Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António GuterresAfyaclass Bongo Social •

Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António Guterres

Wakiwa wamevalia mavazi ya kujikinga, daktari mwanamke anayeongoza kundi la wataalamu wa afya wanaojitolea kuhudumia wagonjwa wa COVID-19 na wanaochunguzwa katika hospitali ya jamii Ufilipino.

Janga la ugonjwa lijalo litakapotokea ni lazima tuchukue hatua kwa ufanisi zaidi kwa kuandaa na kujumuisha mafunzo tuliyojifunza kutokana na janga la COVID-19, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya kimataifa ya kukabili milipuko ya magonjwa ambayo huadhimishwa kila Novemba 27 kama leo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anabainisha kuwa janga la COVID-19 sio tena dharura ya kiafya ya kimataifa, lakini ugonjwa huo bado unazunguka, na athari zake mbaya bado zinaendelea kuhisiwa.

Kwa mujibu wake Bwana Guterres, uharibifu wa kiuchumi unaosababishwa na janga hilo bado haujaondolewa, na mifumo ya afya ya nchi nyingi inakabiliwa na shida kubwa. Zaidi ya hayo, mamilioni ya watoto wako katika hatari ya kuwa wagonjwa kwa kukosa chanjo za kawaida za utotoni. Miaka mitatu baada ya chanjo ya kwanza ya COVID-19 kutengenezwa, mabilioni ya watu bado hawajalindwa – idadi kubwa katika nchi zinazoendelea.

Kuimarisha mifumo

“Kwa kufanya kazi pamoja, dunia lazima iboreshe uchunguzi wa virusi, kuimarisha mifumo ya afya na kutimiza ahadi ya chanjo ya afya kwa wote,” Guterres anahimiza. “Lazima tuondoe uwezekano wa maafa ya kimaadili na kiafya wakati nchi tajiri zinaweka akiba na kudhibiti vifaa tiba ili kupambana na milipuko ya magonjwa, na kuhakikisha kila mtu anapata uchunguzi, matibabu na chanjo.” Katika muktadha huu, kiongozi huyu wa Umoja wa Mataifa anatoa wito wa kuimarishwa kwa mamlaka na kuongeza ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani.

Guterres ana imani kuwa juhudi hizi zinazaa matunda. Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Kuzuia Majanga ya Magonjwa, Maandalizi na Hatua mnamo Septemba mwaka huu ulitoa tamko la kisiasa la dhati. Hii inakamilisha mazungumzo ya mkataba wa majanga ya magonjwa huko Geneva.

Usawa

Katibu Mkuu Guterres anapendekeza kuwa nchi zijitahidi kuendeleza makubaliano ya kina yenye kulenga usawa na Baraza la Afya la Ulimwengu, ambalo litafanyika Mei mwaka ujao 2024.

“Sote tuzingatie masomo ya janga la COVID-19, tujitayarishe na kujenga ulimwengu mzuri na wenye afya kwa wote,” Guterres amehitimisha ujumbe wake.

Tunahitaji kujiandaa dhidi ya janga jingine la ugonjwa: António Guterres
0 Comment

Kijana wa umri wa miaka 20, akutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye matairi ya ndegeAfyaclass Bongo Social •

Kijana wa umri wa miaka 20, akutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye matairi ya ndege.

Kijana wa umri wa miaka 20, amekutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye sehemu ya matairi ya ndege iliyosafiri kutoka Algeria hadi Ufaransa,

Kijana huyo aligunduliwa na wakaguzi wa ndege akiwa katika hali mbaya kiafya na baadaye aliwahishwa hospitalini.

Kwa mujibu wa takwimu za mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Marekani (FAA), watu 132 walijaribu kusafiri kwa kutumia mfumo huo hatari kati ya mwaka 1947 na 2001.

Je, ni sahihi kufanya jaribio hilo kwa lego la kuyasaka maisha?

Kijana wa umri wa miaka 20, akutwa akiwa hai baada ya kujificha kwenye
matairi ya ndege
0 Comment

Dawa ya gono kwa mwanaumeAfyaclass Bongo Social •

Dawa ya gono kwa mwanaume

Ugonjwa wa gonorrhea maarufu kama GONO au Kisonono ni ugonjwa wa zinaa ambao husababishwa na Bacteria ambaye kwa kitaalam hujulikana kama Neisseria gonorrhoeae na kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana.

DALILI ZA UGONJWA WA GONO(KISONONO) NI PAMOJA NA;

Kumbuka; Ugonjwa huu wa kisonono kwa asilimia kubwa ni vigumu mwanamke kuonyesha dalili za moja kwa moja hata kama ameambukizwa. Lakini kama akionyesha dalili basi baadhi ya dalili kama hizi hapa chini huweza kutokea.

MIONGONI MWA DALILI AMBAZO HUWEZA KUJIONYESHA KWA MWANAMKE NI PAMOJA NA;

  1. Mwanamke kupatwa na tatizo la maumivu makali wakati wa kufanya mapenzi
  2. Mwanamke kutokwa na maji maji ukeni ambayo yana harufu sana
  3.  Mwanamke kutokwa na ute ute ambayo umechanganyika na usaha ukeni
  4. Kutokwa na damu baada ya kufanya tendo la ndoa
  5. Kupatwa na shida ya blid mara mbili ndani ya mwezi mmoja
  6. Kupatwa na maumivu makali ya tumbo
  7. Joto la mwili kupanda au kuwa na homa
  8. Kuvimba kwenye eneo la mashavu ya uke

DALILI ZA UGONJWA WA KISONONO KWA MWANAUME NI PAMOJA NA;

– Kutokwa na usaha sehemu za Siri

– Kuwashwa kwenye kitundu ambacho mkojo hupita

– Kupatwa na hali ya kuchomwa wakati wa kukojoa ambayo tunasema kwa kitaalam burning sensation

– Mwanaume kupatwa na tatizo la kushindwa kukojoa kabsa au mkojo kugoma kutoka, kitu ambacho huweza kumsababishia maumivu makali pamoja na mahangaiko

– Kukojoa mkojo ambao umechanganyika na Damu

– Joto la mwili kupanda au kuwa na homa

MATIBABU YA UGONJWA WA KISONONO

Ni vizuri kwenda hospital kufanyiwa vipimo kwanza kabla ya dawa, Na baada ya hapo kama utagundulika una tatizo hili basi utapata matibabu sahihi kulingana na ugonjwa wako pamoja na hatua ulipofikia.

TIBA YA KISONONO(Ugonjwa wa zinaa)

Kwa asilimia kubwa Mgonjwa wa kisonono hupewa Dawa ya Cefriaxone 500mg Single dose ambapo ni sindano anachomwa matakoni au sehemu yoyote yenye msuli Kwa kitaalam tunaita Intramuscular Injection(IM).

Epuka matumizi ya dawa hovio pasipo maelekezo na vipimo kutoka kwa wataalam wa afya. Kwani ni hatari kwa afya yako,badala ya kukutibu inaweza kuwa sumu ya kukuua.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dawa ya gono kwa mwanaume
0 Comment

Nateseka sana lakini kubwa naona aibu mno kuomba msaada kila mara- Carina Msanii BongoMoviesAfyaclass Bongo Social •

Nateseka sana lakini kubwa naona aibu mno kuomba msaada kila mara- Carina Msanii BongoMovies.

Global Tv imefanya mahojiano kwa mara nyingine na Msanii wa Bongo muvi Carina Hussein nyumbani kwao Magomeni jijini Dar es Salaam na kuona kuwa hali ya afya yake inazidi kuwa mbaya.

“Nateseka sana lakini kubwa naona aibu mno kuomba msaada kila mara,ila sina jinsi maana mfuko mmoja wa PTN,unauzwa shilingi 250,000 kwangu mimi ni fedha nyingi maana hatuna tena hata kitu cha kuuza ili fedha zinisaidie” alisema Carina.

Kama unataka kumsaidia Carina, chochote hata nusu ya hela ya kununua mfuko huo wa PTN, waweza kumsaidia kupitia namba;

0769_990045 M-PESA
Carolinhawa Hussein Ebrahim bounin.

0789_095858 Airtel money
FATUMA MIKIDADI maruzuku..

0712_595858 tigopesa
Carolinhawa Hussein Ebrahim bounin

Habari @imeldamtema

Via: Global Tv

Nateseka sana lakini kubwa naona aibu mno kuomba msaada kila mara-
Carina Msanii BongoMovies
0 Comment

je ni sahihi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?, hili ndyo swali lililoulizwa zaidi kwenye mtandao wa Google mwaka 2023Afyaclass Bongo Social •

je ni sahihi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?, hili ndyo swali lililoulizwa zaidi kwenye mtandao wa Google mwaka 2023.

Google imetoa orodha ya Maswali yaliyoulizwa Zaidi mwaka 2023, na kwa Upande wa Maswali yanayohusu kufanya mapenzi(Sex),miongoni mwa Maswali yaliyoulizwa zaidi ni pamoja na hili;

“je ni sahihi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?”

Is it ok to have s3x during pregnancy? – Google releases its top sex questions of 2023

Google has released its “Year in Search,” a roundup of 2023’s top global queries.

Search engine hii ya Google imetoa Maswali yaliyoulizwa zaidi na Watu kwenye kipengele kinachohusu mapenzi(Sex) mwaka 2023, na matokeo ni kama ifuatavyo;

1. Swali lililoulizwa zaidi na kushika namba moja ni “What is the speed bump position?”
(The most googled sex question of 2023 was: “What is the speed bump position?”.)

Historia yake: Neno hili lilijulikana sana baada ya mshindani kwenye “Kisiwa cha Upendo yaani Love Island” kulileta kwenye Series.

“speed bump positon” -Huhusisha mkao wa kuweka mto chini ya makalio ya mtu anapolala kifudifudi wakati wa tendo la ndoa

2. Swali la Pili kwa kuulizwa sana Google lilikuwa hili;

“je ni sahihi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?”

(The second-most googled question was from people desperate to know whether it was okay to have sex during pregnancy).

Kwa Mujibu wa “Australian parenting website Raising Children” walisema;

Kama huna tatizo lolote kipindi cha Ujauzito, Ni salama kabsa kwako kufanya mapenzi na kufika kileleni.

Nanukuu;

“If your pregnancy is going smoothly, it’s safe to have sex and orgasm while you’re pregnant,” states the Australian parenting website Raising Children.

Unaweza kuwa na Wasiwasi kwamba kufanya mapenzi ukiwa mjamzito unaweza kumdhuru mtoto, Lahasha! Ukweli ni kwamba;

Mtoto wako hulindwa zaidi na kufunikwa kabsa ndani ya amniotic sac kwenye tumbo la Uzazi, Hivo huwezi kumdhuru mtoto kwa kufanya mapenzi ukiwa mjamzito.

(“You might worry that sex will harm the baby. But your baby is well protected and sealed off in the amniotic sac, so you can’t hurt your baby by having sex.”)

3. Swali lililoshika namba tatu ni watu kutafuta maana ya “Sex Positivity”

(Searches for the meaning of “sex positivity” came in third).

4. Swali lililoshika namba nne linahusu watu kuuliza;

Kwanini wanavuja damu au kutokwa na damu baada ya kufanya Mapenzi

(People asking why they might be bleeding after sex was the fourth-most asked question).

5. Na Swali lililoshika namba tano linahusu watu kuuliza;

Wengine walitaka kujua ni tarehe ngapi wanapaswa kuchumbiana kabla ya kufanya mapenzi na mtu,

(Others wanted to know how many dates they should go on before having sex with someone).

NB: Na Swali lililoshika namba 10, kwenye Orodha ya Maswali kumi yaliyoulizwa Zaidi Google Mwaka 2023 kwenye kipengele cha Mapenzi(Sex) ni;

Je,ni Jinsi gani samaki hufanya mapenzi?

(How do fishes have sex comes in 10th).

je ni sahihi kufanya mapenzi wakati wa ujauzito?, hili ndyo swali
lililoulizwa zaidi kwenye mtandao wa Google mwaka 2023
0 Comment

Sababu za mtoto kuchelewa kuota menoAfyaclass Bongo Social •

Sababu za mtoto kuchelewa kuota meno

Watoto wanapozaliwa, tayari wanakuwa na meno ambayo  yamefunikiwa kwa fizi. Meno huanza kutoka kwa mara ya kwanza mtoto akiwa na umri wa miezi sita ( 6) japo umri huu unaweza tofautiana kutoka kwa mtoto mmoja hadi mwingine.

Meno mawili ya kwanza yanayoonekana mara nyingi ni yale ya kinywa cha chini katikati yakifuatiwa na ya kinywa cha  juu katikati. Watoto wengi hufikisha meno yote 20 ya kwanza wakiwa na umri wa miaka 3.

Baadhi ya watoto hawaoti meno kama watoto wengine, yao huchelewa au kutokuota kabisa. Hii husababishwa na vitu mbalimbali. Kama mtoto wako hajaota jino hata moja hadi umri wa miezi 18 basi ni muhimu umpeleke hospitali aonane na daktari wa kinywa na meno kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Sababu za meno kuchelewa kuota

Zipo sababu nyingi za meno kuchelewa kuota. Wakati mwingine tatizo la meno kuchelewa kuota huwa ni tatizo la kwenye familia  hivyo linaweza kurithishwa kwa vizazi vinavyokuja. Mzazi pia ujiulize kama meno yako yalichelewa kuota, kama ni ndio basi tambua kwamba hata ya mwanao yataota tu japo kwa kuchelewa.

Sababu zinazochangia meno kuchelewa kuota kwa mtoto ni kama zifuatazo;

– Utapia mlo na upungufu wa madini na vitamini mwilini,

Watoto wenye utapia mlo meno huchelewa kuota kwa sababu ya kukosa virutubisho muhimu vya ukuaji wa meno. Aidha madini ya calcium na vitamini  D ni muhimu sana katika ukuaji wa meno. Hivyo mtoto akipungukiwa na virutubisho hivi meno huchelewa kuota.

– Ugonjwa wa jeni unaofahamika kama Down Syndrome,

Huu ni miongoni mwa mgonjwa wa kuzaliwa nayo (congenital).Ugonjwa huu unatokana na hitilafu kwenye kinasaba cha 21 (chromosome 21). Ugonjwa huu huambatana na tatizo la meno kuchelewa kuota.

– Magojwa yatokanayo na hitalifu kwenye chromosomes (chromosome anomalies)

– Mtoto kuzaliwa njiti-Kuzaliwa njiti au na kuzaliwa  na uzito mdogo kupita kawaida (chini ya 1.5kg) kunahusishwa na kuchelewa kuota kwa meno kwa mtoto. Watoto hawa wanaweza kuwa na matatizo ya meno yenyewe.

– Magonjwa kama Amelogenesis na Regional Odontodysplasia

Amelogenesis ni ugonjwa wa kuzaliwa nao (congenital disease) ambapo mtoto anazaliwa na hitilafu kwenye kwenye protini zinazotengeneza enameli (nyeupe ngumu ya jino) hii hupelekea kuwa  na enameli isiyo ya kawaida na meno yanakuwa ya njano. Hii huambatana na meno kuchelewa kuota.

Regional odondodysplasia ni hitilafu katika ukuaji inayohusisha mesodermal na ectoderm (hizi ndizo zinazotengeneza jino la ndani na nje) za meno. Ugonjwa huu huwa unaathiri sehemu moja tu ya kinywa (localized). Huu sio ugonjwa wa kurithi.

Kwanini uwe na wasiwasi kuhusu meno ya mtoto yanapochelewa kuota?

Watoto ambao hawajaota meno hadi umri wa miezi 18 wapelekwe kumuona daktari wa meno. Watoto wengi huwa na meno manne wakifikia umri wa miezi 12 na huwa na yote 20 wakiwa na miezi 27.

Kama meno ya mtoto wako hayajaota kwa wakati inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa  au upungufu wa madini  au vitamini fulani mwilini.

Je, meno kuchelewa kutoa ni dalili mbaya?

Meno kuchelewa kuota sio jambo kubwa sana ila linaweza kuongeza uwezekano wa mtoto kupata matatizo ya meno ukubwani. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watoto waliopata tatizo la meno kuchelewa kuota wana nafasi kubwa ya kuhitaji matibabu ya meno wakiwa na umri wa miaka 30.

Meno kuota kwa wakati kwa mtoto humsaidia kutafuna vizuri na husaidia meno ya pili kujipanga vizuri kwenye kinywa.

Meno yakichelewa kuota husababisha mtoto kukosa au kupata virutubisho vichache maana atakuwa hawezi kutafuna vizuri hivyo kupata shida ya kumeng’enya chakula.

Jinsi ya kutunza meno mapya ya mtoto wako

✓ Epuka vyakula na vinywaji vyenye sukari

✓ Safisha fizi kwa kutumia kutambaa kisafi mara mbili kwa siku

✓ Epuka kumlaza mtoto na chupa ya maziwa kitandani

✓ Kumbuka kuswaki na kusafisha meno yaliyoota

✓ Utaanza kutumia dawa ya meno pindi mtoto akifikisha miaka 2.

By Dr Hamphrey

Sababu za mtoto kuchelewa kuota meno
0 Comment

Bwana na Bibi Wafariki kwa kupishana saa 23 tuAfyaclass Bongo Social •

Bwana na Bibi Wafariki kwa kupishana saa 23 tu.

Mamia ya Wananchi mjini Njombe wamejitokeza kwenye maziko ya pamoja ya Wanandoa waliofariki kwa kupishana saa 23 katika Mtaa wa Mjimwema,

kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo shinikizo la damu (BP) lililomkuta Elizabeth Sawala (63) baada ya kifo cha Mume wake Inyasi Hongoli (71) kilichotokea asubuhi ya December 25, 2023 siku ya Christmas wakati akipelekwa Hospitali baada ya kudondoka nyumbani kwake.

Lenard Hongoli ni Mtoto wa tatu katika Familia hiyo ambapo ameiambia @AyoTV_ kuwa amekuwa akiwauguza Wazazi wake kwa miezi miwili lakini siku ya Christmas alipokuwa Kanisani ndipo alipopata simu ya jirani aliyemueleza kuwa Baba yake ana hali mbaya na akawahi nyumbani ili kumpeleka Hospitali ambapo wakiwa njiani kwenda Hospitali alifia miguu mwake.

“Tuliporudi nyumbani kwa ajili ya maombolezo Mama akapata presha ikabidi tumkimbize Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Njombe na akalazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi na aliporudishwa kwenye wodi ya wagonjwa wa kawaida tulienda kumuangalia tukaona anacheka akasema Watoto wangu wote njooni hapa akatuchapa makofi matatu kila mmoja kumbe ndio anatuaga maana baada ya muda Madaktari wakasema hali yake sio nzuri akimbizwe Hospitali ya Rufaa Mbeya lakini muda wa saa mbili alifia njiani maeneo ya Igulusi”

Mbunge wa Jimbo la Njombe mjini Deo Mwanyika ametoa wito kwa Wananchi kuwa na imani pamoja na uvumilivu kutokana na tukio hilo ambalo limeumiza Watu wengi kutokana na namna lilivyotokea huku Daktari wa tiba zitokanazo na mimea Titas Mabula akishauri kwa watu wanaojua wana presha kuhakikisha wanafuata njia za kitaalamu ikiwemo kupata muda mzuri wa kupumzika na kunywa maji ya vuguvugu angalau glass moja mara baada ya kupokea taarifa ya mshtuko.

Bwana na Bibi Wafariki kwa kupishana saa 23 tu
0 Comment

Mapigano kati ya kundi la M23 na Wazalendo yazua hofu KongoAfyaclass Bongo Social •

Mapigano kati ya kundi la M23 na Wazalendo yazua hofu Kongo.

Hali ya wasiwasi imetanda katika mji wa Sake mkoani Kivu Kaskazini kufuatia mapigano yanayoendelea kati ya waasi wa M23 na wapiganaji vijana wazalendo kwenye milima ya Mitumbala.

Wakaazi wa mji wa Kibumba wakielezea pia kusikia milio ya risasi kwenye mji huo ambako makundi ya vijana wazalendo walikuwa wakirusha mabomu kuelekeangome za M23.

Ni wakati vikosi vya jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC vikiwasili Goma kupambana dhidi ya M23.

Waasi wa M23 wamezidisha mashambulizi yao dhidi ya vijiji vya walayani Masisi ambako hofu imetanda kwenye meneo yanayolengwa kwa makombora toka kundi hilo.

Kulingana na vyanzo vya kiraia, M23 imekita ngome yake sasa kwenye milima ya kijiji cha Mitumbala nje kidogo na mji wa sake ambako mapigano makali yaliendelea hadi jana Jumatano baina yao na makundi ya wapiganaji wanaojiita wazalendo wanaoungwa mkono na jeshi la kongo.

Waasi wa M23 wanaodaiwa kupata msaada kutoka kwa Rwanda, ambayo inakanusha hilo wameelezwa pia kufika katika milima ya Kagano na Rucika inayokaribia mji wa Bweremana ambao ni muhimu kwa usambazaji wa chakula kwenda mjini Goma.

Wakaazi wa Sake wamethibitisha kutekwa kwa milima ya Mitumbala ambako milio ya risasi ilirindima kwa siku tatu mfululizo wakati vijana wazalendo walipojaribu kuwafurusha M23 bila mafanikio.

Wakati huo huo, jeshi la Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo limetumia hii leo ndege kivita kushambulia ngome za M23 kwenye milima ya karuba ambako mapigano yameendelea hadi mchana wa leo nakuongeza hofu kubwa kwa raia wanaokimbia kuelekea mji wa Madini wa Rubaya wilayani humo.

Pia Ripoti zinasema kuwa, vijana wazalendo wenye silaha walikabiliana jana usiku na M23 nje kidogo na mji wa kibumba kilometa 20 kaskazini mashariki mwa mji wa Goma ambako hali ilikuwa ni ya wasiwasi mchana kutwa wa leo alhamisi.

Hapo jana Jumatano askari wa Afrika Kusini kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC waliwasili Goma wakiwa na agizo la kupambana moja kwa moja na waasi wa M23, tofauti na jeshi la kanda ya Afrika Mashariki ambalo wanajeshi wake wa mwisho waliondoka mapema mwanzoni mwa juma hili.

Kuwasili kwa wanajeshi hao wa Afrika Kusini kumethibitishwa na shirika la habari la Kongo, ASP.

Via: Dw

Mapigano kati ya kundi la M23 na Wazalendo yazua hofu Kongo
0 Comment

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000Afyaclass Bongo Social •

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000

(??????? ?????? ???????? ?? ?????????? ???,??? ???????? ????)

Kaunti ya Nyamira inajitayarisha kuimarisha afya ya watu wake kwa kusambaza vyandarua takribani 449,000,

Zoezi hilo likiongozwa na Katibu Mkuu Mary Muthoni, usajili wa kaya, unaowezeshwa kidijitali kwa uwazi, unaashiria hatua kubwa katika juhudi hizi muhimu.

PS Muthoni aliangazia jukumu kuu la jamii katika kutumia vyandarua hivi dhidi ya malaria, akisisitiza umuhimu wao katika vita vinavyoendelea dhidi ya ugonjwa huo.

Dk. Geoffrey Nyambuti, Mkurugenzi wa Afya wa Nyamira, alitoa shukrani kwa msaada wa Serikali ya Kitaifa, haswa katika kutoa vifurushi vya kina vya afya kwa Wahamasishaji wa Afya ya Jamii, vinavyotarajiwa kuimarisha huduma za afya ya msingi katika mkoa huo.

Kama mojawapo ya kaunti 22 zilizo katika hatari kubwa, kujumuishwa kwa Kaunti ya Nyamira katika zoezi la usambazaji wa vyandarua kwa wingi, lililozinduliwa mwezi wa Novemba, kunawiana na miongozo ya WHO ya kuzuia malaria, ikionyesha juhudi shirikishi muhimu kwa afua madhubuti za afya ya umma.

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000
0 Comment

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000Afyaclass Bongo Social •

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000

(𝐍𝐲𝐚𝐦𝐢𝐫𝐚 𝐂𝐨𝐮𝐧𝐭𝐲 𝐏𝐫𝐞𝐩𝐚𝐫𝐞𝐬 𝐭𝐨 𝐃𝐢𝐬𝐭𝐫𝐢𝐛𝐮𝐭𝐞 𝟒𝟒𝟗,𝟎𝟎𝟎 𝐌𝐨𝐬𝐪𝐮𝐢𝐭𝐨 𝐍𝐞𝐭𝐬)

Kaunti ya Nyamira inajitayarisha kuimarisha afya ya watu wake kwa kusambaza vyandarua takribani 449,000,

Zoezi hilo likiongozwa na Katibu Mkuu Mary Muthoni, usajili wa kaya, unaowezeshwa kidijitali kwa uwazi, unaashiria hatua kubwa katika juhudi hizi muhimu.

PS Muthoni aliangazia jukumu kuu la jamii katika kutumia vyandarua hivi dhidi ya malaria, akisisitiza umuhimu wao katika vita vinavyoendelea dhidi ya ugonjwa huo.

Dk. Geoffrey Nyambuti, Mkurugenzi wa Afya wa Nyamira, alitoa shukrani kwa msaada wa Serikali ya Kitaifa, haswa katika kutoa vifurushi vya kina vya afya kwa Wahamasishaji wa Afya ya Jamii, vinavyotarajiwa kuimarisha huduma za afya ya msingi katika mkoa huo.

Kama mojawapo ya kaunti 22 zilizo katika hatari kubwa, kujumuishwa kwa Kaunti ya Nyamira katika zoezi la usambazaji wa vyandarua kwa wingi, lililozinduliwa mwezi wa Novemba, kunawiana na miongozo ya WHO ya kuzuia malaria, ikionyesha juhudi shirikishi muhimu kwa afua madhubuti za afya ya umma.

Kenya; Kaunti ya Nyamira inajiandaa kusambaza Neti za mbu 449,000
0 Comment

Naona aibu inabidi ninyoe nywele zangu za usoni'Afyaclass Bongo Social •

Naona aibu inabidi ninyoe nywele zangu za usoni’

Glory Chinemerem Ibe ambaye amekuwa akiota nywele za uso kama ilivyo kwa wanaume.

Anaelezea jinsi alivyokabiliana na nywele hizo tangu akiwa na umri wa miaka 14 alipoanza kupata hali hiyo.

Anasema amejaribu mbinu kadhaa ya kuzitoa na hata bidhaa mbalimbali katika jitihada zake za kuondoa nywele hizo za uso lakini bila mafanikio.

Bi Glory anasema alikuwa akiona aibu hivyo ilimbidi kuzinyoa mara kwa mara lakini sasa hana wasiwasi wowote kwani ameamua kujiamini na kujipenda jinsi alivyo.

Tazama Video hii hapa;

Naona aibu inabidi ninyoe nywele zangu za usoni'
0 Comment

Watu wenye tatizo la hypochondriamu kuwa kwenye hatari ya kufa mapema ZaidiAfyaclass Bongo Social •

Watu wenye tatizo la hypochondriamu kuwa kwenye hatari ya kufa mapema Zaidi.

Utafiti mpya wa watu ambao waligunduliwa na tatizo la  hypochondriamu(hypochondria) uligundua kuwa walikuwa na hatari ya asilimia 84% ya kuongezeka kwa vifo vya mapema na waliishi chini ya miaka 5 kuliko watu wasio na ugonjwa huo(karibu miaka 5 ya kuishi kupunguzwa).

“A new study of people who were diagnosed with hypochondria found that they had an 84% increased risk of early death and lived about 5 fewer years than people without the disorder”.

Tatizo la hypochondria kwa jina lingine hujulikana kama “illness anxiety disorder”,

Wataalam wa afya walitazama tatizo hili kama tatizo la afya ya akili yaani psychiatric condition.

Moja ya Dalili zake kubwa ni Mtu kuwa na wasiwasi kupita kiasi hadi kufikia hatua ya kuugua,

Dalili kuu ni wasiwasi mwingi juu ya kuwa mgonjwa sana. Dalili zingine ni pamoja na kuwa na wasiwasi kwamba hisia za kawaida za mwili – kama vile tumbo kunguruma au kuwa na kelele au muwasho mdogo wa ngozi – ni ishara za ugonjwa mbaya.

Kwa Utafiti huu, Watafiti walichambua takwimu za watu Zaidi ya 4,000 wanaoishi nchini Sweden ambao tayari waligundulika kuwa na ugonjwa huu”illness anxiety disorder” kati ya Mwaka 1997 na 2020.

Watafiti walilinganisha watu wenye Ugonjwa huu na wale wasio na ugonjwa huu lakini wenye taarifa za kufanana kama vile; Umri pamoja na Jinsia, Na pia wanaoishi kwenye nchi hiyo hiyo Moja.

Matokeo ya Utafiti yamechapishwa mwezi huu kwenye Jarida la “JAMA Psychiatry” na yameonyesha kuwa;

Watu wenye tatizo la hypochondria wana uwezekano mkubwa wa kufa mapema kwa Sababu zinazofahamika na zisizofahamika(natural or unnatural causes).

Watu wenye tatizo la hypochondriamu kuwa kwenye hatari ya kufa mapema
Zaidi
0 Comment

kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine zakamatwaAfyaclass Bongo Social •

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya Tanzania (DCEA) imekamata jumla ya kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine katika operesheni maalum iliyofanyika jijini Dar es Salaam na Iringa kati ya tarehe 5 hadi 23 mwezi Disemba, 2023. Watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili kati yao wana asili ya Asia.

Kiasi hiki cha dawa za kulevya kinajumuisha kilogramu 2,180.29 za dawa aina ya methamphetamine na kilogramu 1001.71 aina ya heroin zilizokamatwa katika wilaya za Kigamboni, Ubungo na Kinondoni jijini Dar es Salaam pamoja na wilaya ya Iringa mkoani Iringa.

Ukamataji huu umehusisha kiasi kikubwa cha dawa za kulevya ambacho hakijawahi kukamatwa katika historia ya Tanzania tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa za kulevya. Hivyo, watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani.

Aidha, dawa hizi zilizozikamata zilikuwa zimefungashwa kwenye vifungashio vya bidhaa zenye chapa mbalimbali za kahawa na majani ya chai. Mbinu hii inatumika kwa lengo la kurahisisha usafirishaji wake na kukwepa kubainika.

Ukiacha dawa ya heroin inayotengenezwa kwa mchanganyiko wa kemikali kutoka kwenye mimea ya afyuni (opium popy) inayolimwa katika nchi za Asia na baadhi ya kutoka Amerika, dawa aina ya methamphetamine ni dawa mpya ya kulevya iliyopo katika kundi la vichangamshi sawa na cocaine.

Dawa hii huwa kwenye mfumo wa vidonge, unga au chembechembe mithili ya chumvi ang’avu yenye rangi mbalimbali ambayo huzalishwa kwenye maabara bubu kwa kuchanganya aina mbalimbali za kemikali bashirifu.

Dawa hii ni hatari kwa afya ya mtumiaji, madhara yake ni makubwa na hayatibiti kirahisi kwani mtumiaji hupata madhara ya kudumu kwenye ubongo na hivyo hupunguza uwezo wa kutunza kumbukumbu, kusababisha uraibu na kuathiri mfumo mzima wa fahamu.

Kiasi cha dawa za kulevya zilizokamatwa, endapo zingefanikiwa kuingia mtaani zingeweza kuathiri zaidi ya watu 76,368,000 kwa siku. Hivyo, ukamataji huu umeokoa nguvu kazi ambayo ingeangamia kutokana na madhara yatokanayo na matumizi ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa a Kulevya, inatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Mamlaka kwani mafanikio haya yametokana na ushirikiano unaotokana na wananchi wanaotoa taarifa juu ya watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na weledi na uzalendo mkubwa wa maafisa wa Mamlaka katika udhibiti wa biashara ya dawa za kulevya.

Pia, Mamlaka inatoa onyo kwa wote wanaoendelea kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya hapa nchini kuacha badala yake wajikite kwenye biashara nyingine halali kwani Mamlaka imejizatiti kukomesha biashara ya dawa za kulevya kwa kufanya operesheni katika maeneo mbalimbali nchini.

Aidha,Mamlaka inaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuiwezesha Mamlaka katika kutekeleza kazi zake kwa ufanisi mkubwa.

Tukishirikiana, kwa umoja wetu tutaweza kuokoa vizazi vyetu na taifa letu dhidi ya tatizo la dawa za kulevya.

kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya heroin na methamphetamine
zakamatwa
0 Comment

Kaka amuua kwa kumpiga risasi dada yake mkubwa kisa zawadi za KrismasiAfyaclass Bongo Social •

Kaka amuua kwa kumpiga risasi dada yake mkubwa kisa zawadi za Krismasi.

Kaka, mwenye umri wa miaka 14, amuua kwa kumpiga risasi dada yake mkubwa alipokuwa amemshikilia mtoto wa miezi 10 baada ya ugomvi juu ya zawadi za Krismasi.

Mwanamke wa Florida akiwa amemshikilia mtoto wake mchanga kwenye gari la kubebea watoto alipigwa risasi na kuuawa na kaka yake mwenye umri wa miaka 14 alipokuwa akijaribu kusuluhisha mabishano kati yake na kaka yake mkubwa mwenye umri wa miaka 15 ambaye pia alikuwa na silaha, mamlaka ilisema.

ndugu hao walikuwa wakizozana kuhusu zawadi za Krismasi wakati mtoto huyo wa miaka 14 alipompiga risasi dada yao.

Kaka yao huyo mwenye umri wa miaka 15 na yeye alimpiga risasi mdogo wao mwenye umri wa miaka 14, ingawa hakufariki kwa kumuua dada yao Jumapili, Desemba 24, huko Largo, Florida, ambayo iko katika eneo la metro ya Tampa, Ofisi ya Sheriff ya Kaunti ya Pinellas ilisema katika taarifa ya habari.

Mzozo kuhusu zawadi ulianza wakati ndugu hao watatu walipokuwa wakinunua Zawadi za Krismasi na mama yao na wana wawili wa dada huyo, wenye umri wa miaka 6 na 11,

Mzozo huo uliendelea walipoenda nyumbani kwa nyanya yao ambapo dada huyo mwenye umri wa miaka 23, alimwambia mdogo wake aache kugombana na kaka yake mkubwa kwani ilikuwa mkesha wa Krismasi.

Kaka mdogo kisha akamwambia dada yake angempiga risasi yeye na mtoto wake mchanga, kisha akampiga kweli risasi kifuani, ofisi ya sheriff ilisema,

Ndipo kaka yake mwenye umri wa miaka 15 na yeye akampiga risasi mdogo wake nje ya nyumba kwa sababu ya kile alichomfanyia dada yao na akatoroka nyumbani, huku akitupa bunduki yake katika ua wa karibu, mamlaka ilisema.

Alipelekwa katika kituo cha afya ya akili baada ya kupatikana kwa vile alikuwa ametishia kujidhuru. Mara tu atakapoachiliwa kutoka katika kituo cha afya ya akili, atapelekwa katika kituo cha mahabusu ya watoto, taarifa ya habari ilisema.

Kaka huyo mwenye umri wa miaka 14 alishtakiwa kwa mauaji ya daraja la kwanza, unyanyasaji wa watoto na kwa kuwa na bunduki kama mhalifu. Ndugu yake mwenye umri wa miaka 15 alishtakiwa kwa jaribio la mauaji ya daraja la kwanza na kuharibu ushahidi, ofisi ya sheriff ilisema.

Kaka amuua kwa kumpiga risasi dada yake mkubwa kisa zawadi za Krismasi
0 Comment

Sababu ya mashavu ya uke kuwashaAfyaclass Bongo Social •

Sababu ya mashavu ya uke kuwasha

Baadhi ya Wanawake hupatwa na tatizo la mashavu ya uke kuwasha lakini hawajui shida hii imetokana na nini?

Katika Makala hii tumekuchambulia baadhi ya Sababu za mashavu ya uke kuwasha, Soma Zaidi hapa…!!!!

Chanzo cha mashavu ya uke kuwasha

Hizi hapa ni baadhi ya Sababu za mashavu ya uke kuwasha;

1. Maambukizi ya Fangasi(Yeast infections)

Wanawake wengi hushambuliwa na fangasi sehemu za Siri(candida albicans), hali ambayo hupelekea kupata dalili mbali mbali ikiwemo;

  • mashavu ya uke kuwasha
  • Kuhisi kuungua ukeni
  • Kutoa uchafu mweupe kama maziwa mgando ukeni n.k

2. Tatizo la Bacterial vaginosis

Bacterial vaginosis (BV) ni tatizo linalohusisha maambukizi ya bacteria Ukeni,

Hutokea pale ambapo hakuna uwiano sawa kati ya bacteria wazuri wa Ukeni, Wanawake wenye tatizo hili huweza kupata dalili mbali mbali ikiwemo;

  • mashavu ya uke kuwasha(nje)
  • Kuwashwa ndani ya Uke
  • Kupata maumivu ukeni
  • Kuhisi hali ya kuungua ndani ya uke
  • kutokwa na uchafu mwembamba mweupe au kijivu ukeni
  • Kutoa harufu mbaya ukeni hasa baada ya tendo n.k

3. Matatizo ya ngozi(Skin conditions)

Mashavu ya uke kuwasha huweza kusababishwa na matatizo ya ngozi kama vile;

  • Tatizo la psoriasis
  • seborrheic dermatitis
  • Tatizo la Mzio au allergy kwenye ngozi(allergic contact dermatitis)
  • folliculitis
  • dermographism/ skin writing n.k

Pia mashavu ya uke kuwasha  sana inaweza Kuashiria tatizo la lichen sclerosus au ichen planus.

4. Magonjwa ya Zinaa

Tatizo la Mashavu ya uke kuwasha huweza kusababishwa na Magonjwa ya Zinaa, hapa tunazungumzia magonjwa ya Zinaa kama vile;

  • genital herpes
  • Pamoja na trichomoniasis

5. Tatizo la masundosundo(genital warts)

Baada ya Mwanamke kupata tatizo la genital warts kutokana na maambukizi ya kirusi cha Human papilloma Virus(HPV) anaweza pia kukumbana na tatizo la mashavu ya uke kuwasha.

6. Tatizo la maambukizi ya Bacteria kwenye Via vya Uzazi vya Mwanamke(PID)

Ugonjwa wa PID pia unaweza kuchangia tatizo la mashavu ya uke kuwasha.

7. Sababu Zingine…!!!!

Ingawa ni mara chache kutokea lakini matatizo kama vile;

(i) Saratani ya Mashavu ya Uke(Vulvar cancer) huweza kusababisha mashavu ya uke kuwasha,

Aina hii ya Saratani ni adimu sana kutokea, na dalili zake ni pamoja na;

  • mashavu ya uke kuwasha
  • Kuhisi kuungua kwenye mashavu ya uke
  • Kuvuja damu n.k

(ii) Pia Tatizo la uharibifu wa neva(Neuropathy), huweza kusababisha mashavu ya uke kuwasha

8. Miwasho kutokana na matumizi ya baadhi ya Vitu

Wakati mwingine tatizo la mashavu ya uke kuwasha huweza kutokana na matumizi ya vitu vinavyotuzunguka kama vile;

  • Baadhi ya Pedi(menstrual pads)
  • Baadhi ya Materials kwenye nguo za ndani
  • chupi zilizofuliwa na sabuni zenye harufu nzuri ila zina kemikali flani ndani yake
  • Baadhi ya Sabuni za kuogea
  • Baadhi ya Mafuta ya Kupaka,lotions au creams n.k
  • Matumizi ya kondoms(latex condoms)
  • Manukato ndani ya deodorants n.k

Na hapa; Kuwashwa kwenye Mashavu ya Uke kwa kawaida kutaisha baada ya mtu kuacha kutumia bidhaa hizi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Sababu ya mashavu ya uke kuwasha
0 Comment

DCEA kufanya operesheni dhidi ya dawatiba zinazogeuzwa kuwa dawa za kulevyaAfyaclass Bongo Social •

DCEA kufanya operesheni dhidi ya dawatiba zinazogeuzwa kuwa dawa za kulevya.

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA), imetangaza kuanza operesheni dhidi ya matumizi ya dawa tiba zinazogeuzwa kuwa dawa za kulevya.

Kulingana na DCEA, operesheni hiyo itahusisha uchunguzi wa maduka yanayouza dawa hizo kiholela, kwa maana yale yasiyo na vibali vya kufanya biashara hiyo.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam leo Desemba 27, 2023 na Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretus Lyimo alipozungumza na waandishi wa habari.

Operesheni hiyo, amesema imechagizwa na kukithiri kwa matumizi ya dawa tiba zinazogeuzwa kuwa dawa za kulevya.

“Kwa sasa tumefanikiwa kukamatwa mtandao mkubwa wa dawa za kulevya, hakuna tena mfanyabiashara mkubwa wa dawa hizi.

“Kwa sababu dawa za kulevya hazipatikani, kumeibuka matumizi ya dawa tiba zinazogeuzwa za kulevya na hili ndilo linalotusumbua sasa,” amesema.

Kutokana na hali hiyo, Lyimo amesema hivi karibuni operesheni dhidi ya maduka yanayouza dawatiba kiholela itaanza na watuhumiwa watakamatwa.

Kilo 3,000 za heroin zakamatwa

Katika mkutano huo, Kamishna huyo amebainisha kukamatwa kwa kilogramu 3,182 za dawa za kulevya aina ya Heroin na Methamphetamine.

Iwapo dawa hizo zingeingizwa mtaani, amesema zaidi ya watu milioni 76.386 wangeathirika kwa siku.

Kwa mujibu wa Lyimo, dawa hizo zilikamatwa katika operesheni iliyofanyika kuanzia Desemba 5 hadi 23, mwaka huu katika Mikoa ya Dar es Salaam na Iringa.

“Watu saba wamekamatwa kuhusika na dawa hizo ambapo wawili wana asili ya Asia,” amesema Lyimo.

Kati ya dawa hizi za kulevya zilizokamatwa katika Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Kigamboni kwa Dar es Salaam na Wilaya ya Iringa mkoani Iringa, amesema kilogramu 2,180.29 ni aina ya Methamphetamine na kilogramu 1001.71 ni aina ya Heroin.

Hata hivyo, amesema kiasi cha dawa kilichokamatwa kwenye operesheni hiyo, ndiyo kikubwa zaidi kuwahi kukamatwa tangu kuanza kwa shughuli za udhibiti wa dawa hizo.

“Watuhumiwa waliokamatwa ni miongoni mwa mitandao mikubwa ya wauzaji wa dawa za kulevya inayofuatiliwa nchini na duniani,” amesema.

Aidha, amesema katika mtandao huo, watuhumiwa wengine waliokimbilia nje ya nchi ikiwemo Afrika Kusini wanaendelea kufuatiliwa ili watiwe nguvuni.

“Tumeshawasiliana na nchi mbalimbali kuhakikisha watuhumiwa wote wanakamatwa na wakiwakamata watatujulisha,” amesema.

Ukubwa wa tatizo

Alipotafutwa na Mwananchi Digital kuzungumzia ukubwa wa tatizo la matumizi ya dawatiba kama dawa za kulevya, Mkurugenzi wa Pili Misana Foundation Sober House (inayoshughulika na kuwaponya waathirika wa dawa za kulevya), Pili Missanah amesema changamoto ni kubwa.

Kwa sasa amesema waathirika wa Heroin na Cocaine wamepungua, lakini wanaotumia dawatiba kuzigeuza dawa za kulevya ni wengi zaidi.

“Kwenye Kituo changu kwa siku moja naweza kumpokea mraibu mmoja wa unga, lakini nikapokea wathirika 10 wa dawatiba,” amesema.

Kulingana na Pili, wengi wao wanaanzia kwenye matumizi ya dawa za maumivu na baadaye wanapata uraibu.

“Ni dawa hizi za kupunguza maumivu ndizo hasa zinazowaathiri, mtu anatumia kupitiliza hadi inamjengea uraibu. Anajikuta hawezi kufanya lolote bila kupata hizo dawa,” amesema.

Kwa kiasi kikubwa, amesema hali hiyo inasababishwa na uuzwaji holela wa dawa hizo za kulevya.

Kuhusu mpango wa DCEA, amesema ni sahihi na umekuja wakati muafaka, isipokuwa kuna changamoto ya kuwabaini wanaouza kwa njia haramu na halali, kwa kuwa dawa hizo haziuzwi kwa kibali.

“Kwa uelewa wangu dawa hizi haziuzwi kwa kibali yeyote anauza tu dukani, kumjua anayeuza zikatumike vibaya na vizuri ni vigumu.

“Kikubwa ni kuwaelimisha wananchi, pia wapo madaktari wasio waaminifu, mtu akijisikia vibaya anamchoma sindano ya kupunguza maumivu, kesho akienda anamchoma tena na tena na tena hadi anakuwa mraibu,” amesema.

DCEA kufanya operesheni dhidi ya dawatiba zinazogeuzwa kuwa dawa za
kulevya
0 Comment

Roboti ya Tesla yamvamia mhandisi na kumshambulia VikaliAfyaclass Bongo Social •

Roboti ya Tesla yamvamia mhandisi na kumshambulia Vikali.

Mhandisi wa Roboti ya Tesla alishambuliwa na roboti hiyo kwa kile kichoelezwa kuwa ni hitilafu kali katika kiwanda cha Giga Texas karibu na Austin.

Wafanyikazi wengine wawili waliripotiwa kushuhudia shambulio hilo la kutisha huku mfanyakazi mwenzao akishambuliwa na mashine iliyobuniwa kunyakua na kusogeza sehemu mpya za gari za alumini.

Kulingana na Mail Online, roboti hiyo ilikuwa imembandika mwanaume huyo, ambaye alikuwa akitengeneza programu kwa ajili ya roboti mbili za Tesla zinazozimwa kwa karibu,

Ndipo Roboti hyo ikatumbukiza makucha yake ya chuma kwenye mgongo na mkono wa mfanyakazi huyo, na kusababisha ‘damu nyingi kuvuja na kusambaa’ kwenye eneo la kiwanda.

Tukio hilo – ambalo lilimwacha mwathiriwa na ‘jeraha kubwa’ kwenye mkono wake wa kushoto – lilifichuliwa katika ripoti ya majeraha ya 2021 iliyowasilishwa kwa Kaunti ya Travis na wasimamizi wa serikali, ambayo imekaguliwa na DailyMail.

Tukio hilo linakuja huku kukiwa na wasiwasi wa miaka mingi kuhusu hatari za roboti otomatiki mahali pa kazi.

Ripoti za majeraha yaliyoongezeka kutokana na wafanyakazi wenzangu katika vituo vya usafirishaji vya Amazon, madaktari wauaji wa upasuaji, magari yanayojiendesha, na hata vurugu kutoka kwa wakufunzi wa mchezo wa chess wa roboti, zimesababisha baadhi ya watu kutilia shaka ujumuishaji wa teknolojia hiyo mpya.

Ripoti ya majeraha, ambayo Tesla lazima awasilishe kwa mamlaka kwa mujibu wa sheria ili kudumisha malipo yake ya malipo makubwa ya kodi mjini Texas, ilidai kuwa mhandisi hakuhitaji muda wa kutoka kazini.

Lakini wakili mmoja ambaye anawakilisha wafanyikazi wa kandarasi wa Tesla wa Giga Texas ameiambia DailyMail.com anaamini, kulingana na mazungumzo yake na wafanyakazi, kwamba idadi ya majeraha waliyopata kiwandani inazidi kuripotiwa.

Taarifa hiyo ndogo, wakili huyo alisema, ilijumuisha hata kifo cha Septemba 28, 2021 cha mfanyakazi wa ujenzi, ambaye alikuwa amepewa kandarasi ya kusaidia kujenga kiwanda chenyewe.

‘Ushauri wangu ungekuwa kusoma ripoti hiyo, wakili, Hannah Alexander wa shirika lisilo la faida Workers Defense Project, aliiambia DailyMail.

“Tumekuwa na wafanyikazi wengi ambao walijeruhiwa,” Alexander alisema, “na mfanyakazi mmoja ambaye alikufa, ambaye majeraha au kifo chake hakimo katika ripoti hizi ambazo Tesla anapaswa kukamilisha na kuwasilisha kwa kaunti ili kupata motisha ya ushuru. .’

Mfanyikazi huyo wa ujenzi, mkandarasi anayeitwa Antelmo Ramírez, alikufa kutokana na joto kali alipokuwa akisaidia kujenga kiwanda cha Tesla chenye urefu wa zaidi ya ekari 2,000 cha Giga Texas, kulingana na ripoti kutoka kwa daktari wa Travis County.

Mwaka jana, Mradi wa Ulinzi wa Wafanyakazi uliwasilisha malalamiko kwa niaba ya wafanyakazi wa Giga Texas kwa Utawala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA), wakidai wakandarasi wa Tesla na wakandarasi wadogo waliwapa baadhi ya wafanyakazi vyeti vya uongo vya usalama.

“Wafanyakazi wanaripoti kwamba walipohitaji mafunzo, walitumiwa faili za PDF au picha za vyeti kupitia maandishi au WhatsApp baada ya siku chache,” Alexander aliambia mshirika wa NBC KXAN . ‘Hakuna njia inayoweza kuwaziwa wafanyakazi wangeweza hata kuchukua mafunzo yanayohitajika.’

UNA MAONI GANI JUU YA TUKIO HILI? Tuandikie hapa kwenye Comment..!!!

Roboti ya Tesla yamvamia mhandisi na kumshambulia Vikali
0 Comment

Damu imetapakaa kila mahali kwenye hizi hospitali:CaseyAfyaclass Bongo Social •

PICHA: Mvulana mwenye umri wa miaka 3, ambaye nyumba yake ilishambuliwa kwa bomu, anapata nafuu katika hospitali ya Nasser baada ya kukatwa sehemu ya mguu wake wa kulia.

Wahudumu wa afya huko Ukanda wa Gaza Jana jumanne wameendelea na kazi ya kuokoa maisha ya manusura wa mashambulio ya makambora yakiwemo mashambulio karibu na kambi ya wakimbizi kwenye eneo hilo lililozingirwa na Israel, mashambulio ambayo yameripotiwa kuua zaidi ya watu 100, limesema shirika la afya, WHO.

Mratibu wa Timu ya Matabibu wa Dharura Sean Casey amesema wagonjwa zaidi ya 100 walifikishwa Jumatatu kwenye hospitali ya Al-Aqsa ndani ya muda wa dakika 30, kufuatia milipuko karibu na kambi ya wakimbizi ya Al-Maghazi.

Wagonjwa wote hao walikuwa wanahitaji matibabu ya dharura wakiwa na majeraha makubwa,  amesema Afisa huyo wa WHO akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa.

Amesema huku wagonjwa hao wakiletwa hospitali, takribani maiti wengine 100 walifikishwa muda huo huo.

Wamenasa chini  ya vifusi

Nayo Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, OHCHR, imeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya mashambulizi makubwa ya mabomu yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel katikati ya Gaza, ambapo zaidi ya mashambulizi 50 kutoka angani yameripotiwa kufanyika tangu tarehe 24 mwezi huu wa Desemba.

Mashambulio hayo yameripotiwa kuua zaidi ya wapalestina 100 tangu siku hiyo ambapo OHCHR inasema, “hii inatia zaidi wasiwasi kwa ripoti ya kwamba jeshi la Israel limeagiza wakazi walioko kusini mwa eneo la Wadi Gaza, wahamie eneo la kati la Gaza na Tal a-Sultan.”

Kambi tatu za wakimbizi zilipigwa kwa makombora, amesema msemaji wa OHCHR, Seif Magango kwenye taarifa iliyotolewa leo, akitaja kambi hizo kuwa ni Al Bureij, Al-Nuseirat na Al-Maghazi.

“Makombora mawili yalipiga makazi sav ana kuua tarkibani wapalestina 86 na kujeruhi wengine wengi,” amesema Magango huku akiongeza kuwa, “idadi isiyojulikana ya watu yaaminika wamefukiwa kwenye vifusi.”

Tedros achukizwa

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X (zamani ukijulikana kama Twitter) Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amelaani mauaji yanayosababishwa na mashambulizi ya kutoka angani yanayofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Gaza ikiwa ni kisasi cha mashambulizi yaliyofanywa na Hamas tarehe 7 mwezi Oktoba mwaka huu. Takribani watu 1,200 waliuawa na wengine 240 walitekwa nyara siku hiyo.

“WHO ina wasiwasi mkubwa juu ya mzigo mkubwa kwa hospitali chache zinazoendelea kutoa huduma kwenye eneo hilo kutokana na kuendelezwa kwa chuki kati ya pande mbili hizo. Hospitali zilizosalia wazi ni chache ambapo nyingi zao uwezo wa kutoa huduma uko taabani,” alisema Dkt. Tedros siku ya Jumatatu.

Kupitia ukurasa wake wa X, Bwana Casey ameelezea hali katika hospitali ya Al-Aqsa kuwa ni dimbwi la damu. Alionesha Ahmed, mvulana mwenye umri wa miaka tisa ambaye alikuwa amalala kwenye sakafu ya hospitali hiyo baada ya kujeruhiwa kwa kiasi kikubwa na mlipuko wakati akivuka mtaa mmoja karibu na Nuseirat.

“Tumeona watoto, wanawake, vijana wa kiume, wazee wakivuja damu,” amesema Bwana Casey, huku akiongeza kuwa wagonjwa hawawezi kuhamishiwa eneo lingine kwa ajili ya matibabu ya kuokoa maisha yao.

“Damu imetapakaa kila mahali kwenye hizi hospitali. Tunaona wagonjwa wako na viwewe, damu kila mahali, tulishasema, ni mauaji.”

Shule ya Nuseirat iliyoko Gaza Kati inayoendeshwa na UNRWA sasa ni makazi ya maelfu ya watu waliofurushwa makwao kutokana na mashambulizi yanayoendelea Gaza.

Mapigano usiku kucha

“Hakuna mahali salama Gaza,” amesema Bwana Casey. “Hivi sasa hapa Rafah nje ya mlango wa jengo hili niliko, meta 50 hivi, kuna kambi ya maelfu ya watu ambao wamesaka hifadhi hapa. …wanaishi kwenye makazi yaliyofunikwa kwa karatasi za nailoni. Jana usiku tulisikia mashambulizi usiku kucha huku kukiwa na ripoti za kuweko kwa majeruhi wengi, wakipelekwa hospitali zilizoko hapa kusini.”

Uwezo wa hospitali Gaza hivi sasa ni takribani asilimia 20 ya kabla ya tarehe 7 Oktoba mashambulizi yalipoanza. “Takribani hospitali zote zimeacha kufanya kazi.”

Wanasubiri kufa

Bwana Casey amezungumzia pia wagonjwa walioko mahututi huko Gaza Kaskazini ambao kwa sasa wanasubiria kufa tu kwani hospitali ya mwisho iliyokuwa inatoa huduma imefungwa na sasa wako kwenye viwanja vya kanisa wakilala kwenye viti.

“Kiwango cha uharibifu ni kikubwa, barabara zimesheheni vifusi hivyo ni vigumu kufikia wahitaji.”

“Bado tunahitaji kuchukua hatua zaidi kusafirisha hawa wagonjwa, lakini fursa ya kufanya hivyo inazidi kuwa fingu kila uchao kwani ufikiaji wa hospitali ni mgumu,” amesema Bwana Casey.

Kwa mujibu wa Wizara ya Afya Gaza, takribani watu 20,000 yaaminika wameuawa tangu kuanza kwa mapigano Oktoba 7, mwaka huu.

Damu imetapakaa kila mahali kwenye hizi hospitali:Casey
0 Comment

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia TumbakuAfyaclass Bongo Social •

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku.

Kwa Mujibu wa takwimu za shirika la Afya Duniani(WHO); 

Watu bilioni 5.6— sawa na asilimia 71% ya idadi ya watu duniani—sasa wanalindwa kwa angalau na sera moja ya utendaji bora ya WHO kusaidia kuokoa maisha kutokana na matumizi ya tumbaku,
Hii ni mara tano zaidi ya mwaka 2007.

Katika miaka 15 tangu hatua za WHO za MPOWER za kudhibiti tumbaku kuanzishwa duniani kote, viwango vya uvutaji sigara vimepungua,

na karibu asilimia 40% ya nchi mbali mbali sasa zina maeneo ya ndani ya umma yasiyo na moshi yaani “smoke-free indoor public places”.

Haya ni baadhi tu ya mambo muhimu ya afya duniani ambayo yalitoa matumaini katika Mwaka 2023. Katika 2024, tutachukua hatua zaidi kuelekea ulimwengu wenye afya, usalama na haki linasema shirika la Afya Duniani(WHO).

5.6 billion people—71% of the world’s population—are now protected with at least one WHO best-practice policy to help save lives from tobacco use.
This is five times more than in 2007.

In the 15 years since WHO’s MPOWER tobacco control measures were introduced globally, smoking… pic.twitter.com/Y9Bb9387sr

— World Health Organization (WHO) (@WHO) December 25, 2023

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani
kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku
0 Comment

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia TumbakuAfyaclass Bongo Social •

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku.

Kwa Mujibu wa takwimu za shirika la Afya Duniani(WHO); 

Watu bilioni 5.6— sawa na asilimia 71% ya idadi ya watu duniani—sasa wanalindwa kwa angalau na sera moja ya utendaji bora ya WHO kusaidia kuokoa maisha kutokana na matumizi ya tumbaku,
Hii ni mara tano zaidi ya mwaka 2007.

Katika miaka 15 tangu hatua za WHO za MPOWER za kudhibiti tumbaku kuanzishwa duniani kote, viwango vya uvutaji sigara vimepungua,

na karibu asilimia 40% ya nchi mbali mbali sasa zina maeneo ya ndani ya umma yasiyo na moshi yaani “smoke-free indoor public places”.

Haya ni baadhi tu ya mambo muhimu ya afya duniani ambayo yalitoa matumaini katika Mwaka 2023. Katika 2024, tutachukua hatua zaidi kuelekea ulimwengu wenye afya, usalama na haki linasema shirika la Afya Duniani(WHO).

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani
kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku
0 Comment

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia TumbakuAfyaclass Bongo Social •

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku.

Kwa Mujibu wa takwimu za shirika la Afya Duniani(WHO); 

Watu bilioni 5.6— sawa na asilimia 71% ya idadi ya watu duniani—sasa wanalindwa kwa angalau na sera moja ya utendaji bora ya WHO kusaidia kuokoa maisha kutokana na matumizi ya tumbaku,
Hii ni mara tano zaidi ya mwaka 2007.

Katika miaka 15 tangu hatua za WHO za MPOWER za kudhibiti tumbaku kuanzishwa duniani kote, viwango vya uvutaji sigara vimepungua,

na karibu asilimia 40% ya nchi mbali mbali sasa zina maeneo ya ndani ya umma yasiyo na moshi yaani “smoke-free indoor public places”.

Haya ni baadhi tu ya mambo muhimu ya afya duniani ambayo yalitoa matumaini katika Mwaka 2023. Katika 2024, tutachukua hatua zaidi kuelekea ulimwengu wenye afya, usalama na haki linasema shirika la Afya Duniani(WHO).

Watu billion 5.6 Duniani sawa na asilimia 71% ya watu wote duniani
kulindwa na Sera ya kuzuia Tumbaku
0 Comment

Wamiliki wa hospitali binafsi watishia kugoma kutoa hudumaAfyaclass Bongo Social •

Wamiliki wa hospitali binafsi watishia kugoma kutoa huduma.

Wamiliki wa hospitali binafsi nchini wametishia kugomea kutibu wagonjwa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), iwapo bei mpya zilizotangazwa na mfuko huo zitaanza kutumika Januari Mosi kama ilivyopangwa. Anaripoti Mwandishi Wetu….(endelea)

Kupitia taarifa yao kwa vyombo vya habari jana, wamiliki hao wamesema kitita hicho kilipitishwa na serikali bila kuwashirikisha na kitasababisha hospitali nyingi kufungwa kutokana na kupata hasara  iwapo kitaanza kutumika.

“Kwa miaka saba sasa tangu gharama mpya zitangazwe hazikuwahi kuboreshwa na ilikuwa matarajio yetu kwamba NHIF itatangaza ongezeko la gharama za  huduma na siyo kupunguza,” ilisema na kuongeza

“Kwa kuzingatia ukweli huu pamoja na mengine kama ucheleweshaji wa malipo kwa zaidi ya miezi minne, mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola kwa zaidi ya asilimia 20 ndani ya miaka saba APHFTA tumeona tutashindwa tutashindwa kuwahudumia wanachama wa NHIF kama bei hizi zitaanza kutumika rasmi,” ilisema

Ilitoa mfano kuwa kushuka kwa gharama za kumwona daktari, upasuaji na kuchuja damu (dialysis), kutawafanya washindwe kumudu gharama halisi za kuhudumia wagonjwa wanaotibiwa kwao.

Ilisema bei za mwisho ziliwsekwa tangu mwaka 2016 na tangu wakati huo hazijwahi kufanyiwa mapitio licha ya gharama za maisha kupanda sasa kushusha gharama ni sawa na kuzichimbia kaburi hospitali binafsi.

“Malipo yenyewe kwa watoa huduma yanaweza kukaa miezi hata sita hayajalipwa na wakati mwingine wanakataa baadhi ya madai ya malipo bila sababu za msingi sasa haya yote hayajataatuliwa wanakuja kushusha gharama si wanataka kutuua,” ilisema taarifa hiyo.

Taarifa yao ilisema kuwa NHIF iliwaambia wafunge mfumo wa online kwaaajili ya kuwasilisha madai yao ya huduma wanazotoa ili wawe wanalipwa ndani ya siku 14 baada ya kuwasilisha madai hayo lakini hali bado ni ile ile tangu wafunge.

“Tumefunga mfumo ambao umetugharimu shilingi milioni 80 lakini hizo siku 14 walizosema hawalipi na bado tunalazimika kusubiri miezi minne hadi sita, kama wanaona gharama za uendeshaji zimekuwa kubwa wapunguze matumizi yao yasiyo ya lazima lakini watibu watu,” ilisema

“Kwenye hili tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan atusaidie kwasababu kwa hiki kitita ni kama wanataka kuzifunga hospitali binafsi, Rais wetu siku zote amekuwa akisisitiza ushirikishwaji wa sekta binafsi kupitia PPP lakini hawa ni kama hawataki kuona tuna survive,” ilisema

Ilisema APHFTA iliwasilisha mapendekezo ya namna ya kuboresha uhai wa mfuko ikiwemo kuitaka NHIF ipitie upya mapendekezo ya kibiashara kwa bidhaa zake vikiwemo vifurushi vya WEKEZA, TIMIZA, NAJALI na vinginevyo.

Ilisema walipendekeza NHIF itumie mfumo wa ukusanyaji madeni wenye ufanisi  zaidi na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesababu za Serikali (CAG) inamaelezo ya kiasi kikubwa cha fedha ambacho hakikusanywi na NHIF kwa taasisi nyingi.

“Kabla ya kutafuta suluhisho la nje NHIF inapaswa kuonyesha msimamo wa kupunguza gharama za uendeshaji ndani ya mfuko na tukumbuke kwamba vituo vya afya, hospitali na NHIF wanategemeana kwaajili ya kuishi na kuwa endelevu hivyo hatupaswi kudhoofishana,” ilisema

Ilisema kikao cha APHFTA kilikaa na kubaini kuwa baada ya ukaguzi wa madai ya Septemba, Oktoba na Novemba 2023 hospitali zote binafsi kuanzia ngazi ya Dispensari mpaka hospitali za rufaa zingepata hasara asilimia 25 kwa wastani.

“Na hii ni bila kuzingatia makato ya kila mwezi ukizingatia makato hayo yenye wastani wa asilimia 10 ambayo makato yenyewe yamejaa sintofahamu na utata mwingi yanafanya jumla ya hasara kufikia asilimia 35 kwa hospitali binafsi,” ilisema

Wakati huo huo, wakati wakati APHFTA inadai kutoshirikishwa katika mchakato wa kushusha gharama, NHIF wamesema waliwashirikisha katika hatua zote.

Kwenye barua yake kwa hospitali mbalimbali za Mkoa wa Dar es Salaam,  Meneja wa NHIF Mkoa wa Kinondoni, Dk. Christopher Lazeck alisema mwaka 2018 NHIF ilianza mchakato wa kuboresha kitita chake baada ya serikali kutoa mwongozo wa matibabu kwa lengo la kuwianisha  huduma za kitita cha mafao, mwongozo huo na bei ya soko.

Alisema kupitia barua yenye kumbukumbu namba EA.35/269/01-A/32 kuhusu dhamira ya mfuko ya kuanza kutumika kwa kitita cha mafao kwa lengo la kupata maoni, NHIF ilikutana na wadau na kupata maoni mbalimbali kwaajili ya maboresho zaidi.

“Lengo la maboresho ya yaliyofanyika ni pamoja na kuhuisha kitita cha mafao  na miongozo ya tiba nchini, kuweka usawa wa ada ya kumwona daktari bingwa kulingana na taaluma na ikama, kuboresha bei za huduma kulingana na hali halisi ya soko,” alisema

Alisema maboresho yalilenga kuongeza motisha kwa watoa huduma vikiwemo vituo vya ngazi ya Mkoa, Wilaya na vituo vya afya na Zahanati na kuwezesha huduma za kibingwa kupatikana karibu na Wananchi.

Chanzo: tanzaniaweb

Wamiliki wa hospitali binafsi watishia kugoma kutoa huduma
0 Comment

Kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa UpasuajiAfyaclass Bongo Social •

Kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa Upasuaji

Ikiwa unajiuliza kama kujifungua kwa njia ya kawaida inawezekana baada ya kujifungua kwa njia ya upasuaji ujauzito uliopita, jibu ni kwamba inawezekana kwa wanawake wengi lakini kuna sababu zitakazo wasaidia wewe na daktari wako kufikia hitimisho kama inawezekana kwako au la.

Usalama kwako na mtoto wako ni jambo muhimu la kuzingatia. Kujifungua kwa kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji sio salama kwa kila mwanamke.

Ikiwa unajaribu kujifungua kwa njia ya kawaida unakuwa katika hatari kubwa ya kupata matatizo, ambayo yanaweza kusababisha utata wa afya ya wewe na mtoto wako- baadhi kuhatarisha maisha. Ndiyo maana ni muhimu kuongea na daktari wako kuhusu hatari hizi.

Ili daktari na wewe kufikiria uwezekano wa kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya upasuaji, inakubidi wewe na mtoto wako muwe katika afya njema. Unaweza kujaribu kujifungua kwa kawaida hata ukiwa na ujauzito wa mapacha, cha msingi ni daktari kuhakikisha na kusema wote mko katika afya nzuri ya kuhimili zoezi zima.

Sababu hatari ambazo daktari hatakuruhusu kujifungua kwa kawaida baada ya kujifungua kwa upasuaji ujauzito uliopita ni pamoja na:

  • Uzito uliopitiliza (kama BMI yako ni 30 au zaidi)
  • Shinikizo kubwa la damu wakati wa ujauzito (Pre-eclampsia)
  • Umri mkubwa (kawaida zaidi ya 35)
  • Upasuaji wako wa awali ulifanyika miezi 19 iliyopita.
  • Mtoto wako tumboni ni mkubwa sana.
  • Kama wakati wa upasuaji ulichanwa kwa wima (vertical cut) hauruhusiwi kujaribu kujifungua kwa njia ya kawaida. Kuna nafasi kubwa ya mshono wako kuachia wakati wa kusukuma mtoto, hali ambayo italeta madhara makubwa kwako na mtoto wako. Itakubidi kufanyiwa upasuaji tena.

 Faida za Kujifungua kwa Njia ya Kawaida Baada ya Kujifungua kwa Upasuaji.

Asilimia 70 ya wanawake wanaojaribu kujifungua kwa njia ya kawaida wanafanikiwa, wengine inashindikana kwasababu ya dharura zinazotekea wakati wa kujaribu, wanaishia kufanyiwa upasuaji.

Unaweza kutamani kujaribu kujifungua kwa kawaida baada ya upasuaji kwasababu ya sababu mbalimbali, jaribio hili likifanikiwa kuna faida ambazo ni:

  • Hakuna upasuaji utakaofanyika
  • Kiasi kidogo cha damu kitapotea
  • Uponaji wa haraka
  • Inapunguza nafasi ya maambukizi
  • Sio rahisi kusumbuka na kidonda kwenye kibofu, utumbo au ogani nyingine.
  • Inapunguza nafasi ya kuwa na matatizo makubwa wakati wa kujifungua kwa ujauzito ujao.

Kumbuka

Sio kila hospitali inatoa huduma ya mjamzito kujifungua kwa njia ya kawaida baada ya upasuaji katika ujauzito wake wa awali, hivyo katika mpango wako wa kujifungua hakikisha unahusisha hospitali unayotarajia katika mkakati wako ili kujua kama inatoa huduma hiyo. Hata kama nafasi ya mshono uliopita kuachia wakati wa kusukuma ni ndogo, hospitali inatakiwa kujiandaa kwa hali yeyote ya dharura inayoweza kutokea. Baadhi ya hospitali hazina utayari wa vifaa na watu wenye ujuzi kukabiliana na hali ya dharura.

Via:afyatrack

Kujifungua kawaida baada ya kujifungua kwa Upasuaji
0 Comment

Mafuriko yaua 6 na wengine 10 hawajulikani walipo kwenye mkesha wa krismasiAfyaclass Bongo Social •

Mafuriko yaua 6 na wengine 10 hawajulikani walipo kwenye mkesha wa krismasi.

Watu sita wamefariki na watu 10 hawajulikani walipo kufuatia mafuriko yaliyokumba Ladysmith huko KwaZulu-Natal mkesha wa Krismasi.

Idara ya Ushirikiano wa Utawala na Masuala ya Kimila ya KZN ilisema timu za utafutaji na uokoaji ambazo zilifanya kazi siku ya Krismasi kupata waliopotea, zitaanza tena Jumanne.

“Kwa sasa, tuna vifo sita vilivyothibitishwa na bado watu 10 hawajulikani walipo”, afisa wa mamlaka ya mkoa aliiambia AFP Jumanne, akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, akiongeza kuwa msako ulianza tena Jumanne.

Waathiriwa watatu walipatikana katika basi dogo lililokuwa limebeba abiria tisa; wengine sita bado hawajulikani walipo, afisa huyo alisema.

Mtu mmoja alipatikana amekufa katika nyumba iliyoharibiwa na maji. Watu wengine wawili walikuwa ndani na bado hawajapatikana.

Takriban wakaazi wengine wawili walipatikana wamekufa ndani ya magari yao, ambayo yalikuwa yamesombwa na mafuriko.

Mvua kubwa zaidi inatarajiwa kunyesha katika KwaZulu-Natal siku ya Jumanne.

Mafuriko yaua 6 na wengine 10 hawajulikani walipo kwenye mkesha wa
krismasi
0 Comment

Mlipuko kutoka kwa bomba la mafuta lililoharibiwa waua watu 20Afyaclass Bongo Social •

Mlipuko kutoka kwa bomba la mafuta lililoharibiwa waua watu 20.

Takriban watu 20 wamefariki kutokana na mlipuko uliotokea katika eneo la kuchotea mafuta katika eneo la Omoku, Ogba/Egebema/Ndoni katika Jimbo la Rivers nchini Nigeria.

Kisa hicho kilitokea Jumapili asubuhi, Desemba 24, baada ya vijana kudaiwa kuvunja bomba la kampuni moja ya kimataifa ya mafuta inayofanya kazi katika eneo hilo na kuanza kuchota mafuta.

Moto huo uliwaua wale wote waliokuwa wakichota mafuta karibu na bomba hilo,

Huku Watu 20 wakihofiwa kufariki, wengi wao waliungua kwa viwango tofauti na wanapokea matibabu katika hospitali tofauti eneo hilo.

“Ni tukio baya sana. Hebu fikiria vifo vya watu 20 katika wakati kama huu. Tulijifunza kwamba baadhi ya vijana walichoma bomba la kampuni hiyo.

“Ukienda katika Hospitali Kuu na zahanati zingine za kibinafsi huko Omoku, utaona watu wengi waliojeruhiwa wametawanyika kila mahali katika hospitali za serikali na za kibinafsi wakipokea matibabu,” chanzo kiliongeza.

Katibu Msaidizi wa kikundi cha walinzi katika eneo hilo, Baraza la Ushauri la Amani na Usalama la Onelga, Emeka Agbabere, alilaumu tukio hilo kwa uchomaji mafuta kinyume cha sheria.

Agbabere alisema vikundi, Kamati ya Maendeleo ya Jamii na vijana walielekezwa na mfalme katika eneo hilo kusitisha shughuli za uchomaji mafuta huko.

Hata hivyo alielezea kusikitishwa kwake, kwamba kampeni za mara kwa mara za vijana kukomesha uvamizi haramu hazijazaa matokeo.

Mlipuko kutoka kwa bomba la mafuta lililoharibiwa waua watu 20
0 Comment

Mwanamke na watoto wake wanne wapatikana wamekufa ghorofaniAfyaclass Bongo Social •

Mwanamke na watoto wake wanne wapatikana wamekufa ghorofani wakati huo polisi wanamkamata baba yao.

Baba wa watoto wanne, ambaye aliwahi kuchunguzwa kwa vitendo vya unyanyasaji katika familia yake, amekamatwa Jumanne, Desemba 26, baada ya watu watano akiwemo mkewe na watoto wake wanne kupatikana wakiwa wamekufa kwenye nyumba ya familia siku ya Krismasi, Desemba 25, , 2023.

Watoto wanne walikuwa miongoni mwa waliofariki katika mauaji hayo yanayoonekana kuwa makubwa huko Meaux, kaskazini mashariki mwa Paris.

“Miili mitano ilipatikana – Mwanamke mmoja, na watoto wake;wavulana wawili na wasichana wawili – na kusababisha uchunguzi wa mauaji yao,” mwendesha mashtaka wa eneo hilo Jean-Baptiste Bladier alisema Jumanne.

“Mshukiwa mkuu ni babake, mwenye umri wa miaka thelathini na tatu, ambaye alipatikana Jumanne kwenye nyumba iliyo karibu, baada ya kukimbia.”

Data ya eneo kwenye simu yake ilifichua kuwa mwanamume huyo aliondoka kwenye orofa ya familia mwendo wa saa 8.07 usiku wa Siku ya Krismasi.

Watoto waliokufa – wenye umri wa miaka 10, saba, minne na miezi tisa – wote walikuwa ndani ya gorofa ya familia, na mama yao.

Wala mshukiwa, wala waathiriwa, bado hawajatajwa na mamlaka ya Ufaransa.

“Kulikuwa na idadi kubwa sana ya majeraha ya visu kwenye pande za mbele na nyuma, kwenye shina, miguu ya chini na ya juu pamoja na majeraha,” alisema Bw Bladier.

“Waathiriwa wengine wawili, mvulana wa miaka minne na mtoto wa miezi tisa, hawakuwa na majeraha yoyote,” alisema Bw Bladier.

Hii ilisababisha nadharia ya mapema kwamba walikufa kutokana na kuzama au kukosa hewa, alisema mwendesha mashtaka.

Mtu aliyekamatwa tayari alikuwa anajulikana kwa vitendo vya “unyanyasaji wa nyumbani na kwa kusumbuliwa na magonjwa ya akili,” kilisema chanzo kingine cha uchunguzi.

Mnamo 2019 alichunguzwa kwa vitendo vya unyanyasaji wa nyumbani, pamoja na kumshambulia mkewe kwa kisu.

Mwanamke na watoto wake wanne wapatikana wamekufa ghorofani
0 Comment

Ndege iliyoshikiliwa kwa hofu ya biashara ya binadamu yatua IndiaAfyaclass Bongo Social •

Ndege iliyoshikiliwa kwa hofu ya biashara ya binadamu yatua India

Ndege iliyokuwa imewabeba mamia ya raia wa India waliokuwa wamezuiliwa kwa siku kadhaa kwenye uwanja wa ndege nchini Ufaransa kwa hofu ya ulanguzi wa binadamu imewasili nchini India.

Ndege ya kukodi ya Airbus A340, iliyokuwa ikisafiri kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwenda Nicaragua, ilizua shaka wakati wa kujaza mafuta.

Iliondoka ikiwa na abiria 276 lakini watu 25 wakiwemo watoto wawili walisalia Ufaransa baada ya kuomba hifadhi.

Washukiwa wawili wa usafirishaji haramu wa binadamu pia wamesalia nchini Ufaransa kwa uchunguzi zaidi.

Hata hivyo wawili hao waliachiliwa huru na mahakama. Ndege ya Legend Airlines ilitua Mumbai mapema Jumanne kwa saa za huko.

Picha zilizochapishwa na shirika la habari la ANI zinaonesha abiria kadhaa wakiwa wameketi kwenye viti vya plastiki kwenye uwanja wa ndege wa Mumbai baada ya ndege hiyo kutua.

Baadhi ya abiria walionekana wakitoka katika uwanja wa ndege lakini BBC idhaa ya Marathi inaripoti kuwa wengi wao walikataa kujibu maswali kutoka kwa vyombo vya habari.

Ndege hiyo hapo awali ilikuwa imezuiwa kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Châlons-Vatry, yapata kilomita 130 kutoka Paris, siku ya Alhamisi baada ya mamlaka kupokea taarifa isiyojulikana kwamba baadhi ya abiria wanaweza kuwa “waathirika wa biashara haramu ya binadamu,” waendesha mashtaka wa Paris walisema.

Wengi wa waliokuwemo ndani waliaminika kuwa raia wa India wanaofanya kazi UAE.

Theluthi moja ya abiria wanaripotiwa kutoka katika jimbo tajiri la magharibi mwa India la Gujarat.

Mamlaka ya Ufaransa iliripotiwa pia kushuku kuwa huenda watu waliokuwa kwenye meli hiyo walikuwa wakisafiri kwenda Nicaragua kabla ya kujaribu kuingia Marekani au Canada. Haijabainika iwapo mamlaka ilikuwa imeamua kwa uhakika kwamba hakuna uhalifu wowote uliokuwa umetendwa kabla ya kuruhusu ndege hiyo kuondoka.

Haijulikani pia kwa nini ndege hiyo iliKwenda Mumbai badala ya kuendelea na safari yake ya kwenda Nicaragua.

Source:Bbc

Ndege iliyoshikiliwa kwa hofu ya biashara ya binadamu yatua India
0 Comment

Mvua imesababisha vifo vya watu 4 huko DRCAfyaclass Bongo Social •

Mvua imesababisha vifo vya watu 4 huko DRC.

Watu watano waliokolewa na wengine 20 walisombwa na maji. Juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa wengine zinaendelea katika eneo.

Mvua kubwa ilisababisha maporomoko ya ardhi mashariki mwa Congo usiku wa kuamkia Jumatatu na kusababisha vifo vya watu wasiopungua wanne na kuwaacha wengine 20 wakiwa hawajulikani waliko, afisa mmoja wa eneo hilo amesema.

Maporomoko hayo yalitokea Jumapili jioni karibu na mji wa Kamituga katika mkoa wa Kivu Kusini kulingana na Naibu Meya Alexandre Ngandu Kamundala. Kiasi cha watu 25 wengi wao wakiwa wachimba migodi walipata hifadhi kutokana na mvua zilizonyesha kwenye mabanda wakati maporomoko ya ardhi yalipochukua makazi yao na kuyapeleka katika mto uliofurika, Kamundala alisema.

Watu watano waliokolewa kwa urahisi na wengine 20 walisombwa na maji. Miili minne ilipatikana ikiwa imekufa, alisema Kamundala. Juhudi za kuwatafuta na kuwaokoa zinaendelea ili kuwapata wale ambao bado hawajulikani waliko. Mwaka 2020 watu wasiopungua 50 katika mji huo huo wa Kamituga walifariki dunia katika maporomoko ya ardhi yaliyopiga eneo la mgodi wa dhahabu katika eneo hilo.

Ajali zinazopelekea vifo ni za kawaida katika migodi mingi ambayo haijadhibitiwa nchini Kongo huku idadi kubwa ya vifo haviripotiwi kutokana na maeneo yao madogo kuwepo katika milima na misitu.

Chanzo: Voa

Mvua imesababisha vifo vya watu 4 huko DRC
0 Comment

Ifahamu historia ya ‘boxing day’Afyaclass Bongo Social •

Ifahamu historia ya ‘boxing day’

Kila ifikapo Desemba 26, dunia husherehekea sikukuu ya ‘boxing day’ ambayo mara nyingi huenda sambamba na kutoa na kupokea zawadi.

Hii ni siku ya pili baada ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi. Zaidi ya Sh22.7 trilioni zinatarajiwa kutumika duniani mwaka huu katika manunuzi ya zawadi za siku hiyo kwa mujibu wa mtandao wa ‘The Sydney Morning Gerlad’ wa nchini Australia.

Matumizi hayo yatakuwa ni ongezeko la asilimia 1.6 ya matumizi yaliyofanyika katika kipindi kama hicho mwaka 2022. Utafiti huo unaonyesha katika bidhaa zitakazoongoza kununuliwa zaidi ni vifaa vya kazi, nguo, vyakula na mapambo.

Historia ya ‘boxing day’

Tovuti ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) inasema ‘Boxing Day’ ilianza kuitwa hivyo wakati Malkia Victoria wa Uingereza akiwa madarakani mwaka 1800, kutokana na utamaduni uliokuwapo wakati huo uliohusisha familia za kitajiri kutoa zawadi kwa familia za kimasikini.

“Kwa kuwa watumishi wa watu wa tabaka la juu walitakiwa kufanya kazi siku ya Krismasi, hivyo siku iliyofuata waajiri waliwapatia wafanyakazi masanduku yenye zawadi, fedha na mabaki ya Krismasi kama vile bonasi ya likizo,” imeandika tovuti hiyo katika moja ya makala yake iliyoelezea asili ya sikukuu ya boxing day.

Hata hivyo, tovuti ya www.history.com inaeleza nadharia nyingine kuhusu asili ya sikukuu hiyo ya kupeana zawadi, “Jina la ‘boxing day’ lilitokana na masanduku ya sadaka yaliyowekwa makanisani kwa ajili ya kukusanya michango kwa wale wanaohitaji, kisha Desemba 26 makasisi hutoa fedha hizo kwa masikini kwa heshima ya sikukuu ya Mtakatifu Stefano, shahidi Mkristo anayejulikana kwa matendo ya hisani,” imeeleza tovuti hiyo.

Wachumi waielezea

Mack Patrick, ambaye ni mchumi anasema sikukuu ya hiyo pamoja na nyingine za mwishoni mwa mwaka zinachochea ukuaji na ongezeko la biashara duniani na nchini pia.

“Katika kitu ambacho nchi za Ulaya kinanufaika nacho katika kujiimarisha kiuchumi ni sikukuu za mwishoni mwa mwaka, kwao huo ni muda wa manunuzi hasa na hii inasababisha mzunguko wa fedha kuongezeka,” amesema.

Alisema, “Kumbuka biashara zinapofanyika pia Serikali inapata kodi ambayo itatumika kutekeleza miradi mingine ya maendeleo.

Kuhusu boxing day, Patrick alisema bado Tanzania inashindwa kutumia vizuri sherehe hiyo katika upande wa biashara. “Bado hatuna tabia ya manunuzi katika kipindi hiki japokuwa ukienda baadhi ya maeneo kama vile Moshi, kule biashara inafanyika hasa na katika nyakati hizi watakuwa wanakusanya sana kodi,” amesema.

Ifahamu historia ya ‘boxing day’
0 Comment

Je, unajua kucha zako zinaweza kuonyesha hali ya afya yako kwa ujumla?Afyaclass Bongo Social •

Je, unajua kucha zako zinaweza kuonyesha hali ya afya yako kwa ujumla? gafla kucha kukakamaa, kuvunjika au kupasuka kwa urahisi,kubadilika rangi n.k

Hali ya kucha zako inaweza kuwa dalili ya kuonyesha kwamba kuna kitu hakipo sawa nwilini,

Mfano; kucha kuanza kukakamaa kwa gafla,kuvunjika au kupasuka kwa urahisi tofauti na huko nyuma, kubadilika rangi n.k

Hii inaweza kuwa Ishara ya magonjwa mbali mbali kama vile: Ugonjwa wa tezi(thyroid disease), upungufu wa virutubisho kama vile proteins,magonjwa kama kisukari n.k

Hivo ukiona hali hii inakutokea kwa gafla ni Vizuri kuchukua hatua,Waone wataalam wa afya kwa Uchunguzi Zaidi…!!!!

SOMA ZAIDI: Magonjwa yanayohusiana na kucha Zako.

Je, unajua kucha zako zinaweza kuonyesha hali ya afya yako kwa ujumla?
0 Comment

Ugonjwa wa Mpox waendelea kuisumbua DRCAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa Mpox waendelea kuisumbua DRC, WHO yasaidia.

Mpox ugonjwa nadra lakini hatari yake ni sawa na virusi vya ndui ambavyo sasa vimetokomezwa.

Kuanzia Januari 1 hadi katikati ya Novemba mwaka huu 2023, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imerekodi zaidi ya wagonjwa 13,000 wanaoshukiwa kuwa na virusi vya Mpox na zaidi ya vifo 600 vimehusishwa na ugonjwa huo.

Hii ndiyo idadi kubwa zaidi ya maambukizi ya kila mwaka yaliyoripotiwa ikilinganishwa na kilele cha awali cha zaidi ya wagonjwa 6,000 walioripotiwa mwaka wa 2020.

“Mlipuko huo unaenea kijiografia, ikiwa ni pamoja na mikoa ambayo haikuwahi kuwa na Mpox. Maambukizi ya Mpox yameripotiwa katika kanda za afya 156 kutoka mikoa 22 kati ya 26 (85%).” Ameeleza leo Dkt Rosamund Lewis, Kiongozi wa wataalamu wa Mpox katika shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO alipozungumza na wanahabari hii leo mjini Geneva, Uswisi.

WHO hivi majuzi ilikamilisha kazi nchini DRC kutathmini hali na kuunga mkono mwitikio wa kitaifa. Hii ni hali tata sana, ikizingatiwa kwamba DRC inakabiliwa na masuala mengine ya dharura ikiwa ni pamoja na kipindupindu na migogoro ya kibinadamu.

Wataalamu wa afya wa mashinani na kitaifa wanajitahidi kukabiliana na janga ambalo linaenea kijiografia, na kuongeza kasi ya maambukizi kupitia ngono kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Maambukizi ya ngono ya mpox yamerekodiwa kwa muda, ikiwa ni pamoja na mlipuko wa Nigeria unaoendelea tangu 2017. Ilikuwa njia kuu ya maambukizi katika nchi ambazo zilikumbwa na milipuko endelevu kwa mara ya kwanza mnamo 2022 – na nyingi za nchi hizi zinaendelea kushuhudia maambukizi hadi leo.

Afisa huyo wa WHO ameeleza kuwa kuna haja ya haraka ya kuwekeza katika uwezo wa kutambua, kuthibitisha na kughughulikia. WHO inafanya kazi na Wizara ya Afya ya DRC kusaidia usambazaji wa vufaa vya kukusanya sampuli na kusafirisha, na kuchunguza sampuli kutoka kwa watu wanaoshukiwa huko Kinshasa, Kivu Kusini na maeneo mengine yaliyoathirika. Kwa sasa, ni asilimia tisa tu ya maambukizi ya Mpoksi yamethibitishwa kimaabara.

Dkt. Rosamund Lewis amesisitiza akisema, “Mlipuko wa ugonjwa wa Mpox nchini DRC ni ukumbusho wa haja ya kuendelea kwa ushirikiano na uratibu wa kimataifa ili kudhibiti na hatimaye kukomesha maambukizi ya Mpox kutoka kwa binadamu hadi kwa binadamu. Mapema mwezi huu, WHO iliarifiwa kuhusu mlipuko unaoshukiwa kuwa kwenye meli ya kitalii yenye ratiba kusini-mashariki mwa Asia.

Tunawahimiza watu binafsi, mamlaka za afya za mitaa na waandaaji wa safari za baharini na mikusanyiko mingine mingi kuendelea kushirikishana taarifa, kuongeza ufahamu na kuchukua hatua zote ili kupunguza hatari ya milipuko ya Mpox.”

Ugonjwa wa Mpox waendelea kuisumbua DRC
0 Comment

Watu 16 Wapoteza Maisha,Mapigano ya Wakulima na WafugajiAfyaclass Bongo Social •

Watu 16 Wapoteza Maisha,Mapigano ya Wakulima na Wafugaji.

Jumla ya Watu 16 wameuawa kufuatia shambulio lililotokea kijiji cha Mushu kilichopo kaskazini kati jimbo la Plateau Nchini Nigeria, eneo ambalo hukumbwa na mapigano baina ya jamii za wakulima na wafugaji kila mara.

Kwa mujibu wa taarufa iliyotolewa na Jeshi nchini humo imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea usiku wa manane kuamkia Desemba 24, 2023 ambapo milio ya risasi ilisikika na Washambuliaji waliwauwa na kuwajeruhi baadhi ya wanakijiji na wengine kutekwa.

Plateau ni jimbo linapatikana mpaka unaotenganisha eneo la kaskazini mwa Nigeria lenye idadi kubwa ya waislamu na kusini kukiws na wakristo wengi ambapo kwa miaka kadhaa limekuwa kitovu cha mivutano ya kikabila na kidini.

Inaarifiwa kuwa wengi wa jamii ya wafugaji ni waislamu na wakulima ni wakristo na mara kadhaa pande hizo mbili zimekuwa zikitumbukia kwenye mapigano ya kugombea ardhi na wakati mwingine mizozo ya imani za kidini.

Watu 16 Wapoteza Maisha,Mapigano ya Wakulima na Wafugaji
0 Comment

Ugonjwa wa uti wa mgongoAfyaclass Bongo Social •

Ugonjwa wa uti wa mgongo

Utangulizi kuhusu Ugonjwa wa uti wa mgongo, Soma Hapa;

Fahamu,Ugonjwa wa uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi.

Ugonjwa wa Uti wa mgongo husababishwa na nini?

Ugonjwa huu husababishwa na vimelea mbalimbali vya makundi ya bakteria, virus na hata fungus. Tukivigawanya visababishi hivi katika makundi haya, tutaona kuwa bakteria wanaosababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni kama vile; bakteria wajulikanao kama Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae pamoja na Mycobacteria tuberculosis, ambao pia ni maarufu kwa kusababisha ugonjwa wa kifua kikuu.

Aidha kutoka kundi la virus, virus wanaojulikana kwa kusababisha ugonjwa huu wa uti wa mgongo ni pamoja na Herpes simplex type 2, HIV pamoja na Varicella zoster.

Vimelea vya fungus ambavyo hujulikana kwa kusababisha ugonjwa wa uti wa mgongo ni pamoja na wale wajulikanao kama Coccoidiodomycosis pamoja na Cryptococci meningetides.

Chanzo cha Ugonjwa wa Homa ya uti wa mgongo(Meningitis)

Homa ya uti wa mgongo  kwa kitaalam hujulikana kama meningitis, ni tatizo ambalo huhusisha maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kwenye sehemu kuu mbili ubongo pamoja na Uti wa mgongo.

Homa ya uti wa mgongo hutokea iwapo utando unaofunika ubongo na uti wa mgongo utapatwa na maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa,soma hapa chini kujua visababishi vya tatizo la homa ya uti wa mgongo.

VISABABISHI VYA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1. Maambukizi ya Bakteria mbali mbali kama vile; Beta-streptococci, Hemophilus influenza, Escherichia coli, Listeria monocytogenes, Neisseria meningitides, Streptococci pneumoniae na Mycobacteria tuberculosis

2. Maambukizi ya Virus mbali mbali kama vile; Herpes simplex type 2, HIV na Varicella zoster.

3. Maambukizi ya Fangasi mbali mbali kama vile; Coccoidiodomycosis na Cryptococci meningetides.N.k

DALILI NA VIASHIRIA VYA TATIZO LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1•Shingo kukakamaa na kuwa ngumu isivyo kawaida

2•Mgonjwa kujihisi homa kali au joto la mwili kuwa juu sana

3•Mgonjwa kupata Maumivu makali sana ya kichwa

4•Mgonjwa kupoteza fahamu au uwezo wa kukumbuka vitu

5•Mgonjwa kupatwa na degedege (seizures) na mwili kukakamaa

6•Mgonjwa kushindwa kuvumilia mwanga (photophobia)

7•Mgonjwa kutoweza kukaa sehemu yenye makelele (phonophobia)

8•Kwa watoto, kuvimba utosi n.k

MADHARA YA TATIZO HILI LA HOMA YA UTI WA MGONGO NI PAMOJA NA;

1•Kuamshwa kwa chembechembe za damu zinazo sababisha damu kuganda kitaalamu hujulikana kama – Disseminated Intravascular Coagulopathy (DIC).

2•Kuvuja damu katika tezi za adrenalin na kupelekea kutokea kwa ugonjwa ambao kitaalamu unaitwa – waterhouse friderichsen syndrome.

3•Kwa watoto, ugonjwa huu unaweza kusababisha mtoto kuwa na kichwa kikubwa – hydrocephalus pamoja na madhara mengine.

MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA UTI WA MGONGO

Kwa wagonjwa waliopoteza fahamu ni vizuri kuhakikisha wanapumua vizuri, na njia za hewa ziko wazi. Halikadhalika, iwapo itathibitika kuwa bakteria ndiyo wanaosababisha ugonjwa huu, mgonjwa anaweza kupewa mojawapo ya dawa hizi za antibiotiki kama cefotaxime au Cefriaxone. Aidha baadhi ya madaktari hupendelea kuongeza dawa za steroids kama dexamethasone kama sehemu ya matibabu.

Iwapo itathibitika ugonjwa huu umesababishwa na virus, dawa kama Acyclovir huweza kutumika. Hali kadhalika, ikithibitika kuwa vimelea waliosababisha ugonjwa huu ni wa kundi la fungus, dawa kama Amphotericin B au flucytosine zaweza kutumika. Mgonjwa pia hupewa Paracetamol kwa ajili ya kushusha homa na kuondoa maumivu ya kichwa.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Ugonjwa wa uti wa mgongo
0 Comment

Ndege ya Malaysia MH370 iliyopotoea na watu 239 inaweza kupatikana, wataalam wanadaiAfyaclass Bongo Social •

Ndege ya Malaysia MH370 iliyopotoea na watu 239 inaweza kupatikana, wataalam wanadai.

Wataalamu wametoa wito wa kutafutwa upya kwa ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH370 iliyotoweka ikiwa na abiria 239 katika safari hiyo,

Mtaalamu wa masuala ya anga, Jean-Luc Marchand na rubani Patrick Blelly walitoa wito wa kutafutwa upya.

Wawili hao walidai kuwa fumbo la kupotea kwa ndege linaweza kutatuliwa katika kipindi cha “siku” ikiwa kungekuwa na utafutaji mpya.

Wakati wa hotuba mbele ya Jumuiya ya Kifalme ya Aeronautical huko London, wanandoa hao walisema eneo jipya la utafutaji linaweza kuchunguzwa kwa siku 10 kwa wito wa wazi huku kukiwa na usaidizi.

“Inaweza kuwa jambo la haraka. Hadi mabaki ya MH370 yanapatikana, hakuna anayejua [kilichotokea]. Lakini, huu ni mwelekeo unaokubalika,” Marchand alisema, kulingana na tovuti ya habari ya Australia news.com.au.

Katika ripoti hiyo hiyo ya tovuti ya habari, wawili hao walitoa wito kwa Mamlaka ya Usalama wa Usafiri ya Australia, serikali ya Malaysia, na Ocean Infinity – kampuni ya uchunguzi – kuanza utafutaji mpya.

Marchand alisema utaftaji wa “haraka” unaweza kuwa msingi mzuri wa uthibitisho wa teknolojia mpya ya utaftaji ya baharini isiyo na rubani.

Alielezea kama “safari mbaya ya njia moja”, ambayo aliamini kuwa huenda ilifanywa na rubani mwenye uzoefu wa ndege.

“Tunafikiri, na utafiti ambao tumefanya umetuonyesha, kwamba utekaji nyara huo labda ulifanywa na rubani mwenye uzoefu,” Marchand alisema.

“Hakika, ndege hiyo haikuonekana isipokuwa wanajeshi. Jamaa huyo alijua kwamba ikiwa utafutaji na uokoaji ungeanzishwa, utakuwa kwenye njia ya ndege.

Wawili hao walibishana kwamba transponder ya ndege hiyo ilizimwa na kwamba “U-turn” iliyofanyika mbali na njia ya ndege haikuweza kuwa ya otomatiki.

Jioni ya Machi 8, 2014, ndege ya Malaysia Airlines iliyokuwa na watu 239 iliondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur kuelekea Beijing lakini ikatoweka kwenye skrini za rada takriban saa mbili baada ya kuondoka.’

Kufuatia hilo, oparesheni kubwa za utafutaji zilizohusisha nchi kadhaa zilifanyika kusini mwa Bahari ya Hindi, lakini ndege hiyo wala mabaki yake hayakupatikana.

Ndege ya Malaysia MH370 iliyopotoea na watu 239 inaweza kupatikana,
wataalam wanadai
0 Comment

Tatizo la Mtoto Kutanguliza Makalio au matako wakati wa kuzaliwaAfyaclass Bongo Social •

Tatizo la Mtoto Kutanguliza Makalio wakati wa kuzaliwa (Breech Presentation)

Breech presentation: ni ile hali ya Mtoto kuzaliwa akiwa ametanguliza Matako au makalio,

Ipo milalo mbali mbali ya Mtoto akiwa kwenye tumbo la Uzazi,

Mtoto huweza kutanguliza;

  • Kichwa
  • Matako/makalio n.k

UJAUZITO:

Ni hali ambayo mwanamke anaipitia wakati kiumbe kinakuwa ndani ya mfuko wa uzani. Kipindi hiki kinaambatana na mabadiliko ya mwili (physiological changes),

Katika ukuaji wa mimba kutokana na nafasi mtoto aliyokuwa nayo ndani ya mji wa mimba huwa anahali ya kuzunguka mara kwa mara na kusababisha kuwa na matokeo tofauti ya mikao ya watoto,

Mikao ya watoto ndani ya mji wa mimba ipo aina nyingi ila ulio wa hatari zaidi ni ule ambao makalio yanakuwa yametangulia (breech presentation).

Tatizo hili la kutanguliza makalio kwa watoto linachukua asilimia 3-4% kwa wazazi wanaofika mda wa kujifungua. Pia asilimia kubwa zaidi inapatwa na tatizo hili kama mimba inakuwa haijakomaa.

Hii inamaana kwamba walio hatarini zaidi ni wenye mimba zilizo chini ya wiki 34 kwani kipindi hiki watoto wanakuwa bado hawajageuka.

Chanzo cha Mtoto kuzaliwa akiwa ametanguliza Makalio

Sababu zinazopelekea kwa watoto kutanguliza makalio ni kama zifuatazo:

1.  Ufupi wa kitovu (short cord) na kitovu kuzunguka shingo ya mtoto (nuchal cord): tatizo hili linafananishwa na mtu kujitundika kwenye kitanzi ambapo huwezi ukafurukuta zaidi ya kuendelea kukaa katika mlalo mmoja na kupelekea makalio kutangulia. Huwa inatokea zaidi kama zalio pia lipo juu (fundal placenta)

2.   Maji kuwa mengi (polyhydramnious): yanaruhusu mtoto kuwa na uwezo wa kuzunguka sana (unstable lie).

3.  Maji kuwa kidogo (oligohydramnious): yanamfanya mtoto akose nafasi ya kuzunguka ambapo kuta za mji wa uzazi zinamshikilia mtoto katika mlalo mmoja ambao pia unaweza leta vilema vya viungo.

4.  Uvimbe kwenye kuta za mji wa mimba (myoma uteri): uvimbe huu unaweza punguza eneo la chumba cha mtoto na kusababisha mtoto asipate nafasi ya kugeuka mwishowe kuishia mlalo mmoja wa kutanguliza makalio.

5.  Kutangulia kwa kondo au zalio (praevia): zalio (placenta) linapaswa kujishikiza kwenye mji wa mimba mbali na shingo ya uzazi. Lakini pale inapotokea likajipandikiza kwenye shinyo ya uzazi (cervix) na kuifunika inapelekea kwa watoto kutanguliza makalio na tatizo hili njia ya kujifungulia ni kwa upasuaji hata kama mtoto ametanguliza kichwa.

6.    Vilema vya watoto (fetal anomalies): kwa asilimia kubwa hii inatokea kwa watoto wenye vichwa maji (hydrocephalus).

7.    Mapacha (twins): kutokana na uhaba wa chumba, watoto wanapokuwa wawili katika mji wa mimba wanashindwa kugeuka mara kwa mara na hii inapelekea kukaa katika mkao mmoja.

Matokeo ya mlalo huu (breech presentation) unapofikia zaidi ya wiki 37 wazazi wengi wanapangiwa kuzalishwa kwa njia ya upasuaji (caesarean section) kwani ndio njia salama kwa mama na mtoto.

Kwa baadhi ya wajawazito, madaktari wanaweza kujaribu kuwageuza watoto (external cephalic version) kabla ya kupatwa na uchungu na kisha kuwaweka kwenye uchungu.

Kwa bahati mbaya maeneo mengine wajawazito wanakuwa hawana taarifa za milalo ya watoto wao kwani mimba ikishafika zaidi ya wiki 36 huwa wanaambiwa wakasubirie uchungu nyumbani ambapo sio sahihi.

Mara nyingi makalio ya watoto yanakuwa madogo kuliko kichwa hivyo wakati wa uchungu mtoto anaweza akapitisha makalio kiurahisi kwenye njia ya uzazi lakini kichwa kikagoma kupita na kupelekea maji kuingia kwenye njia ya hewa (aspiration pneumonia) na wakati mwingine kupoteza uhai. Hii ndio sababu kuu inayopelekea sisi madaktari kuchagua upasuaji kama njia salama ya kujifungua.

Hitimisho: kwa wajawazito wote ili kuweza kujifungua kwa njia ya kawaida ni vyema kujua mlalo wa mtoto wako kati ya wiki 36-38.

Ni nyema pia kuendelea kwenda clinic mpaka mwisho wa ujauzito. Pale inapotokea kwamba unahitajika kufanyiwa upasuaji wa kuzaa kutokana na mlalo wa mtoto usio sahihi ni vyema kukubaliana na daktari wako ili kuepusha matatizo makubwa yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto. Kinga ni bora kuliko tiba.

Tatizo la Mtoto Kutanguliza Makalio au matako wakati wa kuzaliwa
0 Comment

TAHADHARI: Virusi vya UVIKO aina ya JN.1 vyazidi kuongezeka katika nchi nyingi dunianiAfyaclass Bongo Social •

Huku msimu wa baridi kali ukiendelea barani Ulaya, virusi vya UVIKO aina ya JN.1 vinaongezeka katika nchi nyingi duniani.

Lakini hatari ya jumla kwa umma inatathminiwa kuwa chini, huku chanjo zilizopo zikiendelea kutoa ulinzi kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).

Ujerumani imeshuhudia kuongezeka kwa viwango vya wagonjwa wanaolazwa hospitalini kutokana na maambukizi ya Uviko yanayohusiana na kirusi aina ya JN.1.

Kulingana na takwimu rasmi, watu 302,100 nchini Ujerumani wameambukizwa kirusi hicho kufikia Desemba 20, idadi iliyoongezeka kutoka maambukizi 110,000 mnamo Oktoba 20 na 195,000 Novemba 20.

Rajib Dasgupta, mtaalam wa magonjwa katika Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, nchini India, amesema India pia inakabiliwa na hali mbaya ya maambukizi, haswa katika majimbo ya Kerala na Karnataka, ambapo viongozi wameimarisha ufuatiliaji wa magonjwa na kuwashauri watu kuchukua hatua zinazofaa.

Mtaalamu wa afya ya umma katika Chuo Kikuu cha Washington huko St. Louis, Ziyad Al-Aly amesema hali hii sio tu kwa Ujerumani na India pekee, na kwamba hali inazidi kuwa mbaya na kirusi hicho kinaendelea kuenea duniani kote.

Hata hivyo viwango halisi vya maambukizo ya UVIKO vinauwezekano wa kuwa juu zaidi kuliko vile vinavyoripotiwa kwa sababu ya ukosefu wa upimaji.

Nchi nyingi ziliacha kuripoti utaratibu wa matokeo ya vipimo mwishoni mwa 2022 au mapema 2023, na kuna watu wachache tu ambao bado wanapimwa na vigumu kubaini idadi ya maambukizo kote ulimwenguni.

Umuhimu wa chanjo

Al-Aly aliiambia DW kwamba ni muhimu sana kwa watu kupata chanjo mpya na pia kupata chanjo nyengine za kujikinga dhidi ya mafua. Na akaongezea kusema kwamba habari njema, ni kwamba chanjo za ziada zilizopo bado zinafaa dhidi ya kirusi cha JN.1.

Hata hivyo, chanjo za kuimarisha kinga hazipatikani kila mahali duniani, alisema Dasgupta: “India imesitisha chanzo hizo. Kwa hakika, utoaji wa dozi ya tatu ya nyongeza umekuwa nyuma sana ya dozi mbili za kwanza.”

Vile vile kutokana na hali hii Shirika la Afya Ulimwenguni WHO linapendekeza kuvaa barakoa katika maeneo ya umma au kuepuka mikusanyiko ya kijamii ikiwa unajihisi mgonjwa ili kusaidia kupunguza kuenea kwa virusi.

TAHADHARI: Virusi vya UVIKO aina ya JN.1 vyazidi kuongezeka katika nchi
nyingi duniani
0 Comment

Mwimbaji Celine Dion hupata tiba ya physical therapy kila siku ili kupambana na ugonjwa wa stiff-person syndromeAfyaclass Bongo Social •

Mwimbaji Celine Dion hupata tiba ya physical therapy kila siku, kupambana na ugonjwa usiotibika wa stiff-person syndrome.

Celine Dion anaripotiwa kupata ‘matibabu ya mwili yaani physical therapy kila siku’ huku akipambana na ugonjwa wa stiff-person syndrome, ugonjwa usio na tiba.

Mwimbaji huyo wa Kanada mwenye umri wa miaka 55, ambaye amepoteza udhibiti wa misuli yake kutokana na kuugua ugonjwa unaojulikana kama stiff-person syndrome, ugonjwa huu mpaka sasa hauna Tiba kamili,

kulingana na dada yake, Celine Dion anafanya kazi kwa bidii ili kuondokana na hali yake, kulingana na vyanzo mbali mbali vya habari.

‘Celine ni mpiganaji,’ mdadisi wa ndani aliambia  US Weekly. ‘Hana udhibiti mwingi juu ya misuli yake kama alivyokuwa hapo awali, lakini anafanya kazi na madaktari na wataalamu wa tiba ya mwili ili kupata nafuu.’

Chanzo hicho kilidai, ‘Celine amekuwa akichukua muda kuangazia afya yake lakini anapanga kupanda jukwaani tena mara tu atakapopewa idhini na timu yake ya matibabu.’

Mtu mwingine wa ndani pia aliongeza kuwa mwimbaji huyo ‘anaendelea kuimarika afya yake na amekuwa mwenye furaha zaidi na anamfanyia mazoezi ya mwili kila siku.’

‘Kurudi jukwaani kwa namna fulani ni ndoto yake ya mara kwa mara, hata kama hawezi tena kuimba; anataka tu kuona nyuso hizo zinazong’aa.’

Ugonjwa wa Stiff-person syndrome ni ‘ugonjwa nadra wa mfumo wa neva wa autoimmune ambao kwa kawaida husababisha kukakamaa kwa misuli na mikazo yenye uchungu ambayo huja na kuondoka na inaweza kuwa mbaya zaidi baada ya muda,’ kulingana na John Hopkins Medicine.

Mshindi huyo wa Grammy alionekana mara ya mwisho kwenye mchezo wa magongo huko Las Vegas akiwa na mapacha wake Eddy na Nelson, wenye umri wa miaka 13, na mwanawe mkubwa Charles-Rene, mwenye umri wa miaka 22, wakitazama Montreal Canadiens.

Celine Dion alisema;

“My boys and I had such a fun time visiting with the Montreal Canadiens after their hockey game with Vegas Golden Knights in Las Vegas Monday night,’ the My Heart Will Go On singer posted November 1.

‘They played so well, what a game!! Thank you for meeting us after the game, guys! That was memorable for all of us. Have a great season! – Celine xx”… ‘

Mwimbaji Celine Dion hupata tiba ya physical therapy kila siku ili
kupambana na ugonjwa wa stiff-person syndrome
0 Comment

Mwendokasi, kuzidisha abiria chanzo ajali msimu wa sikukuuAfyaclass Bongo Social •

Mwendokasi, kuzidisha abiria chanzo ajali msimu wa sikukuu

Jeshi la Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani limetoa onyo kwa madereva wanaokiuka sheria na kanuni za usalama barabarani na kusema watawatoza faini za papo kwa papo pamoja na kuwafikisha Mahakamani.

Onyo hilo limetolewa hii leo Desemba 24, 2023 na Afisa Mnadhimu Makao makuu ya Trafiki nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Pili Misungwi wakati akizungumza na Madereva, Abiria na Mawakala wa mabasi stendi kuu Makatanini iliyopo Babati Manyara.

Amesema, madereva, abiria na mawakala hao wanatakiwa kuzingatia sheria kwa kujali matumizi sahihi ya barabara na kuepuka kupakia abiria kupita kiasi kwani imekatazwa kisheria.

Aidha, amewatahadharisha madereva kukagua vyombo vyao vya moto mara Kwa mara kabla ya kuanza safari ili kubaini kama kuna changamoto iweze kutatuliwa mapema kabla haijasababisha ajali.

Awali, Kamanda wa Kikosi hicho Mkoa wa Manyara Mrakibu wa Polisi, Fredinand Mpolo amemuhakikishia Kamishna huyo kuwa watafanya kazi usiku na mchana na kuhakikisha wanawakamata madereva wazembe barabarani.

Kamishna Misungwi yupo Mkoani Manyara katika ziara ya kikazi kukagua utendaji kazi wa Askari kikosi hicho, pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani kwa madereva na abiria.

Chanzo: Dar24

Mwendokasi, kuzidisha abiria chanzo ajali msimu wa sikukuu
0 Comment

Afyaclass tunakutakia sikukuu njema ya ChristMas(Merry Christmas to you)Afyaclass Bongo Social •

Afyaclass tunakutakia sikukuu njema ya ChristMas(Merry Christmas to you).

Asante kwa kuendelea kuwa mdau muhimu sana wa afyaclass,

Wewe ambaye kwa namna moja au nyingine ulishirikiana na afyaclass kwa njia mbali mbali ikiwemo;

  • Kuwa Msomaji wa kila siku na kuendelea kujifunza mambo mbali mbali kuhusu afya
  • Kupata Huduma za afya ndani ya afyaclass
  • Na Feedback nyingi ambazo mnatupa kila siku kwa huduma mnazopata ndani ya afyaclass
  • Shuhuda Zenu zinatupa nguvu ya kuendelea na kujua kwamba tuna jamii kubwa nyuma yetu inanufaika na huduma hii…

Tunakuthamini sana mdau muhimu wa afyaclass, endelea kuwa pamoja nasi, Na tunakutakia Sikukuu Njema ya Christmas,

Sherekea kwa Amani,Upendo na Utilivu..!!!!

Afyaclass tunakutakia sikukuu njema ya ChristMas(Merry Christmas to you)
0 Comment

Faida za limao katika mwiliAfyaclass Bongo Social •

Faida za limao katika mwili,Soma hapa kujua

Limao, lenye jina la kisayansi Citrus limon, ni tunda lenye faida nyingi kiafya. Kutokana na virutubisho vyake, limao linaweza kuchangia kuboresha afya ya mwili kwa njia kadhaa. Hapa chini ni baadhi ya faida za limao mwilini:

1. Chanzo kizuri cha Vitamini C na Ascorbic acid:

Limao ni chanzo kikubwa cha vitamini C, ambayo ni muhimu kwa mfumo wa kinga ya mwili,

Vitamini C husaidia kupambana na magonjwa na kuimarisha mwili dhidi ya maambukizi.

Asidi ascorbic inayopatikana katika limao pia ina jukumu muhimu katika kuboresha afya ya ngozi na kudumisha afya ya tishu.

2. Husaidia Kupunguza Uzito wa Mwili:

Limao linafaida kwa wale wanaopambana na uzito. Asidi ya limao inaweza kusaidia katika kuchoma mafuta na kudhibiti hamu ya kula.

Kunywa maji yenye limao asubuhi inaweza kuchangia kuanza siku vizuri na kuweka mchakato wa kimetaboliki kwenye kiwango cha juu,

Hii ni faida kwa wale wanaohitaji kudhibiti Uzito wa Mwili..

3. Mfumo wa Upumuaji:

Limao linaweza kuleta afueni kwa watu wanaosumbuliwa na matatizo ya kupumua kama vile pumu. Aina fulani za asidi zinazopatikana katika limao zinaweza kusaidia kupunguza dalili na kuboresha upumuaji.

4. Kusaidia kuboresha afya ya Figo:

Limao lina vitu vinavyoweza kusaidia katika kuyeyusha mawe ya figo na kuondoa sumu mwilini. Kunywa maji yenye limao kunaweza kuwa njia ya kiafya ya kusaidia mfumo wa figo kufanya kazi vizuri.

5. Kupunguza Msongamano wa Damu:

Limao lina kiwango cha juu cha potasiamu, ambacho ni muhimu kwa kudhibiti shinikizo la damu. Hii inaweza kusaidia kuzuia matatizo ya moyo na mishipa ya damu.

6. Kuboresha Uwiano wa pH:

Ingawa limao ni tunda la asidi, linaweza kuwa na athari ya kubadilisha uwiano wa pH mwilini. Limao linaweza kuwa na athari kwenye alkali mwilini baada ya kufanyika kimetaboliki, na hivyo kusaidia kupunguza asidi mwilini.

7. Kuboresha Mzunguko wa Damu:

Vitamini C inayopatikana katika limao inaweza kusaidia kuboresha mzunguko wa damu. Hii ni muhimu kwa afya ya moyo na kuzuia matatizo ya mishipa ya damu(cardiovascular disorders).

8. Kusaidia kuboresha Afya ya Ini:

Limao linaweza kusaidia katika kusafisha ini na kuongeza uzalishaji wa nyongo(bile). Hii inaweza kuchangia kuboresha mmeng’enyo wa chakula na afya ya ini.

Hizo ndyo baadhi ya Faida za limao katika mwili.

Kumbuka; Ni muhimu kutambua kwamba ingawa limao lina faida nyingi, watu wenye matatizo ya tumbo au dawa maalum wanapaswa kushauriana na wataalamu wa afya kabla ya kuanza matumizi ya mara kwa mara.

Pia, kama sehemu ya lishe inayofaa, limao linaweza kuchangia kwa jumla katika kudumisha afya bora.

Asante…!!!!!!

Faida za limao katika mwili
0 Comment

Mlipuko wa Dengue Afrika 2023, watu 700 walikufa-WHOAfyaclass Bongo Social •

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani(WHO); Mlipuko wa Dengue Afrika 2023, watu 700 walikufa, Burkina Faso ilikuwa na wagonjwa wengi

Ugonjwa wa Dengue umeendelea kuwa ‘mwiba’ barani Afrika ambapo mwaka huu pekee umesababisha vifo vya watu 700 kati ya wagonjwa 170,000 walioripotiwa kwenye nchi 47 za ukanda wa Afrika wa shirika la afya duniani, WHO.

Dkt. Diana Rojas Alvarez akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi leo wakati akiwapatia hali ya ugonjwa huo duniani amezitaja nchi za Afrika zilizokuwa na mlipuko wa dengue kuwa ni 15 na miongoni mwao ni Benin, Cape Verde, Chad, Cote d’Ivoire, Ethiopia, Ghana, Guinea, Mali, Nigeria na Burkina Faso.

Burkina Faso ilikuwa na wagonjwa wengi zaidi, takribani 150,000 kati ya watu  wote hao 170,000 waliothibitika kuwa na ugonjwa huo unaoenezwa na mbu aina ya Aedes.

“Nadhani bara la Afrika lina uzoefu mkubwa wa kukabiliana na ugonjwa wa Malaria, ambao ni mgonjwa mwingine unaoenezwa na vimelea vya mbu aina ya Anopheles anayeishi ndani ya nyumba. Hata hivyo huyu ni mbu tofauti kabisa na wana tabia tofauti,” amesema Dkt. Alvarez.

Amefafanua kuwa baadhi ya hatua na mikakati inayochukuliwa kukabili maambukizi ya Malaria haiwezi kukabili maambukizi ya Dengue ambayo huenezwa na Aedes.

Hivyo amesema kwenye kumkabili Aedes, kinachotakiwa sio tu matumizi ya dawa za kuua vijidudu pekee, bali pia mbinu za kuwadhibiti kuanzia wanapokuwa viluwiluwi au lava, ambapo utatumia dawa ya kuua lava.

Amesema mbu hao pia wanaishi kwenye mimea ya maua inayowekwa ndani ya nyumba, au chombo chochote cha kuhifadhi maji masafi.

“Kwa hiyo jambo muhimu ni kusaka njia ya kuondoa mazalia ya hao mbu kama njia mojawapo ya kudhibiti viluwiluwi na mbu wakubwa,” amesema Afisa huyo wa WHO.

Hivyo amesema kwa sasa WHO wanashirikiana na wadau kupata mbinu ya kuhakikisha hakuna ugonjwa huo au wanapunguza kiwango cha uwepo wa ugonjwa huo ukanda wa Afrika.

Mlipuko wa Dengue Afrika 2023, watu 700 walikufa-WHO
0 Comment
Notification
Karibu Afyaclass Bongo Social Jukwaa linalojadili mambo mbali mbali ikiwemo afya,Magonjwa na Updates Zote,Tembelea hapa kila Siku,Pia Share Maoni yako kwenye jukwaa hili Afyaclass Bongo Social ASANTE.
UNDERSTOOD