIMISHO; hivo kwa kuhitimisha, kutokana na maelezo niliyoyatoa hapo juu, ni kweli kwamba mzunguko wa hedhi huweza kuathiri uwezo wa mwanamke kubeba mimba

fahamu pia; Kuna asilimia chache sana ya wanawake ambao huweza kubeba mimba wakiwa katika siku zao za hedhi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mzunguko wa HEDHI kuathiri uwezo wa Mwanamke kubeba Mimba
0 Comment

Fanyeni tafiti ili kuboresha huduma za maabaraAfyaclass Bongo Social •

Fanyeni tafiti ili kuboresha huduma za maabara

Na: WAF, Dodoma

Wahititimu wa mafunzo ya uongozi wa maabara chini ya programu ya Global laboratory Leadership Program (GLLP) wametakiwa kufanya tafiti katika huduma za uchunguzi wa magonjwa katika sehemu ya usimamizi wa huduma za maabara ili kudumisha huduma za uhakika katika maabara Nchini.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Dharura na maafa Wizara ya Afya Dkt. Elias Kwesi wakati akimuwakilisha Katibu mkuu wa Wizara ya afya Dkt. John Jingu katika mahafali ya mafunzo ya uongozi wa maabara kupitia programu ya Global Laboratory Leadership Program iliyofanyika Novemba 29, 2023 jijini Dodoma.

Dkt. Kwesi amesema kupitia tafiti ambazo zitafanywa na wahitimu haoz itasaidia katika kuchunguza na kugundua namna ya kuboresha huduma za maabara katika hospitali, vituo vya afya na zahanati.

“Nendeni mkafanye tafiti, tafiti hizi zitasaidia katika kuboresha huduma za maabara hasa katika uchunguzi wa magonjwa na kuboresha huduma zenyewe”. Amesema Dkt. Elias.

Aidha Dkt. Kwesi amesema ili kuweza kufanikiwa ni vyema kwa wahitimu wakazingatia na kuyafanyia kazi mafunzo waliopata ili kudumisha ubora Nyanja za maabara kwa kutoa huduma nzuri..

Hata hivyo Dkt. Kwesi ameongeza kuwa eneo la maabara ni eneo la heshima, hivyo ukiingia maabara unatakiwa uwe na heshima kwai ni sehemu nyeti kwa ajili ya uchunguzi na utoaji wa huduma.

Fanyeni tafiti ili kuboresha huduma za maabara
0 Comment

Fahamu kuhusu andropause, "ukomo wa uzazi kwa wanaumeAfyaclass Bongo Social •

Andropause, “ukomo wa uzazi kwa wanaume

Viwango vya chini vya testosterone vinaweza kutokea na kusababisha athari hususani katika afya ya ngono.

Maumbile ya kibaiolojia ya wanaume na wanawake huwa hayana mfumo unaofanana kila wakati. Mfano wa hili ni mabadiliko ya baadhi ya homoni za kawaida.

Kwa upande wa vitu kama vile homoni za estrojeni hatua kwa hatua huacha kuzalishwa katikati ya muongo wa tano wa maisha.

Kwa wakati huu, unaojulikana kama ukomo wa hedhi, mwanamke hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi kutoka kwenye ovari na kupata hedhi na kuwa vigumu kupata mimba kwa njia za asili kwasabau hupoteza uwezo wa kuzalisha mayai ya uzazi.

Kwa upande mwingine kwa binadamu hakuna mchakato unaofanana. Homoni ya kiume inayohusishwa na uzalishaji wa mbegu za kiume (testosterone ) miongoni mwa kazi zake nyingine, huonekana kuendelea kubaki mara kwa mara katika maisha yote ya mwanamume , hata baada ya kufikia umri wa miaka 50, 60 au 70.

Ikiwa tunafuata hoja hii, neno “andropause” – ambalo limepata umaarufu kuelezea aina ya “kufikia ukomo wa uwezo wa kuzalisha wa wanaume”, na kupunguza uwezekano wa uzalishaji wa testosterone baada ya umri fulani – haina maana ya kimantiki, kulingana na wataalam.

Lakini ni muhimu kufikiria kuwa: kuna visa vinavyotokana na msururu wa matukio ambavyo huweza kusababisha kushuka kwa homoni za kiume testosterone na hivyo kusababisha athari mbaya ambazo hazikutarajiwa.

Hali hizi, zinazojulikana kama hypogonadism (ukomo wa uzazi wa kiume), zina vigezo vya uchunguzi na matibabu.

Hivi karibuni, miongozo ya usimamizi wa upungufu wa homoni za kiume imepitia mfululizo wa mabadiliko, kwa lengo la kuzuia matumizi ya kupita kiasi ya testosterone kama steroid ya anabolic, kwa madhumuni ya urembo kwa wanaume au wanawake

Hadithi ya andropause

“Maelezo yoyote ya andropause lazima yaanze na ukweli kwamba haipo,” anasema Dk Alexandre Hohl, rais wa zamani wa Jumuiya ya Brazil ya wataalamu wa magonjwa mbali mbali ya homoni (SBEm).

“Neno hili ni neologism lilibuniwa kutokana na dhana ya ukomo wa uzazi, asili yake ikiwa ni kutoka lugha ya Kilatini: linahusiana na usumbufu unaotokana na ukomo wa hedhi. Kwa maneno mengine, kumaliza hedhi ni kukomesha hedhi” , anaelezea.

“Kutoka hapo, mtu alikuwa na wazo la bahati mbaya la kuunda dhana ya andropause, ambalo linasababisha tu utambuzi wa makosa na matumizi yasiyo ya lazima ya testosterone,” analalamika Dk Hohl.

Daktari Luiz Otávio Torres, katibu mkuu wa Jumuiya ya madaktari wa maradhi ya kibofu cha mkojo ya Brazil, anakubaliana.

Dkt Hohl anaeleza kuwa katika maisha yao yote, wanaume hawana uzoefu wa jambo kama la kumaliza hedhi, kama wanawake wanavyofanya.

“Kibaiolojia , wanaume hupungukiwa kwa taratibu na uzalishaji wa homoni za kiume za kuzalisha testosterone, hasa baada ya umri wa miaka 40 au 50. Lakini kama ni mtu mzima mwenye afya, huenda akafikia miaka yake ya 60, 70 au hata 80 na viwango vya kutosha vya homoni hii, bila ya haja ya kuingilia kati au kuibadilisha,” anaelezea.

Upungufu huu wa taratibu na wa asili katika homoni ya kiume, ambayo huzalishwa na korodani, hutokea kwa kiwango cha asilimia 1.2 kwa mwaka kutoka umri wa miaka 40 au 45.

“Kwa maneno mengine, wanaume wanaweza hata kuwa na kupungua kwa testosterone, lakini hawaachi kuzalisha homoni kama wanawake,” Torres anaelezea kwa kifupi.

Lakini kushuka kwa homoni hii kunaweza kuongezeka kutokana na sababu nyingine , kama vile ugonjwa wa kisukari au kuongezeka kwa unene wa kupindukia wa mwili.

Kwa watu wenye magonjwa haya au mengine sugu, viwango vya testosterone vinaweza kupungua zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Hali hii inaitwa hypogonadism ya kiume.

Sababu nyingine zinazoweza kusababisha kupungua kwa homoni hii ni pamoja na magonjwa yanayoathiri tezi ya pituitary (muundo wa ubongo unaohusika na kudhibiti uzalishaji wa testosterone katika korodani) au viungo vya uzazi vya kiume vyenyewe.

Pia kuna watu ambao, kwa sababu za maumbile, hawapitii michakato inayohusiana na kubalehe na matokeo yake hawakupata ukuaji katika uume wao, korodani na nywele za siri.

Lakini je ni wakati gani madaktari wanashuku hypogonadism?

Fahamu kuhusu andropause, "ukomo wa uzazi kwa wanaume
0 Comment

WHO inataka data mpya kutoka China kufuatia mlipuko wa nimonia kwa watotoAfyaclass Bongo Social •

Shirika la Afya Duniani (WHO) linaomba data zaidi kutoka China huku kukiwa na mlipuko wa nimonia kwa watoto.

Daktari Maria Van Kerkhove, mtaalam wa magonjwa WHO, alisema shirika hilo ‘linafuatilia Uchina’ huku hospitali kote nchini zikiendelea kuzidiwa.

Kuvaa mask au barakao na kuepuka kukaa kwenye mikusanyiko ya watu vinapendekezwa tena nchini.

Nchi inasemekana kukabiliwa na ugonjwa wa nimonia, unaoitwa ‘ugonjwa wa mapafu meupe’ kwa sababu ya jinsi uharibifu wa mapafu unavyoonekana kwenye uchunguzi miongoni mwa watoto, ambapo ugonjwa huu umehusishwa na kurudi tena kwa magonjwa ya kupumua badala ya virusi vipya kabisa.

China ilikuwa na baadhi ya watu waliofungiwa(kuwekwa lockdown) kwa muda mrefu zaidi kuliko nchi yoyote duniani ambapo WHO inasema iliwanyima watoto kinga muhimu dhidi ya magonjwa ya msimu.

Dk Van Kerkhove aliuambia mkutano leo: ‘Ndiyo, tunaona ongezeko la magonjwa ya kupumua duniani kote.

“Tuko katika vuli na tunaingia katika miezi ya msimu wa baridi, kwa hivyo tunatarajia kuona kuongezeka kwa maambukizo ya kupumua bila kujali.

“Tunafuatilia China. Wanaona ongezeko kutokana na idadi ya maambukizo tofauti.

‘Tunafuatilia mtandao wetu wa kimatibabu nchini China.

“Kuhusiana na magonjwa ya kupumua kwa papo hapo, tunaangalia mzigo kwenye mifumo ya huduma ya afya na kuangalia uwezo wa huduma za afya kwenye mifumo.”

Inakuja baada ya msemaji wa Wizara ya Afya ya China Mi Feng kuwataka watu nchini humo kufikiria tena kuvaa barakoa na kujitenga.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumapili, alisema: ‘Juhudi zinapaswa kuchukuliwa kuongeza ufunguzi wa kliniki husika na maeneo ya matibabu, kuongeza muda wa huduma na kuongeza usambazaji wa dawa.

“Ni muhimu kufanya kazi nzuri katika kuzuia na kudhibiti janga katika maeneo muhimu yenye watu wengi.

‘[Hii inajumuisha] shuleni, taasisi za kulelea watoto na nyumba za wauguzi, na kupunguza mtiririko wa watu na ziara.’

WHO inataka data mpya kutoka China kufuatia mlipuko wa nimonia kwa
watoto
0 Comment

Chongolo ajiuzulu akiwa kama Katibu Mkuu wa CCMAfyaclass Bongo Social •

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda @baba_keagan amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Chongolo ajiuzulu akiwa kama Katibu Mkuu wa CCM
0 Comment

Watu 13 wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Ally's kugonga Treni ManyoniAfyaclass Bongo Social •

Watu 13 wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Ally’s lenye namba za usajili T.178 DVB lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda Jijini Mwanza baada ya kugonga Treni za mizigo maeneo ya Manyoni leo Novemba 29,2023 majira ya Saa 11 alfajiri.

Watu 13 wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la Ally’s lenye namba za usajili T.178 DVB lililokuwa likitokea Jijini Dar es salaam kwenda Jijini Mwanza baada ya kugonga Treni za mizigo maeneo ya Manyoni leo Novemba 29,2023 majira ya Saa 11 alfajiri.

Watu 13 wamefariki dunia na 25 kujeruhiwa katika ajali ya Basi la
Ally's kugonga Treni Manyoni
0 Comment

Mwigizaji nguli wa Nigeria Amaechi Muonagor anaugua ugonjwa wa figo, kisukari, na kiharusi: binamu athibitishaAfyaclass Bongo Social •

Tony Oneweek, binamu wa mwigizaji mkongwe wa Nigeria, Amaechi Muonagor,ambaye wengi tulimuona akiigiza kama baba kwenye filamu ya Aki na Ukwa amefichua kuwa mwigizaji huyo anapambana na ugonjwa wa figo, kisukari na kiharusi.

Aliongeza kuwa ‘mwigizaji anayekabiliwa na maradhi haya anahitaji usaidizi wa Wanigeria wenye nia njema ili kumsaidia kufadhili dawa yake ili aendelee kuishi’.

‘zaidi kwamba Amaechi anafanyiwa dialysis kila wiki na physiotherapy kutibu kupooza kunakosababishwa na kiharusi’.

Katika chapisho kwenye ukurasa wake wa Facebook,  aliandika maneno yaliyoambatana na picha ya thespian kwenye kitanda cha hospitali ilisema, “Picha hii ilipigwa wiki mbili zilizopita nilipomtembelea binamu yangu Amaechi Monagor (Aguiyi) katika Hospitali ya Mafunzo ya Nnewi.

Hapo awali nilitaka kusaidia kimyakimya kadri nilivyoweza, lakini baadaye niliamua kuandika chapisho hili ili kufafanua baadhi ya mambo ili marafiki zangu, mashabiki na mashabiki wa Amaechi na kwa kweli jumuiya ya mtandaoni iweze kufahamishwa vyema.

“Amaechi kwa sasa ana ugonjwa wa figo, kisukari na kiharusi na alikuwa akidhibiti ugonjwa wa kisukari kwa miaka mingi na kuishi maisha yake.

Kwa sasa anafanyiwa usafishaji damu kila wiki na matibabu mengine katika Hospitali ya Kufundishia ya Chuo Kikuu cha Nnamdi Azikiwe Nnewi.

Familia yake ilikuwa ikibeba gharama kwa miaka mingi hadi kiharusi cha hivi majuzi kilifanya kesi yake kuwa mbaya zaidi na kwa kweli kuwa ghali zaidi kupigana peke yake, na hivyo kutangazwa.

Mwigizaji nguli wa Nigeria Amaechi Muonagor anaugua ugonjwa wa figo,
kisukari, na kiharusi: binamu athibitisha
0 Comment

Mambo 13 Usiyoyajua Kuhusu Adolf Hilter Ikiwemo la Kuwa na Korodani MojaAfyaclass Bongo Social •

Nani ambaye hamjui Dikteta Adolf Hitler? Adolf Hitler ni mtawala maarufu zaidi katika karne ya ishirini, kiongozi wa chama cha Kinazi aliyeitawala ujeruman kati ya mwaka 1934 mpaka 1945. Kama ulikuwa hujui, hitler ndiye mwanzilishi mkuu wa vita ya pili ya dunia.

Yafuatayo ni mambo  usiyoyajua kuhusu Adolf Hitler.

Alipendelea zaidi kuangalia Filamu za mauaji, wafuasi wake walipenda kurekodi video pale walipokuwa wanawauwa wafungwa na kumpelekea Hitler!

Adolf Hitler Ndiye aliyeanzisha sheria ya kutovuta sigara hadharani. Alikuwa mvuta sigara enzi za ujana wake na alikuja kuacha baadae akidai ni utumiaji mbaya wa fedha.

Licha ya kufurahia Kuua sana binadamu, adolf alipinga sana ukatili wa wanyama, na alikuwa hali nyama ya aina yeyote ile.

Hitler aliokolewa kufa maji na mfanyakazi wa kanisa alipokuwa na umri wa miaka minne (4), na kwa kipindi hicho, hitler ilipenda saana awe mfanyakazi wa kanisa akiwa mkubwa.

Mpenzi wa kwanza wa Hitler alikuwa myahudi na aliona aibu kumueleza hisia zake. Baadae aligeuka na kuamua kuua kila myahudi aliyekuwepo ujerumani, kasoro daktari mmoja ambaye alisaidia bure familia ya hitler kuwatibu kutokana na ugumu wa maisha kipindi adolf akiwa mdogo.
Akiwa jela, Hitler aliwahi kuandika barua kwenda kampuni ya mercedes benz akiomba mkopo wa gari.

Alishawahi kushindania tuzo ya nobel mwaka 1939.

Alikuwa na Korodani Moja Baada ya Moja Kukatwa kutokana na kujeruhiwa vitani

Hakuwa anajua kuendesha gari mpaka alipokufa

Hakumaliza High School aliachia njiani

Hakupenda aina yoyote ya michezo licha ya kupenda kutolea mifano ya kabumbu katika hotuba zake.
Adolf Hitler alikuwa na baadhi ya tabia za kike akiwa na umri mdogo, alikuwa pia na mwandiko wa kike. Vilevile hitler alipenda sana chokoleti kiliko vyakula vyote!——————-

Mambo 13 Usiyoyajua Kuhusu Adolf Hilter Ikiwemo la Kuwa na Korodani Moja
0 Comment

Inawezekana kuutokomeza kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030Afyaclass Bongo Social •

Umoja wa Mataifa umesema inawezekana kuutokomeza kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030 endapo tu Mashirika ya Kijamii na Watu walioko katika mstari wa mbele kupambana na ugonjwa huo watawezeshwa.

Ripoti ya Shirika hilo imeeleza kuwa ingawa Dunia bado haijakomesha kabisa UKIMWI kama tishio la afya kwa umma kuna matumaini ya lengo hilo kufikiwa toka lilipotangaza mpango huu mwaka 2015.

Kwa sasa kuna Watu milioni 39 wanaoishi na virusi vya HIV Duniani kote na kati ya hao milioni 20.8 wako Mashariki na Kusini mwa Afrika huku wengine milioni 6.5 wakiwa Asia na Pasifiki huku milioni 9.2 yao wakiwa hawana dawa za kupunguza makali ya virusi hivyo, imeripoti @dw_kiswahili

Inawezekana kuutokomeza kabisa UKIMWI ifikapo mwaka 2030
0 Comment

Vita vya Urusi na Ukraine: Mke wa mkuu wa Ujasusi wa kijeshi wa Ukraine awekewa sumuAfyaclass Bongo Social •

Mke wa mkuu wa upelelezi wa kijeshi wa Ukraine awekewa sumu ya metali nzito na anaendelea na matibabu, serikali ya Kyiv imefichua.

Msemaji wa shirika la ujasusi la kijeshi la Ukraine, au GUR, alisema Marianna Budanova, mke wa Kyrylo Budanov, alikuwa akipokea matibabu hospitalini.

“Ndiyo, naweza kuthibitisha taarifa hizo. Kwa bahati mbaya, ni kweli,” msemaji wa GUR Andriy Yusov aliambia Reuters siku ya Jumanne bila kufafanua ni lini sumu hiyo alipewa au ni nani aliyehusika.

Budanov amekuwa mtu maarufu nchini Ukraine kwa jukumu lake katika kupanga operesheni za siri dhidi ya Urusi, ambayo ilianzisha uvamizi wake kamili dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022.

Yusov alisema mwaka huu kwamba Budanov alinusurika majaribio 10 ya kuuawa na Shirikisho la usalama la Urusi, au FSB.

Bado haijabainika mara moja ni nani aliyehusika na tuhuma za kuwekewa sumu mke wake, lakini Yusov alisema kuwa maafisa wengine wa GUR wamepata dalili za sumu kali zaidi.

Hapo awali Urusi ilishutumiwa kwa kuwapa sumu wapinzani, akiwemo mwanasiasa Alexey Navalny na wahamiaji wawili wa Urusi waliohudhuria mkutano wa kilele mjini Berlin ulioandaliwa na mkosoaji wa Urusi.

Moscow pia imeilaumu Ukraine kwa kushukiwa kuhusika katika mauaji ya mwanablogu wa Urusi anayeunga mkono vita na mwandishi wa habari anayeunga mkono vita katika ardhi ya Urusi, madai ambayo Ukraine inakanusha.

Urusi iliivamia Ukraine mnamo Februari 24, uvamizi wake umesababisha hasara nyingi ikiwemo maisha kwa maelfu ya watu, pamoja na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

Vita vya Urusi na Ukraine: Mke wa mkuu wa Ujasusi wa kijeshi wa Ukraine
awekewa sumu
0 Comment

Vita vya Urusi na Ukraine: Mke wa mkuu wa Ujasusi wa kijeshi wa Ukraine awekewa sumu Afyaclass Bongo Social •

Mke wa mkuu wa upelelezi wa kijeshi wa Ukraine awekewa sumu ya metali nzito na anaendelea na matibabu, serikali ya Kyiv imefichua.

Msemaji wa shirika la ujasusi la kijeshi la Ukraine, au GUR, alisema Marianna Budanova, mke wa Kyrylo Budanov, alikuwa akipokea matibabu hospitalini.

“Ndiyo, naweza kuthibitisha taarifa hizo. Kwa bahati mbaya, ni kweli,” msemaji wa GUR Andriy Yusov aliambia Reuters siku ya Jumanne bila kufafanua ni lini sumu hiyo alipewa au ni nani aliyehusika.

Budanov amekuwa mtu maarufu nchini Ukraine kwa jukumu lake katika kupanga operesheni za siri dhidi ya Urusi, ambayo ilianzisha uvamizi wake kamili dhidi ya Ukraine mnamo Februari 2022.

Yusov alisema mwaka huu kwamba Budanov alinusurika majaribio 10 ya kuuawa na Shirikisho la usalama la Urusi, au FSB.

Bado haijabainika mara moja ni nani aliyehusika na tuhuma za kuwekewa sumu mke wake, lakini Yusov alisema kuwa maafisa wengine wa GUR wamepata dalili za sumu kali zaidi.

Hapo awali Urusi ilishutumiwa kwa kuwapa sumu wapinzani, akiwemo mwanasiasa Alexey Navalny na wahamiaji wawili wa Urusi waliohudhuria mkutano wa kilele mjini Berlin ulioandaliwa na mkosoaji wa Urusi.

Moscow pia imeilaumu Ukraine kwa kushukiwa kuhusika katika mauaji ya mwanablogu wa Urusi anayeunga mkono vita na mwandishi wa habari anayeunga mkono vita katika ardhi ya Urusi, madai ambayo Ukraine inakanusha.

Urusi iliivamia Ukraine mnamo Februari 24, uvamizi wake umesababisha hasara nyingi ikiwemo maisha kwa maelfu ya watu, pamoja na mamilioni ya watu kuyahama makazi yao.

Vita vya Urusi na Ukraine: Mke wa mkuu wa Ujasusi wa kijeshi wa Ukraine
awekewa sumu
0 Comment

Dalili za mwanzo za kisukari kwa mwanaumeAfyaclass Bongo Social •

Dalili za mwanzo za kisukari kwa mwanaume

Kuna ishara nyingi za tahadhari zinazotokea mapema pamoja na dalili za mwanzo kabsa za ugonjwa wa kisukari kwa wanaume.

Kwa vyovyote vile, wasiliana na daktari na usiwahi kutumia dawa wewe mwenyewe, kwa sababu inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi.

Hizi hapa ni baadhi ya Dalili za mwanzo za kisukari kwa mwanaume;

1. Kuwa na Kiu pamoja na njaa kupita kiasi(Excessive Thirst and Hunger)

Kwa kuwa kiwango cha sukari kwenye damu ni kikubwa, huvuta maji kutoka kwenye seli na kumfanya mgonjwa ahisi kiu kupita kiasi.

Watu wanaougua kisukari huhisi njaa mara kwa mara kwa sababu ya Mwili kutoweza kutumia ipasavyo sukari ya damu kwa kuigeuza kuwa nishati. Ikiwa unajikuta unakunywa galoni za maji au unaanza kula chakula ghafla mara kwa mara na kuhisi njaa kila wakati, zungumza na daktari wako.

2. Kukojoa mara kwa mara(Frequent Urination)

Watu wanaougua ugonjwa wa sukari huanza kukojoa mara kwa mara. Kiu nyingi,kunywa maji mengi,husababisha kukojoa mara kwa mara, na Wanaume wengi wanakabiliwa na shida ya kupata usingizi mzuri usiku.

Wagonjwa wazee wanaweza hata kupata shida ya kukojoa kitandani. Mwili hujaribu kutoa glucose ya ziada katika damu kupitia mkojo. Hiyo ni sababu nyingine ya kukojoa mara kwa mara.

3. Mwili kuchoka kupita kiasi

Iwapo kwa ujumla umekuwa ukijihisi kuchoka sana na kuteseka kutokana na uchovu bila sababu zozote zinazoeleweka, unaweza kuwa na kisukari.(Ingawa KiSukari sio sababu pekee ya wewe kuchoka sana, hata magonjwa mengine na sababu zingine huweza kupelekea shida hii)

Uchovu usioelezeka kwa mgonjwa wa Sukari ni kwa sababu ya matumizi duni ya nishati. Kipimo cha Sukari(glukosi) kitakupa majibu kwa hivyo fanya vipimo mara moja.

4.Uzito kupungua kwa kasi sana pasipo na sababu inayoeleweka

Men suffering from diabetes undergo unexplained weight loss. The body is unable to use blood sugar to transform it into energy. This leads to sudden weight loss. If you have lost weight without any reason, please consult your doctor.

5. Kupata maambukizi ya ngozi mara kwa mara(Skin Infections)

Kwa sababu ya kiwango cha sukari kwenye damu kuwa Juu, wanaume wanaougua ugonjwa wa kisukari hupata maambukizi ya ngozi mara nyingi sana.

Hali Hii inaweza kusababisha kuwashwa kwenye sehemu za siri au hata kupata fangasi kwa urahisi(thrush),

Sukari ikiwa juu hutengeneza mazingira mazuri ya kuzaliana kwa fangasi ambao husababisha maambukizo haya.

6. Kupata matatizo ya macho kutokuona vizuri

Wanaume wanaougua kisukari hupata uoni hafifu na kupoteza uwezo wa kuona kwa ujumla,

Viwango vya juu vya sukari mwilini ni hatari kwa viungo vingi lakini macho huwa ya kwanza kuumia. Tafuta matibabu mara moja ikiwa umepata shida ya macho kutokuona vizuri kwa gafla.

7. Vidonda kuchelewa Kupona

Wanaume wanaougua ugonjwa wa kisukari hupata majeraha/vidonda kwa urahisi na majeraha yao huchukua muda kupona.

Sukari nyingi katika damu hupunguza kinga na huathiri uwezo wa mwili wa kujiponya,

Kwa kuwa hali hiyo inaweza kuzidisha tatizo la gangrene na hata kupelekea mtu kukatwa viungo, ikiwa una jeraha ambalo haliponi, tafuta ushauri wa kitabibu.

8. Kupata Tatizo la Upungufu wa nguvu za kiume(Erectile Dysfunction)

Kisukari hasa aina ya 2 kwa kawaida huhusishwa na tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri au uume kutokusimama kabsa(erectile dysfunction), kwani uwepo wa sukari nyingi kwenye damu kwa muda mrefu huweza kuharibu mishipa ya fahamu na mishipa ya damu na kusababisha matatizo ya uume kushindwa kusimama kabsa au kushindwa kusimama vya kutosha.

Wanaume wanaougua ugonjwa wa kisukari hupata shida ya nguvu za kiume kutokana na mzunguko mdogo wa damu kwenye viungo kama vile eneo la pelvisi.

Vitu hivi huongeza hatari ya Kupata Ugonjwa wa Kisukari kwa Mwanaume

Sababu nyingi huchangia au kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari na matatizo yanayohusiana na ugonjwa huu, baadhi ya Sababu hizo ni pamoja na:

  • Kuongezeka Uzito kwa haraka sana(Uzito mkubwa kupita kiasi)
  • Uvutaji wa Sigara
  • Unywaji wa Pombe kupita kiasi
  • Kuwa na shida ya presha kubwa kwenye damu(High blood pressure)
  • Kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu mwilini(high cholesterol)
  • Kutokufanya mazoezi ya mwili
  • Kuwa na umri wa Zaidi ya miaka 45 n.k

Jikinge na Ugonjwa wa Kisukari kwa kufanya haya

✓ Epuka kabsa Uvutaji wa Sigara

✓ Epuka matumizi ya pombe kupita kiasi

✓ Hakikisha unadhibiti Uzito wako wa mwili na kuepuka kuwa na Uzito kupita kiasi

✓ Fanya Mazoezi mbali mbali ya Mwili angalau kwa dakika 30(nusu saa) kila siku

✓ Kula Mlo bora kwa afya yako, Epuka ulaji wa vitu vya sukari nyingi,chumvi nyingi au mafuta mengi sana.n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dalili za mwanzo za kisukari kwa mwanaume
0 Comment

Kila mtu aeleza alivyoguswa na Mtanzania aliyeuawa IsraelAfyaclass Bongo Social •

Wanafunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha Sokoine (Sua) pamoja na marehemu Clemence Mtenga (22), ambaye aliuawa nchini Israel, wameelezea namna walivyoishi naye huku wakidai wataukosa upendo na namna alivyojali wengine.

Wametoa simulizi hiyo leo Novemba 28, 2023 nyumbani kwa marehemu Kirwa, wilayani hapa, wakati walipofika kushiriki maziko ya Clemence ambayo yanafanyika leo.

Akizungumza Mwananchi Digital, Anthony Kanyanza mmoja wa wanafunzi hao, amesema kuwa kifo hicho kimewasikitisha na kuwashtua kwa kuwa kilitokea ghafla na kimewapa wakati mgumu kukubali ukweli huo.

“Mimi ni miongoni mwa wanafunzi tuliobahatika kusoma na kukaa na Clemence, kwa kweli taarifa za kifo chake tulizipokea kwa masikitiko makubwa maana zilikuwa za ghafla na za kushtua na muda si mrefu tulikuwa tumewasiliana naye.

“Hatukuweza kuzipokea kwa wepesi na ilikuwa ni ngumu kukubali na kwa kiwango kikubwa mpaka sasa bado kuna ugumu wa kupokea na kuzikubali taarifa za kifo chake, ila ni mipango ya Mungu hatuna budi,”amesema Kanyanza.

Kwa mujibu wa simulizi hiyo, Kanyanza amesema marehemu alikuwa mtu mwenye upendo kwa wenzake na alijijengea utaratibu wa kuwapigia simu rafiki zake kila ilipofika saa moja usiku, kwa lengo la kuwajulia hali.

Ameongeza kuwa, “Aanaweza kukupigia tu akakuuliza vipi umeshindaje, siku yako imeendaje na ni kitu ambacho alikuwa nakifanya mara kwa mara, kila siku alitamani kujua marafiki zake wana hali gani na wanaendeleaje.

Aidha Kanyanza amesema marehemu ukimueleza tatizo lako, si mtu wa kusikiliza na kuacha, alikuwa akikupa moyo na kupiga hatua moja katika kuangalia namna ya kukusaidia, “kwenye masuala ya uongozi alikuwa mfuatiliaji sana.

Amesema pia marehemu alikuwa mwanakwaya, na kwamba alishiriki kikamilifu shughuli za kitaaluma, kidini na kijamii. Kwa upande wake Jovin Shirima ambaye mbali na kuwa mwanafunzi mwenzake hapo Sua, aliimba naye kwaya.

“Kifupi marehemu nimefahamiana naye tangu tunasoma kidato cha tano na sita ambapo marehemu alikuwa kiongozi wa TYCS Umbwe Sekondari, wakati mimi nikiwa kiongozi wa TYCS Lyamungo Sekondari na baadaye tukakutana Sua,” amesema.

Mwili wa Clemence uliwasili nchini jana Novemba 27, 2023, saa 2:51 usiku, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uholanzi (KLM), kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) ambapo ulipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu aliyekuwa ameongozana na kamati ya usalama mkoa na kuukabidhi kwa familia.

Novemba 17, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ilithibitisha kupokea taarifa za kifo cha Clemence Mtenga, ambaye alikuwa miongoni mwa Watanzania wawili ambao pamoja na raia wa mataifa mengine walikuwa hawajulikani walipo baada ya kuanza kwa vita kati ya Hamas na Israel.

Taarifa hiyo iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano ya Serikali cha wizara hiyo, ilieleza Clemence alikuwa miongoni mwa vijana wa Kitanzania 260, waliokwenda Israel kushiriki mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vitendo, chini ya mpango wa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Israel.

Kila mtu aeleza alivyoguswa na Mtanzania aliyeuawa Israel
0 Comment

Asilimia 99% ya huduma za mifupa zinapatikana hapa nchiniAfyaclass Bongo Social •

TANZANIA KUWA KITOVU CHA TIBA UTALII

Na. WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. @ummymwalimu amesema kuwa Tanzania inakwenda kuwa kitovu cha Tiba Utalii kwa kutoa huduma za Afya kwa wagonjwa maalumu wa ndani na nje ya nje.

Waziri Ummy amesema hayo leo Novemba 28, 2023 baada ya kufungua mradi wa kliniki mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa iliyopo katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) itakayotoa huduma za kliniki kwa wagonjwa wa ndani na nje ya nchi.

“Haya tutakayoyashuhudia leo ni matokeo ya uwekezaji mkubwa ambao Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amefanya katika Sekta ya Afya lakini pia niwapongeze Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) chini ya Prof. Abel Makubi na Mwenyekiti wa Bodi Prof. Charles Mkony kwa kazi nzuri na kubwa ya kuokoa maisha ya Watanzania”. Amesema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amewaomba Watanzania wenye uhitaji wa tiba kwa haraka (kliniki ya wagonjwa maalum na Wakimataifa) ikiwa ni mtumishi au mfanyabiashara waende MOI ambapo ndani ya masaa mawili unamaliza kila kitu na kuendelea na shughuli zako.

Aidha, Waziri Ummy ameitaka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) iendeshe kliniki hiyo mpya ya wagonjwa maalum na wa kimataifa kwa ubia na wawekezaji wengine ili kuboresha zaidi huduma zitolewazo.

“Ni jambo zuri sana mmelianzisha lakini tusije kukwama njiani hivyo tushirikiane na wadau wengine ili huduma hii iendelee na ni matarajio yangu kwamba kliniki hii mpya ya wagonjwa maalumu na wagonjwa wa Kimataifa itakuwa kliniki ya mfano ambayo itakua kivutio kikubwa kwa wagonjwa kutoka katika Mataifa mbalimbali”. Amesema Waziri Ummy.

Amesema, Kutokana na uwekezaji mkubwa katika miundombinu vifaa tiba na wataalamu, Taasisi ya MOl imefanikiwa kupunguza rufaa za wagonjuwa kwenda nje ya nchi ambapo hivi sasa 99% ya huduma za mifupa zinapatikana hapa nchini na 97% ya huduma za kibingwa za Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Gahamu zinapatikana hapa chini.

Pia, Waziri Ummy ametoa maelekezo kwa Hospitali nyingine kuwa na huduma za haraka kwa kuwa Watanzania wanataka huduma za haraka na zilizobora kwa kuzingatia Weledi, Maadili na Taaluma wakati wa kumhudumia mgonjwa kwa kuanza na mapokezi mazuri.

Waziri Ummy amewataka Watanzania kuzingatia ulaji bora ikiwemo kupunguza matumizi ya sukari nyingi, chumvi nyingi pamoja na mafuta mengi ili kuepuka Magonjwa Yasiyoambukiza ikiwemo shinikizo la juu la Damu (Presha) na Kisukari kwa kuwa magonjwa hayo yamekuwa yakiongezeka Tanzania.

Mwisho, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikiliza kilio cha Watanzania na kuboreha huduma za Afya ikiwemo kutoa fedha kwaajili ya majengo, vifaa na vifaa tiba na Sasa tunakwenda kuwa kitovu cha Tiba Utalii.

Asilimia 99% ya huduma za mifupa zinapatikana hapa nchini
0 Comment

Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi ya Israel sasa inazidi 15,000Afyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya eneo la Gaza, Jumatatu, ilisema idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi mabaya ya Israel kwenye eneo hilo sasa inazidi 15,000, pamoja na maelfu ya wengine ambao bado hawajulikani walipo chini ya vifusi, Shirika la Anadolu linaripoti.

Katika taarifa yake, Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali yenye makao yake makuu Gaza ilisema idadi ya waliofariki ni pamoja na watoto 6,150 na wanawake 4,000, pamoja na idadi isiyojulikana ya maiti zilizotawanyika mitaani.

Imeongeza kuwa pia kuna takriban watu 7,000 waliopotea chini ya vifusi, wakiwemo watoto 4,700 na wanawake.

Taarifa hiyo ilibainisha kuwa, miongoni mwa Wapalestina waliokufa, ni wahudumu wa afya 207, wanachama 26 wa timu za uokoaji za ulinzi wa raia na waandishi wa habari 70.

Zaidi ya Wapalestina wengine 36,000 pia walijeruhiwa, asilimia 75 kati yao wakiwa watoto na wanawake, ofisi hiyo iliongeza.

Kuhusu majengo ya makazi, ilisema karibu nyumba 50,000 ziliharibiwa kabisa pamoja na karibu nyumba 240,000 zilizoharibiwa vibaya.

Jumla ya misikiti 88 iliharibiwa kabisa na mingine 174 kuharibiwa kwa sehemu na mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza, pamoja na makanisa matatu yaliyolengwa na jeshi la Israel.

Idadi ya vifo vya Wapalestina kutokana na mashambulizi ya Israel sasa
inazidi 15,000
0 Comment

kupiga vita mila potofu ambazo ni chanzo ukatili wa kijinsiaAfyaclass Bongo Social •

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, Wakazi wa Kata ya Luanga Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya wametakiwa kupiga vita mila potofu ambazo ni chanzo ukatili wa kijinsia.

Wito huo umetolewa hii leo Novemba 28, 2023 na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mbeya Mkaguzi wa Polisi, Lovenes Mtemi katika kampeni ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Amesema, “acheni kukumbatia mila potofu, ukeketaji na ngoma za asili ambazo husababisha vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto na wanawake.”

Naye Afisa maendeleo ya jamii Wilaya ya Mbarali, Neema Swila amekemea makundi ya kijamii ambayo yanashindwa kutimiza wajibu wao katika suala nzima la malezi ya mtoto.

“Timizeni wajibu wenu katika malezi ya watoto, acheni kupeleka watoto kwa bibi na babu, jukumu la malezi ni la wazazi, baba na mama” Alisema Bi.Neema Swila.

Nao wazee wa kimila, wazee mashuhuri na viongozi wa dini waliohudhuria kampeni hiyo, wamekemea mila potofu kama vile ngoma za chakulaga kwa kusema ni chanzo cha vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa mabinti na wanawake.

Elimu hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi Dawati la Jinsia na Watoto, Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mbarali na Shirika lisilo kuwa la Kiserikali la TUMAINI.

kupiga vita mila potofu ambazo ni chanzo ukatili wa kijinsia
0 Comment

Daktari aliyegundua na kumtibu mgonjwa wa kwanza wa UKIMWI TanzaniaAfyaclass Bongo Social •

Imetimia miaka 40 sasa tangu kugundulika kwa ugonjwa wa UKIMWI ambao uliingia Afrika Mashariki mwaka 1983.

Maelfu ya watanzania walipoteza Maisha, huku ikiwa vigumu kuweza kukabiliana nao kutokana na mila potofu.

Callixte Twagirayezu alikua daktari aliyemtibu mgonjwa wa kwanza kabisa wa virusi vya UKIMWI.

Katika mahojiano na BBC, daktari huyu ambaye kwa sasa ana miaka 93 anasema kilikua miongoni mwa vipindi vigumu kuwahi kushuhudia maishani mwake.

Source:Bbc

Daktari aliyegundua na kumtibu mgonjwa wa kwanza wa UKIMWI Tanzania
0 Comment

Rais Wa IPU Dkt. Tulia Ackson Awasili Mashariki Ya Kati Kwa Ziara Ya Siku MbiliAfyaclass Bongo Social •

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson, Novemba 27, 2023 amewasili Mashariki ya Kati kwa ziara ya siku mbili yenye lengo la kujadili jinsi jumuiya ya kimataifa kupitia IPU inaweza kuunga mkono juhudi za kupata suluhu ya mgogoro unaoendelea baina ya Israel na Palestina.

Katika ziara hiyo ya kidiplomasia, Dkt Tulia anatarajia kukutana na Viongozi wa pande zote mbili kwa lengo la kutafuta amani katika eneo hilo.

Rais Wa IPU Dkt. Tulia Ackson Awasili Mashariki Ya Kati Kwa Ziara Ya
Siku Mbili
0 Comment

Vyakula Bora na Vibaya Zaidi kwa Ini LakoAfyaclass Bongo Social •

Vyakula Bora na Vibaya Zaidi kwa Ini Lako

Hapa tumefanya uchambuzi wa baadhi ya vitu vya kufanya na kuzingatia, pamoja na vitu vya kuepuka kwa afya ya Ini lako, Pia kuna baadhi ya vyakula vya kuepuka na vingine vya kuvizingatia zaidi ili kuwa na Ini lenye afya bora.

1. Epuka kabsa vyakula vya mafuta mengi

Kula vyakula vingi sana vyenye mafuta mengi inaweza kufanya iwe vigumu kwa ini kufanya kazi yake. Baada ya muda inaweza kusababisha kuvimba kisha kupelekea Ini kuwa na kovu au tatizo ambalo kwa kitaalam linajulikana kama cirrhosis.

2. Kahawa(Coffee)

Kunywa kahawa kwa kiasi. Baadhi ya tafiti zinaonyesha kwamba kunywa vikombe viwili hadi vitatu kwa siku kunaweza kulinda ini lako kutokana na uharibifu unaosababishwa na pombe nyingi au mlo usiofaa.

Pia kuna Utafiti mmoja ulionyesha kuwa kahawa inaweza kupunguza hatari ya kupata saratani ya ini(Liver cancer).

3. Epuka kula vitu vyenye Sukari nyingi

Sukari nyingi sana zinaweza kuathiri ini lako. Hiyo ni kwa sababu moja ya kazi ya Ini ni kubadilisha sukari kuwa mafuta.

Ukizidisha, ini lako hutengeneza mafuta mengi, ambayo huishia kuning’inia mahali pasipohusika,

Ikiwa Kwa muda mrefu, unaweza kupata magonjwa kama vile ugonjwa wa mafuta kwenye ini kwa kitaalam fatty liver disease.

Kwa hivyo unaweza kulinda afya ya ini lako kwa kuepuka matumizi ya sukari nyingi.

4. Matumizi ya chai ya kijani(Green Tea)

Chai hii ina aina ya antioxidant inayofahamika kama catechins. Tafiti zinaonyesha kwamba catechins huweza kukulinda na Saratani mbali mbali ikiwemo Saratani ya Ini.

Hivo matumizi ya green tea ni bora kwa afya ya Ini.

5. Unywaji wa maji ya kutosha

Moja ya njia bora sana ya kutunza afya ya Ini lako ni kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku,

Jenga Tabia ya kunywa maji badala ya vinywaji vilivyotiwa sukari nyingi kama vile soda, hii ni bora zaidi kwako.

9. Matumizi ya Karanga

Tafiti zinaonyesha kwamba, karanga zina virutubisho vya kutosha ikiwemo vitamin E,

Virutubisho hivi huweza kulinda Ini dhidi ya magonjwa kama vile ugonjwa wa mafuta kwenye ini kwa kitaalam fatty liver disease.

10. Matumizi ya mboga za majani ikiwemo Spinach

Mboga za majani zina antioxidant inayofahamika kama glutathione, ambayo inaweza kusaidia ini lako kufanya kazi vizuri.

11. Epuka kabsa matumizi ya Pombe au kunywa kwa kiasi kidogo sana(Be Moderate With Alcohol)

Kunywa kupita kiasi kunaweza kuharibu ini lako. Baada ya muda inaweza kusababisha tatizo la cirrhosis.

Hata unywaji wa kupindukia mara kwa mara ni hatari kwa afya yako —  Kunywa vinywaji vinne kwa mara moja kwa wanawake na vitano kwa wanaume — vinaweza pia kuwa na madhara.

Jaribu kujiwekea kikomo cha kunywa mara moja kwa siku ikiwa wewe ni mwanamke au mbili kwa siku ikiwa wewe ni mwanaume.

12. Punguza kula Vyakula Vilivyofungwa

Mara nyingi vyakula ambavyo ni packed foods vinakuwa na Kiwango kikubwa cha sukari,chumvi,mafuta n.k, Vitu hivi ni hatari kwa afya ya Ini lako.

13. Epuka matumizi ya kupita kiasi kwa baadhi ya dawa kama vile Acetaminophen

Acetaminophen Inapatikana katika dawa zaidi ya 600, pamoja na dawa nyingi za baridi na mafua. Watu wazima wengi hawapaswi kupata zaidi ya miligramu 4,000 kwa siku. Zaidi inaweza kuleta madhara kwenye ini lako.

14. Fanya ngono Salama jikinge na magonjwa ya Zinaa

Unataka kujilinda  wewe na mwenza wako dhidi ya hali zinazoweza kuenea kwa njia ya ngono, ikiwa ni pamoja na nyingi ambazo hatimaye zinaweza kuumiza ini lako.

Moja ni, Ugonjwa wa homa ya Ini-hepatitis C, B n.k, huambukiza moja kwa moja na inaweza kuleta madhara makubwa. Watu wengi hawatambui kuwa wana ugonjwa huu hadi miaka mingi baadaye wakati uharibifu mwingi umefanywa. Daktari wako anaweza kupima ili kuona kama unayo, hivo fanya vipimo.

15. Hakikisha unadhibiti shida ya uzito Mkubwa

Hiyo inamaanisha kufanyia kazi zaidi Uzito wako ili kuweka index ya uzito wa mwili (BMI) kuwa kati ya 18 na 25.

Mazoezi na mlo kamili ndio njia bora zaidi ya kukusaidia kudumisha uzito unaokufaa na kupunguza uwezekano wa kupata ugonjwa wa ini. Daktari wako anaweza kukusaidia kuweka mikakati ya kupunguza uzito ambayo itasaidia kuweka mwili wako mzima vizuri kwa muda mrefu.

Vyakula Bora na Vibaya Zaidi kwa Ini Lako
0 Comment

UWT tunampongeza Rais Samia kwa kutengua uteuzi wa Gekul, uchunguzi ukamilike kwa harakaAfyaclass Bongo Social •

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM Tanzania (UWT), Mary Chatanda amesema Umoja huo umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma zinazomkabili Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul kuhusu kumfanyia ukatili Kijana Hashim Ally Babati Mjini Mkoani Manyara ambapo wamesema ikithibitika ametenda kosa hilo achukuliwe hatua kali.

“UWT tunazunguka nchi nzima kupinga na kukemea ukatili wa kijinsia na kuporomoka kwa maadili, hivyo tunapinga vikali kitendo hiki na endapo tuhuma hizi za Gekul zitathibitika hatua stahiki zichukuliwe na adhabu kali itolewe dhidi yake, UWT haitovumilia Kiongozi yoyote Mwanamke atakayethibitika anafanya vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“UWT tunampongeza Rais Samia kwa kutengua uteuzi wa Gekul kama Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na tunaviomba Vyombo vya Dola kukamilisha uchunguzi kwa haraka ili kuleta imani kwa Wananchi.”

UWT tunampongeza Rais Samia kwa kutengua uteuzi wa Gekul, uchunguzi
ukamilike kwa haraka
0 Comment

kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro kilitokana na uzembe sio kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000Afyaclass Bongo Social •

Tume iliyoundwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuchunguza kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro imesema kifo hicho kilitokana na uzembe wa Wataalamu wa Afya na sio kutokana na kukosa fedha za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000.

Kifo cha Mariam Zahoro kilitokea November 11,2023 katika Kituo cha Afya cha Kabuku Mkoani Tanga baada ya kushindwa kujifungua kwa njia ya kawaida na kuhitaji kufanyiwa upasuaji na kuchelewa Kwa huduma ya dharura ya upasuaji.

Akiongea katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kabuku Waziri Ummy amesema tayari Baraza la Madaktari pamoja na Wauguzi na Wakunga linaendelea na utaratibu wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa Wataalamu wawili wa afya katika kituo hicho.

“Tutahakikisha baada ya hili hakuna kifo kinachotokana na uzembe kinatokea hapa nchini kwani tumejipanga kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa Watumishi wa Afya wazembe”

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dkt. Ali Said amesema chanzo cha kifo ni kutokana na uzembe wa Wataalamu hao kushindwa kuchukua hatua za haraka Ili hali mgonjwa akiwa katika hali ya hatari “Mwanamke huyo alichelewa kupatiwa huduma ya upasuaji kutokana na kukosekana kwa Mtaalamu wa dawa ya usingizi ambaye hakuwa anapatikana huku Daktari wa upasuaji akishindwa kutoa maamuzi ya rufaa kwa wakati kwenda kwenye Hospitali ya Wilaya”

kifo Cha mjamzito Mariam Zahoro kilitokana na uzembe sio kukosa fedha
za matibabu kiasi cha Tsh. 150,000
0 Comment

Vitundu vya pua vyaziba baada ya kuficha mistari ya kuzeeka (picha)Afyaclass Bongo Social •

Mwanamke mmoja ambaye aliamua kupata huduma ya face fillers ili kuficha mistari  inayoonyesha “kuzeeka” hasa wakati wa kutabasamu, kwa bahati mbaya huduma ilienda vibaya sana na kusababisha pua yake kutoka na kudondoka pamoja na vitundu vya pua kuziba(nostrils).

Krysta Carson, kutoka Seattle, Washington, anasema daktari wake alimdunga sindano “ya kutatanisha” kwenye mshipa mkubwa wa damu, ambayo ilisababisha mwili wake kufa ganzi wiki mbili baadaye.

Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 52 aliamua kupata dermal filler ili kuficha mistari ya kuzeeka kwenye ngozi ambayo ilikuwa inaonekana sana hasa wakati akitabasamu.

Krysta anasema alikuwa amedungwa kichungi kwenye mistari ya tabasamu kila mwaka tangu 2016 na alipenda matokeo, kabla ya kuziba kwa mishipa mnamo 2020,na kusababisha ngozi ndani ya mdomo wake, pua na karibu na pua yake ya kushoto kuwa necrotic na kuanguka.

Baadhi ya Picha za kutisha zilionyesha jinsi pua yake yote ilivyobadilika kuwa nyeusi na kuoza, kabla haijadondoka.

Mtumbuizaji huyo mtaalamu anasema “alipoteza tumaini la kuishi” baada ya hali ya mshtuko kuharibu kazi yake ya miaka 30, licha ya daktari wake kudai kuwa atakuwa sawa ndani ya wiki sita za tukio hilo.

Pia Krysta anasema kuwa anashukuru mumewe, Redd Gill mwenye umri wa miaka 42, maana alipata mtaalamu wa viungo bandia vya usoni baada ya kukesha akifanya utafiti.

Vitundu vya pua vyaziba baada ya kuficha mistari ya kuzeeka (picha)
0 Comment

LATRA yatangaza nauli mpya za MabasiAfyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600

Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900.

LATRA yatangaza nauli mpya za Mabasi
0 Comment

Bohari ya Dawa (MSD), imetwaa tuzo ya Mlipa kodi Bora kwa mwaka 2023 ya Mamlaka ya Kodi TanzaniaAfyaclass Bongo Social •

Tuzo hizo zilitolewa jana usiku katika hafla maalum ya wiki ya Mlipakodi zilizofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijiini Dar es Salaam ambako Bohari hiyo imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha walipakodi wa Kati kwa Mkoa wa Kikodi wa Temeke.

Akipokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai amesema ushindi huo una maana kubwa kwa Bohari hiyo na Watanzania .

Amesema MSD ambayo ni moja ya Taasisi za kimkakati za Serikali inayohusika na kuzalisha, kununua, kutunza na kusambaza bidhaa za afya kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali nchini inafuata taratibu, sheria na miongozose ikiwa ni pamoja na kulipa kodi stahiki

“Maendeleo yoyote ya nchi yanategemea kodi zinazolipwa hivyo ni vyema kila mlipa kodi akalipa kodi stahiki ili kuwezesha muendelezo wa biashara na kuimarisha maendeleo kwa mustakali wa ustawi wa jamii, ” ameongeza Tukai katika hafla hiyo ambako mgeni Rasmi alikuwa Naibu Waziri Mkuu, Dk Dotto Biteko.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Tukai, MSD sasa iko katika mkakati wa kujiendesha kibiashara hivyo hatua ya kulipa kodi kwa utaratibu uliowekwa hadi kutambuliwa ni fursa ya kuaminika kwa wadau wetu katika huduma tunazotoa.

Awali Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na Mawasiliano TRA, Richard Kayombo alisema vigezo vilivyotumika kupata washindi ni kulipa kiasi kikubwa cha kodi na hiari pamoja na kutunza kumbukumbu vizuri.

Bohari ya Dawa (MSD), imetwaa tuzo ya Mlipa kodi Bora kwa mwaka 2023 ya
Mamlaka ya Kodi Tanzania
0 Comment

Chanzo cha UKE MKAVU pamoja na Matibabu yakeAfyaclass Bongo Social •

Tatizo La Kuwa Na Uke Mkavu,Sababu Na Tiba Yake

Tatizo hili la mwanamke kuwa na uke mkavu linawapata wanawake wengi sana kwa hivi sasa, ambapo wengine hupata madhara mbali mbali kama maumivu makali wakati wa tendo la Ndoa N.K.

Tatizo hili huweza kuhusishwa na sababu mbali mbali ikiwemo ile ya baadhi ya magonjwa,mabadiliko ya vichocheo mwilini N.K. Sababu za mwanamke kuwa na uke mkavu zimeelezewa vizuri hapa chini;

SABABU ZA MWANAMKE KUWA NA UKE MKAVU NI PAMOJA NA;

1. Mvurugiko wa vichocheo mwilini yaani kwa kitaalam Hormone imbalance, hasa hasa vichocheo aina ya ESTROGEN ambavyo huhusika kwa kiasi kikubwa kuleta hali ya unyevu unyevu,ute pamoja na ulainishi ndani ya sehemu za siri za mwanamke.

2. Matumizi ya baadhi ya vitu vyenye kemikali katika kusafisha sehemu za siri za mwanamke Mfano; baadhi ya Sabuni.

3. Kupatwa na maambukizi ya magonjwa mbali mbali ya zinaa Kama vile; Ugonjwa wa kisonono au kaswende.

4. Kupatwa na maambukizi katika njia au mfumo Mzima wa mkojo wa mwanamke yaani Urinary track infection(UTI).

5. Kuwa na tatizo la Fangasi ambazo haziishi,zinazojirudia rudia mara kwa mara licha ya matumizi ya dawa nyingi.

6. Mwanamke kupatwa na maambukizi katika via vyake vya uzazi yaani PELVIC INFLAMMATORY DISEASE(PID)

DALILI ZA TATIZO LA MWANAMKE KUWA NA  UKE MKAVU

• Kupatwa na maumivu makali wakati wa kufanya mapenzi

• Kupatwa na maumivu ya kiuno baada ya kufanya mapenzi

• Kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa,hiki ni kiashiria cha uke mkavu,pamoja na kutokea kwa michubuko wakati wa tendo la ndoa.

• Mwanamke kupoteza hamu ya kufanya mapenzi

• Huwa na hali ya kukamaa pamoja na ukavu katika sehemu za siri za mwanamke

MADHARA YA MWANAMKE KUWA NA TATIZO LA UKE MKAVU NI PAMOJA NA;

✓ Mwanamke Kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa

✓ Mwanamke kukosa hamu kabsa ya tendo la ndoa

✓ Kupata michubuko wakati wa tendo la ndoa

✓ Kuwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa ukimwi pamoja na magonjwa mengine ya zinaa kutokana na hali ya michubuko ukeni

✓ Mwanamke kuwa katika hatari ya kupata maambukizi katika via vyake vya uzazi yaani PID

✓ kutokwa na damu ukeni wakati wa kufanya mapenzi

MATIBABU YA TATIZO LA MWANAMKE KUWA NA UKE MKAVU

– Matibabu ya tatizo la uke mkavu hutegemea na chanzo cha tatizo husika hivo basi ni vizuri kuongea na wataalam wa afya ili kupata vipimo,kujua chanzo cha uke mkavu pamoja na matibabu yake.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Chanzo cha UKE MKAVU pamoja na Matibabu yake
0 Comment

Watu 13 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama UgirikiAfyaclass Bongo Social •

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea kuwatafuta watu 13 waliopotea baada ya meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Comoro kuzama leo asubuhi katika kisiwa cha bahari ya Aegean cha Lesbos nchini Ugiriki.

Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea kuwatafuta watu 13 waliopotea baada ya meli ya mizigo iliyokuwa na bendera ya Comoro kuzama leo asubuhi katika kisiwa cha bahari ya Aegean cha Lesbos nchini Ugiriki. Meli hiyo iliyokuwa na watu 14 ilikuwa inatoka Dekheila nchini Misri, kuelekea Istanbul.

Kikosi cha ulinzi wa Pwani kimesema kuwa helikopta ya jeshi la wanamaji imemuokoa mfanyakazi mmoja kutoka kwa meli hiyo inayojulikana kama RAPTOR, ambaye alipelekwa katika hospitali Kuu ya Lesbos.

Watu 500 wahofiwa kufariki katika ajali ya boti Ugiriki

Msemaji wa kikosi hicho cha walinzi wa Pwani, Nikos Alexiou, ameliambia shirika la habari la AFP kwamba, mfanyakazi huyo yuko katika hali ya mshtuko lakini hakutoa maelezo zaidi.

Hatima ya abiria wengine 13 waliokuwa katika meli hiyo bado haijulikani.

Meli tano za mizigo, meli tatu za walinzi wa pwani, jeshi la anga na helikopta za jeshi la wanamaji zimejiunga katika juhudi hizo za uokoaji.

Watu 13 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama Ugiriki
0 Comment

Mbunge Pauline Gekul kukabiliwa na tuhuma nzito za kumwingizia chupa sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wakeAfyaclass Bongo Social •

Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limemhoji Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul kufuatia tuhuma zinazomkabili za ukatili na unyanyasaji dhidi ya mfanyakazi wake, Hashim Ally.

Gekul anatuhumiwa kutoa maelekezo kwa kundi la vijana wake kumwingizia chupa sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wake, Hashim Ally au kumpiga risasi kwa madai kwamba alitumwa kimkakati kwenda kwenye hoteli yake ya Paleii Lake View Garden.

Sakata hilo liliibuka baada ya video kusambaa mitandaoni ikimwonyesha Hashim akieleza jinsi alivyofanyiwa ukatili huo na Gekul ambaye hadi jana, alikuwa ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, jana usiku.

Jana Novemba 26, 2023, Gekul amehojiwa na Jeshi la Polisi mkoani Manyara kufuatia tuhuma hizo zilizoibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huku watu wakitoa maoni tofauti.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, George Katabazi amekiri mbunge huyo kufika kituo cha polisi Babati leo majira ya saa 10 jioni kwa ajili ya kutoa maelezo juu ya suala hilo na kisha kuruhusiwa kuondoka.

Wakati jeshi la polisi likimhoji Gekul, wanasheria na wanaharakati wa haki za binadamu wametaka hatua zaidi za kisheria zichukuliwe dhidi ya mbunge huyo kama tuhuma zinazomkabili zitathibitika kuwa za kweli.

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Fulgence Massawe amesema uamuzi uliotolewa na Rais Samia ambaye ndiyo mamlaka ya uteuzi ulilenga kurejesha imani kwa wananchi kufuatia kile kilichotokea.

“Kwa kuwa mbunge huyo anakabiliwa na tuhuma za uhalifu, uchunguzi ufanyike na hatua zinazofaa zichukuliwe dhidi ya wote waliohusika katika tukio hilo,” amesema.

Massawe amesema ili mradi Waziri anafanya biashara halali na iliyotangazwa na sheria na katiba, hatakiwi kutumia mamlaka yake ya uongozi kuwatia hasara washindani wake.

“Hili limekuwa jambo muda mrefu kwamba viongozi wakuu wa kitaifa wamekuwa wakitumia nyadhifa zao kufaidika na biashara zisizo za haki au kufanya mabadiliko ya kisera na kisheria kwa manufaa yao binafsi,” amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.com

Mbunge Pauline Gekul kukabiliwa na tuhuma nzito za kumwingizia chupa
sehemu ya haja kubwa mfanyakazi wake
0 Comment

TV 15 zaibwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa NjombeAfyaclass Bongo Social •

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amemuelekeza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuwasimamisha kazi baadhi ya Watumishi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe akiwemo Katibu wa Afya, Watu wa Idara ya manunuzi pamoja na Idara ya TEHAMA ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za wizi wa TV 15 pamoja na kompyuta tatu katika Hospitali hiyo.

Mtaka ametoa maagizo hayo mara baada ya kushtukiza katika Hospitali hiyo baada ya kupata taarifa ya upotevu wa vifaa hivyo vilivyopotea miezi mitano iliyopita huku akimtaka Afisa manunuzi wa Hospitali hiyo Aloyce Kavumika kulipa takribani shilingi milioni.11 kwa ajili ya kununua TV 15 zilizoibwa.

Awali Afisa manunuzi akitoa taarifa ya wizi huo alisema alipata taarifa ya wizi wa TV July 08,2023 akiwa nje ya ofisi ambapo baada ya kurejea ofisini hapo alilazimika kukaa na Watumishi wenzake kwa nyakati tofauti huku wakikubaliana Watumishi wa Idara hiyo kuingia gharama zao kulipa TV hizo.

Amesema baada ya makubaliano hayo walikwenda kwenye moja ya duka la Mfanyabiashara mmoja mjini Njombe na kuagiza TV nyingine ambazo walipewa kwa makubaliano ya kuzilipa baada ya miezi miwili yaani mpaka mwezi huu wa November na waliweza kupewa bila maandishi yoyote kwakuwa wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali ambapo mpaka sasa fedha hiyo pia bado haijalipwa kwa mwenye duka.

TV 15 zaibwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe
0 Comment

Tatizo la kubana kwa govi ni nini?Afyaclass Bongo Social •

KUBANA KWA GOVI:Sababu,dalili,matibabu yake

Kubana kwa govi

Tatizo la kubana kwa govi ni nini?

Tatizo la kubana kwa govi (paraphimosis) ni tatizo hatari linaloweza kuwapata wanaume na wavulana ambao bado hawajatahiriwa. Kubana kwa govi kuna maanisha govi limebana na kukwama nyuma ya kichwa cha uume na  huwezi kulirudisha kwenye sehemu yake ya kawaida.

Nini sababu ya tatizo la kubana govi?

Kubana kwa govi

Wanaume ambao hawajatahiriwa wakati mwingine wanavuta govi nyuma wakati wa kushiriki ngono, wanapokwenda chooni au wanapokuwa wanasafisha uume. Madaktari au manesi wanaweza pia kuvuta govi nyuma wanapokuwa wakifanya uchunguzi wa uume au kuweka mpira wa mkojo.

Wakati mwingine daktari au nesi anaweza kusahau kurudisha govi mahala pake. Kama govi litaachwa nyuma ya kichwa cha uume kwa muda mredu, uume unaweza kuvimba sana kiasi kwamba govi linakwama na kushindwa kurudi.

Nifanye nini ili kuzuia kupata tatizo la kubana kwa govi?

  • Baada ya ngono, kutoka chooni au baada ya kujisafisha, hakikisha unarudisha govi mahala pake.
  • Kamwe usiache govi nyuma ya kichwa cha uume kwa muda mrefu zaidi ya inavyohitajika
  • Kama umekewa mpira wa mkojo, jiangalie kama govi limerudishwa mahala pake na kufunika kichwa cha uume

Ni nini kinachotokea nikipata tatizo la kubana kwa govi?kubana kwa govi

Tatizo la kubana kwa govi linasababisha maumivu makali, lakini sio wakati wote. Unaweza kupata maambukizi kwenye uume. Unaweza kushindwa kabisa kukojoa. Kama unaona inakuwa ngumu kurudisha govi ni vizuri kumwona daktari haraka sana.

Kitu cha kwanza atakachofanya daktari ni kutibu uvimbe uliopo. Hili linaweza kufanyika kwa kubonyeza uume kwa mikono au kwa kuufunga kwa nguvu kwa bandeji. Baada ya uvimbe kupungua, daktari ataweza kuvuta govi na kulirudiha mahala pake. Kama bado govi limebana, daktari anaweza kuhitaji kukata kidogo sehemu ya govi ili kufanya iwe rahisi kurudisha.

Vyanzo

https://medlineplus.gov/ency/article/001281.htm

Tatizo la kubana kwa govi ni nini?
0 Comment

Ukiwa na Wasiwasi unaweza kukumbana na dalili hiziAfyaclass Bongo Social •

Ukiwa na Wasiwasi unaweza kukumbana na dalili hizi,

Kila mtu kwenye vipindi flani vya maisha huweza kukumbana na wasiwasi, hofu na wasiwasi huweza kuwa shida ya muda mfupi au likawa tatizo la muda mrefu(Chronic anxiety).

Wasiwasi huweza kuja kutokana na matukio mbali mbali ya maisha mfano;

  • Wakati wa Interview
  • Wakati wa mitihani kwa wanafunzi n.k

Hizi ni dalili za wazi wazi ambazo mtu mwenye wasiwasi huweza kuzipata(physical symptoms of anxiety);

– Mapigo ya Moyo kwenda mbio

– Kupata hali ya kizunzuzungu

– Kupata maumivu ya tumbo

– Na wengine kuharisha

– Kupata maumivu ya kifua

– Kupata maumivu ya Kichwa

– Mwili kuchoka kupita kiasi

– Kupata shida ya kukosa Usingizi(insomnia) n.k

Je umewahi kukutana na hali kama hii…!!!!

Ukiwa na Wasiwasi unaweza kukumbana na dalili hizi
0 Comment

Papa Francis arejea Vatican baada ya kufanyiwa vipimoAfyaclass Bongo Social •

Haya yanajiri wiki moja kabla ya safari ya Papa Francis kuelekea Dubai ambapo atashiriki Desemba 2 mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya Hewa wa COP28.

Uongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Vatican umetangaza kuwa kiongozi wake Papa Francis amefanyiwa vipimo vya mapafu leo hii na hakukutwa na ugonjwa wowote. Hayo ni baada ya Papa Francis kuahirisha mikutano yake yote iliyokuwa imepangwa leo kutokana na ugonjwa wa mafua.

Haya yanajiri wiki moja kabla ya safari ya Papa Francis kuelekea Dubai ambapo atashiriki Desemba 2 mkutano wa Umoja wa Mataifa wa hali ya Hewa wa COP28, ambako anatarajiwa kukemea ukosefu wa hatua na kuhimiza kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira.

Afya ya Papa Francis imekuwa ikidhoofika katika miezi ya hivi karibuni, na kumlazimu kutumia kiti cha magurudumu na hivyo kuzusha uvumi wa kujiuzulu kwake, kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Papa Benedict wa XVI.

Papa Francis arejea Vatican baada ya kufanyiwa vipimo
0 Comment

TANZIA: Askofu Erasto Kweka afariki duniaAfyaclass Bongo Social •

Askofu Mstaafu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Erasto Kweka amefariki dunia Novemba 25, 2023, kweye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), alilokuwa anapatiwa matibabu.

Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa hilo, Zebadiah Moshi kupitia taarifa yake aliyoitoa leo, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kueleza kuwa, Dk Kweka amekuwa kiongozi wa Dayosisi ya Kaskazini toka mwaka 1976 mpaka 2004 alipostaafu.

“Uongozi wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini una masikitiko makubwa kutangaza kutwaliwa kwa baba Askofu Mstaafu Dk Erasto Kweka, kifo kimetokea leo, Novemba 25, 2023 saa nne asubuhi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),” imeeleza taarifa hiyo.

TANZIA: Askofu Erasto Kweka afariki dunia
0 Comment

Tukio la Mwanamke mmoja kuolewa na Wanaume wawili(polyandrous)Afyaclass Bongo Social •

Mwanamke mmoja ambaye yupo katika uhusiano wa polyandrous aonyesha waume zake wawili na watoto wao,

Tukio hilo limetokea,Baada ya Siku ya Alhamisi huko Marekani, mwanamke huyo anayejulikana kwa jina la Passion Jones kutoa shukurani zake,

Passion alipiga picha na wanaume wawili ambao anaishi nao pamoja na watoto zao.

Aliongeza kwenye nukuu kwamba alishukuru kwa “ujasiri na uhalisi wa kuishi kwa sauti kubwa na familia nzuri kama hii”.

Wafuasi wake pia waliungana naye katika kusherehekea familia yake, huku wengine wakitaja kuwa wanataka vivyo hivyo kwao wenyewe.

Tukio hili limeshangaza wengi, huku kukiwa na maoni tofauti ya watu, hasa ukizingatia Misingi ya Kidini na amri za Mungu…!!!!

Tukio la Mwanamke mmoja kuolewa na Wanaume wawili(polyandrous)
0 Comment

Rais Samia atengua uteuzi wa Naibu WaziriAfyaclass Bongo Social •

Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Naibu Waziri wa Wizara ya Katiba na Sheria, Pauline Gekul kuanzia Novemba 25, 2023.

Gekul anatolewa katika nafasi hiyo, ikiwa ni kipindi kifupi tangu kuibuka tuhuma za ukatili wa haki za binadamu katika mitandao ya kijamii zikimuandama Mbunge huyo wa jimbo la Babati Mjini kuhusika na udhalilishaji.

Taarifa za kutenguliwa kwa Naibu Waziri huyo, zimetolewa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus kupitia mitandao ya kijamii ya Ikulu.

Rais Samia atengua uteuzi wa Naibu Waziri
0 Comment

UTPC:kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsiaAfyaclass Bongo Social •

Katika kuendelea kuunga mkono Serikali Kupinga Vitendo vya kikatili Nchini ,Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania leo umezindua rasmi kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, ambapo imelenga kuwaunganisha waandishi wa habari nchini pamoja na wadau wengine kupaza sauti kwa pamoja kupinga vita vitendo hivyo.

Akizindua kampeni hiyo kwa niaba ya Rais wa UTPC, Deo Nsokolo, Mjumbe wa Bodi ya UTPC, Lilian Lucas amesema kuwa waandishi wa habari wanayo nafasi kubwa kupitia kalamu zao kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto vinakomeshwa.

Amesema wanahabari wanadhamana kubwa katika kuhakikisha jamii inatambua madhara ya ukatili kwa jamii hivyo wanapaswa kutumia kalamu zao vizuri kupata sauti

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa UTPC, Keneth Simbaya amesema kuwa vitendo vya ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto ni miongoni mwa ukiukwaji mkubwa uliokithiri wa haki za binadamu na kuwataka wanahabari kushiriki vyema katika kuielimisha jamii hasa juu ya sera, sheria pamoja na miongozo ambayo itasaidia kuleta mabadiliko na kupunguza ama kuondoa kabisa ukatili.

UTPC:kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
0 Comment

Hali ya msanii wa Bongo Muvi, Carina Hussein, imezidi kuwa mbaya tena,afanyiwa upasuaji mara 21Afyaclass Bongo Social •

Hali ya msanii wa Bongo Muvi, Carina Hussein, imezidi kuwa mbaya tena, baada ya kufanyiwa upasuaji wa mara ya 21 kutokana na mshono mkubwa wa tumboni kwake kufumuka tena na kinyesi kuanza kutoka mfululizo.

Hali ya msanii huyo imezidi kudhoofika sana tofauti na awali huku akisema kuwa katika operesheni zote alizofanya hii imekuwa ya maumivu sana na kubwa zaidi hajapata haja kubwa karibia mwezi na mkojo hautoki mpaka amewekewa mpira wa kutolea mkojo.

” Nimekuwa kwenye mateso makubwa sana sikuwa napenda tena kueleza maana kama nawachosha watu, lakini ukweli nina maumivu makali na dawa nanunua elfu 92000, kila baada ya siku tatu, bado kubadilisha kidude shingoni zaidi ya laki moja, tumeshauza chochote tulichonacho hatuna hata cha kuuza tena, nateseka jamani” alisema hawa kwa tabu kutokana na kudhoofika sana.

Globaltvonline imefanya naye mahojiano nyumbani kwao Magomeni jijini Dar, na kuona wazi kuwa Carina, anahitaji msaada sana kwa sasa hivyo amewaomba watanzania wasimchoke, anateseka mno amepungua sana, maana hana anachokula kikaa tumboni.

” Nateseka mpaka natamani Mung, afanye chochote juu yangu, sina matumaini tena” alisema Carina

Kama unataka kumsaidia chochote waweza kumsaidia kupitia namba

0769_990045 M-PESA
Carolinhawa Hussein Ebrahim bounin.

0789_095858 Airtel money
FATUMA MIKIDADI maruzuku..

0712_595858 tigopesa
Carolinhawa Hussein Ebrahim bounin

Hali ya msanii wa Bongo Muvi, Carina Hussein, imezidi kuwa mbaya
tena,afanyiwa upasuaji mara 21
0 Comment

Andry Rajoelina achaguliwa tena kuwa rais wa MadagascarAfyaclass Bongo Social •

Tume ya uchaguzi yasema Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16.

Tume ya uchaguzi nchini Madagascar imetangaza hii leo kuwa rais aliyopo madarakani Andry Rajoelina ameshinda kwa mara nyingine katika duru ya kwanza ya uchaguzi ambao ulisusiwa na takriban wagombea wote wa upinzani.

Tume hiyo imesema Rajoelina mwenye umri wa miaka 49, amepata asilimia 58.95 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi iliyofanyika Novemba 16.

Idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo baada ya wagombea 10 kati ya 12 wa upinzani kutoa wito wa kususia uchaguzi huo wakilalamika kuwa ni “mapinduzi ya kitaasisi” kwa faida ya mgombea aliye madarakani

Andry Rajoelina achaguliwa tena kuwa rais wa Madagascar
0 Comment

Ahukumiwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na mkono wa SokweAfyaclass Bongo Social •

Mahakama ya Wilaya Uvinza mkoani Kigoma imemuhukumu mshitakiwa Jeremia Ngendabanka (31), mkulima, mkazi wa Kijiji cha Buhingu wilayani Uvinza, kwenda jela miaka 20 baada kumtia hatiani kwa kosa la kupatikana na nyara za Serikali.

Mshtakiwa huyo, anadaiwa kutenda kosa hilo Septemba 22, 2022 baada ya kupatikana nyara za Serikali mkono mmoja wa sokwe mtu, kichwa kimoja cha sokwe mtu na ngozi moja ya sokwe mtu vyenye thamani ya shilingi12,056,304.

Akitoa hukumu hiyo Novemba 23, 2023 Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Uvinza, Misana Majura amesema kuwa Mahakama imejiriridhisha pasipo shaka na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimae kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa hili.

Mshitakiwa amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uwindaji haramu ambavyo vinapelekea uharibifu wa rasilimali za taifa ikiwemo Wanyama pori.

Ahukumiwa Jela miaka 20 kwa kukutwa na mkono wa Sokwe
0 Comment

Chanzo cha mwanaume kushindwa kurudia tendoAfyaclass Bongo Social •

Chanzo cha mwanaume kushindwa kurudia tendo

Baada ya mwanaume kufanya mapenzi na kuridhika awamu ya kwanza huweza kurudia tendo na kuendelea kwenye awamu ya pili, hapo katikati hukutana na kipindi ambacho kitaalam hujulikana kama refractory period

Refractory period: Hiki ni kipindi cha muda baada ya kufika kileleni ambapo mtu hana msisimko wa kufanya tendo.

(the span of time after having an orgasm during which a person is not sexually responsive).

Ukiwa kwenye kipindi hiki huwezi kufanya tena tendo la ndoa,wala kufika kileleni.

Muda wa Kipindi hiki hutofautiana kati ya mtu na mtu, huweza kuchukua dakika chache mpaka hata zaidi ya siku moja,

Ukiwa na afya bora ya mwili kwa ujumla ikiwemo afya ya moyo,kula vizuri,kufanya mazoezi n.k huweza kupunguza muda wa kipindi hiki.

Chanzo cha mwanaume kushindwa kurudia tendo

mwanaume kushindwa kurudia tendo au kushindwa kwenda roundi ya pili,tafsiri yake ni kwamba yupo kwenye kipindi cha refractory period,

Swala la kwamba amekaa muda gani au hali hii imedumu kwa muda gani,kwa lugha nyingine tunaweza kusema refractory period yake imekuwa ya muda mrefu au muda mfupi.

Kumbuka: Kama tulivyosema awali, mtu akiwa kwenye kipindi ambacho hujulikana kama “refractory period”,

hupoteza hisia au hamu ya kufanya tendo tena na wakati mwingine hushindwa kabsa kufanya tendo tena,

huweza kupata shida ya uume kushindwa kusimama tena, na kushindwa kufika kileleni.

Chanzo halisi ya refractory period kuchukua muda mrefu ni nini?

Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja,kwanini baadhi ya watu huwa na kipindi kirefu zaidi “Long refractory period” kuliko wengine,

Ingawa baadhi ya tafiti zimeonyesha vitu vyenye uhusiano wa karibu sana na tatizo hili, vitu hivo ni pamoja na;

1. Mabadiliko ya vichocheo mwilini ikiwemo kichocheo cha Prolactin,

Utafiti wa mwaka 2002 ambao ulifanyika kwa kijana wa kiume mwenye umri wa miaka 25 ulionyesha uhusiano wa karibu kati ya refractory period na uzalishwaji wa vichocheo aina ya prolactin.

Pia utafiti huu ulionyesha kwamba vichocheo vya Prolactin vinaweza kuhusika katika uwezo wa mwanaume kufika kileleni kwa zaidi ya mara moja yaani “multiple orgasms”.

2. Sababu zingine ni pamoja na;

  • Afya ya mtu kwa ujumla ikiwemo; afya ya moyo,mishipa ya damu,usukumaji wa damu,presha ya damu,magonjwa kama kisukari n.k
  • Ubora wa mahusiano husika, je tendo hilo linafanyika kwa mtu unayempenda,unavutiwa naye,unakuwa na hamu naye kila wakati, je hufanyi tendo ukiwa na hasira?, je hampo kwenye ugomvi,migogoro n.k
  • Kuwa na shida ya msongo wa mawazo au Stress
  • Pia mnafanya tendo mara ngapi(frequency of sex), unaweza kuchukua muda mrefu kwenye kipindi cha refractory period ikiwa unafanya tendo mara nyingi zaidi, hii inaweza kusababisha wewe kushindwa kabsa kurudia tendo,kushindwa kufika kileleni,uume kushindwa kabsa kusimama n.k

Zingatia mambo haya ili kukabiliana na tatizo hili;

✓ Hakikisha unafanya mazoezi ya mwili ikiwemo;

  • Kutembea
  • Kukimbia n.k

✓ Hakikisha unazibiti shida ya Uzito mkubwa

✓ Hakikisha unakula mlo kamili,mlo wenye afya, epuka vyakula vya mafuta mengi sana,chumvi nyingi n.k

✓ Kama una magonjwa ya moyo, Ugonjwa kama kisukari,Presha n.k hakikisha unapata tiba

✓ Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi

✓ Epuka uvutaji wa Sigara au kutumia dawa zozote za kulevyia.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

rejea za mada:

Chanzo cha mwanaume kushindwa kurudia tendo
0 Comment

Sababu za kufariki baada ya kuongezewa makalio zatajwaAfyaclass Bongo Social •

Wataalamu bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile nchini, wametaja sababu tatu zinazoweza kusababisha anayepatiwa huduma ya kuongeza shepu na makalio kufariki dunia.

Sababu hizo zimetajwa kuwa ni hali ya kiafya ya mteja husika, utaalamu wa watoa huduma na mazingira yaliyopo wakati na baada ya upasuaji.

Wataalamu hao wamesema hayo jana Alhamisi, Novemba 2023 ikiwa ni siku chache tangu kutolewa taarifa kuhusu watu wengi wanaokwenda nchini Uturuki kuongeza makalio na shepu kufariki dunia wakipatiwa huduma au baada.

Ripoti ya upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwaka 2023 iliyofanywa nchini Marekani na tovuti ya ‘Research and Market’ inaonyesha asilimia 42.7 ya waliofanyiwa upasuaji huo walipata madhara ikiwamo kifo.

Takwimu hizi zinaonyesha takribani nusu ya wote waliofanyiwa upasuaji wa kurekebisha maumbile hupata madhara hasi.

Daktari bingwa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile wa Hospitali ya Aga Khan, Aidan Njau akizungumza na Mwananchi Digital amesema mgonjwa mwenyewe namna anavyochagua akapate huduma wapi, anayetakiwa kumfanyia huduma na baada ya upasuaji ni vitu vya msingi kabla ya kufanya uamuzi.

“Ukiangalia soko la huduma hiyo kwa sasa linahamia Uturuki ukilinganisha na sehemu nyingine kama India na kwingineko, inaelezwa gharama ni za chini zaidi, utalaamu na mazingira,” anasema na kuongeza:

“Lakini sasa mtu ana hali gani kiafya? anaweza kuwa na matatizo ya moyo, figo, magonjwa mengine ambayo sawa hayana mahusiano ya karibu na kile alichokifuata, maana amekwenda pale kutaka kurekebisha maumbile yake, lakini anaweza kuwa na umri mkubwa, kisukari, presha na magonjwa kama hayo.”

Dk Njau amesema anapofanyiwa upasuaji na tayari ana matatizo mengine hawezi kuangaliwa kwa maana wao wanaangalia kipato kwa kile alichokifuata.

“Hospitali inaingiza kipato, nchi pia inaingiza kipato sababu ni utalii wa matibabu. Huduma hiyo ni ndefu, ikileta changamoto hasa kwa matatizo mengine, nafasi ya kusogelea kifo inakua kubwa zaidi,” amesema.

Dk Njau amesisitiza utaalamu ni kitu cha pili muhimu zaidi katika huduma za urekebishaji maumbile. Amesema kwa mzoefu anafanya vizuri zaidi tofauti na wanaojifunza mitandaoni au hawana utaalamu husika, bali wanatafuta fedha.

“Ni mbaya, ni ukweli lazima tuseme, wengi sasa hivi wanatafuta mtandaoni watu hawajui bila kujua mitandao inaweka kila kitu anaingia huko na kuanza kuwasiliana na watu asiowajua, wala utaalamu walionao, wala uzoefu,” amesema.

Anasema upasuaji huo unahitaji mtu anayejua nini anafanya na ana uzoefu mkubwa.

“Anaweza kukosea yakatokea makosa ya kibinadamu yakasababisha kifo au madhara pamoja na kwamba teknolojia ipo juu kuliko sisi, lakini bado kuna suala la utaalamu, vifaa, dawa na vingine,” amesema.

Ameeleza suala la mazingira mtu anapokwenda nchi za watu wengine kufuata huduma mara nyingi hufikia hotelini na hana ndugu wala watu wa karibu, jambo linalochangia wengi kupata maambukizi.

“Wengi hukwepa gharama, kuna watu wanakuwa kama mawakala wanawapeleka kule wanawekwa kwenye hoteli au nyumba moja wanawekewa mpishi. Sasa kuna huduma zinahitajika kuangalia kidonda kuhakikisha unapata dawa inavyohitajika,” amesema na kuongeza:

“Mazingira yanatakiwa kuwa masafi, sasa kutokana na foleni na gharama unakaa siku mbili au moja hospitali unarudi hotelini kule huna mwangalizi, mazingira mabovu, nafasi ya kupata maambukizi ni kubwa ikitokea shida ni ngumu kulalamika, wao ni wahudumu wa hoteli tu,” amesema.

Dk Njau amesema gharama za upasuaji huo nje ya nchi ni kubwa kwa kuanzia nauli ya ndege, kulala hotelini, mizunguko na gharama za huduma, mtu wa kuongozana naye au kutokuwa na ndugu na bado wakirudi wanapata changamoto.

Anasema, “Wanaporudi wengi wanapata athari, wanakuja Aga Khan wana vidonda ambavyo vimeharibika na vingine vinakuwa na usaha inabidi turudie upya na wengine vinavilia damu, inahatarisha maisha yake na ile shepu ambayo alikuwa anaihitaji haipati tena.”

“Hawa wengi wakimpigia daktari wake hawapati mawasiliano na wakati mwingine daktari anamkimbia, kurudi kule hawezi anapata wapi tena Sh20 milioni ya kurudi,” anahoji.

Daktari bingwa wa kurekebisha maumbile katika Hospitali ya Muhimbili-Upanga, Dk Lauren Rwanyuma amesema wakati mwingine upasuaji unaweza kuwa ndivyo sivyo na matokeo yaliyotarajiwa yasipatikane.

“Akiwa na bahati matokeo yake shepu ya mwili ikawa kubwa au ndogo tofauti na matarajio, lakini kama ana bahati mbaya anapoteza maisha na hii sababu kubwa ni utaalamu duni. Kuna wengine nyama zinagoma kuungana na kukaa katika hali ya kawaida na nzuri, hivyo kuwalazimu kufanya upasuaji mwingine, hali hiyo inaweza kuchangiwa na umri,” amesema.

Dk Rwanyuma amesema ni vyema mhusika akawa makini kufuatilia kwa kina hospitali au mtaalamu anayekwenda kumfanyia huduma hiyo, kwa maana kama atafanyiwa na mtu asiye mzoefu madhara ni makubwa.

Licha ya uwapo wa madhara ambayo wataalamu wa afya huyasema, bado soko la upasuaji wa kurekebisha maumbile linazidi kushika hatamu duniani, wastani wa ongezeko la utolewaji wa huduma hiyo ni asilimia 9.2 kila mwaka.

“Soko la kimataifa la upasuaji wa kurekebisha maumbile lilikua kutoka Dola za Marekani bilioni 42.55 (Sh106.2 trilioni) mwaka 2022 hadi makadirio ya Dola bilioni 46.45 (Sh116.16 trilioni) mwishoni mwa mwaka 2023,” imesema ripoti ya upasuaji wa kurekebisha maumbile ya mwaka 2023.

Sababu za kufariki baada ya kuongezewa makalio zatajwa
0 Comment

Mwanamke Tumia vidokezo hivi kujikinga na maambukizi ya BACTERIA UkeniAfyaclass Bongo Social •

Ukweli ni kwamba wanawake wengi husumbuliwa na maambukizi ya bacteria ya mara kwa mara sehemu zao za siri, huku wengine kufikia hatua ya kuwa na tatizo la UTI sugu licha ya kutumia dawa nyingi sana.

Moja ya maambukizi ambayo huwatesa wanawake wengi ni maambukizi ya bacteria kwenye mfumo mzima wa mkojo yaani UTI.

MAMBO YA KUFANYA ILI KUJIKINGA NA MAAMBUKIZI YA BACTERIA UKENI

– Mwanamke kuepuka tabia ya kuweka vitu mbali mbali sehemu za siri mara kwa mara kama vile; Vidole, sex toys N.K

– Mwanamke kuepuka kujisafisha kutoka nyuma kwenda mbele baada ya kujisaidia chooni

– Epuka matumizi ya maji ambayo yamekaa kwa muda mrefu chooni

– Epuka matumizi ya vyoo vichafu

– Epuka matumizi ya vitu vyenye kemikali kama baadhi ya sabuni kujisafisha ukeni

– Epuka kuvaa nguo za ndani ambazo hubana sana

– Vaa nguo za ndani zenye material ya pamba zaidi

– Usivae nguo ya ndani kwa muda mrefu au badilisha tu pale inapoloa au kuchafuka

– Usivae nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri

– Epuka kushirikiana tendo la ndoa na mtu ambaye ana dalili za magonjwa ya zinaa

N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Mwanamke Tumia vidokezo hivi kujikinga na maambukizi ya BACTERIA Ukeni
0 Comment

"Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: 'Mfanye kama mvulanaAfyaclass Bongo Social •

Uso wa Nilofar Ayoubi, mwenye umri wa miaka 4 tu, bado ulikuwa mwekundu kutokana na kofi alilokuwa amepigwa na mgeni wakati akicheza katika mitaa ya Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan. Pigo hilo lilikuwa la kikatili sana kiasi kwamba alianguka sakafuni.

“Nilirudi nyumbani nikilia baba yangu alikuwa mwekundu kwa hasira,” Nilofar ameiambia BBC, miaka ishirini na mitatu baada ya tukio hilo ambalo anasema limewekwa katika kumbukumbu zake. “Namkumbuka akirudi nyuma na kukasirika, akipiga kelele na kusema ‘anawezaje kukugusa?’”

Muda mfupi kabla ya kumpiga, mgeni huyo alikuwa amemgusa kifua chake, akitafuta ishara za “uke.” Kisha akamtishia na kumwambia kwamba ikiwa hatavaa kilemba chake, wakati mwingine, angemshambulia baba yake.

Baada ya muda mfupi wa hasira, baba yake Nilofar alifanya uamuzi mkali: “Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: ‘Mfanye kama mvulana.’”

Nilofar alikulia Afghanistan wakati wa enzi ya kwanza ya utawala wa Taliban – kuanzia mwaka 1996 hadi 2001 – na kwa karibu miaka 10, aliishi maisha ya mtoto, akitoroka udhibiti wa ukandamizaji ambao Sharia, sheria za Kiislamu, zinazokandamiza wanawake.

Leo, akiwa uhamishoni, anakumbuka jinsi mambo yalivyokuwa wakat iwa makuzi yake katika moja ya maeneo ya kihafidhina zaidi duniani, ambayo jinsia unayozaliwa nayo inafafanua mipaka ya haki unazoweza kupata.

Tofauti kati ya maisha ya mvulana na msichana nchini Afghanistan mara nyingi ni mbaya.

Kukulia katika Kunduz

Nilofar alizaliwa mwaka 1996, lakini nyaraka zake za utambulisho zinasema alizaliwa mwaka 1993. Baba yake alifanya mabadiliko hayo ili binti yake aweze kuanza shule haraka iwezekanavyo baada ya Marekani kuingilia kati mwaka 2001 kuipindua serikali ya Taliban.

” Kunduz sio mji wa kuvutia kwa mwanamke kukulia katika .”Ni vigumu kuwa mwanamume, na ni vigumu zaidi kuwa mwanamke,” aliiambia BBC.

“Kama mtoto, una nguvu moja kwa moja, hata kama wewe ni mtoto wa miaka 2 inamaanisha unapokea heshima zaidi kuliko mama yule yule aliyekuzaa. Kuanzia umri wa miaka 4, unaweza kuwa msimamizi wa kisheria wa mwanamke ambaye kuletwa wewe katika dunia (…) na yeye ni mtumwa wako. “Kama wewe ni mwanamke, wewe ni asiyeonekana.”

Chini ya sheria kali kama hizo kali , Nilofar anaeleza kuwa ilikuwa kawaida kwa familia yao kuwavalisha mabinti zao kama wavulana hasa kama familia haikuwa na mtoaji wa msingi: chini ya sharia, mwanamume yeyote anaweza kumkaribia mwanamke ambaye hana wa kumhudumia na kumlazimisha kuwa mke wake wa tano au wa sita.

“Kwa upande wangu, hali ilikuwa tofauti. Haikuwa kwa kukosa mtoa mtu wa kunisaidia lakini ilikuwa ni kuweza kuishi maisha kwa uhuru.”

Nilofar anakumbuka msaidizi wao , baba yake, alikuwa mtu maalum kwa wakati huo nchini Afghanistan: “Alichukia siasa.”

Utawala wa Taliban unaweka sheria kali ya Sharia, inayozuia haki nyingi za wanawake.

Akiwa amesimama mbele ya baba yake, huku nywele zake zikiwa zimenyolewa na kuvaa nguo za mmoja wa ndugu zake, Nilofar alikuwa karibu kuanza maisha tofauti kabisa na ya wasichana wengine wa umri wake, wakiwemo dada zake.

“Nilianza kuishi maisha kama ya kaka zangu, niliweza kwenda na baba yangu sokoni nikiwa nimevaa kama kijana. Tuliweza kutembea kwa maili na maili. Tulienda kwa basi kutazama michezo, nilikuwa na marafiki katika kitongoji na nilitumia muda wote kucheza mitaani.”

Dada zake, kwa upande mwingine, walilazimika kufunika nywele zao – hata ndani ya nyumba – na kuvaa kihafidhina, kitu ambacho baba yao alichukia.

“Baba yangu hakuwahi kukubaliana na suala la sisi kuvaa nguo hizo nyumbani, siku zote alipigana na mama yangu na kumuuliza kwa nini hakuvaa vizuri. ” Nguo hii ni ndefu sana, kwa nini ni pana sana? “Baba yangu alikuwa mtu wa aina yake .”

Kwa miaka mingi, baba yake Nilofar alipokea vitisho.

Kujenga uaminifu

Kukua katika ulimwengu wenye vitambulisho viwili, Nilofar daima alihisi utofauti. Labda yule ambaye angeweza kuelewa vizuri kile alichokuwa akipitia alikuwa jirani yake, msichana wa umri huo ambaye pia alivaa kama mvulana na ambaye alifanya maovu mengi.

“Tulikuwa tunafanya mambo sawa. Wakati wowote walipokuwa wakikaribia kumkamata mmoja, mwingine alikuja kumuokoa,” anasema Nilofar, akisisitiza kuwa hatari ya kutambuliwa kama wanawake ilikuwa ya mara kwa mara.

“Pia ilinisaidia sana kwamba nilikuwa na uhakika kuwa nilikuwa mvulana kwamba ilikuwa vigumu kwa watu kufikiri sikuwa nilivyo. Nakumbuka kwamba katika mikutano, mimi ndiye niliyesema”‘acha tuwasumbue wasichana’, nikiwaambia, ‘oh wewe ni mrembo, jinsi ulivyo mzuri tena mzuri sana.’”

Maisha ya Nilofar yalikuwa ya kucheza karate, judo na kuendesha baiskeli, wakati dada zake wakiishi na kucheza michezo ya kawaida ya wasichana Kunduz, kukaa nyumbani, kuishi maisha ya kimya kimya na nje ya macho ya wanaume.

“Sikuwahi kuwa na uhusiano na dada zangu. Sikuwahi kuelewa jinsi dunia yao ilivyokuwa. Na ndio maana sikujua kwamba wasichana walipata hedhi.”

Nilofar alikuwa ameona matangazo ya kuuza taulo za hedhi, lakini haikuwa wazi kwake kazi yake ilikuwa nini.

“Mara tu nilipopata taulo za hedhi nikaenda kwa baba yangu: ‘Baba, baba, angalia, ni kama wale kwenye TV, ni ya kuchekesha. Ni kwa ajili ya nini?’ “Baba yangu hakujua la kunijibu.”

“Baada ya hapo nilimpelekea kwa dada yangu. Nakumbuka alichukua kutoka kwangu na alinitukana. Hata wakati huo, hakuna mtu aliyefikiria kuniambia hedhi ni nini.”

Nilofar anasema uzoefu wake kama mtoto ulimpa ujasiri kwamba kamwe asingekua kama msichana.

Kurejea katika ukweli halisi wa jinsia yake

Akiwa na umri wa miaka 13, na baada ya kucheza judo kwenye jua kali la mchana, Nilofar alirudi nyumbani akiwa amechafuka: miguu yake iliumia na alitaka kulala chini. Alipoingia bafuni na kuona kwamba alikuwa anavuja damu, alikuwa na wasiwasi, lakini hakufikiria kwamba kile kinachokuja kitabadilisha maisha yake.

“Siku iliyofuata nilimwambia rafiki yangu. Alicheka na akaniuliza iwapo nilikuwa mjinga, kama dada zangu hawakuwa wameniambia chochote.”

“Nilipofika nyumbani, mama yangu aliona kitu kwenye nguo zangu na badala ya kunikumbatia na kunifariji, alikuwa akinilaani na kuniuliza ‘Kwa nini umekua haraka sana?’”

Mama yake Nilofar alianza kulia kwa sababu alijua kwamba siku za usoni alimsubiri binti yake kama yeye na binti zake wengine, waliofungwa ndani ya kuta nne za nyumba yake.

“Alikuwa amezoea wazo kwamba angeweza kuhisi kuwa nina uhakika kwamba niko salama na huu ndio wakati alipogundua kuwa yote yalikuwa bure.”

Nilofar alianza mchakato mwingine wa kiwewe, wakati huu, akichukua halisi ya utambulisho wa jinsia ambayo alikuwa amezaliwa: “Tulikuwa na hadithi hii kwamba ikiwa ungeenda chini ya upinde wa mvua, jinsia yako ingebadilika.”

Kufuatia kuanguka kwa Taliban mwaka 2001, wasichana waliweza kurudi madarasani nchini Afghanistan.

Miaka ya kuishi kama mwanamume iliashiria utambulisho wa jina Nilofar, na kumpa usalama ambao wasichana wengine shuleni mwake hawakuwa nao.

Afghanistan ilikuwa ikipitia kipindi kipya cha ukosefu wa utulivu wa kisiasa, kufuatia uingiliaji wa Marekani nchini humo baada ya Septemba 11, 2001.

Serikali mpya ilikuwa imewekwa na ilikuwa ikijitahidi kudumisha udhibiti, lakini baadhi ya haki, kama vile elimu, zilianza kuwafikia wanawake.

Nilofar aliweza kwenda shule, ingawa alibaki na roho hiyo ya uasi tangu utotoni wake.

“Niliunda kikundi hiki kinachoitwa ‘Niñas del Norte’. Na kupitia kundi hilo, tulianza harakati zetu za kuwaelimisha wasichana shuleni kuhusu mambo ambayo hawakufundishwa, kama kubalehe.”

“Kila kitu ni mwiko kwa msichana nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na hatua zinazosababisha kuwa mwanamke wakati mwili unapoanza kubadilika. Wasichana wana aibu sana kuhusu mabadiliko haya ya ukuaji wao.”

Licha ya ziara zake mbalimbali katika ofisi ya mkurugenzi, utendaji wa kitaaluma wa Nilofar ulikuwa wa kushangaza na hilo lilifungua milango kwa yake ya kuweza kusoma nje ya nchi, nchini India.

Ilikuwa wakati huu katika maisha yake, wakati alipokuwa akifanya kazi bila kuchoka kuelekea shahada ya uzamili, ndipo alipoanza alifikiria wazo la ndoa.

“Kwa kuwa nilikuwa mdogo nilipokea maombi mengi, ambayo baba yangu aliyajibu kila wakati ‘Usithubutu kumkaribia.’ Yeye si wa kuolewa kwa sasa, atamaliza masomo yake na kisha achague yeye mwenyewe bwana wa kuishi naye’’

Hilo ndilo lililokwama kwenye ubongo wangu, ‘Nitapata shahada ya uzamili na kisha, nitampata mume .’”

Nilofar alifunga ndoa mwaka 2016, alipofikisha umri wa miaka 19, labda, anasema, alikuwa akitaka kujaza pengo lililoachwa moyoni mwake na kifo cha baba yake, ambaye alikufa mnamo 2015.

“Wakati mume wangu aliposema alikuwa sawa na baba yangu wakati huo sikuiona, hakuna mtu angeweza kuwa kama baba yangu, lakini aliishia kuwa karibu kama yeye. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi ya baba yangu, lakini alijaza utupu huo na amenipa msaada mkubwa kama baba yangu alivyonipa. ”

Aliporudi Afghanstan kwa msaada wa mumewe, Nilofar aliuwa mjasiriamali, akibundi mitindo ya mavazi , kuuza samani na alimiliki kampuni ya kuuza mapambo ya ndani ambayo ililenga kutoa kazi kwa wanawake ambao hawakuwa na msaada wa kifedha. Alikuwa na wafanyakazi 300 na maduka kadhaa katika jiji.

Kutoroka

Kurejea kwa Taliban madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021 kulizua hofu na sintofahamu miongoni mwa watu wanaotaka kuondoka nchini humo.

Licha ya mafanikio ya kifedha ambayo familia ya Nilofar ilikuwa nayo nchini Afghanistan, hali ya kisiasa nchini humo ilianza kuonekana kuzorota kutokana na ukosefu wa usalama.

Na kisha, Agosti 2021 ilifika. Taliban walikuwa wakipata ardhi kwa miezi kadhaa, na mwezi Agosti, walifika Kabul, mji mkuu, tena.

“Mume wangu alipokea simu kutoka kwa waziri wa serikali ambaye alimwambia aandae kitambulisho na pasipoti haraka kwa ajili ya binti yangu,” anasema Nilofar. Mtoto wangu alikuwa na umri wa miezi 11 tu.

Simu pia zilianza kutoka dukani kwake, na wafanyakazi waliokata tamaa hawajui cha kufanya. Nilofar alimpigia simu mtoto wake na kumuomba afunge mizigo yake.

Aliporudi, aliwachukua watoto wake na mizigo yoyote aliyoweza na kuelekea nyumbani kwa mama yake. Lakini vurugu zilitawala katika mji huo.

“Wakati huu niliona mambo ambayo yatanisumbua maisha yangu yote: Nilimuona mtu aliyevalia sare ya polisi kwenye baiskeli akimwambia mwingine: ‘Chukua bunduki yangu, chukua baiskeli yangu, nipe nguo za kiraia.’ Alilia na kusema kwamba walikuwa wamesalitiwa.”

Kwa maelfu ya watu ambao walikuwa wameifanyia kazi serikali inayoungwa mkono na Marekani, kurejea kwa madarakani kwa Taliban -utawala ambao uliadhibu hata makosa madogo zaidi kwa njia za kikatili, kulimaanisha hukumu ya kifo.

Nilofar hakuweza kufika nyumbani kwa mama yake, na alilazimika kujificha na watoto wake katika eneo la karibu, kutoka mahali ambapo – kutokana na roho yake ya uasi – alihojiwa na waandishi wa habari kutoka duniani kote, ambapo aliwaelezea juu ya kile kilichokuwa kikimzunguka.

“Katika mahojiano na mwandishi wa habari kutoka Poland, aliniuliza ikiwa nilikuwa kwenye orodha yoyote ya kuhamishwa kutoka Afghanstan kwenda nchi ya kigeni nikamwambia hapana. Aliniomba kwa muda na alipopiga simu tena, aliniambia kwamba kulikuwa na ndege ya Poland ambayo, labda, inaweza kututoa nje ya nchi.

Maisha mapya

Nilofar na familia yake waliondoka Kabul na wanaamini hawataweza kurudi tena

Nilofar anasema kuwa mwandishi huyo alimwongeza kwenye kundi la WhatsApp na kumwambia kuwa wakati anapopokea simu hiyo, atakuwa na saa 24 za kwenda uwanja wa ndege akiwa na mifuko miwili tu.

“Mama yangu alikuwa huko, na kitabu kitakatifu mkononi mwake. Kuangalia uso wa mama yangu kulionyesha kwamba alijua kuwa hataniona tena. Na hiyo ilikuwa mara ya mwisho kumuona mama yangu, na nyumbani kwetu…”

PICHA: Leo Nilofar ni mwandishi wa habari na anazungumzia hali ya wanawake katika nchi yake ya asili ya Afghanistan.

Na anasema uzoefu wake, baada ya kuweza kuishi maisha ya mwanamume na mwanamke nchini Afghanistan, umekuwa “baraka na laana” kwa kila kitu ambacho kimetokea tangu wakati huo.

“Siwezi kuwa mwanamke wa 100%, wala 100% mwanaume. Lakini ilikuwa baraka kwa sababu niliweza kupata uzoefu wa pande zote mbili na hilo limenifanya kuwa mwanamke mwenye nguvu leo.”

Nguvu ambayo anahitaji kusonga mbele na ndoto yake kuu: “Sitaki kuwa mtu ambaye alizaliwa, aliishi miaka michache na kufa bila kuchangia chochote,” anasema, kufuatia ushauri wa baba yake, mtu huyo ambaye bado yuko naye moyoni mwake leo na hiyo inaelezea maisha yake milele.

“Naweza kuona uso wake. Siku zote aliniambia niache siasa, na kwenda kila mahali kutafuta kuleta mema.”

Baada ya safari ya “kutisha” ya siku tatu, familia iliwasili Poland kuanza maisha mapya. Ilikuwa ni nchi ambayo walikuwa wameisikia taarifa chache kuihusu.

“Ni vigumu sana kutokuwa na familia yoyote hapa. Hasa kwa mwanangu. Anakumbuka Kabul kwa kiasi kikubwa. Ananiuliza kuhusu bibi yake na kuuliza kwa nini hawezi kuwa hapa na sisi.”

Bila majibu ya kuridhisha, kitu pekee ambacho Nilofar anaweza kufanya ni kufanya kazi kwa ajili ya watu walioachwa nyuma, kwa mama yake, wafanyakazi wake na dada ambao hawakuweza kuondoka na ambao leo wanaishi tena chini ya Taliban.

Ametembelea Brussels, Ujerumani na Marekani, akizungumza katika mikutano ya haki za binadamu kuhusu haki za wanawake nchini mwake, na anaendelea kusaidia mashirika ambayo yanawasaidia wanawake wasiojiweza.

Source:Bbc

"Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: 'Mfanye
kama mvulana
0 Comment

"Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: 'Mfanye kama mvulanaAfyaclass Bongo Social •

Uso wa Nilofar Ayoubi, mwenye umri wa miaka 4 tu, bado ulikuwa mwekundu kutokana na kofi alilokuwa amepigwa na mgeni wakati akicheza katika mitaa ya Kunduz, kaskazini mwa Afghanistan. Pigo hilo lilikuwa la kikatili sana kiasi kwamba alianguka sakafuni.

“Nilirudi nyumbani nikilia baba yangu alikuwa mwekundu kwa hasira,” Nilofar ameiambia BBC, miaka ishirini na mitatu baada ya tukio hilo ambalo anasema limewekwa katika kumbukumbu zake. “Namkumbuka akirudi nyuma na kukasirika, akipiga kelele na kusema ‘anawezaje kukugusa?'”

Muda mfupi kabla ya kumpiga, mgeni huyo alikuwa amemgusa kifua chake, akitafuta ishara za “uke.” Kisha akamtishia na kumwambia kwamba ikiwa hatavaa kilemba chake, wakati mwingine, angemshambulia baba yake.

Baada ya muda mfupi wa hasira, baba yake Nilofar alifanya uamuzi mkali: “Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: ‘Mfanye kama mvulana.'”

Nilofar alikulia Afghanistan wakati wa enzi ya kwanza ya utawala wa Taliban – kuanzia mwaka 1996 hadi 2001 – na kwa karibu miaka 10, aliishi maisha ya mtoto, akitoroka udhibiti wa ukandamizaji ambao Sharia, sheria za Kiislamu, zinazokandamiza wanawake.

Leo, akiwa uhamishoni, anakumbuka jinsi mambo yalivyokuwa wakat iwa makuzi yake katika moja ya maeneo ya kihafidhina zaidi duniani, ambayo jinsia unayozaliwa nayo inafafanua mipaka ya haki unazoweza kupata.

Tofauti kati ya maisha ya mvulana na msichana nchini Afghanistan mara nyingi ni mbaya.

Kukulia katika Kunduz

Nilofar alizaliwa mwaka 1996, lakini nyaraka zake za utambulisho zinasema alizaliwa mwaka 1993. Baba yake alifanya mabadiliko hayo ili binti yake aweze kuanza shule haraka iwezekanavyo baada ya Marekani kuingilia kati mwaka 2001 kuipindua serikali ya Taliban.

” Kunduz sio mji wa kuvutia kwa mwanamke kukulia katika .”Ni vigumu kuwa mwanamume, na ni vigumu zaidi kuwa mwanamke,” aliiambia BBC.

“Kama mtoto, una nguvu moja kwa moja, hata kama wewe ni mtoto wa miaka 2 inamaanisha unapokea heshima zaidi kuliko mama yule yule aliyekuzaa. Kuanzia umri wa miaka 4, unaweza kuwa msimamizi wa kisheria wa mwanamke ambaye kuletwa wewe katika dunia (…) na yeye ni mtumwa wako. “Kama wewe ni mwanamke, wewe ni asiyeonekana.”

Chini ya sheria kali kama hizo kali , Nilofar anaeleza kuwa ilikuwa kawaida kwa familia yao kuwavalisha mabinti zao kama wavulana hasa kama familia haikuwa na mtoaji wa msingi: chini ya sharia, mwanamume yeyote anaweza kumkaribia mwanamke ambaye hana wa kumhudumia na kumlazimisha kuwa mke wake wa tano au wa sita.

“Kwa upande wangu, hali ilikuwa tofauti. Haikuwa kwa kukosa mtoa mtu wa kunisaidia lakini ilikuwa ni kuweza kuishi maisha kwa uhuru.”

Nilofar anakumbuka msaidizi wao , baba yake, alikuwa mtu maalum kwa wakati huo nchini Afghanistan: “Alichukia siasa.”

Utawala wa Taliban unaweka sheria kali ya Sharia, inayozuia haki nyingi za wanawake.

Akiwa amesimama mbele ya baba yake, huku nywele zake zikiwa zimenyolewa na kuvaa nguo za mmoja wa ndugu zake, Nilofar alikuwa karibu kuanza maisha tofauti kabisa na ya wasichana wengine wa umri wake, wakiwemo dada zake.

“Nilianza kuishi maisha kama ya kaka zangu, niliweza kwenda na baba yangu sokoni nikiwa nimevaa kama kijana. Tuliweza kutembea kwa maili na maili. Tulienda kwa basi kutazama michezo, nilikuwa na marafiki katika kitongoji na nilitumia muda wote kucheza mitaani.”

Dada zake, kwa upande mwingine, walilazimika kufunika nywele zao – hata ndani ya nyumba – na kuvaa kihafidhina, kitu ambacho baba yao alichukia.

“Baba yangu hakuwahi kukubaliana na suala la sisi kuvaa nguo hizo nyumbani, siku zote alipigana na mama yangu na kumuuliza kwa nini hakuvaa vizuri. ” Nguo hii ni ndefu sana, kwa nini ni pana sana? “Baba yangu alikuwa mtu wa aina yake .”

Kwa miaka mingi, baba yake Nilofar alipokea vitisho.

Kujenga uaminifu

Kukua katika ulimwengu wenye vitambulisho viwili, Nilofar daima alihisi utofauti. Labda yule ambaye angeweza kuelewa vizuri kile alichokuwa akipitia alikuwa jirani yake, msichana wa umri huo ambaye pia alivaa kama mvulana na ambaye alifanya maovu mengi.

“Tulikuwa tunafanya mambo sawa. Wakati wowote walipokuwa wakikaribia kumkamata mmoja, mwingine alikuja kumuokoa,” anasema Nilofar, akisisitiza kuwa hatari ya kutambuliwa kama wanawake ilikuwa ya mara kwa mara.

“Pia ilinisaidia sana kwamba nilikuwa na uhakika kuwa nilikuwa mvulana kwamba ilikuwa vigumu kwa watu kufikiri sikuwa nilivyo. Nakumbuka kwamba katika mikutano, mimi ndiye niliyesema”‘acha tuwasumbue wasichana’, nikiwaambia, ‘oh wewe ni mrembo, jinsi ulivyo mzuri tena mzuri sana.'”

Maisha ya Nilofar yalikuwa ya kucheza karate, judo na kuendesha baiskeli, wakati dada zake wakiishi na kucheza michezo ya kawaida ya wasichana Kunduz, kukaa nyumbani, kuishi maisha ya kimya kimya na nje ya macho ya wanaume.

“Sikuwahi kuwa na uhusiano na dada zangu. Sikuwahi kuelewa jinsi dunia yao ilivyokuwa. Na ndio maana sikujua kwamba wasichana walipata hedhi.”

Nilofar alikuwa ameona matangazo ya kuuza taulo za hedhi, lakini haikuwa wazi kwake kazi yake ilikuwa nini.

“Mara tu nilipopata taulo za hedhi nikaenda kwa baba yangu: ‘Baba, baba, angalia, ni kama wale kwenye TV, ni ya kuchekesha. Ni kwa ajili ya nini?’ “Baba yangu hakujua la kunijibu.”

“Baada ya hapo nilimpelekea kwa dada yangu. Nakumbuka alichukua kutoka kwangu na alinitukana. Hata wakati huo, hakuna mtu aliyefikiria kuniambia hedhi ni nini.”

Nilofar anasema uzoefu wake kama mtoto ulimpa ujasiri kwamba kamwe asingekua kama msichana.

Kurejea katika ukweli halisi wa jinsia yake

Akiwa na umri wa miaka 13, na baada ya kucheza judo kwenye jua kali la mchana, Nilofar alirudi nyumbani akiwa amechafuka: miguu yake iliumia na alitaka kulala chini. Alipoingia bafuni na kuona kwamba alikuwa anavuja damu, alikuwa na wasiwasi, lakini hakufikiria kwamba kile kinachokuja kitabadilisha maisha yake.

“Siku iliyofuata nilimwambia rafiki yangu. Alicheka na akaniuliza iwapo nilikuwa mjinga, kama dada zangu hawakuwa wameniambia chochote.”

“Nilipofika nyumbani, mama yangu aliona kitu kwenye nguo zangu na badala ya kunikumbatia na kunifariji, alikuwa akinilaani na kuniuliza ‘Kwa nini umekua haraka sana?'”

Mama yake Nilofar alianza kulia kwa sababu alijua kwamba siku za usoni alimsubiri binti yake kama yeye na binti zake wengine, waliofungwa ndani ya kuta nne za nyumba yake.

“Alikuwa amezoea wazo kwamba angeweza kuhisi kuwa nina uhakika kwamba niko salama na huu ndio wakati alipogundua kuwa yote yalikuwa bure.”

Nilofar alianza mchakato mwingine wa kiwewe, wakati huu, akichukua halisi ya utambulisho wa jinsia ambayo alikuwa amezaliwa: “Tulikuwa na hadithi hii kwamba ikiwa ungeenda chini ya upinde wa mvua, jinsia yako ingebadilika.”

Kufuatia kuanguka kwa Taliban mwaka 2001, wasichana waliweza kurudi madarasani nchini Afghanistan.

Miaka ya kuishi kama mwanamume iliashiria utambulisho wa jina Nilofar, na kumpa usalama ambao wasichana wengine shuleni mwake hawakuwa nao.

Afghanistan ilikuwa ikipitia kipindi kipya cha ukosefu wa utulivu wa kisiasa, kufuatia uingiliaji wa Marekani nchini humo baada ya Septemba 11, 2001.

Serikali mpya ilikuwa imewekwa na ilikuwa ikijitahidi kudumisha udhibiti, lakini baadhi ya haki, kama vile elimu, zilianza kuwafikia wanawake.

Nilofar aliweza kwenda shule, ingawa alibaki na roho hiyo ya uasi tangu utotoni wake.

“Niliunda kikundi hiki kinachoitwa ‘Niñas del Norte’. Na kupitia kundi hilo, tulianza harakati zetu za kuwaelimisha wasichana shuleni kuhusu mambo ambayo hawakufundishwa, kama kubalehe.”

“Kila kitu ni mwiko kwa msichana nchini Afghanistan, ikiwa ni pamoja na hatua zinazosababisha kuwa mwanamke wakati mwili unapoanza kubadilika. Wasichana wana aibu sana kuhusu mabadiliko haya ya ukuaji wao.”

Licha ya ziara zake mbalimbali katika ofisi ya mkurugenzi, utendaji wa kitaaluma wa Nilofar ulikuwa wa kushangaza na hilo lilifungua milango kwa yake ya kuweza kusoma nje ya nchi, nchini India.

Ilikuwa wakati huu katika maisha yake, wakati alipokuwa akifanya kazi bila kuchoka kuelekea shahada ya uzamili, ndipo alipoanza alifikiria wazo la ndoa.

“Kwa kuwa nilikuwa mdogo nilipokea maombi mengi, ambayo baba yangu aliyajibu kila wakati ‘Usithubutu kumkaribia.’ Yeye si wa kuolewa kwa sasa, atamaliza masomo yake na kisha achague yeye mwenyewe bwana wa kuishi naye’’

Hilo ndilo lililokwama kwenye ubongo wangu, ‘Nitapata shahada ya uzamili na kisha, nitampata mume .'”

Nilofar alifunga ndoa mwaka 2016, alipofikisha umri wa miaka 19, labda, anasema, alikuwa akitaka kujaza pengo lililoachwa moyoni mwake na kifo cha baba yake, ambaye alikufa mnamo 2015.

“Wakati mume wangu aliposema alikuwa sawa na baba yangu wakati huo sikuiona, hakuna mtu angeweza kuwa kama baba yangu, lakini aliishia kuwa karibu kama yeye. Kwa kweli, hakuna mtu anayeweza kuchukua nafasi ya baba yangu, lakini alijaza utupu huo na amenipa msaada mkubwa kama baba yangu alivyonipa. ”

Aliporudi Afghanstan kwa msaada wa mumewe, Nilofar aliuwa mjasiriamali, akibundi mitindo ya mavazi , kuuza samani na alimiliki kampuni ya kuuza mapambo ya ndani ambayo ililenga kutoa kazi kwa wanawake ambao hawakuwa na msaada wa kifedha. Alikuwa na wafanyakazi 300 na maduka kadhaa katika jiji.

Kutoroka

Kurejea kwa Taliban madarakani nchini Afghanistan mnamo Agosti 2021 kulizua hofu na sintofahamu miongoni mwa watu wanaotaka kuondoka nchini humo.

Licha ya mafanikio ya kifedha ambayo familia ya Nilofar ilikuwa nayo nchini Afghanistan, hali ya kisiasa nchini humo ilianza kuonekana kuzorota kutokana na ukosefu wa usalama.

Na kisha, Agosti 2021 ilifika. Taliban walikuwa wakipata ardhi kwa miezi kadhaa, na mwezi Agosti, walifika Kabul, mji mkuu, tena.

“Mume wangu alipokea simu kutoka kwa waziri wa serikali ambaye alimwambia aandae kitambulisho na pasipoti haraka kwa ajili ya binti yangu,” anasema Nilofar. Mtoto wangu alikuwa na umri wa miezi 11 tu.

Simu pia zilianza kutoka dukani kwake, na wafanyakazi waliokata tamaa hawajui cha kufanya. Nilofar alimpigia simu mtoto wake na kumuomba afunge mizigo yake.

Aliporudi, aliwachukua watoto wake na mizigo yoyote aliyoweza na kuelekea nyumbani kwa mama yake. Lakini vurugu zilitawala katika mji huo.

“Wakati huu niliona mambo ambayo yatanisumbua maisha yangu yote: Nilimuona mtu aliyevalia sare ya polisi kwenye baiskeli akimwambia mwingine: ‘Chukua bunduki yangu, chukua baiskeli yangu, nipe nguo za kiraia.’ Alilia na kusema kwamba walikuwa wamesalitiwa.”

Kwa maelfu ya watu ambao walikuwa wameifanyia kazi serikali inayoungwa mkono na Marekani, kurejea kwa madarakani kwa Taliban -utawala ambao uliadhibu hata makosa madogo zaidi kwa njia za kikatili, kulimaanisha hukumu ya kifo.

Nilofar hakuweza kufika nyumbani kwa mama yake, na alilazimika kujificha na watoto wake katika eneo la karibu, kutoka mahali ambapo – kutokana na roho yake ya uasi – alihojiwa na waandishi wa habari kutoka duniani kote, ambapo aliwaelezea juu ya kile kilichokuwa kikimzunguka.

“Katika mahojiano na mwandishi wa habari kutoka Poland, aliniuliza ikiwa nilikuwa kwenye orodha yoyote ya kuhamishwa kutoka Afghanstan kwenda nchi ya kigeni nikamwambia hapana. Aliniomba kwa muda na alipopiga simu tena, aliniambia kwamba kulikuwa na ndege ya Poland ambayo, labda, inaweza kututoa nje ya nchi.

Maisha mapya

Nilofar na familia yake waliondoka Kabul na wanaamini hawataweza kurudi tena

Nilofar anasema kuwa mwandishi huyo alimwongeza kwenye kundi la WhatsApp na kumwambia kuwa wakati anapopokea simu hiyo, atakuwa na saa 24 za kwenda uwanja wa ndege akiwa na mifuko miwili tu.

“Mama yangu alikuwa huko, na kitabu kitakatifu mkononi mwake. Kuangalia uso wa mama yangu kulionyesha kwamba alijua kuwa hataniona tena. Na hiyo ilikuwa mara ya mwisho kumuona mama yangu, na nyumbani kwetu…”

PICHA: Leo Nilofar ni mwandishi wa habari na anazungumzia hali ya wanawake katika nchi yake ya asili ya Afghanistan.

Na anasema uzoefu wake, baada ya kuweza kuishi maisha ya mwanamume na mwanamke nchini Afghanistan, umekuwa “baraka na laana” kwa kila kitu ambacho kimetokea tangu wakati huo.

“Siwezi kuwa mwanamke wa 100%, wala 100% mwanaume. Lakini ilikuwa baraka kwa sababu niliweza kupata uzoefu wa pande zote mbili na hilo limenifanya kuwa mwanamke mwenye nguvu leo.”

Nguvu ambayo anahitaji kusonga mbele na ndoto yake kuu: “Sitaki kuwa mtu ambaye alizaliwa, aliishi miaka michache na kufa bila kuchangia chochote,” anasema, kufuatia ushauri wa baba yake, mtu huyo ambaye bado yuko naye moyoni mwake leo na hiyo inaelezea maisha yake milele.

“Naweza kuona uso wake. Siku zote aliniambia niache siasa, na kwenda kila mahali kutafuta kuleta mema.”

Baada ya safari ya “kutisha” ya siku tatu, familia iliwasili Poland kuanza maisha mapya. Ilikuwa ni nchi ambayo walikuwa wameisikia taarifa chache kuihusu.

“Ni vigumu sana kutokuwa na familia yoyote hapa. Hasa kwa mwanangu. Anakumbuka Kabul kwa kiasi kikubwa. Ananiuliza kuhusu bibi yake na kuuliza kwa nini hawezi kuwa hapa na sisi.”

Bila majibu ya kuridhisha, kitu pekee ambacho Nilofar anaweza kufanya ni kufanya kazi kwa ajili ya watu walioachwa nyuma, kwa mama yake, wafanyakazi wake na dada ambao hawakuweza kuondoka na ambao leo wanaishi tena chini ya Taliban.

Ametembelea Brussels, Ujerumani na Marekani, akizungumza katika mikutano ya haki za binadamu kuhusu haki za wanawake nchini mwake, na anaendelea kusaidia mashirika ambayo yanawasaidia wanawake wasiojiweza.

Source:Bbc

"Alimuomba mama yangu mkasi, akakata nywele zangu na kumwambia: 'Mfanye
kama mvulana
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD