Afyaclass Mtawa kuchunguzwa baada ya kukutwa na sanduku lenye mwili wa rafiki yake aliyekufa

Mtawa kuchunguzwa baada ya kukutwa na sanduku lenye mwili wa rafiki yake aliyekufa

Nchini Chile, polisi wanachunguza kisa cha mtawa mmoja, 80 kuacha sanduku lililojaa mabaki ya mwili wa rafiki yake aliyekufa mwaka mmoja uliopita huko mjini Santiago.

Sanduku hilo lililojaa mifupa liligunduliwa siku ya Jumatatu baada ya mzoa takataka kusikia harufu mbaya alipolisogelea sanduku hilo.

Mwanamke huyo aliwaambia polisi kwamba yeye na rafiki yake ambaye pia alikuwa mtawa waliingia mapatano ya kuwa pamoja hata baada ya kifo kutokana na mapenzi waliyokuwa nayo.

Polisi hawakumkamata kwa kisa hicho, lakini pengine mtawa huyo atawekewa vikwazo chini ya kanuni za afya ya umma kwa kutojulisha mamlaka kuhusu kifo cha rafiki yake ili azikwe au kuchomwa moto.

You, Mehreen and others
Hashtag:

WEKA MAONI HAPA(Reply)

Notification
My blog is in the process of editing and perfecting the new template, so there are still some functions to click but not yet used. Note which blogs associated with your side please read this lesson to update the blog logo.
UNDERSTOOD